Ulimwengu wa roho upoje?

Man Jau

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
461
682
Nimeanzisha uzi huu ili tujaribu kufikiri kwa undani, na kukusanya kila taarifa, clues na chochote tunachokijua kuhusu ulimwengu huu usioonekana.

Chochote unachokijua unakaribishwa kuchangia ili kukuza uelewa wetu na maarifa..

Wote tunafahamu kuwa Mwili na vingine vyote vinavyoonekana ni vimo katika ulimwengu huu, wa galaxies, solar systems, stars and clusters, etc.

Lakini upo ulimwengu mwingine ambao umeshikamana na huu wa kwetu, ila hauonekani kwa macho yetu haya ya 3D+ TIME.

Nimeona posts kadhaa za watu mbalimbali wakijadili namna ya kutembea, kusafiri na kuishi maisha ya kiroho, iwe kiimani au kiuhalisia, zikigusia ulimwengu huu, lakini kuna misconceptions nyingi kwa sababu hatujui mengi kuhusiana na ulimwengu huu.

Kwa uelewa wangu mfupi, ninatambua kuwa Hapa duniani kuna milango (gateways) za kwenda popote pale ulimwenguni, mf. Galactical travellers, sayari na nyota zilizo mbali mno kufikika.. ila tech yetu ni bado haijafikia level ya kuweza ku access na kuzigundua hizo njia (ni kama wormholes)..ila ni suala la muda tuu, soo soon tutazigundua..maana kuna wengine wanaendelea kutafiti huko chile wameona michoro na alama zinazodhaniwa kutumiwa na watu waliopita..anyway, nisipotelee huko, ila umepata idea.

Ila pia, kwa upande wa kiroho, zipo pia gateways za kwenda kuzimu, mbinguni, na mahala pengine pa ulimwengu huo wa roho ambapo nafsi ndio zinatamba na identities zake. Ushahidi wa hayaa tunauona kwenye jamii zetu, na maajabu ya hapa na pale, waumini wa dini, wachawi, uwepo wa majini, na kadhalika, na kadhalika

Mkumbuke kuwa roho haisafiri, bali ni powering machine ya nafsi yako ambayo creator wako kakupa. (kakuumba) na nadhani nilisoma mahala pia kuwa roho ndio inamsaidia mwanadamu kuwasiliana na Mungu kwa urahisi, nadhani ni Biblia na Msaafu, na hata kwenye mavitabu ya logic na meditations pia wanagusia kuwa roho ina nguvu ya kuweza kuisafirisha nafsi yako kwenda mbali zaidi kwa muda mfupi mno, like in a thought.

Ndio maana watu wa imani wakikuambia mbinguni ni juu, usimcheke wala akikuambia hell (motoni) ni chini, usimshangae pia.

Hio milango ipo.

Hata zile stories za Nuhu kutokea gharika ya mvua kwa siku arobaini (zaidi ya miezi au miaka kadhaa ya dunia ya sasa) na kufunguliwa kwa vilindi vya maji juu angani na duniani..sio ajabu. Hivo vitu vipo.

Au zile stori unazozisikia za yesu kupaa, Elia kupaa na jeshi la Kiroho pia, moto wa Sodoma na Gomora, bustani ya Edeni na kadhalika...na kadhalika.

Point yangu ni kuwa, kubishia vitu vya ulimwengu wa roho kwa mifano ya ulimwengu wa mwili, huenda ukakosa kuuelewa kabisa ulimwengu mwingine kama Upo...maana ulimwengu wa roho ni wa higher dimensions ambazo mwanadamu wa sasa anaendelea kuhangaika kuzifungua.

Huu ulimwengu wa roho ni wa sayansi ya juu zaidi na ya milele, sayansi ambayo haina makosa, sayansi ya juu zaidi ya hii yetu tuliyoumbwa ambayo Mungu aliifanya.

Hii miili yetu tunaamini kuwa Mungu hakosei, lakini Mungu mwenyewe anathibitisha kuwa hii ni sayansi yake ambayo ni ya mpito, ya muda tuu, ambayo mwanadamu anapitia, ili kuifikia hio ya milele, ya rohoni.

So, kwa ufupi mwanadamu anaishi sayansi ya mwili na ulimwengu wake pamoja na wa kiroho, ila akifa ataacha ulimwengu wa mwili na kubakia na wa kiroho peke yake,

So, ni muhimu kusali na kuwa fiti kiroho ili muda wa kuuacha mwili ukifika, uwe salama kiroho, na usije ukapotea na kuangukia kwenye mikono isiyo salama.

Wapi utapata msaada wa kiroho, hio ni shauri lako mwenyewe...siez kulazimisha kupanda basi kwenda mwanza wakati unaeza kupanda ndege, au kama unataka kutembea kwa miguu
 
I can close my eyes and see what happen in Dodoma but I am in Arusha.
True, lakini you can open your eyes and watch a live tv and see what happens in Dodoma na nipo Dar.

Hii sasa inaitwa teknolojia, ya ulimwengu wa mwili.

Ila kama hautumii tech hii, na ukairuhusu roho yako iboost mwili wako na kuona yanayoendelea dodoma in a higher sense..hapo ndio utakuwa mnoma sana, na kutumia nguvu za roho zaidi huku umefumba macho
 
Kuanza kuhoji ulimwengu wa roho upoje, ina maanisha kwamba huo ulimwengu haupo bali ni dhana na mawazo ya kufikirika.

