Asubuhi ya leo nimetoka kumuona mgonjwa katika wodi ya watoto waliovunjika mifupa iliyopo Muhimbili chini ya taasisi ya MOI. Nilichokikuta kinasikitisha sana, na nilichosimuliwa na wazazi/walezi wanaowatazama watoto hao kinasikitisha zaidi
Nilichoona:
Vitanda vyote 23 katika wodi A vina wagonjwa wawili wawili, yaani maana yake kuna wagonjwa 46. Ukubwa wa wodi kwa uzoefu wangu wa metric units, ni 6m x 18m = 108 sq. metres
Kwa lugha ya ujumla, chumba chenye eneo la mita za mraba 108 kinatumika kuwalaza watoto 46, na hapo bado waangalizi wao wanaoshinda nao, ambao nao wapo 46, kufanya jumla ya msongamano wa watu 92 ndani ya kaeneo hako! Hapo nimeamua kuneglect watu wanaofika na kuondoka kwa lengo la kuwaona wagonjwa, kama mimi. Hiyo ni hali ya population density ambayo niliiona kwa macho yangu
Nilichosimuliwa:
Mzazi wa mtoto niliyeenda kumuona pamoja na mzazi wa mtoto mwezie wanaoshea kitanda, wamenieleza jinsi huduma ya hovyo inavyotolewa. Daktari anapopita hamuangalii mgonjwa na kutumia utaalamu wake kujua hali yake, bali anamuuliza muangalizi kuwa mgonjwa anaendeleaje, chochote atakachosema muangalizi ndicho hicho daktari anaandika na kuondoka kwenda kitanda kingine!
Hana muda wa kuangalia kiungo cha mtoto kilichovunjika kinaendeleaje, bali anatumia maelezo ya muangalizi pekee, halafu wala hachanganyi utaalamu wake, anaandika na kuondoka. Dada wa pembeni akalalamika kuwa ameambiwa asaini document ambayo hajui inahusu nini, na kwa kutumia udhaifu wa uelewa wa watu wetu, daktari/muuguzi amemsainisha tu.
Watoto wamewekewa mawe yananing'inia tu, hawapewi dawa yoyote! Jamani hakuna siasa hapa, waliopo Dar waende wodi ya watoto waliovunjika viungo leo hii wakafanye mahojiano hata kwa siri siri, halafu waje tuone kama kuna kuongeza chumvi au ndio hali iliyopo!
Wito:
Serikali iachane na siasa katika afya za wanadamu wananchi wake. Wataalamu wanaposema kuna upungufu wa vifaa,rasilimali watu au miundombinu ya hospitali, hatua za kurekebisha zichukuliwe, au walau watu waambiwe ukweli ili wajipange na wagonjwa wao kukabiliana na hali ya hospitalini. Wagonjwa wanaposema kuna uzembe wa wafanyakazi, hatua zichukuliwe. Hakuna haja ya kubishana kwenye vyombo vya habari kuficha uovu
Karibuni Muhimbili wodi ya watoto waliovunjika viungo, nyuma ya wodi ya Sewa Haji
cc: HKigwangalla
Tunasema kila siku hii nchi doctor patient ratio na nurse patient ratio ni kubwa mno! Kwa hiyo tufanyeje sasa? Wagonjwa ni wengi, watoa huduma wachache na utawala hautuheshimu matokeo yake ndo hayo.
Ndugu unajua kuwa "profesa" maji marefu analipwa mshahara mkubwa kuliko wa profesa Janabi mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya jakaya Kikwete, hapa ndo Penye tatizo hayo ya wito ni upuuzi na ubatili mtupu.Kazi ya kuhudumia wagonjwa ni ya wito. Unapokuta dakitari anapita bila kumcheki mgonjwa ujue hakuna madili kwa mhusika na pia hajali kazi yake. Najua vijana wengi wanaosomea udakitari kwa sasa wanawaza kutoka na siyo kuutumia utaalamu wao kutatua changamoto, bali kila kijana anawaza anunue BMW, anawaza ajenge gorofa, anawaza awazidi wenzake.
Kuhusu vifaa kwa kweli nadhani ni janga la kitaifa, ni tofauti sana na nchi za wenzetu.
Mkuu nimekuelewa vizuri ,mbeya wazima lakini ?Solution hapa ni kuajiri Watumishi wengi kwenye kada za Udaktari na Unesi.
