Ibada ya kwanza
JF-Expert Member
- Mar 21, 2013
- 3,282
- 1,810
cdm ni wauza sumu, hakuna mtu mbinafsi duniani kama Babu Slaa
mambo vipi mwigamba?upo kaka?
cdm ni wauza sumu, hakuna mtu mbinafsi duniani kama Babu Slaa
Mbowe ndiyo kirusi ndani ya CHADEMA akiondoka madarakani(mwenyekiti) chama kitafika mbali zaidi.
Japo mimi sio mwanachama wa Chadema, siamini kuwa ni kweli kuna hii hali tete unayoizumza hapa!.
Ila naamini kuna uwezekano mkubwa Mhe. Mbowe, sasa ameukubali ukweli halisi kuwa Chadema peke yao kamwe hawawezi kuliondoa hili dubwana CCM bila ushirikiano wa kuunganisha nguvu na wapinzani wengine wote wa kweli kutengeneza umoja ni nguvu, utakaopelekea kusimamisha mgombea mmoja mwenye nguvu na atakayekubalika na wengi ili uchaguzi wa 2015, uwe ni wa ama Sao, ama zetu na kuondokana na ule utitiri wa wagombea hivyo mfaidika ni CCM!.
Dr ni mtu wa chuki, hasira, visasi na kinyongo, hivyo akikumbuka alivyoteseka ile 2010 huku hao wanaojiita wapinzani wakishirikiana na CCM, anaweza asikubali ushirikiano wa aina yoyote na watu wasioaminiana!. Huu ni mwendelezo tuu wa ukosefu wa busara. Chadema peke yao kamwe hawawezi!.
Amini nawaambieni, isinge kuwa chuki, hasira, visasi na ukosefu wa busara japo kidogo tuu, hata hili suala la Zitto na ule waraka, lisinge fika hapa lilipofikishwa!.
Mhe. Mbowe pamoja na weaknesses zake kama binadamu na uwezo mdogo as charismatic leader, bado ni very visionary leader anayeona mbali, very diplomatic, very compromising asiye na chuki, visasi kwa yaliyopita, na mnaweza kushangaa katika Baraza Kuu, ndie yeye anaweza to forgive, forget and open a new chapter in Chadema kufungua milango ya political diversity kukubali na accommodate differing political views za mawazo tofauti kitu ambacho ni kigumu sana kukubalika na ex seminarians waliolelewa kwenye very conservatism doctrine ya kukubali kwa kusema yes bila kuuliza, na ukitofautiana nao hata katika jambo dogo, kwao ni uasi!.
Pasco
INASEMEKANA takataka KAMA HIZI ZINAPENDWA SANA NA VIONGOZI WA JF !
Shetani anaweza kuwashauri waumini eti askofu wenu ndio tatizo akiondoka tu kanisa linakua na wote mnaenda mbinguni?!!!We gamba tu suburi mnyolewe kwanza maana mmeshindwa kumnunua kamanda wa anga!
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Chama Cha Mapinduzi, kimebeba mzigo wa madeni. Msiri wangu hapa Lumumba amenidokeza kuwa chama kinadaiwa hadi na vyombo vya habari.
Kimeshindwa kuwasilisha makato ya wafanyakazi wake; madeni kutoka taasisi za fedha yamelundikana hadi kufikia zaidi ya Sh. 1.3, huku nikielezwa kuwa Akaunti zake zimefilisika. Mabilioni haya ya fedha yametafanwa na wakubwa wakiongozwa na Mwigulu Nchemba.
Soma kiambatanisho hiki hapa chini kilichotoka kwa Mwigulu Nchemba kwenda kwa Zakia Meghi. Ni wakati Nchemba alipokuwa akikabidhi madaraka ya Katibu wa Uchumi na Fedha kwa Zakia Meghji.
MAKABIDHIANO YA IDARA YA UCHUMI NA FEDHA
KATI YA MHE. MWIGULU L. NCHEMBA (MB)(MNEC)
NA MHE. ZAKIA H. MEGHJI (MB) KATIBU
WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
WA UCHUMI NA FEDHA
2. IDARA YA UCHUMI NA FEDHA
Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana mjini Dar es Salaam tarehe 27 - 29 Januari, 2004 pamoja na mambo mengine ilipitisha muundo mpya wa Idara ya Uchumi na Fedha. Awali Idara hii ilijulikana kama Idara ya Fedha na Mali za Chama. Badiliko hili la muundo linazingatia mambo yafuatayo:-
.
