Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Aliyewahi kuwa Makamu wa kwanza wa Rais katika Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson wamechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania

Mtu mwingine aliyechukua fomu ni Patrick Nkamaha. Mchakato huu umeanza baada ya CCM kutangaza kutaka muwakilishi kugombea nafasi iliyoachwa na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai

  • Patrick Nkamah
  • Stephen Masele
  • Tulia Ackson Mwansasu
  • Godwin Kunambi
  • Hamidu Ubaidi Chamani
  • Joseph Kasheku Musukuma
  • Mussa Azzan Zungu
  • Emmanuel Mwakasaka
  • Goodluck Ole Medeye
  • Sophia Simba
  • Profesa Handley Mafwenga
 
Masele anaweza bila shaka yoyote ila naye atakuwa pale kwa mgongo wa ndiyo ndiyo tu
 
Tulia hatakiwi kugombea, anatakiwa aendeshe mchakato wa kumpata spika.
Sasa anaachia kiti alichopewa kikatiba kugombea kingine bila kuwepo anayekaimu?
Huyu hafai kwa sababu ana tamaa ya madaraka.
Uspika ataupata tu baada ya miaka mitano.
Kama alikubali kushiriki matendo ya kishirikina kisa apate ubunge wa Mbeya mjini atashindwaje kugombea uspika?

Huyu kati ya watu wasiyo faa kupata uongozi basi ni huyu
 
Huyu Tulia baada ya Statement zake za leo tutegemee Bunge kutokuwa tu a Rubber Stamp bali hio Stamp itakwenda kabisa Ikulu ili wamalize huko huko hakuna haja hata ya ku-consult Bunge
Hakuna bunge tena hapo
 
Back
Top Bottom