Hakuna atakayeachia ngazi sakata la Escrow

Status
Not open for further replies.
Baada ya kusikiliza ripoti rasmi ya PAC iliyowasilishwa na Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe nnadiriki kusema kuwa hakuna cha maana kwenye ripoti yao cha kuwafanya mawaziri kuwachia ngazi.

Ni drama tu lakini hakuna kipengele chochote cha sheria ambacho hakijibiki au kilichooneshwa kuwa kimekiukwa.

Hukumu ya Mahakama ni ya halali na haina utata na Zitto wala CAG wala TAKUKURU hawajaonesha kuwa ilikuwa ni batili au ya kughushi.

Zitto kapiga porojo nyingi sana kuliko ukweli, na mwanasheria yoyote mahiri anazisambaratisha hoja zake zote ndani ya nusu saa.

Zitto ametetea sana BoT lakini alichoshindwa kuelewa ni kuwa Bot kama wakala ndiye alitakiwa aridhike na vielelezo vyote kabla hajalipa na kama havijakamilika hawezi kutoa fedha. Zitto anasema eti Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye alimuamuru Gavana hizo fedha zitolewe, toka lini Gavana wa benki anatoa fedha kwa amri ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Utata wa IPTL na Standard Chartered ni huko-huko kwao si IPTL iliyokopa, iliyokopa ni Mechmar na Mechmar haiwezi jitokeza kwani imeshafilisika kisheria, Standard Chartered karata yao ya mwisho ni hii na hapa wamepata mwanya.

Nnasikitika kusema na nnaliona linakuja la Serikali kuingia gharama kubwa ya kulipa zaidi ya mara mbili au tatu hizi fedha ikiwa watafata akili za akina Zitto.

Nnashauri, wajadili hili suala bungeni lakini shauri liwachwe kesi kumi zilizopo mahakamani zinazoihusu IPTL zikamilike.

Mapendekezo ya Zitto ya watu kuachia nyadhifa zao ni ya kishabiki na hayana mshiko, watu hawaachii tu nyadhifa zao kwa habari kama hizi ambazo hazina mshiko wa kisheria.

Isitoshe, fedha zilizolipwa escrow si kamili, hizo zilizobaki zilizuiliwa kwanini? Jibu tutalipata kesho na ndilo litakalosambaratisha hoja ya kodi ya Zitto.

Kuna mengi sana ya kuchambua lakini tusubiri kesho, tusiandikie mate na wino upo. Ni matumaini yangu kuwa wote waliotajwa watapewa fursa ya kujibu. Na hapo ndipo mtamjuwa Chenge ni kichwa.

Tusiwe na haraka tusubiri hiyo kesho kama tulivyosubiria taarifa kusomwa leo
 
Sijawahi kusema kuwa ripoti haisomwi, kama uliona mahala nimesema hilo, leta ushahidi.

Nilikuwa nasisitiza siku zote ripoti rasmi itoke na tuione, ingawa mpaka sasa sijaiona yote kamili na vielelezo, nimeisikia na kwa niliyoyasikia naona haina mshiko, ni ufataani tu.

Tulieni dawa iwaingie vizuri. Wamekwiba pesa na hilo ni kosa la jinai na lazima kuwajibika. Hizi zako spin tu kutaka umaarufu JF
 
Utasema yote na kuwashwa kwako kakojoe ulale wenzio hawalali huko kesho aibu ya kuondoka bila ving’ora

Wakati wangu wa kulala haujafika ukifika ntafata ushauri wako.

Hakuna anaeachia ngazi kesho. Sijui, mimi si mtabiri, lakini sioni sababu.
 