(a) Kwa mujibu wa Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010 - 2020 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 Chama kinatakiwa kusimamia kwa nguvu mpya Sera zake za Uchumi hususan modenaizesheni ya Uchumi na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
(b) Aidha suala la Vitega Uchumi na Uwekezaji katika Chama linatakiwa kupewa umuhimu na msukumo mkubwa ili kukiimarisha Chama kimapato na hatimaye kiweze kujitegemea.
HESABU ZA CHAMA NA KAMATI YA KUHAKIKI MALI ZA CHAMA
(a) HESABU ZA CHAMA
Hesabu za Chama zimekaguliwa na wakaguzi wa nje TAC-Associates kwa mwaka wa Fedha 2009/2010 na 2010/2011. Hesabu hizo zimeshawasilishwa kwa Mwenyekiti kwa ajili ya kuwekwa saini na baadaye kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Zoezi la kuziwasilisha kwenye vikao vya Chama litafuata baadaye. Kwa mujibu wa hesabu hizo, Chama kina mali zenye thamani ya Shs. 49.2bn/= hadi tarehe 30.06.2011. Thamani ya mali inashuka kila mwaka kutokana na Chama kutofanya uthamini wa mali zake. Mara ya mwisho uthamini ulifanyika mwaka 1992. Kwa hiyo Wakaguzi wameshauri kuwa Chama kifanye upya zoezi la uthamini. Kutokana na ukubwa na upana wa kazi hii, zoezi hili linahitaji wataalam wengi, kwa sababu hiyo Chama huwa kinawatumia Chuo cha Ardhi kwa kuwa wao wanawatumia wanafunzi wao katika kuifanya kazi hii na hivyo kuharakisha zoezi hilo.
(b) KAMATI YA KUHAKIKI MALI ZA CHAMA
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana Aprili, 2007 mjini Dar es Salaam iliunda Kamati ya Wataalam kwa ajili ya uhakiki mali za Chama. Majina ya Wataalam hao ni:-
(1) Ndg. Peter Machunde - Fedha na Vitega Uchumi
(2) Ndg. George Fumbuka - Fedha na Vitega Uchumi
(3) Ndg. Sam Mapande - Mwanasheria
(4) Ndg. Kanyoni Salum Kanyoni - Mhandisi
(5) Ndg. Jacquiline Noni - Mfanyabiashara
(6) Ndg. Simon Mapolu - Mchumi
(7) Ndg. Janeth Mbene - Mchumi
(8) Ndg. Ussi Faki - Mkaguzi
Katibu wa Kamati hiyo alikuwa Ndugu L.L. Burugi - Meneja Miliki wa Chama.
Kamati ilianza kazi tarehe 19/6/2007 na kukamilisha tarehe 28/10/2007. Kazi ya Kamati hii ililenga mali za Kudumu za Chama zilizopo Makao Makuu, Mikoani na katika Wilaya zilizopo kwenye Makao Makuu ya Mikoa. Aidha, zoezi hili lilihusisha pia mali za Jumuiya za Chama katika maeneo hayo pamoja na kufanya tathmini ya mwenendo wa Makampuni ya Chama.
12. BAADHI YA MADENI AMBAYO CHAMA KINADAIWA
(1) MADENI YA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA
NBC Ltd. - 143,763,404.00
NSSF - 831,822,961.50
Ukaguzi wa Hesabu - 72,240,000.00
1,107,826,365.50
Deni la NBC ni la tangu mwaka 1994 kupitia Kampuni ya Chama TANTI kwa kuweka rehani nyumba 10 za CCM zilizoko Area C - Dodoma.
Mkopo wa NSSF unahusu Jengo la CCM Shinyanga. NSSF walimalizia kujenga Jengo. Mazungumzo yalifanyika kati ya CCM/NSSF na kufikia makubaliano ya Chama kununua Jengo hilo kwa shs. 1,109,097,282/= kiasi cha 25% kimelipwa.
Deni la ukaguzi linatokana na ukaguzi wa hesabu za mwaka 2009/2010 na 2010/2011.
