Hakuna mawasiliano ya kiroho kati ya wafu

Hakuna mawasiliano ya kiroho kati ya wafu

Tafuta vitabu soma kuhusu Reincarnation.
Ni kweli kabisa mtu akifa mchezo umeishia hapo hakuna kinachoendelea.

Lakini kiongozi kuna kitu nakifikiriaga sana ni kwamba Mtu akifa kwa wakati wake huyo Roho yake hupumzika ama huenda kwenye kiumbe kipya kinachozaliwa na kama mtu atakufa kabla ya wakati wake basi hiyo roho yake itataabika sana kutafuta makazi na pengine kuanza kusumbua familia ilikokuwa
Unaweza kunipa ufafanuzi kidogo wa hizi fikra zangu ama ni potofu tu
 
Imani au Ujuzi?
Mtu akiishakufa hawezi kutokea tena hata ndotoni. Hao ni mashetani wanakuingiza mkenge

2 KOR. 11:14 -15

14Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
 
Kwenye kitabu cha Gospel of Thomas unlevield kuna mahala kinasema katika kufundisha wanafunzi wake, Yesu alikuwa amekaa na wanafunzi wake, akapita Msamaria mmoja akienda safari huko Judea (Jordan) akiwa amebeba kondoo, maswali na majibu;

YESU: Kwa nini yule anasafiri akiwa amebeba kondoo?

WANAFUNZU: Ili huko safarini akisikia njaa amchinje ale.

YESU: Kwani hawezi kumla akiwa mzima

WANAFUNZI: Ndivyo

YESU: Kwa hiyo mpaka amchinje awe maiti ndio amle.

WANAFUNZI: Sasa atafanyaje vinginevyo, si lazima amchinje.

YESU: Utafuteni utukufu wa mungu mkiwa hai, msingoje mufe muwe maiti ya kuliwa kama kondoo, kwani hamtaupata wakati mkiwa mfu.

Sasa nikisikia hadithi za atakuja mawinguni eti maiti zitafufuka nachoka kabisa.
Kweli kabisa. Hili linamhusu hata Papa. Zile ngonjera za marehemu awekwe mahali pema peponi hazina kitu wakuu
 
Mshana naomba nisaidie kwenye mara nyingi nimeshamuota rafiki yangu wa karibu sana ambaye amefariki kipindi cha mwaka mmoja uliopita, nini madhara yake na nifanyeje? Kuna mtu alishawahi kuniambia kuwa hakuna mawasiliano kati ya mfu na mtu aliye hai...
 
Mawasiliano kati ya walio hai na wafu yapo lakini huwa katika hali isiyo timilifu kwakuwa kimoja ni mwili na roho na kingine ni mwili pekeyake
Mshana naomba nisaidie kwenye mara nyingi nimeshamuota rafiki yangu wa karibu sana ambaye amefariki kipindi cha mwaka mmoja uliopita, nini madhara yake na nifanyeje? Kuna mtu alishawahi kuniambia kuwa hakuna mawasiliano kati ya mfu na mtu aliye hai...
 
.
 

Attachments

  • FB_IMG_1683520489533.jpg
    FB_IMG_1683520489533.jpg
    71.5 KB · Views: 20
Mada ilikuwa inafanyiwa screening.... Siku hizi ukipost intelligence mada haiendi hewani moja kwa moja
Ishu za hisia, fikra na mawazo ni mambo ya kimwili katika dunia iliyobeba mwili uharibikao.. Mwili wenye kikomo cha kuwa... Baada ya hapo roho ikishaacha mwili huenda zake into the vast world... Ikiwa wakati huo ni energy huru... Ambayo imeshavuka zile boundaries za vikomo vya kidunia
Memory haifutiki, history yako yote hubaki na nafsi isiyopo tena... Lakini kukiwa na alama ulizoacha

Wanalalamikia uhuru wakati sensorship inafanyika.
 
Niliwahi kufika Kaole Bagamoyo kule kwenye makumbusho... Pale kuna kaburi moja maarufu sana... Wamezikwa watu wawili kwa pamoja mke na mume ambao walipendana sana kiasi kwamba walikufa pamoja...
Roho ndio nishati ya mwili, yaani ndio pumzi ya uzima kwenye mwili... Bila roho mwili ni mfu na haukawii kuharibika... Kati ya hivi vitu viwili, roho na mwili kuna kitu cha tatu ambacho ni nafsi ama utambulisho... Nafsi ni matokeo ya muunganiko wa roho na mwili... Nafsi ndio software ya uhai inayobeba muktadha na miamala yote kwenye mwili wenye roho kuanzia, kuweka kumbukumbu, kupanga jambo, kutoa maamuzi, hisia nk nk.... Nje ya nafsi kwenye utenganisho wa mwili na roho hakuna kinachoendelea
Kwenye vitabu vya kiimani, kwenye kipengele cha mahusiano na ndoa hasa kwa wakristo.. Kuna maneno yanasema... NITAKUPENDA HADI KIFO KITAKAPOTUTENGANISHA....
Mapenzi ni hisia... Hisia huzaliwa, hukua, huzeeka na hatimaye hukoma kuwa yaani hufa.. Yaani hisia zikifa wawili hutengana na kuachana... Lakini kama bado wako hai kuna wakati hukumbukana, ndio maana baadhi hurudiana...
Hii ni tofauti kabisa kwenye KIFO... Mwisho wa mawasiliano yenu kihisia ama kindugu ni kifo... Roho zinapofikia ukomo wake mwilini na kusema hakuna mawasiliano tena... Kila moja huchukua njia yake kwenye vast galaxy... Ulimwengu mpana usio na kikomo....
Hii inathibitishwa pia kwenye mambo ya kiimani kwamba hata huko mbinguni, peponi au jehanum hakuna featuring wala mawasiliano yoyote... Kila roho inasimama yenyewe
Codes zote za kifamilia, kirafiki, ndugu na mahusiano mengine yoyote yale hukatika na kukoma kuwa pale ufu unapotamalaki... Reincarnation pia inatoa ithibati zinazofanana na hizo... Simulizi zote za reincarnation sio kati ya roho na roho bali kati ya mwili wenye roho na roho na kinyume chake...
Simulizi za ndoto za kutokewa na marehemu ni kati ya mwili wenye roho na roho... Hakuna hata siku moja mtu alishawahi kutokewa ndotoni na wapendwa wote wawili kwa wakati mmoja mfano wazazi na wakakwambia kwa pamoja huko waliko kukoje ama kuna nini...
Mara nyingi kama si zote utatokewa na mmoja tuu tena katika vague image kwakuwa yeye si mtu kamili tena... Kiubinadamu tu na katika bali ya kuoneshana upendo mtaahidiana kupendana milele lakini kiuhalisia ni kudanganyana live kwakuwa mwisho wa mawasiliano yenu ni KIFO... Baada ya hapo hakuna kitu tena....
NOT TRUE, at least according to AI (see below).

Belief systems suggest that spirits communicate with each other in various ways, including through emotions, thoughts, and energy exchange. Some religious perspectives state that souls in heaven can communicate with each other more perfectly than humans can on Earth.

  • Emotional and energetic exchange:
    Spirits can share and exchange emotions, thoughts, feelings, and ideas with each other.

  • Spiritual unity:
    Within some religious beliefs, it is said that souls in the afterlife can communicate with each other and continue to fulfill their will in relation to others and creation.

  • Awareness of others:
    Some mediums and psychics suggest that spirits are aware of each other's presence, even if overt communication isn't always apparent.
 
Back
Top Bottom