Askari Polisi na DAS waamriwa kumlipa raia milioni 10 kwa kumuweka ndani bila kosa

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
92
1,684
ASKARI POLISI NA DAS WAAMRIWA KUMLIPA RAIA MILIONI 10 KWA KUMUWEKA NDANI BILA KOSA.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Mahakama kuu Kanda ya Manyara imeamuru askari polisi(OC-CID) na DAS wa wilaya ya Babati kumlipa bwana Lawrence Sulumbu Tara kiasi cha Shilingi Milioni 10 kwa kosa na kumuweka ndani(mahabusu) bila sababu za msingi .

Katika shauri hilo Na. 16/2023 bwana Tara aliitwa kituoni na OC-CID Richard Mwaisemba kisha kuwekwa ndani kwa madai ya maagizo kutoka juu.

Baadae alijulishwa kuwa kosa lake ni kuandika barua kwa Rais kumsema vibaya Mkuu wa Mkoa na kuleta uchochezi.

Pia aliarifiwa kuwa maagizo yametoka kwa DAS ndugu Halfan.A.Matipula.

Baada ya kuachiwa kwa dhamana aliwafungulia mashtaka wote wawili DAS na OC CID.

Mahakama kuu tarehe 9/5/2024 iliamuru wamlipe milioni 10 kwa kumuweka ndani(mahabusu) bila sababu za msingi ambapo kila mmoja alipe milioni 5.

Watu wanapaswa kujua kuwa hakuna aliye juu sheria. Yeyote DAS, RAS, DC, RC, WAZIRI, IGP, CDF wanaweza kushitakiwa.

Makosa ya kuweka watu ndani bila sababu(False imprisonment), na kubambikiwa makosa(Malicious Prosecution) yapo kisheria kabisa ni nyie tu hampendi kuyatumia.

Niliwahi kuwaambia kipindi kile ma RC na MaDC wanaweka watu ndani hovyo kuwa muwashitaki.

Washitaki halafu dai fidia kutokana na namna ulivyoumizwa kimwili, kiakili na kiuchumi. Sheria inaruhusu mambo haya ni basi tu watumiaji wa sheria hawako tayari kuchukua hatua.

Askari anakubambikia kesi, anakuweka ndani bila kosa na bila dhamana na ukitoka huko unamshukuru Mungu unaenda kulala, raia gani nyie.

Hivi vitendo haviwezi kuisha kama hamchukui hatua. Lau kama kila mmoja anayetendewa haya akachukua hatua hawa watu wataacha tu kuonea. Nao ni waoga akiambiwa akulipe milioni 10 ataipata wapi ya haraka.

Hakuna shaka matendo ya kuonea yatapungua kabisa. Shida ya Watanzania mnataka kusaidiwa kila kitu hata yale ambayo umesharuhusiwa na sheria kuyafanya.

Lazima wewe ndo uwe wa kwanza kulinda haki zako, na kama kuna wa kukusaidia atakuja mbeleni.

Hawa DAS na OC CID walipobanwa wakasema walikuwa wakifanya kazi ya serikali na walikuwa wakitekeleza majukumu ya umma(vicarious liability).

Jaji KAHYOZA akakataa, akasema unapovunja sheria unakuwa umejitoa katika kutekeleza majukumu ya serikali na hapo unakuwa unatekeleza mambo yako binafsi kwasababu serikali haimtumi kiongozi yeyote kuvunja sheria.

Mambo kama kukamatwa bila kufuata utaratibu, kupigwa na askari au kiongozi, kupekuliwa bila kufuata utaratibu, kuhojiwa bila kufuata utaratibu, kuwekwa ndani(mahabusu) bila kosa, kukataliwa dhamana wakati kosa linadhaminika,kubambikiwa kesi, kutishiwa,kutukanwa, kunyanyaswa vituoni nk, nk ni makosa kama mlikuwa hamjui.

Ni makosa ya madhara yanaitwa "TORT" ambayo unatakiwa umshitaki muhusika aliyekutendea ili akulipe fidia.

Makosa kama FALSE IMPRISONMENT/kuwekwa mahabusu bila sababu za msingi, na MALICIOUS PROSECUTION/kubambikiwa kesi au kosa yapo rasmi kwa ajili ya watu kama maaskari na viongozi. Yapo ila wa kuyatumia ndo haonekani. Mpaka yanaozea kwenye vitabu.

