Hali halisi ya Mtanzania kiuchumi

kiraremapojoni

JF-Expert Member
Nov 30, 2018
390
500
Jana nilibahati kakukaa wa wanazengo katika mitaa ya kati kujadili changamoto za kimaisha na hasa kwa wanaoishi mjini. Nimegundua kwamba maisha ni magumu kwa kila mtu sio mfanyakazi wala mfanyabiashara. Kila mtu analalamika upande wake

Mfanyakazi anakwambia hakuna nyongeza ya mshahara kwa mwaka wa tatu mfululizo na hata zile haki ambazo ni za kikatiba pia hawapati. Suala la masaa ya ziada ndo limekuwa kama anasa ingawa wanakaa kazini na wanatekeleza majukumu. Wanapojaribu kudai wanaambiwa wanatekeleza majukumu yao wakati mkabata wa ajira unawaamuru kufanya kazi mpaka saa tisa unusu au saa kumi

Mfanyabiashara analia kushuka kwa mauzo kiasi ambacho anakaa na bidhaa zake kwa muda mrefu na hii inamuongezea gharama za kuhifadhi mzigo (Storage costs) na anapopata mteja anauuza kwa bei ya hasara nagalau afidie gharama nyengine za kuendesha duka. Wale ambao wanamioyo dhaifu ndo wanaamua kufunga biashara mara baada ya kuona amepata hasara kwa miaka miwili mfu;lulizo na mtaji unakata bila ya sababu yamsingi.

sijazungumzia kundi athirika la vyeti feki na wale waliotumbuliwa ambao kesi zao hazijaanza wala hawajajua kama zitakwisha lini. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa
 
nzoka boy

JF-Expert Member
Oct 14, 2017
1,187
2,000
nashuli wafanya biashara kama kweli wanaona wanapata hasara kila siku wafunge tuu biashara!! kuna aliewalazimisha kufanya biashata?? mbona sisi wakulima wa mahindi tumekaa kimyaa??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,630
2,000
Hali sio ngumu hila tunaishi ishi maisha halisi yanayotatikana kama unafanya biashara halali unalipa kodi uwezi kuwa na wasi wasi lakini kama umezoea kukwepa kodi lazima ulalamike tu..
 
ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
4,815
2,000
Hujamaliza hapo wakulima,wafanyabiashara ndogo ndogo mfano biashara za chakula zimekua ngumu mno,pubs na kumbi za starehe kwa ujumla hali tete,mafundi wajenzi hawapati kazi,maduka ya vifaa vya ujenzi wateja wamepungua,gari za mizigo kazi zimepungua sana! Ni njaa kwa kwenda mbele,sijui biashara ya tex...ki ujumla tunaumia sana sekta binafsi pia..ada,kodi za nyumba,vikoba,mikopo,vitu havinunuliki...haviuziki..
Jana nilibahati kakukaa wa wanazengo katika mitaa ya kati kujadili changamoto za kimaisha na hasa kwa wanaoishi mjini. Nimegundua kwamba maisha ni magumu kwa kila mtu sio mfanyakazi wala mfanyabiashara. Kila mtu analalamika upande wake

Mfanyakazi anakwambia hakuna nyongeza ya mshahara kwamwaka wa tatu mfululizo na hata zile haki mabazo ni za kikatiba pia hawapati. Suala la masaa ya ziada ndo limekuwa kama anasa ingawa wanakaa kazini na wanatekeleza majukumu. Wanapojaribu kudai wanaambiwa wanatekeleza majukumu yao wakati mkabata wa ajira unawaamuru kufanya kazi mpaka saa tisa unusu au saa kumi

Mfanyabiashara analia kushuka kwa mauzo kiasi ambacho anakaa na bidhaa zake kwa muda mrefu na hii inamuongezea gharama za kuhifadhi mzigo (Storage costs) na anapopata mteja anauuza kwa bei ya hasara nagalau afidie gharama nyengine za kuendesha duka. Wale ambao wanamioyo dhaifu ndo wanaamua kufunga biashara mara baada ya kuona amepata hasara kwa miaka miwili mfu;lulizo na mtaji unakata bila ya sababu yamsingi.

sijazungumzia kundi athirika la vyeti feki na wale waliotumbuliwa ambao kesi zao hazijaanza wala hawajajua kama zitakwisha lini. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom