Hakuna urafiki kati ya Askari Polisi na raia. HAKUNA!

Polisi wanazingua sana aisee ndio maana uhalifu haushi mitaani kwa tabia zao watu hawataki hata kuwapa ushirikiano hata kama anaumia yeye na jamii yake
Wangekuwa sio wazinguaji naamini hata kazi yao kwa namna fulani ingekuwa nyepesi
 
Ndo hivyo kuna makosa ukiyafanya wema pekee atakao kufanyia polisi ni kukukwepa usionane nae maana hata ukionana nae yeye hana uwezo wa kukusaidia
Sio polisi tu kazi nyingi ziko hivyo.
Ila ndo ivo binadamu kupenda kutupia lawama watu wengine kwa makosa yao.

Mfano hapo mtu anatuhumiwa kwa jambo fulani ambalo ni kweli kalifanya na ushahidi upo wazi, ila atataka polisi (rafiki yake) amsaidie ili ajinasue kwenye huo msala.
Polisi akila kona basi mtu huyo ataanza kulaumu na kusema hamna urafiki kati ya polisi na raia.

Ila ni ukweli uliodhahiri polisi wakandamizaji ni wengi nchini.
 
Kuna mmoja alijichanganya kwa mwana mmoja karudi kupumzika siku kadhaa katoka Congo mzigoni,ilikuwa usiku jamaa anakatiza mitaani kavaa kiraia akamstopisha jamaa akaheshimu akasimama anamuhoji maswali jamaa anamjibu tu fresh shida jamaa kutaka kumtia presha kumtisha alitembezewa walivyokuja wenzake mmoja anamjua jamaa ndo kuwasanua wenzake ila mwenzao alishapata joto la jiwe
 
Nature ya kazi ya polisi imewekewa misingi isiyo na urafiki kuna baadhi ya makosa ukifanya hata huyo rafiki yako polisi anakua hana uwezo wa kukusaidia hata akitaka kukusaidia wala hataweza, ndo pale unaona anakukwepa , kwahiyo usijenge urafiki na polisi ukiamini atakusaidia hilo halipo
kuna chakujifunza hapa
 
Polisi ni watu wema sana. Nilichogundua wale sawa na wajeda ambao hatuchangamani nao sana wanafanya kazi kwa maelekezo. Ndio maana leo anaweza kuwa rafiki yako kesho akakutwanga makofi. Hana namna ikiwa ni maelekezo kapewa. Hii inawaathili hadi kwenye mambo ya kawaida wanakuwa ni watu ambao sio wa kuwaamini sana kukuchenjia ni dakika sufuri.
 
Back
Top Bottom