Hakuanza leo kutoheshimu mihimili mingine

Mkuu! Huoni kwamba unajikanganya (unaji-contradict) hapo? Unawaponda wengine unaposema "wana-kremu mambo....." wakati na wewe unafanya hivyohivyo kwa ku-kremu hicho kitu unachoita "Kuhn's Theory of Scientific Revolution". Halafu unasema tujenge "mfumo wenye kuheshimu watu......." Mbona wewe unaonekana kutoheshimu maoni ya wengine hata kama hukubaliani nayo? Ina maana kwako "watu ni wale wanaofikiri kama wewe tu? Unaposema democracy imepitwa na wakati unamaana kunyume chake ambacho ni udikteta ndio mfumo unaopendekeza?. Nchi hii imekuwa kama maabara ya kujaribu theory za kila mtawala (kwa mfano vijiji vya ujamaa, ujamaa wenyewe na azimio la Arusha, Azimio la Zanzibar, MKUKUTA, MKURABITA, na hii ya leo) badala ya kufuata conventional wisdom, ikiwa ni pamoja na misingi ya Democracy and The Rule of Law! Nadhani kuna tofauti kati ya 'ethics and logic' on the one hand, na 'scientific theories'. Revolution/evolution of science is one thing, while logic, philosophy and ethics are each, another thing all together.
Finally; naheshimu mawazo yako hata kama sikubaliani nayo!
VIVA DEMOCRACY!

Angalau ungekuwa unafahamu tu maana ya kukremu tungepata mjadala wa maana sana. Kukremu hakuvuki hatua ya kumbukumbu, kukremu hakwendi kwenye application kama unafahamu Bloom taxonomy learning. Nimesema umepitwa na wakati kwa kutoa mifano kamaa lengo letu ni maendeleo. Kukosoa mawazo nikuyaheshimu, asiyekosoa huyo ndio hayaheshimu, I see what you were trying to insinuate, we are calling them red herring. Mengine uliyoyasema huyafahamu vizuri, hasa ya Azimio la Arusha. Ungekuwa kweli ni mfuasi wa demokrasia usingedharau hizo unazoziita theory za Azimio la Zanzibar, MKUKUTA na MKURABITA. Naona unayapenda sana maneno ya 'ethics na logic', nakuombea Mungu siku moja uwezekuyafamu vyema ili uyatumie ipasavyo. Hauna haja ya kuji confuse na maneno maneno " 'scientific theories'. Revolution/evolution of science is one thing, while logic, philosophy and ethics are each, another thing all together" kama unataka kujifunza na kushiriki katika mjadala wa maana. Angalau unaweza ukayatumia ili nawe moyoni mwako ujisikie wa maana. Karibu tujadiliaane.
 
Acha theories za kura za Twaweza, we need scientifically proven theories. Norway imekuwa kama ilivyo baada ya mafuta na kuwa democratic. Nimekuwa huko wanasema viongozi wao

Wewe umepata maelezo kutoka kwa first hand people, mimi nimesoma kutoka official document za Norway which they public and accessible. Maelezo yangu yana mamlaka, maelezo yako yana hisia. Kwa kuwa waliokuambia siwezi kuwapata ila wewe unaweza kusoma, basi soma halafu uniambie hapa wamedanganya au wamekosea ukilinganisha na maelezo yako ya 'my first hand people'. Lugha ya kebehi kuna watu ni weledi sana nayo, lakini inamsaidia nani sasa? Kama nchi zisizozidi tano dunia nzima ndizo zinaaminika zimepata maendeleo kutokana na demokrasia kwanini sasa sisi tujipachike huko kwenye njia ngumu walizopitia mataifa machache? Tufikiri kidogo tu!
 
