Hakukuwa na sababu ya Dkt. Tulia kurudia rudia kusema anamwakilisha Spika Ndugai, msiba siyo kikao cha Serikali

Ile ni shughuli ya kiserikali kama shughuli nyingine yoyote. Lazima ualikwe, haupeleki tu pua yako kwenye shughuli inayohudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali. Acha ujinga.
Wewe ndo mjinga, onesha hata barua moja ya mwaliko wa kuhudhuria msiba. Watu huenda msibani na wakikuona wanakupa heshima unayostahili na usipokwenda huulizwi.
 
Binafsi niliamini Naibu Spika Dr Tulia analiwakilisha bunge zima pale msibani kwa Balozi Kijazi kumbe nilikosea alikuwa anamwakilisha Spika wa bunge ambaye yuko mbali.

Nijuavyo mazishi siyo kama vikao vya serikali au chama ambavyo kuna watu ni lazima wahudhurie kwa mujibu wa vyeo vyao.

Kwenda msibani ni jambo la hiyari kwa namna Mungu alivyokujalia.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani akiyasema umma ukajua kuna tatizo gani?
Mbona mnapenda kuficha maradhi?
 
Tatizo la kuleta siasa kila mahali ndio matokeo yake wanaibua maswali amvayo hata hayakutakiwa watu wajiulize au kuyauliza...

Kwani Spika yuko wapi? Angenyamaza nani angeshupalia kutaka lujua hilo? Ikiwa Mpango katuma sms kwamba yuko salama naamini wengine nao itatafutwa namna ya kujuzwa hali zao huko waliko.
Hapo tutashukuru tukisha watia machoni
 
Umesema sahihi kabisa,Tulia aliwakilisha Bunge na si Spika.
Kwani Ndugai yupo wapi hadi awakilishwe kwenye tukio hili zito?
Kwamaana Dodoma ni epicentre ya changamoto ya upumuaji.
Huo ndo umbumbu wa Awamu ya Tano ya kukweza watu badala ya Taasisi ndiyo maana tunashuhudia kwa mara kwanza toka Uhuru Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri nk anakwenda kufungua choo, Soko Stand ya Mabasi nk au anahudhuria, ndani ya nchi au nje, Mikutano, Warsha, Kongamano hata ya Kitaaluma nk, atajigamba kuwa anafanya hivyo kumuwakilisha Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli akiwa ametulia tuli Chato. Nchi yetu na watu wake ambayo ndo Mwanachama wa Taasisi za Kimataifa kama UN, AU WHO, IMF, SADC, nk haiwakilishwi ingawa mezani kuna kibao UNITED REPUBLIC OF TANZANIA kuonyesha mwakilishi wetu atakapokaa ikiwa na maana yeyote (hata Kibajaji) atakayekalia Kitu hicho ndo mwakilishi wa Jamhuri yetu. Ni ujinga Waziri wa Afya kumuwakilisha JPM Mikutano wa WHO, Geneva au aende mwenyewe.
 
Yeye kama yeye hakujiuwakilisha ?

Haya yote ni kwasababu ya kugeuza misiba sehemu za kuuza sura
 
Acha ujinga, una uhakika aliyetumiwa mwaliko ni Tulia na sio ofisi ya spika?

mwaliko ukitumwa kwa ofisi ya spika basi yeyote atakaye teuliwa kwenda anakwenda kwa niaba ya spika. Ni lazima aseme anamuwakilisha spika.

Kinyume na hapo itaonekana spika ameamua kupuuza mwaliko.
Mwaliko msibani 😵
 
Binafsi niliamini Naibu Spika Dr Tulia analiwakilisha bunge zima pale msibani kwa Balozi Kijazi kumbe nilikosea alikuwa anamwakilisha Spika wa bunge ambaye yuko mbali.

Nijuavyo mazishi siyo kama vikao vya serikali au chama ambavyo kuna watu ni lazima wahudhurie kwa mujibu wa vyeo vyao.

Kwenda msibani ni jambo la hiyari kwa namna Mungu alivyokujalia.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Huyu kwenye msiba wa Diwani mstaafu Mbeya wananchi walimtimua. Bado ana wenge na misiba.
 
Acha ujinga, una uhakika aliyetumiwa mwaliko ni Tulia na sio ofisi ya spika?

mwaliko ukitumwa kwa ofisi ya spika basi yeyote atakaye teuliwa kwenda anakwenda kwa niaba ya spika. Ni lazima aseme anamuwakilisha spika.

Kinyume na hapo itaonekana spika ameamua kupuuza mwaliko.
Umewahi kualikwa msibani??
 
itoshe tu kusema huna akili
 
Binafsi niliamini Naibu Spika Dr Tulia analiwakilisha bunge zima pale msibani kwa Balozi Kijazi kumbe nilikosea alikuwa anamwakilisha Spika wa bunge ambaye yuko mbali.

Nijuavyo mazishi siyo kama vikao vya serikali au chama ambavyo kuna watu ni lazima wahudhurie kwa mujibu wa vyeo vyao.

Kwenda msibani ni jambo la hiyari kwa namna Mungu alivyokujalia.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Msiba wa Kitaifa/Serikali una protokali. Kama katika ratiba ya msiba huo kulikuwa na nafasi ya Spika kutoa neno na bahati mbaya hakuwepo, atakayeongea ama kwa maagizo ya mhusika au yeye mwenyewe baada ya kuona pengo, anaongea kwa niaba ya muhusika (Spika) ni jambo la kawaida. Kuna kiongozi ameongea msiba mwingine karibuni kwa niaba ya Rais ambaye hakuwepo msibani. Hatuwezi kusema amekosea sababu nae pia ni kiongozi wa Serikali na ameiwakilisha serikali.
 
Rais ni taasisi na Bunge ni taasisi lakini Spika ni mtu tu!
 
Hakuna kitu kinaitwa kuwakilisha kwenye misiba. Dunia imebadilika sasa hivi,kila mtu anahidhuria kutokana na nafasi/utashi wake period. End of the story,nafunga huu uzi tudiscuss mambo mengine
 
Back
Top Bottom