Mara hela zote ni za serikali, mara ni za serikali na IPTL, mara serikali ilikosa kodi ya Bilioni 20, which is which now? Tatizo la Escrow ni kuwa serikali imekosa kodi stahiki au hela za serikali zimeibiwa? Kama tatizo ni kodi si waishtaki IPTL kwa kukwepa kodi? Tukubaliane tatizo ni urais
Sasa kama hela ni za umma inakuaje tena waseme wamekosa kodi ya bilioni 20?.
wanatakiwa report iwe na msimamo mmoja,ni pesa za umma.
ni za iptl ama zilikuwemo na umma na za iptl na ni kiasi gani
 
FaizaFoxy ww unataarifa nyingine tofauti na iliyosomwa bungeni? Unafikiri kichwa kama Advocate Ngwilimi kinaweza kikatimuliwa kirahisi bila madhara? Subiria uone moto wa kweli Mkuu...
 
Watu waliachia ngazi ya Richmond kwa maslahi ya Taifa laaling'ang'anini si kwa kuwa walikuwa na hatia.

Kwa hiyo katika hili hakuna maslahi ya taifa..?? FF we shangaa kwa nini wenzio akina Lizaboni, Simiyu yetu et el..hawaonekani

Mwenzio Pinda aling'ang'an kuwa walizogawana hazikuwa hela za uma... sasa na wewe kwa uzi wako huu utakisuta kesho
 
Sasa kama hela ni za umma inakuaje tena waseme wamekosa kodi ya bilioni 20?.
wanatakiwa report iwe na msimamo mmoja,ni pesa za umma.
ni za iptl ama zilikuwemo na umma na za iptl na ni kiasi gani

Hapo sasa!
 
umechelewa mama tafuta njia nyingine ya kuwasaidia hao maja mba wa zi
 
Huyu faiza nahisi nae katumwa kupotosha watu humu! Hivi hata aibu huoni ndugu? Unachotetea ww ni nini hasa? Kwa hiyo unataka sisi tuamini ripoti yako au? Acha kujipendekeza, unafikiri utapewa ubunge wa viti maalumu nini? Manake mtoto umekomaa mwanzo mwisho? Kawadanganye mataahira wenzio sisi tushajitambua kitambo!
 
Baada ya kusikiliza ripoti rasmi ya PAC iliyowasilishwa na Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe nnadiriki kusema kuwa hakuna cha maana kwenye ripoti yao cha kuwafanya mawaziri kuwachia ngazi.

Ni drama tu lakini hakuna kipengele chochote cha sheria ambacho hakijibiki au kilichooneshwa kuwa kimekiukwa.

Hukumu ya Mahakama ni ya halali na haina utata na Zitto wala CAG wala TAKUKURU hawajaonesha kuwa ilikuwa ni batili au ya kughushi.

Zitto kapiga porojo nyingi sana kuliko ukweli, na mwanasheria yoyote mahiri anazisambaratisha hoja zake zote ndani ya nusu saa.

Zitto ametetea sana BoT lakini alichoshindwa kuelewa ni kuwa Bot kama wakala ndiye alitakiwa aridhike na vielelezo vyote kabla hajalipa na kama havijakamilika hawezi kutoa fedha. Zitto anasema eti Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye alimuamuru Gavana hizo fedha zitolewe, toka lini Gavana wa benki anatoa fedha kwa amri ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Utata wa IPTL na Standard Chartered ni huko-huko kwao si IPTL iliyokopa, iliyokopa ni Mechmar na Mechmar haiwezi jitokeza kwani imeshafilisika kisheria, Standard Chartered karata yao ya mwisho ni hii na hapa wamepata mwanya.

Nnasikitika kusema na nnaliona linakuja la Serikali kuingia gharama kubwa ya kulipa zaidi ya mara mbili au tatu hizi fedha ikiwa watafata akili za akina Zitto.
Nnashauri, wajadili hili suala bungeni lakini shauri liwachwe kesi kumi zilizopo mahakamani zinazoihusu IPTL zikamilike.

Mapendekezo ya Zitto ya watu kuachia nyadhifa zao ni ya kishabiki na hayana mshiko, watu hawaachii tu nyadhifa zao kwa habari kama hizi ambazo hazina mshiko wa kisheria.

Isitoshe, fedha zilizolipwa escrow si kamili, hizo zilizobaki zilizuiliwa kwanini? Jibu tutalipata kesho na ndilo litakalosambaratisha hoja ya kodi ya Zitto.

