FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,776
Mleta uzi unaujua msemo usemao nabii hakubaliki kwao?. Mwalimu alifanya mengi ambayo yanaifanya Tanzania ibakie kama ilivyo hivi sasa. Maono yake yaliondoa kabisa ukabila na ukanda. Kama tusingekuwa na mawazo na mitazamo yake, leo hii ni makabila machache sana ambayo yangekuwa yamestawi kiuchumi na mengi mengine yangekuwa ni makabila yenye kuwatumikia hao wachache.
Kiuchumi hakufanikiwa lakini ni marais wachache sana walioasisi nchi za Afrika ambao wanaweza kujisifu kwamba walifanikiwa kiuchumi.
Ni jukumu la hawa viongozi wa sasa kutumia rasilimali watu yenye elimu, kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi nzima na ule wa mwananchi mmoja mmoja.
Si kweli.
Nyerere hakukuta ukabila na ukanda, hata yeye alikuwa wakuja Dar na akapokelewa na kulazzwwa, kulishwa kuvishwa na akina Sykes. Hilo lipo wazzi kabisa.
Ingekuwa kuna ukabila na ukanda au udini kama unavyotaka kutuaminisha, jee Nyerere angekaribishwa na Waislam wa Dar? Fikiri.
Ukabila tulikuja kuuona baada ya azimio la Arusha, mpaka ukapewa jina "udugunaizeshen". Sijuwi kama ulikuwepo.