Hakuna ruhusa ya DC, RC, WAZIRI, Polisi au kiongozi yoyote kumuweka mtu ndani bila kosa au kwa kosa la kutengeneza. Haipo, na haipo.

Baada ya matukio hayo unachotakiwa kufanya ni kwenda moja kwa moja Mahakamani na kumfungulia mhusika shauri.

Tena mahakama za mwanzo ikiwa unadai fidia ndogo hazihitaji hata Wakili, ni wewe unatoa maelezo yako yanaandikwa, mdaiwa anaitwa kisha shauri linaanza.

Msiwe wanyonge sana wanangu sheria zipo. Aliyetunga sheria za kukamata ndo huyohuyo aliyetunga sheria za kuzuia kuonewa

Shida Mnakuwa sana Wanyonge. Manenomaneno mengi kwenye mitandao yakija mambo ya msingi mnafeli.

Haya bana.
 
safi sana Lawrence Tara yule ni mtu na nusu ni kati ya wairaqw wanaojitambua pale babati, ni mpinzani wa kweli na ni mtu wa haki hataki longolongo
 
Kuna bwege mmoja yupo hukohuko mikoa ya kaskazini ningefurahi siku ajichanganye kwa mtu muelewa kama huyo halafu jaji naye ajifanye hamnazo atoe order ya kumpeleka Kisongo japo kwa siku 2 tu watu wakajilie ule mgongo wa tembo.
 
Umenikumbushaa mbali nilikuwa tarime nkikazi enzihizo za magu na binti mmoja wa kigandaa hahaha dc mmoja wa tarime akamaindi flag binti akaniambia dc amekuja hotelin naomba twende wote tukaenda haha kufika jamaa ananiambia nimemuita huyu sijakuita wewe nkakaa pemben binti akasemaa pls need him here siwezi ongea chochote

Akaoondoka jamaaaaa

Asb tukadamkia kazin safii nikafatwa na mkaka mmoja oyaa unamuaribia boss kapanga kukuweka ndan uwe make nkamwambia aje tu

Nkampigia wajomba wangu watatu 2 walikuwa dc nkamweka sawa manzi oya ikitokea kitu wajulishee

Mdadaa no
1.walikuwa wanaleta gari kutuchukua akawapiga stop
2.kufika ofisin sa a nne kuna chai akapiga stop
3.akaomba twende ofisin kwake tukaenda kufika nikamrekodi akamaliza yake tukaondoka
4.nikasambaza kwenye nyeti zangu kama siku ya ijumaaaa baada ya wiki mbili jamaaa akaondolewa na magu

Jamaa alikuwa anakaa bar akilewa anajiita raisi wa tarime kaweka bastola mezan anasema yoyote anaemtaka hamkosi watu wakachukua recoding

Kifupi alikuwa n
Dc

Wanatumia madaraka vibayaa sanaa askofu shaooo analia kila siku vijana nnaopewa madaraka muyatumie kwa hekima msifikiri ndio sehemu ya kuwaadhibu watu
 
ASKARI POLISI NA DAS WAAMRIWA KUMLIPA RAIA MILIONI 10 KWA KUMUWEKA NDANI BILA KOSA.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Mahakama kuu Kanda ya Manyara imeamuru askari polisi(OC-CID) na DAS wa wilaya ya Babati kumlipa bwana Lawrence Sulumbu Tara kiasi cha Shilingi Milioni 10 kwa kosa na kumuweka ndani(mahabusu) bila sababu za msingi .

Katika shauri hilo Na. 16/2023 bwana Tara aliitwa kituoni na OC-CID Richard Mwaisemba kisha kuwekwa ndani kwa madai ya maagizo kutoka juu.

Baadae alijulishwa kuwa kosa lake ni kuandika barua kwa Rais kumsema vibaya Mkuu wa Mkoa na kuleta uchochezi.

Pia aliarifiwa kuwa maagizo yametoka kwa DAS ndugu Halfan.A.Matipula.

Baada ya kuachiwa kwa dhamana aliwafungulia mashtaka wote wawili DAS na OC CID.

Mahakama kuu tarehe 9/5/2024 iliamuru wamlipe milioni 10 kwa kumuweka ndani(mahabusu) bila sababu za msingi ambapo kila mmoja alipe milioni 5.

