Hali ni mbaya ward A na B za watoto walioko MOI (Muhimbili)

Hizo wodi za muhimbili & Moi hiyo ni kawaida sana mkuu,madaktari siku zote hawana muda wanawahi kazi binafsi ..........Ukiwa mgonjwa ndio utajua tabia ya madaktari na manesi hasa ukiwa umelazwa.Tuombe mungu
Mkuu ukweli hausemwi tu ila watumishi wengi (sio wote) wa serikali wana mgomo fulani hivi! na shida ya nchi zetu za kiafrika ni priority zetu, kwetu sisi ni bora kununua magari mengi ya washawasha, kuliko kuimarisha huduma za afya! Kwa sasa watumishi wengi wa serikali wanaingia kazini ontime ila kacheki output yao mwisho wa siku ndo utajua tofauti ya gov na private sector! tukubali tukatae ni lazima serikali icheki tena namna pesa za walipa kodi zinavyotumika, hebu cheki vipato wanavyopata wabunge halafu leo hii mtu kasota kusoma chuo kama muhimbili tena karudiarudia weeee halafu anaanza kazi na anategemewa atende kazi kwa moyo wake wote! then kuna bint mbiiiichi kama yule mtoto wa Bulmbb ambaye hata miaka 24 hajafika keshapata mkopo wa gari ML 90, je ni wangapi watakuwa hivyo maana si wote wenye hofu kwamba wanawajibika kwa Mungu kabla ya wanadamu! Kiukweli vitu vya public quality duni!

Ndo maana ukifuatilia sana matendo ya serikali unaweza ishia mkufuru Mungu! cha msingi ni mtu kutafuta mafanikio kwa bidii na kutumia fursa zilizopo ili kuinufaisha jamii yako!
 
ALAFU WABADILSHE MAJINA YA HIZO WODI MANA HIYO SEWA HAJI INAENDANDA NA MATENDO VILEo_O
 
Yeye anaangalia ila huwezi kujua kama anaangalia, kulala wawili wawili sio ishu ya madaktari au manesi, hiyo ni ishu ya Wizara husika
Suala la kulala wawili wawili ni tatizo na linatakiwa kushughulikiwa. Iwe ni wizara husika au MOI.
Huduma zetu za afya kwa kiwango kikubwa ni mbovu. Madaktari na wafanyakazi wengine wanakosa vifaa tiba, madawa, na vitendanishi. Kinachoudhi ni pale serikali inaposema vitu hivi vipo vya kutosha. Kauli hizi zinajenga chuki. Wananchi wanaona waganga ni wezi na wana roho mbaya.
 
Nazungumzia wodi ya watoto waliovunjika viungo, sizungumzii waendesha bodaboda kwani wao ni wakubwa na wala sijawahi kuingia kwenye ward yao

Kwani hao watoto sababu za kuvunjika viungo ni zipi?
Kucheza kijoti tu?? Ajali za barabarani hazihusiki?
 
NB: Nilitaka nichukue picha lakini nafsi ikanisuta. Pamoja na nia yangu njema ya kutolea taarifa, lakini nikajiuliza kuwa kwa upande mwingine, hawa wauguzaji wanaweza wasijisikie vizuri kuchukuliwa picha katika mazingira hayo. Lakini nasisitiza, kwa aliyepo Dar, awe kama vile anapita tu, aingie ward hiyo ajionee

Picha walikataza wateule wa Mungu
 
Jamani Moi kunashida kubwa. Niwapepongezi madactari bingwa pamoja n uchache wao wanajitahidi . Huduma wodini n mbaya. Manesi hawajali wagonjwa kibisaa japo sio wote. Madaktari wa wodini wanapopita round wasikilize mgonjwa analalamika nn. Wapunguze kasi. Kuna mtu kasema eti hawatakiwi kumshika shika mgonjwa waliye vunjika. Sidhani km yupo sahihi naogapa kusema n hoja ya kituko. Serikali isomeshe madaktari bingwa wawe wengi n maslahi yao yaongezwe. Mm nilikuwa n mgonjwa Moi kuna shida kubwa.
 
Bwana Ngosha zile hasira na kufoka foka kumeishia wapi? Arudi tena Muhimbili akatumbue...
 
Asubuhi ya leo nimetoka kumuona mgonjwa katika wodi ya watoto waliovunjika mifupa iliyopo Muhimbili chini ya taasisi ya MOI. Nilichokikuta kinasikitisha sana, na nilichosimuliwa na wazazi/walezi wanaowatazama watoto hao kinasikitisha zaidi

Nilichoona:
Vitanda vyote 23 katika wodi A vina wagonjwa wawili wawili, yaani maana yake kuna wagonjwa 46. Ukubwa wa wodi kwa uzoefu wangu wa metric units, ni 6m x 18m = 108 sq. metres

Kwa lugha ya ujumla, chumba chenye eneo la mita za mraba 108 kinatumika kuwalaza watoto 46, na hapo bado waangalizi wao wanaoshinda nao, ambao nao wapo 46, kufanya jumla ya msongamano wa watu 92 ndani ya kaeneo hako! Hapo nimeamua kuneglect watu wanaofika na kuondoka kwa lengo la kuwaona wagonjwa, kama mimi. Hiyo ni hali ya population density ambayo niliiona kwa macho yangu

Nilichosimuliwa:
Mzazi wa mtoto niliyeenda kumuona pamoja na mzazi wa mtoto mwezie wanaoshea kitanda, wamenieleza jinsi huduma ya hovyo inavyotolewa. Daktari anapopita hamuangalii mgonjwa na kutumia utaalamu wake kujua hali yake, bali anamuuliza muangalizi kuwa mgonjwa anaendeleaje, chochote atakachosema muangalizi ndicho hicho daktari anaandika na kuondoka kwenda kitanda kingine!

Hana muda wa kuangalia kiungo cha mtoto kilichovunjika kinaendeleaje, bali anatumia maelezo ya muangalizi pekee, halafu wala hachanganyi utaalamu wake, anaandika na kuondoka. Dada wa pembeni akalalamika kuwa ameambiwa asaini document ambayo hajui inahusu nini, na kwa kutumia udhaifu wa uelewa wa watu wetu, daktari/muuguzi amemsainisha tu.

Watoto wamewekewa mawe yananing'inia tu, hawapewi dawa yoyote! Jamani hakuna siasa hapa, waliopo Dar waende wodi ya watoto waliovunjika viungo leo hii wakafanye mahojiano hata kwa siri siri, halafu waje tuone kama kuna kuongeza chumvi au ndio hali iliyopo!

Wito:
Serikali iachane na siasa katika afya za wanadamu wananchi wake. Wataalamu wanaposema kuna upungufu wa vifaa,rasilimali watu au miundombinu ya hospitali, hatua za kurekebisha zichukuliwe, au walau watu waambiwe ukweli ili wajipange na wagonjwa wao kukabiliana na hali ya hospitalini. Wagonjwa wanaposema kuna uzembe wa wafanyakazi, hatua zichukuliwe. Hakuna haja ya kubishana kwenye vyombo vya habari kuficha uovu

Karibuni Muhimbili wodi ya watoto waliovunjika viungo, nyuma ya wodi ya Sewa Haji

cc: HKigwangalla
Tunasema kila siku hii nchi doctor patient ratio na nurse patient ratio ni kubwa mno! Kwa hiyo tufanyeje sasa? Wagonjwa ni wengi, watoa huduma wachache na utawala hautuheshimu matokeo yake ndo hayo.
 
Hata kumuangalia kwa macho pia itadisturb? Kulala wawili wawili je?

Muumbuaji,
Hizi habari zinasikitisha sana ukizingatia tuko kwenye awamu ya mzee wa kutumbua majipu.
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi kuna kipindi tuliambiwa Vitanda mamia kadhaa vimenunuliwa kutokana na Fedha iliyokatwa kwenye sherehe za Uhuru au sijui Bunge lilibana matumizi!!!!
Je, hivo vitanda vilikuwa HEWA au vipi? Sipati picha ya watoto kulala 2/2. Lazima kutakuwa na tatizo hapa. Tunataka Umi Mwalimu tumsikie akitoa tamko la kukanusha. Maana kama akikubali tu basi hana Uwaziri tena.
 
