Hakukuwa na sababu ya Dkt. Tulia kurudia rudia kusema anamwakilisha Spika Ndugai, msiba siyo kikao cha Serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
Binafsi niliamini Naibu Spika Dkt. Tulia analiwakilisha bunge zima pale msibani kwa Balozi Kijazi kumbe nilikosea alikuwa anamwakilisha Spika wa bunge ambaye yuko mbali.

Nijuavyo mazishi siyo kama vikao vya serikali au chama ambavyo kuna watu ni lazima wahudhurie kwa mujibu wa vyeo vyao.

Kwenda msibani ni jambo la hiyari kwa namna Mungu alivyokujalia.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Tatizo la kuleta siasa kila mahali ndio matokeo yake wanaibua maswali amvayo hata hayakutakiwa watu wajiulize au kuyauliza...

Kwani Spika yuko wapi? Angenyamaza nani angeshupalia kutaka lujua hilo? Ikiwa Mpango katuma sms kwamba yuko salama naamini wengine nao itatafutwa namna ya kujuzwa hali zao huko waliko.
 
Acha ujinga, una uhakika aliyetumiwa mwaliko ni Tulia na sio ofisi ya spika?

mwaliko ukitumwa kwa ofisi ya spika basi yeyote atakaye teuliwa kwenda anakwenda kwa niaba ya spika. Ni lazima aseme anamuwakilisha spika.

Kinyume na hapo itaonekana spika ameamua kupuuza mwaliko.
 
Mwaliko wa kuzika! Mkuu unajua unachoongea au hii mada umeivaa kizalendo mpaka hujui nini kinazungumzwa?
 
Acha ujinga, una uhakika aliyetumiwa mwaliko ni Tulia na sio ofisi ya spika?

mwaliko ukitumwa kwa ofisi ya spika basi yeyote atakaye teuliwa kwenda anakwenda kwa niaba ya spika. Ni lazima aseme anamuwakilisha spika.

Kinyume na hapo itaonekana spika ameamua kupuuza mwaliko.
Mwaliko wa kwenda msibani? Mataga mnatabu sana aisee.
 
Ile ni shughuli ya kiserikali kama shughuli nyingine yoyote. Lazima ualikwe, haupeleki tu pua yako kwenye shughuli inayohudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali. Acha ujinga.

Kwani ukilewa lazima uje huku jukwaani kubishana? Tumeenda misiba kibao ya viongozi na viongozi kibao walikuwepo na hakuna aliyetualika. Huenda una hoja, ila unakosa maneno sahihi ya kuyaweka mpaka unaonekana mlevi fulani.
 
Acha ujinga, una uhakika aliyetumiwa mwaliko ni Tulia na sio ofisi ya spika?

mwaliko ukitumwa kwa ofisi ya spika basi yeyote atakaye teuliwa kwenda anakwenda kwa niaba ya spika. Ni lazima aseme anamuwakilisha spika.

Kinyume na hapo itaonekana spika ameamua kupuuza mwaliko.
Misiba siku hizi ina mialiko? Mbona wewe ndo mjinga kuliko mleta mada?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom