Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,602
- 5,569
Inasikitisha sana kuona wasio na hatia wakilemazwa na kuuawa, Nilitahadharisha mapema humu ndani kabla nini kingelitokea, nilionekana mwoga na nisiyependa kuona nguvu ya umma ikitumika! Mazingira ya Tanzania si tofauti na nchi nyingine za Afrika, ni kwamba tunajisahaulisha tu na kuona kwamba matokeo yanaweza kuwa sawa na fikra zetu. Kuna kumbukumbu nyingi zinaonesha matokeo ya maandamano Tanzania mwisho wake ni upi.
Anzieni miaka ya sabini, kisha enzi za Mtikila na Magabachori, Mrema wakati wa NCCR, Mwembechai, Maandamano ya CUF Zanzibar na Dar es Salaam. Je leo mlitarajia kwamba tumeshabadilika? Hata haijapita siku toka zipigwe risasi za moto buguruni... Sidhani na sitarajii kama kuna mtanzania atapata haki zake za kikatiba katika katiba hii iliyopo sasa inayowalinda watawala hata kama wametenda uovu.
Inatia uchungu naishia hapa kwa sasa.