Asubuhi ya leo nimetoka kumuona mgonjwa katika wodi ya watoto waliovunjika mifupa iliyopo Muhimbili chini ya taasisi ya MOI. Nilichokikuta kinasikitisha sana, na nilichosimuliwa na wazazi/walezi wanaowatazama watoto hao kinasikitisha zaidi

Nilichoona:
Vitanda vyote 23 katika wodi A vina wagonjwa wawili wawili, yaani maana yake kuna wagonjwa 46. Ukubwa wa wodi kwa uzoefu wangu wa metric units, ni 6m x 18m = 108 sq. metres

Kwa lugha ya ujumla, chumba chenye eneo la mita za mraba 108 kinatumika kuwalaza watoto 46, na hapo bado waangalizi wao wanaoshinda nao, ambao nao wapo 46, kufanya jumla ya msongamano wa watu 92 ndani ya kaeneo hako! Hapo nimeamua kuneglect watu wanaofika na kuondoka kwa lengo la kuwaona wagonjwa, kama mimi. Hiyo ni hali ya population density ambayo niliiona kwa macho yangu

Nilichosimuliwa:
Mzazi wa mtoto niliyeenda kumuona pamoja na mzazi wa mtoto mwezie wanaoshea kitanda, wamenieleza jinsi huduma ya hovyo inavyotolewa. Daktari anapopita hamuangalii mgonjwa na kutumia utaalamu wake kujua hali yake, bali anamuuliza muangalizi kuwa mgonjwa anaendeleaje, chochote atakachosema muangalizi ndicho hicho daktari anaandika na kuondoka kwenda kitanda kingine!

Hana muda wa kuangalia kiungo cha mtoto kilichovunjika kinaendeleaje, bali anatumia maelezo ya muangalizi pekee, halafu wala hachanganyi utaalamu wake, anaandika na kuondoka. Dada wa pembeni akalalamika kuwa ameambiwa asaini document ambayo hajui inahusu nini, na kwa kutumia udhaifu wa uelewa wa watu wetu, daktari/muuguzi amemsainisha tu.

Watoto wamewekewa mawe yananing'inia tu, hawapewi dawa yoyote! Jamani hakuna siasa hapa, waliopo Dar waende wodi ya watoto waliovunjika viungo leo hii wakafanye mahojiano hata kwa siri siri, halafu waje tuone kama kuna kuongeza chumvi au ndio hali iliyopo!

Wito:
Serikali iachane na siasa katika afya za wanadamu wananchi wake. Wataalamu wanaposema kuna upungufu wa vifaa,rasilimali watu au miundombinu ya hospitali, hatua za kurekebisha zichukuliwe, au walau watu waambiwe ukweli ili wajipange na wagonjwa wao kukabiliana na hali ya hospitalini. Wagonjwa wanaposema kuna uzembe wa wafanyakazi, hatua zichukuliwe. Hakuna haja ya kubishana kwenye vyombo vya habari kuficha uovu

Karibuni Muhimbili wodi ya watoto waliovunjika viungo, nyuma ya wodi ya Sewa Haji

cc: HKigwangalla
" Nchi yangu ni Tajiri "
 
Hata mimi nilijaaliwa kufika hapo nilisikitika sana,mpaka nikawa najisemea hivi hii nchi haina viongozi wenye uchungu wakapaza sauti zao katika masuala ya msingi kama haya.
 
Kwa kweli madaktari ni wachache sana nchi hii na wao wanazidiwa na wingi wa wagonjwa, serikali sikivu, fungueni basi! Ajira za watu wa afya waje kuokoa jahazi, hali ni mbaya sana katika sekta ya afya"
 
tatizo la hii nchi viongozi wengi wanachumia tu matumbo yao, hawana habari na wananchi wanyonge.....wao wakiugua wanapelekwa kutibiwa india,ukifikiria sana kuhusu hii nchi utapata kichaaa bure
 
Madaktari wengi wako Muhimbili kama location tu ila mioyo yao iko private hospitals. Wauaji wakubwa hawa. Yaani unaingia kwa Dr. anakuuuliza eti una kadi ya afya. Ukijibu ndiyo anaweza kukuambia nifuate Regency au Hindu Mandal!!! Ohh my Godness.
 
Back
Top Bottom