Hakuna atakaye take risk kwa niaba yako, elewa hivyo

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,872
9,261
Habari wakuu,

Swala la Ujasiriamali ni swala gumu sana na watu wengi hujichanga mashahara wake wa miaka hata 5 ili aanze project, Mtu hujinyima kula, kustarehe na mambo mengine ili tu akusanye mtaji wa kuanza biashara.

Wengine hukopa, wengine huuza Mali, na kadhalika.

Sasa kosa huanza pale unapoa anza biashara mfano ya:
- Hoteli
-Baa
- Ufugaji wa kuku
-Kilimo
-Duka na kadhalika

Kuanzia ile siku ya kwanza tu mtu anakaimisha madaraka kwa aither Shemeji, mke/mme, Dada ake, kaka ake, mjomba, shangazai na kadhalika.
Hapo ni project ya milioni hadi 40 au 50, baada ya hapo mwenye mali huendelea na kazi na kuanza kuongoza kwa simu,
- Vipi leo wateja wamekuja wengi?
-Vipi mauzo?
- Vipi kuku wametaga leo?
Kuku wamekula?
- Mboga umemwagilia leo?

Hapa wewe unajivua risk na kukabidhi watu wengine.

Elewa kwamba hakuna atakaye take risk kwa niaba yako, wewe mwenye idea simamia biashara yako, wewe ndo unajua unataka kufika wapi na biashara yako, Hata mke/mme hawezi jua,

Kuanza biashara siku ya kwanza na kukaisha ndo safari ya kushindwa inapo anzia.
 
kweli mkuu chasha, tatizo kubwa kwa wengi wetu. nakumbuka statement moja ya former prez Mkapa alisema tatizo sio mtaji wala kuanzisha biashara tatizo ni kuisimamia hiyo biashara tangu siku ya kwanza unapoanza. ndio maana kuna biashara nyingi zimeanzishwa na nyingi zimekufa ukifatilia moja ya sbb kufa ni kumtumia mtu since day one. siku zote inapendeza biashara kua under direct management ya owner sbb yeye ndo anajua uchungu wa kutafuta mtaji na risk atakayopata incase biashara ina kufa, hata ikitokea biashara imekufa utakua na clear pic ya nn exactly killed ur bizness na utakua kwny position nzr ya kupambana tena ili kuiuisha
 
yes ndo hivyo, Biashara siku za mwanzo inahitaji mwenye nayo kuweka base.
Wale wanao weka kusimamia hawajali ndo maana ukienda kama hakuna wateja unaweza wakuta haya wamelala, badala ya kuwaza wanapata vipi wateja utakuta wamelala au wanasikiliza miziki. Ila the owner umekaa asubuhi hadi jioni hujaona mtu lazima uumize kichwa kutafuta jinsi ya kufanya
 
Back
Top Bottom