Hakuna haja ya Nyerere Day

Hakuna haja ya Nyerere Day

“Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu” – Mwl. J.K Nyerere ,
 
Labda nikujibu kwa mfano ndo utaelewa kuna wachezaji zaidi ya 5000 lakini mchezaji bora huwa mmoja tu ambaye anasaidiwa na wachezaji zaidi ya mia mbili ili yeye awe bora kama hukunielewa kuwa muwazi
 
Nyerere naye alikuwa binadamu pamoja na mazuri yake kuna mapungufu ambayo alifanya lakini usiseme hakufanya kitu mkuu, fikiria mpya.
 
hana llte zaidi ya kutuachia nchi mbovu inayoitwa jamhuri ya muungano ni kiini macho tu!
 
Rais Nyerere hafai kukumbukwa kwa lolote

Ukisema kaleta Uhuru kasome makala za Mohammed said utaelewa kazi ya viongozi wa TAA juu ya Uhuru na kazi ya Nyerere.

Nani alimruhusu kusema nchi haina dini halafu akatupa wimbo wa taifa tumuombe Mungu. Nani alimruhusu kuwa tunataka ujamaa? Alifanya referendum wapi? Nani alimruhusu kutaifusha Mali za watu,viwanda,viwanja,mashule,vyuo,nk? Nani alimruhusu kukusanya watu kwenye vijiji na maroli huku wakiwa chini ulinzi kwa waliopinga.

Nani alimruhusu kuua demokrasia na kupiga marufuku vyama vingi?
Serikali yake ikajaa umangimeza, hakuna wakuihoji, zikadumu fikra za mwenyekiti kwa mdamrefu, nan alimruhusu?

Akatumia rasilimali na fedha za chi kukomboa bara zima la Afrika bila kuweka mkataba kuwa fedha zile sio zake Bali za wananchi kwa hiyo wakipita Uhuru wao wazirudishe matokeo yake hata South Africa tuliowasaidia wenyeji hawataki wahamiaji na wanawaua, je rasilimali zetu zilizowanufaisha sisi tumenufaika na nini?

Nina mengi sana lakini ngoja niachie hapa, sasa najiuliza Nyerere tunamkumbuka kwa lipi hata tuweke eti Nyerere day?

Tafakari
Mkuu hoja hizi ni nzito sana....wasubiri wenyewe waje.
 
iekwe siku ya kuwakumbuka wapigania uhuru.....wapigania uhuru wapo wa muhimu zaidi kuliko nyerere...
tena nyerer yeye katafuta uhuru bila kumwaga damu,....wakina kinyekitile ngwale,mkwawa walikufa kwa ajili ya nchi hii,.leo unamuenzi nyerere it seems wale wengine hawana umuhimu kwa taifa hili kuliko julius nyerere
Labda kwa sababu ni mkristo....

CC FaizaFoxy
 
Kwako wewe huyo Mohammed Saidi ni nani hasa mpaka uamini alichoandika,

Nenda Maktaba kasome history ya Tanzania utaelewa umuhimu wa Nyerere, Kambona, Bibi Titi Mohammed na wengineo.

Tatizo unaongozwa na mihemko.
Kwani mtu usipokuwa na dini huwezi kumuomba Mungu wewe binafsi!!

Wimbo wa taifa ni sala ya pamoja kwa wenye dini,wapagani, Wakristo kwa waislamu.


Punguza Mihemko ndugu, Tanzania ni yetu site.
 
Mleta uzi unaujua msemo usemao nabii hakubaliki kwao?. Mwalimu alifanya mengi ambayo yanaifanya Tanzania ibakie kama ilivyo hivi sasa. Maono yake yaliondoa kabisa ukabila na ukanda. Kama tusingekuwa na mawazo na mitazamo yake, leo hii ni makabila machache sana ambayo yangekuwa yamestawi kiuchumi na mengi mengine yangekuwa ni makabila yenye kuwatumikia hao wachache.
Kiuchumi hakufanikiwa lakini ni marais wachache sana walioasisi nchi za Afrika ambao wanaweza kujisifu kwamba walifanikiwa kiuchumi.
Ni jukumu la hawa viongozi wa sasa kutumia rasilimali watu yenye elimu, kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi nzima na ule wa mwananchi mmoja mmoja.
 
Yaani wewe ukiisha msoma huyo Mohammed wako baaaaasi. ...Dunia yako inaishia kwa huyo bwana, na kwingineko hawajuhi lolote kuhusu Mwl. Nyerere?
Hawa ni wale vijana wa mwendokasi, akili za kufikiria mambo kwa undani, wamezipata katika miaka ya karibuni.
 
Well, nijuavyo jina sahihi ni Nyerere Death Day.

Sioni sababu ya kutosherehekea siku ya kifo cha Nyerere kama kilivyowekwa rasmi kitaifa.
 
Back
Top Bottom