Tatizo lililopo kwa sasa ni Serikali hii kukosa vipaumbele. Mkuu wa kaya hataki kuajiri mpaka sasa anafanya uhakiki wa vyeti feki na mwaka unaishia. Wanatuambia wamekuta wafanyakzi hewa 17,000+ na hawa walikuwa wanalipwa mishahara ya Mabilioni.
Kwanini sasa wasiajiri Watu muhimu kama Madaktari ili hiyo pesa iliyokuwa inatumika kulipa HEWA iwalipe Madaktari wapya??
Mtukutu Rahisi hela kanunulia ndege.Huwezi amini...kuna watakaobisha.
Na ndiyo maana ili uonekane umefanikiwa Tz ni kwenda kugombea ubunge. Ila kusoma ni sawa na kujinyea kinyesi kichwani. Hakuna anayewajali ma dr, hakuna anayejua chnagamoto za wauguzi mahospitali. Wanasiasa wanaleta siasa kwenye afya za watu. Ila la wito lipo pale pale!Ndugu unajua kuwa "profesa" maji marefu analipwa mshahara mkubwa kuliko wa profesa Janabi mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya jakaya Kikwete, hapa ndo Penye tatizo hayo ya wito ni upuuzi na ubatili mtupu.
Naungana na wewe kuhusu madaktari hasa wa Muhimbili.Kazi ya kuhudumia wagonjwa ni ya wito. Unapokuta dakitari anapita bila kumcheki mgonjwa ujue hakuna madili kwa mhusika na pia hajali kazi yake. Najua vijana wengi wanaosomea udakitari kwa sasa wanawaza kutoka na siyo kuutumia utaalamu wao kutatua changamoto, bali kila kijana anawaza anunue BMW, anawaza ajenge gorofa, anawaza awazidi wenzake.
Kuhusu vifaa kwa kweli nadhani ni janga la kitaifa, ni tofauti sana na nchi za wenzetu.
Si waziri kasema nchi haina tatizo la huduma za afya? Huu utakuwa uchochezi. Haiwezekani kutumia mitandao kuipinga serikali!
Atuko kisiasa bali tunaeleza hali halisi ya hapo muhimbili!kuna shemu wangu aliwahi kulazwa kwenye hiyo wodi siku niliyoenda kumuona sio siri roho iliniuma sana.NB: Nilitaka nichukue picha lakini nafsi ikanisuta. Pamoja na nia yangu njema ya kutolea taarifa, lakini nikajiuliza kuwa kwa upande mwingine, hawa wauguzaji wanaweza wasijisikie vizuri kuchukuliwa picha katika mazingira hayo. Lakini nasisitiza, kwa aliyepo Dar, awe kama vile anapita tu, aingie ward hiyo ajionee
Mkuu nimekuelewa sana.....tatizo siku hizi mkweli ni mmoja tu nchi hii.Bahati mbaya maslahi pekee ninayoweza ku'declare katika uzi huu ni uzalendo. Niliyeenda kumuona ni mtoto wa jirani yangu. Sina haja ya kufanya uchochezi, na ndio maana nikatoa wito kwa watu wenye sauti zaidi yangu waipaze huko juu, maana kwa hali ie, mtu anaenda kutibiwa lakini ajiandae pia kuambukizwa!
Hapo kwenye wito ndo Penye kosa hapo, wanasiasa wanafuja mahana ya wito!. Kwanini basi wito usiwe universal kwa kila mmoja?. Usifanye siasa kama huna wito wa siasa, nirudie tena hicho unacho kiita wito ni uhuni wa wana siasa dhidi ya wana taaluma. Kumbuka dr, nurses, mwalimu hapeleki wito dukani na kupewa sukari!Na ndiyo maana ili uonekane umefanikiwa Tz ni kwenda kugombea ubunge. Ila kusoma ni sawa na kujinyea kinyesi kichwani. Hakuna anayewajali ma dr, hakuna anayejua chnagamoto za wauguzi mahospitali. Wanasiasa wanaleta siasa kwenye afya za watu. Ila la wito lipo pale pale!
mkuu una hoja, lakini ungeenda kumuuliza afisa uhusiano wa MOI ungepata majibu sahihi, badala ya hao wamama.Na mimi wala sijaelekeza jumba bovu kwa madaktari pekee, bali kwa yeyote anayewajibika katika eneo linalomuhusu