Ulimwengu wa roho ungekuwepo kusingekuwa na utata wa ku ufahamu upoje, kwa vile upo.

Lakini haupo, ndio maana mnajaribu kuunda dhana na mawazo ya kufikirika (illusion) ya uwepo wa ulimwengu wa roho usio kuwepo na haupo.
 
Kuna vitu vipo lakini hauvioni.

Kuna mambo yapo lakini hauyaoni

Kuna viumbe vipo lakini hauvioni.

Hapa kwanza tupo pamoja??

Kama jibu ni ndio, kwanini ukatae uwepo wa ulimwengu wa roho??

Na kama unakataa, basi we ni bonge moja la boya, au ni kweli hauna uelewa wa chochote kile zaidi yako..
 
Ukisha sema vitu vipo si lazima vionekane kwa vile vipo, Hata Upepo hauonekani lakini Upo kwa kusikika upo.

Huo ulimwengu wa roho Haupo ndio maana bado mna hoji upoje, Ungekuwepo kusingekuwa na utata kuhusu uwepo wake.

Ulimwengu wa roho ni dhana na mawazo ya kufikirika (imaginations).
 
True, lakini you can open your eyes and watch a live tv and see what happens in Dodoma na nipo Dar.

Hii sasa inaitwa teknolojia, ya ulimwengu wa mwili.

Ila kama hautumii tech hii, na ukairuhusu roho yako iboost mwili wako na kuona yanayoendelea dodoma in a higher sense..hapo ndio utakuwa mnoma sana, na kutumia nguvu za roho zaidi huku umefumba macho
Hata hivyo si lazima kufumba macho, roho ikiwa active vya kutosha unaingia ulimwengu wa roho ukiwa timamu na macho ya kimwili yapo wazi.
 
Ukisha sema vitu vipo si lazima vionekane kwa vile vipo, Hata Upepo hauonekani lakini Upo kwa kusikika upo.

Huo ulimwengu wa roho Haupo ndio maana bado mna hoji upoje, Ungekuwepo kusingekuwa na utata kuhusu uwepo wake.

Ulimwengu wa roho ni dhana na mawazo ya kufikirika (imaginations).
Siyo kila mtu amebahatika kujua siri za mambo haya. Lakini nakuambia kwa hakika ulimwengu wa roho upo tena ni halisi na ndiyo uliozalisha hata haya ya mwlini. Maadam wewe ni mwanadamu, naamini ipo siku utakuja kupata hakika ya mambo haya.
 
Leo nakuelewesha kilazima hata kama hautaki.

Ushawaza kwanini mtu anaota? Najua ushawahi kuota, ila unadhani kwanini unaota?

Haya twende..

Ushawahi kuota kitu alafu baada ya muda fulani kikawa kweli? Au kusikia mtu kaota kitu dulani baada ya muda kinatokea kweli?

Au ushawahi kusikia waganga au wapiga ramli wanaotabiri mambo mengine yanayotokea mbeleni na kisha yanakua?

Kwenye hili nakutolea mfano sheikh Yahaya Hussein (Mungu amrehemu popote alipo) aliwahi kutabiri kifo chake, na pia aliwahi kutabiri kuwa atakuja rais mkali na atakufa madarakani na kisha baadae atakuja rais mwanamke? Sikumbuki ilikua kipindi cha kikwete au mkapa lakini aliwahi kutabiri, wenye ushahidi watasema.

Sasa hayo yote na mengine mengi watu hawajitungii tuu na kujisemeaswmwa hovyo kwa sababu yanakuja tuu naturally, hapana...yanajiandika kila kitu kwenye ulimwengu wa roho, na hapo aligned na hayawezi kubadilika hata iweje.

Sina uhakika kuhusu nyota za watu zinakuaje, maana baskia hizi watu wanapendaga sana kuziiba na kuzitekenyua kwa manufaa yao binafsi.
 
J.F.Kennedy "Duniani Kuna Vita kuu mbili mbaya ambazo zote hazionekani ila zilishaanzaga
Akazitaja kuwa ni Psycho na spiritual
Anaesema haupo aongelee Mawazo yake yanafananaje ktk umbo
 
Siyo kila mtu amebahatika kujua siri za mambo haya. Lakini nakuambia kwa hakika ulimwengu wa roho upo tena ni halisi na ndiyo uliozalisha hata haya ya mwlini. Maadam wewe ni mwanadamu, naamini ipo siku utakuja kupata hakika ya mambo haya.
Ulimwengu wa roho kama upo,

Upo wapi?

Au Uchawi, Uliopo duniani ndio mmeupa jina Ulimwengu wa roho?
 
Huwa sivutiwi sana na mabishano kwenye elimu nyeti kama hii. Navutiwa zaidi na hali ya kuelimishana na kupata uelewa zaidi, siyo vizuri kuwekeza nguvu kubwa mahali pasipokuwa na tija
Elimu nyeti na unashindwa kujibu huo ulimwengu ulipo?

Naku uliza hivi huo ulimwengu upo wapi?

Au tuna elimishana imaginations na dhana za kufikirika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom