Hakuna Fao la Kujitoa NSSF duniani kote - Ramadhan Dau | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna Fao la Kujitoa NSSF duniani kote - Ramadhan Dau

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Oct 24, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi wa NSSF Dr Ramadhan Dau amesema Fao la kujitoa limeondolewa ili kuendana na mfumo wa kimataifa kwani duniani kote hakuna Fao la kujitoa.

  Amesema hata Zanzibar na Kenya hakuna kitu kama hicho.

  Mkurugenzi huyo alitoa tamko hilo alipokuwa akihojiwa na Kamati ya bunge ya mashirika ya umma inayoongozwa na Zitto Kabwe.

  Source: ITV Habari

  UPDATES.
  -----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
  [h=2]Muswada wa mafao wawaliza wafanyakazi[/h]


  Muswada wa marekebisho ya sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa Kumi wa Bunge, umewaacha solemba wanachama wa mifuko mingine baada ya marekebisho hayo kurejesha fao hilo kwa mfuko mmoja pekee.

  Sheria ya mafao ilipitishwa katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu na kuwazuia wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuruhusiwa kuchukua mafao yao hadi wafikishe umri kati ya miaka 55 na 60.

  Baada ya wanachama wa mifuko hiyo na wadau wengine wakiwamo wabunge kuipinga sheria hiyo, serikali iliahidi kuwa itaifanyia marekebisho na kuwasilisha muswada kwa hati ya dharura.

  Tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, amekwishawasilisha muswada huo katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam, ikiwa na maana kuwa utajadiliwa kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

  Muswada huo unakusudia kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali.

  Kwa mujibu wa muswada huo, ambao NIPASHE imeuona, sehemu ya sita inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), sura ya 372 kwa kuongeza kifungu kipya cha 44 ili kutoa fursa kwa mfuko huo kutoa fao la kujitoa kwa mwanachama wake.

  Kwa maana nyingine ni kwamba wanachama wa mifuko mingine kama NSSF itaendelea kutumia sheria ambayo imelalamikiwa na wafanyakazi.

  HOJA YA JAFO YAZIKWA

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kisarawe (CCM), Seleman Jafo, ambaye wakati wa mkutano wa Bunge wa Bajeti, alitaka kuwasilisha muswada binafsi, alisema amepata barua kutoka kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, ikimtaarifu kwamba, serikali itawasilisha muswada wa marekebisho hayo, hivyo hana sababu ya kuandika muswada mpya.

  Jafo alisema kwa kuwa alikwishawasilisha hoja ya kutaka marekebisho kwenye sheria ya hifadhi ya jamii, Bunge lilimweleza kwamba ni fursa kwa serikali au Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii; hivyo serikali imeazimia kuiwasilisha kwenye mkutano ujao.

  “Lakini kwa hali hii ni kwamba serikali haitatatua matatizo ya msingi ya hoja yangu, muswada unatakiwa uguse mifuko yote kwa sababu malalamiko ni ya wafanyakazi wote,” alisema.

  SUGU AIONYA SERIKALI

  Kwa upande wake, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, aliionya serikali kutochezea wafanyakazi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhamasisha fujo.

  Alisema ni vyema marekebisho yatakayowasilishwa bungeni yakarejesha fao la kujitoa kwa mifuko yote kwa kuwa wafanyakazi wengi hawana usalama kazini.

  “Tunajua faida ya pensheni uzeeni kwa sababu ni msaada mtu anapostaafu, lakini kwa mfumo wa nchi yetu ambayo wafanyakazi hawana usalama wa kazi haiwezi kufanyakazi ipasavyo,” alisema.

  Sugu alisema wafanyakazi kama wa migodini au hostelini wanafanyakazi katika mazingira magumu na wanaweza kuachishwa kazi wakati wowote hivyo fao la kujitoa litawasaidia.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, alisema fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii halimo katika sheria za kimataifa.

  Dk. Dau, alisema hayo alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) katika kikao kati ya kamati hiyo na bodi na menejimenti ya shirika hilo, katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema pia ni Tanzania Bara pekee ndiko ambako kuna fao la kujitoa katika mifuko hiyo, lakini katika nchi za Kenya, Uganda, duniani kote, hata Zanzibar, suala hilo halipo.