(2) MADENI YA VYOMBO VYA HABARI
1. Clouds Entertainment Media Group 13,080,000.00
2. Radio Tumaini 424,800.00
3. ITV 3,778,360.00
4. Sahara Media Group Ltd 44,244,000.00
5. Sports Dream Co. Ltd 810,000.00
6. KIUTA 9,430,350.00
7. Colour Print 22,619,792.00
8. Business Times Ltd (Majira) 4,988,945.00
9. Habari Corporation 6,850,000.00
10. Mwananchi Communication Ltd 9,620,000.00
11. TSN 8,271,160.00
12. Guardian Ltd 11,702,160.00
13. TBC 7,687,360.00
14. Uhuru Publication Ltd 55,049,040.00
15. WAPO Radio 1,000,000.00
16. Zanzibar Leo 4,500,000.00
17. Raia Mwema 1,129,000.00
18. FTV Production 1,980,000.00
Jumla Tshs. 201,866,807.00
Tunaendelea kufuatilia nyaraka nyingine na kila zitakapopatikana tutawaletea.
Reply With Quote
Dhambi ya ubaguzi imeanza kuwatafuna. MWANZO WA MWISHO umewadia.
slaa na mbowe ni majanga
Niajiri mi niwe mwalimu wako
Uzushi huo,na ingekuwa mmemsema Zito ungeweza hata kufungiwa.Nadhani mnajua kusoma nyakati,mfadhili wenu Nchemba amepanda cheo.Maneno kama hayo unaweza kupata hela kwa nchembaCHADEMA HALI BADO TETE. SASA NI MBOWE vs SLAA. Baada ya kutokufanikiwa kumvua uanachama wake na kufanikiwa kumvua nyadhifa zake zote ndani ya chama na ndani ya bunge sasa hali sio nzuri ndani ya chama na hasa viongozi wakuu M/kiti na Katibu wake ndani ya chama. Mwanaripota wetu ndani ya mtaa wa UFIPA yaliopo makao makuu ya chama anadai kumekuwepo na vikao vya Mara kwa Mara baada tu kusigana na Mzalendo zito zuberi kabwe. Moja kati ya ajenda jadiliwa kwenye kikao ni namna gani wataunda baraza kivuli la mawaziri baada ya kumvua nyadhifa zake zito., Msuguano mkubwa uliopo kati ya Mbowe na Slaa ni huu. Mbowe anataka kuunda baraza kivuli akivishirikisha vyama pinzani bungeni vyenye wabunge yeye km kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ameona upungufu huo na kutakakuunganisha nguvu. Nae katibu wa chama kama mgombea urais aliepita yeye hakubaliani na M/kiti wake na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ktk suaka la kuunda kambi ya pamoja ya upinzani bungeni.,yeye anataka wasifanye badiliko lolote ndani ya bunge . Mimi najiuliza Je?ni nani mwenye sauti ndani ya chama?kati ya Mbowe na Slaa, sijapata jibu hapo. Kusigana huko kwenye vikao kulifanya kutengeneza Makundi mengine mawili tena, Sasa kuna kundi la Mbowe vs Slaa ndani ya chama ukiliweka pembeni lile la Mzalendo. Tujiulize nini Matokeo yake na mwisho WAO. Kwa chuki zao mbaya, Roho zao mbaya na hata Ubinafsi WAO wakuwachukia wenzao maeneo wanayotokea bila kujali utaifa na umaskini tulionao. Yamebainika nayatatokea mengi ndani ya CHADEMA. Watanzania na wanachadema wako viongozi makini kwenye vyama hivi vya upinzani tusione haya kuhamia huko kwani hiyo sio dini useme utaulizwa na Baba au mkee hiyo ni siasa na ni MFUMO wa Maisha yk pindi unapopata kiongozi mzuri.
Chadema kwisha habari yao
dhambi ya ubaguzi inaendelea kukitafuna chama?
Mnatia aibu sasa...Maana mpo kama misukule hapa JF..
Nyi mazuzu kweli,nani asiye jua kuwamnaona bosi wenu Nchemba amepanda cheo ndiyo wakati umefika kuendeleza pumba zenu humu.Kwa akili yenu,ukitaka kupata hela kwa Nchemba mseme tu Mbowe.Maana hata yeye anapo changia bungeni lazima amseme Mbowedhambi ya ubaguzi inaendelea kukitafuna chama?