Kuna mengi sana ya kuchambua lakini tusubiri kesho, tusiandikie mate na wino upo. Ni matumaini yangu kuwa wote waliotajwa watapewa fursa ya kujibu. Na hapo ndipo mtamjuwa Chenge ni kichwa.
mbona siku hizi sioni ushirikiano wenu kabisa bi faizaFoy , Ritz , THE BIG SHOW na co wengine? kunani? wengine wanamsifia ustaadh Zitto kuliumbua kanisa katoliki, wengine wanamdhihaki, imekaaje hii?

cc Nguruvi3 Mchambuzi , TUJITEGEMEE , Elli
 
Last edited by a moderator:
Pesa watu walizopewa wamepewa na JL, JL ni mmiliki halali wa IPTL na kauza shares zake kihalali na ana haki ya kuzitumia fedha zake atakavyo.

Unataka kutuaminisha mtu anakupa 1.6B hivi hivi tu kwa sababu anakupenda sana?? Faiza ndugu yangu usichutame kiasi hicho unajitia aibu, wengi tunajua uelewa wako!!!
 
yule mhindi unaemtetea unajua hawa watu huwa wanakula 0717....
 
Baada ya kusikiliza ripoti rasmi ya PAC iliyowasilishwa na Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe nnadiriki kusema kuwa hakuna cha maana kwenye ripoti yao cha kuwafanya mawaziri kuwachia ngazi.
Faiza, nillikushauri toka juzi kuwa utulie hii sindano inawaingia pole pole. Mwambie tu dadaako asharose ajiandae kuvaa viatu vya pinda.....tezi dume limeshapona! Sioni namna serikali hii inaweza kupona katika sakata hili....nasema tena sioni! Tutaongeza muda wa bunge kwa wiki moja ili rais aweze kupata PM mpya na kupitishwa na bunge.

Nakubaliana na wewe kuhusu BOT....kwa kweli PAC haijawapa "stahili" yao. Kwa uchafu na matusi waliyofanya kina Ruge, (stanbic na mkombozi) kwa hakika BOT walipaswa kufanya zaidi ya walichofanya. Hizi pesa watu wanagawana tu utafikiri hii nchi haina sheria yoyote ya fedha na BOT wanaangalia tu?
 
Kwa hiyo katika hili hakuna maslahi ya taifa..?? FF we shangaa kwa nini wenzio akina Lizaboni, Simiyu yetu et el..hawaonekani

Mwenzio Pinda aling'ang'an kuwa walizogawana hazikuwa hela za uma... sasa na wewe kwa uzi wako huu utakisuta kesho

Sikiliza, hakuna mwenzangu humu. Wala kuwajuwa siwajui, CCM tuko wengi sana lakini tuna demokrasia, si lazima wote tuwe na mawazo aina moja, sisi si misukule.
 
Mimi nilidhani utaanza kuchambua hoja moja baada ya nyingine na kuonyesha kuwa kwa maelezo na vielelezo waliovyotoa watu wa PAC havimtii aliyehusika na wizi huo hatiani....!!!
 
Faiza, nillikushauri toka juzi kuwa utulie hii sindano inawaingia pole pole. Mwambie tu dadaako asharose ajiandae kuvaa viatu vya pinda.....tezi dume limeshapona! Sioni namna serikali hii inaweza kupona katika sakata hili....nasema tena sioni! Tutaongeza muda wa bunge kwa wiki moja ili rais aweze kupata PM mpya na kupitishwa na bunge.

Nakubaliana na wewe kuhusu BOT....kwa kweli PAC haijawapa "stahili" yao. Kwa uchafu na matusinwaliyofanya kina Ruge, (stanbic na mkombozi) kwa hakika BOT walipaswa kufanya zaidi ya walichofanya. Hizi pesa watu wanagawana tu utafikiri hii nchi haina sheria yo tote ya fedha na BOT wanaangalia tu?

Mpaka sasa sijakiona cha maana cha kuiangusha Serikali, nnachokiona ni fitna na watu wamepata pakutokea kisiasa lakini hoja zao kisheria hazina mshiko.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom