Hali ilivyo nchini Somalia

mapesa yamejaa

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
1,412
3,403
Mwezi March nilienda nchini Somalia kikazi chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa liitwalo Internation Organization for Migration.

Ili kufupisha maada. Nilichokishuhudia huko nchini Somalia kilinishangaza sana nikilinganisha na hali ya nyumbani Tanzania. Yaani Somalia ukiondoa ile hofu ya Al-Shabaab vitu vingine vyote ni rahisi kuliko nchini kwetu Tanzania.

Mfano, niliuliza gunia la mchele la kilo 100 na bei ilikuwa hela za kitanzania 60,000 kwa mjini mogadishu na miji ya pembezoni bei ilikuwa ya chini zaidi mafuta (petroli ilikuwa Tsh 2500), diesel ni tshiling 2000.na mafuta ya taa ni 1,500.Bei hizi ni za kuanzia mwezi wa 8.2022.

Miundombinu kama barabara, hosipitali na umeme zinajengwa kwa kasi sana nchini Somalia tofauti na Tanzania ambapo ni mwendo wa konokono, pesa ya Somalia ina thamani kubwa dhidi ya pesa ya Tanzania.

Watanzania wenzangu kwa nini tunazidiwa na Somalia kimaendeleo? Yaani nchi ina vita toka 1990 hadi leo lakini ina maendeleo zaidi kuliko Tanzania. Sababu ni nini inayotufanya Watanzania maisha yawe magumu kuliko Somalia?
 
Wametuzidi kwa sababu kuna vita. Wale watu lege lege wavivu wavivu wamepakimbia na kwenda sehemu zenye amani kama Tanzania na kuja kuunganika nao kuendelea kulala, kukaa vijiweni bila kazi, kufuatilia udaku n.k..

Wale wapambanaji wa kivita na kimaisha wameendelea kubaki huko huko na ndio hao wanaleta maendeleo kwa sababu hawataki mchezo!

"NO STRAIN, NO GAIN"
 
Mogadishu kwenye kupangilia mji wao, dar ikasome. Sehemu ambazo hata makazi bado kote kumepimwa(surveyed) na barabara zimechongwa vizuri sana. Kifupi hakuna viwanja holela
Umefika lini Mogadishu we mataga? Kwanza achana na JF we karani watu wanawasubiri majumbani huko we kishikwambi unaperuzia JF haya toka haraka sana kahesabu kaya zako.
 
Wametuzidi kwa sababu kuna vita. Wale watu lege lege wavivu wavivu wamepakimbia na kwenda sehemu zenye amani kama Tanzania na kuja kuunganika nao kuendelea kulala, kukaa vijiweni bila kazi, kufuatilia udaku n.k..

Wale wapambanaji wa kivita na kimaisha wameendelea kubaki huko huko na ndio hao wanaleta maendeleo kwa sababu hawataki mchezo!

"NO STRAIN, NO GAIN"
Hiyo sio sababu. Kuna nchi hazina Vita na zina Maendeleo makubwa sana kutuzidi mfano Botswana.

Na Kuna nchi zina Vita Ila hazina Maendeleo yoyote mfano Sudan.

Weka hoja zako vizuri.
 
Hiyo sio sababu. Kuna nchi hazina Vita na zina Maendeleo makubwa sana kutuzidi mfano Botswana.

Na Kuna nchi zina Vita Ila hazina Maendeleo yoyote mfano Sudan.

Weka hoja zako vizuri.
Sasa ulitaka awekeje. Yaan unafananisha na Sudan ya kusin hii iliyopata uhuru juzi juzi tu hapa. make wao tangu wapate uhuru wanapigana. Make Ile ya warabu inatuzidi maendleo mbali sana.
 
Kama ni kuzuri kwanini Kila siku wanakimbia kwao? Umewahi kuona watu wanakimbilia Somalia?

Ukienda Ethiopia si ndo utasema ni mbinguni ila Kila siku Ethiopians wanashikwa kwenye malori hapa.

Grass is always greener on the other side.
 
Umefika lini Mogadishu we mataga? Kwanza achana na JF we karani watu wanawasubiri majumbani huko we kishikwambi unaperuzia JF haya toka haraka sana kahesabu kaya zako.
Wewe dada sikia, Mogadishu Somalia nimewahi kufika kwa project maalum. Kuanzia Jaabad hadi Degmada kuna maelfu ya plots zimepimwa na kutengenezwa barabara ila hakuna nyumba wala mkazi yoyote. Kifupi wao miundombinu inaanza alafu watu ndio wanafatia.

Ni maelfu ya plots yapo tupu na bado wanaendelea kupima na kuchonga barabara
 
Sasa ulitaka awekeje. Yaan unafananisha na Sudan ya kusin hii iliyopata uhuru juzi juzi tu hapa. make wao tangu wapate uhuru wanapigana. Make Ile ya warabu inatuzidi maendleo mbali sana.
Hata huelewi nilichojibu. Sababu aliyotoa sio ya kweli ndio maana nikamtolea hiyo mifano.
 
Back
Top Bottom