  Hata hivyo, alisema mwanachama wa NSSF anapoamua kujitoa, anaupunguzia Mfuko mzigo wa kumtunzia pensheni yake ya uzeeni, badala yake na kujiumiza mwenyewe.

  Shinikizo la kutaka serikali kuirekebisha sheria hiyo ili wanachama wa mifuko walipwa mafao wakati wanapoacha kazi, liliilazimisha serikali kukubali yaishe na kuahidi kuwasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2012.

  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, aliliambia Bunge la bajati kwamba kabla ya kuwasilishwa, muswada huo utapelekwa kwa wadau ili watoe maoni na pia Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) itatoa elimu kuhusu fao la kujitoa.

  Hata hivyo, alisema wapo baadhi ya watu waliotafsiri kuwa kusitishwa kwa fao la kujitoa kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imefilisika kwa kuwa imewekeza kwenye miradi mibaya, jambo alilosema sio la kweli.

  Kabaka alisema kuwa mifuko hiyo haina hali mbaya kifedha wala haijafilisika na kwamba kuzuia fao la kujitoa ni utekelezaji wa sheria.

  Waziri Kabaka alisema mchakato wa kuwasilisha muswada huo utaanza mara moja kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

  Kabla ya kauli ya Kabaka, Bunge lilipitisha Azimio lililowasilishwa na Jafo, la kuletwa bungeni muswada wa dharura wa marekebisho ya Sheria Na. 5 ya mwaka 2012 inayozungumzia marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ndani yake inaelezea kuzuiwa kwa fao la kujitoa kwa wafanyakazi.

  Kutokana na mapendekezo ya muswada huo kutowatuhusu wanachama wa mifumo kingine kuchukua mafao kabla ya miaka 55 au 60, wanachama hao huenda wakashinikiza kwa njia za maadamano na migomo.

  Aidha, upo uwezekano wa kuzuka mjadala mkali bungeni kwa kuwa na wabunge nao ni wanachama wa m
  ifuko hiyo.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimemsikiliza kwakweli nimepatwa na hasira sana, mbaya zaidi anaongea akijichekesha chekesha.
  Anadai utaratibu unatakakiwa ukifukuzwa kazi utafute kazi pengine uendelee kuchangia!
   
 3. Imany John

  Imany John Verified User

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Jamani hivi mtu katoka mgodini(mwanafunzi), alikuwa anakatwa nssf naye asubiri miaka 60?

  Mgodini wanafukuza na kuajiri kila siku,hao wachimbaji waliofukuzwa watapata lini mafao yao?

  Je makampuni ya madini yana uwezekano wa kuendesha mgodi kwa miaka tajwa na nssf?

  Kuna viongozi wanakuwa hawajui mazingira halisi ya wafanyakazi,na wakiendelea namsimamo wao ya RSA yatatokea TZ.
   
 4. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  aitishe mkutano na wafnyakazi wamgawane...huko duniani hakuna tabu kama hapa kila kitu kipo dawa,barabara mabus ...
  mfano mdogo tu wakushangaza kenya mirungi ni sawa na sigara lakini hapa kwetu du ....mirungi ni sawa na cocaine
   
 5. c

  ckjs Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi,
  Nimekereka sana na majibu ya mtu mmoja ktk ITV aliposema " duniani kote hakuna Nchi ambayo wanasheria ya kujitoa kabla ya umri wa kustaafu" habari hii imeniharibia siku.
  1) Kwa nini huyu bwana anatushurutisha sisi kufuata taratibu za nchi nyingine ambazo hatuna mkataba nazo. Kwani sisi tunaishi huko kwingine?
  2) Kwa nini sisi hatuna utaratibu wetu wenyewe kulingana na sheria yetu wenyewe kulingana na mazingira yetu na taifa letu ?
  3) Imesemwa wastani wa maisha ya mtanzania ni miaka 45 huyu anatulazimishaje kufikia umri anaotaka yeye, ndiyo atupe hela zetu. Ana uhakika gani kama ntafika umri huo??
  4) Ukweli unampa hela mtu ana miaka 60 wakati kachoka hawezi kuzitumia na wala mipango hata weza kufatilia kwa karibu jinsi ya kuendeleza maisha yake! Kwa nini usimpe hela yake akiwa na nguvu aweze kupanga maisha yake mwenyewe?
  5) Wenzetu ambao tunashurutishwa kufuata sheria zao wana taratibu zao za kumpa mtu msaasa anapokuwa hana kazi, leo mtanzania una acha kazi alafu unasota mtaani huna msaada wakati kuna mijitu imekalia hela zako! Inaudhi sana alafu mtu anatoa majibu rahisi tuu et hakuna nchi duniani inafanya hivyo !!

  Kwa nini tusianze sisi waige kwetu.
  Kwa nini sisi tunaiga yale machungu tuu lakini hatuigi yenye neema??? Why???
  Kwa nini tuige why tusitunge sheria yetu??

  Imeniharibia siku
  Naenda glocery ya jirani hapo!!
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni aibu kubwa kuwa na mkurugenzi wa aina hii asiye hata na aibu anapotamka upuuzi
   
 7. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Huyu jamaaaa ana mapungufu mengi sana, ni afdhali nikafe kwenye kudai haki yangu hata kama jeshi litakuja nina dai haki ya msingi ya mamamayaake
   
 8. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Nimemsikia mkuu, anaongea utafikiri hana akili vizuri. Mbona hajasema kuwa hizo nchi zingine pia zina utaratibu wa kutoa pensheni kwa wazee wote wanaozidi miaka 60 hata kama kabla walikuwa ni wakulima au wafanyabiashara? Maana na wao wamechangia maendeleo ya taifa kwenye shughuli zao. Huyo jamaa kanikera sana.
   
 9. m

  mwabakuki JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mwambie atoke nje ya box. huo ni utetezi wa kipuuzi kutolewa na msomi kama Dr.Dau. tatizo la wasomi wetu ni kufikiri kwamba ni lazima jambo lianzie ulaya afu wao waige. huu ni upuuzi mpevu kabisa. huyu ni mmoja kati ya wakurugenzi wanakusanya pesa ambazo hAwaumizi vichwa kuzipata.they are ready made na ndo maana he cant thnk nje ya box
   
 10. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ila sio utashi wake bali anatekeleza matakwa ya mkuu baada ya kupiga
   
 11. Imany John

  Imany John Verified User

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Wewe sio wa ALPF?
   
 12. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UKIWA NA UWEZO WA KUTUMIA AKILI ZAKO HUWEZI UKATOLEA MFANO KWA KILA NCHI. HEBU JARIBUNI KUFANYA VITU AMBVYO NCHI ZA WENGINE ZITATUTOLEA MFANO. MAFAO NI YANGU KWA NINI ANAJITOKEZA MTU KUNIPANGIA WKT WA KUCHUKUA MAFAO? kati ya mambo binafsi ambayo nayachukia pamoja na ukoo wangu wote basi hili na fao la kujitoa .HAPA NAILAANI CCM MPAKA KABURINI
   
 13. Imany John

  Imany John Verified User

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Hata zanzibar wanasheria zao,yani anakuja na utetezi kuwa wazungu wanatozwa na sisi tukubali kizembe tu, dr. Dau anakwama,atakuwa nesi muda si mrefu,mana uchambuzi wake niwaki puzi sana.
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huyu kilaza Dau ni janga sana kwa taifa letu na pia ana udini sana. Natamani 2015 ifike haraka ili tumuondoe hapo haraka sana.
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Bila aibu anasema hata kama mtu umeachishwa kazi ukiwa na miaka 25 basi tafuta kazi nyingine vinginevyo subiri miaka 60
   
 16. Muk

  Muk JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 552
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hta mie kaniboa, afu kwani ni lazima tufanane?a
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huyu Ramadhan Dau anasababisha watu wazidi kuichukia CCM
   
 18. Fanto

  Fanto JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hata kama Duniani kote hakuna Fao la Kujitoa, tunashindwa nini kuwa na utaratibu ambao ni wa kwetu tu? Kwani kila kitu lazima tuige kutoka kwingine? Bw Dau hawezi kuwasemea wafanyakazi wa kawada. Aliyeko Peponi hawezi kuwasemea waliopo Jehanam.
   
 19. Imany John

  Imany John Verified User

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli waache wazingue,tukiwazingua tutaonekana wasumbufu.
   
 20. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Pamoja na udokita wake "amezoea kukopi na kupaste" na anawaza kuwa JAMBO ZURI HALIWEZI KUANZIA TZ wala mambo au taratibu zilizopo haziwezi kurekebishwa na Tanzania.
  Kweli "uchungu wa mwana aujua mzazi".
   
Loading...