Watu wanapaswa kujua kuwa hakuna aliye juu sheria. Yeyote DAS, RAS, DC, RC, WAZIRI, IGP, CDF wanaweza kushitakiwa.

Makosa ya kuweka watu ndani bila sababu(False imprisonment), na kubambikiwa makosa(Malicious Prosecution) yapo kisheria kabisa ni nyie tu hampendi kuyatumia.

Niliwahi kuwaambia kipindi kile ma RC na MaDC wanaweka watu ndani hovyo kuwa muwashitaki.

Washitaki halafu dai fidia kutokana na namna ulivyoumizwa kimwili, kiakili na kiuchumi. Sheria inaruhusu mambo haya ni basi tu watumiaji wa sheria hawako tayari kuchukua hatua.

Askari anakubambikia kesi, anakuweka ndani bila kosa na bila dhamana na ukitoka huko unamshukuru Mungu unaenda kulala, raia gani nyie.

Hivi vitendo haviwezi kuisha kama hamchukui hatua. Lau kama kila mmoja anayetendewa haya akachukua hatua hawa watu wataacha tu kuonea. Nao ni waoga akiambiwa akulipe milioni 10 ataipata wapi ya haraka.

Hakuna shaka matendo ya kuonea yatapungua kabisa. Shida ya Watanzania mnataka kusaidiwa kila kitu hata yale ambayo umesharuhusiwa na sheria kuyafanya.

Lazima wewe ndo uwe wa kwanza kulinda haki zako, na kama kuna wa kukusaidia atakuja mbeleni.

Hawa DAS na OC CID walipobanwa wakasema walikuwa wakifanya kazi ya serikali na walikuwa wakitekeleza majukumu ya umma(vicarious liability).

Jaji KAHYOZA akakataa, akasema unapovunja sheria unakuwa umejitoa katika kutekeleza majukumu ya serikali na hapo unakuwa unatekeleza mambo yako binafsi kwasababu serikali haimtumi kiongozi yeyote kuvunja sheria.

Mambo kama kukamatwa bila kufuata utaratibu, kupigwa na askari au kiongozi, kupekuliwa bila kufuata utaratibu, kuhojiwa bila kufuata utaratibu, kuwekwa ndani(mahabusu) bila kosa, kukataliwa dhamana wakati kosa linadhaminika,kubambikiwa kesi, kutishiwa,kutukanwa, kunyanyaswa vituoni nk, nk ni makosa kama mlikuwa hamjui.

Ni makosa ya madhara yanaitwa "TORT" ambayo unatakiwa umshitaki muhusika aliyekutendea ili akulipe fidia.

Makosa kama FALSE IMPRISONMENT/kuwekwa mahabusu bila sababu za msingi, na MALICIOUS PROSECUTION/kubambikiwa kesi au kosa yapo rasmi kwa ajili ya watu kama maaskari na viongozi. Yapo ila wa kuyatumia ndo haonekani. Mpaka yanaozea kwenye vitabu.

Hakuna ruhusa ya DC, RC, WAZIRI, Polisi au kiongozi yoyote kumuweka mtu ndani bila kosa au kwa kosa la kutengeneza. Haipo, na haipo.

Baada ya matukio hayo unachotakiwa kufanya ni kwenda moja kwa moja Mahakamani na kumfungulia mhusika shauri.

Tena mahakama za mwanzo ikiwa unadai fidia ndogo hazihitaji hata Wakili, ni wewe unatoa maelezo yako yanaandikwa, mdaiwa anaitwa kisha shauri linaanza.

Msiwe wanyonge sana wanangu sheria zipo. Aliyetunga sheria za kukamata ndo huyohuyo aliyetunga sheria za kuzuia kuonewa

Shida Mnakuwa sana Wanyonge. Manenomaneno mengi kwenye mitandao yakija mambo ya msingi mnafeli.

Haya bana.
Tumekuelewa chief...
 
Huyo polisi ni lazima aombe mkopo

Dawa yao hawa kutumia vifungu vyote viwili ,kulipa na kufungwa zaidi ya miezi 6 akitoka kazi imeisha
 
Mkuu ikiwa nimekubwa na maswaibu hayo uliyoeleza kwa makini hapo juu je naweza kuwasiliana na wewe unipe huduma ya uwakili bure au malipo baada ya?
 
Mbona fidia ndogo sana
 
Back
Top Bottom