Sawa mkuu nimeelewa vema kabisa,
Kuna tukio moja huwa linaniacha njia panda. Nilikuwa sina mahusiano mazuri na mzazi wangu baada ya kututesa na kuikimbia familia, niliahidi sitamsamehe. baada ya miaka kadhaa akiwa huko aliugua sana nikaitwa mara kadhaa sikufika kwasababu na mimi sikuwa na amani wala upendo kwake, akiwa anaumwa sana siku moja nikaota ndoto ananiomba msamaha mimi kwa niaba ya familia nzima, anaomba kwa uchungu sana na kuonyesha kujutia mno.
Nilipanga sitamsamehe, ila kutokana na uombaji ule tena mzazi Nikamsamehe katika ndoto na nikaachia yote moyo ukawa mweupe hata nilipoamka na nikapanga safari kwenda siku hiyo baada ya kuamka,
Wakati najiandaa nitoke asubuhi hiyo nikaambiwa mzee alifariki.
Hapa ndio naona kama ridhaa yangu kumsamehe ndio nikawa nimemuua.
Hakika wanadamu tunashi katika roho hai na mwili