Umenikumbusha post yangu ya siku za nyuma;

Uendeshaji wa TAZARA sasa wakabidhiwa kwa Mchina

Watakuwa surprised zaidi wakigundua kuwa hakuna nchi iliyowahi kuhama kutoka umaskini kwenda utajiri kwa kupractice demokrasia tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, watashangaa zaidi wakigundua nchi zilizohama toka umaskini kwenda utajiri hazikuruhusu full demokrasia na uhuru kamili wa habari. Ajabu nyingine ndani ya Africa yetu hii hii nchi karibu zote zenye unafuu wa kimaendeleo kutoka misri na jamaa zake wote wa kiarabu hadi Africa ya kusini zimeeendelea katika kipindi zikiwa hazina demokrasia. Having said that, simaanishi demokrasia ni kitu kibaya au haifai, ni vile tu hatujui matumizi sahihi ya demokrasia katika maendeleo. Kwa wengi wetu demokrasia ni kupeana Zamu za kutawala....Then What????

Angalia nchi zenye demokrasia zaidi africa kwa sasa
  • Sierra Leon.
  • Tanzania. ...
  • Senegal. ...
  • Lesotho. ...
  • Benin. ...
  • South Africa. ...
  • Namibia. ...
  • Botswana.

Halafu angalia nchi zenye uchumi mzuri zaidi africa (By GDP) kwa data za 2015
  • Nigeria
  • Africa kusini
  • Misri
  • Algeria
  • Angola
  • Morroco
  • Libya
  • sudan
  • Kenya
  • Ethiopia
Endelea kujidanganya na akili zako za kushikiwa kwamba udikiteta na matamko kunaweza kuitoa nchi yoyote kwenye umasikini. Umasikini wa Tanzania na watanzania kwa mfano unawahusu watanzania wote zaidi ya milioni 50 na wote wana solution na namna ya kujitoa kwenye umasikini,sasa kama hakuna Uhuru wa kutoa,kusambaza na kupokea habari hawa watanzania watacommunicate vipi hizi solutions zao?Kazi ya serikali ya kidemocrasia ni kuchoose optimum solution out of the many but serikali zenye poor listening skills haziwezi kusikiliza,sijajifanya zenyewe ndo zenye akili kuliko watu wote,
 
Jamaa anasema serikali ni boss wa mihimili mingine kwa kuwa ndio inakusanya kodi,ndo yenye pesa,anasahau kuwa hizo pesa anazikusanya kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge na inatofasiriwa na mahakama ili kumuwezesha kukusanya hizo pesa, kwamba bila collaboration hiyo asingeweza kukushanya hizo pesa,aibu yake na ccm yake
Lowassa alituambia elimu, elimu, elimu
 
Wewe umepata maelezo kutoka kwa first hand people, mimi nimesoma kutoka official document za Norway which they public and accessible. Maelezo yangu yana mamlaka, maelezo yako yana hisia. Kwa kuwa waliokuambia siwezi kuwapata ila wewe unaweza kusoma, basi soma halafu uniambie hapa wamedanganya au wamekosea ukilinganisha na maelezo yako ya 'my first hand people'. Lugha ya kebehi kuna watu ni weledi sana nayo, lakini inamsaidia nani sasa? Kama nchi zisizozidi tano dunia nzima ndizo zinaaminika zimepata maendeleo kutokana na demokrasia kwanini sasa sisi tujipachike huko kwenye njia ngumu walizopitia mataifa machache? Tufikiri kidogo tu!

Na bila democracy hakuna maendeleo ndiyo maana africa ya kusini inarudi nyuma baada ya kuingia madictators.
 
Endelea kujidanganya na akili zako za kushikiwa kwamba udikiteta na matamko kunaweza kuitoa nchi yoyote kwenye umasikini. Umasikini wa Tanzania na watanzania kwa mfano unawahusu watanzania wote zaidi ya milioni 50 na wote wana solution na namna ya kujitoa kwenye umasikini,sasa kama hakuna Uhuru wa kutoa,kusambaza na kupokea habari hawa watanzania watacommunicate vipi hizi solutions zao?Kazi ya serikali ya kidemocrasia ni kuchoose optimum solution out of the many but serikali zenye poor listening skills haziwezi kusikiliza,sijajifanya zenyewe ndo zenye akili kuliko watu wote,

kwanza usitukane wala kutoa lugha za kashifa hapa;
Baada ya hapo kafanye homework yako juu ya nchi zifuatazo namna zilivyotoka kwenye umaskini;
1. china
2.korea kusini
3. Japan
4. Singapore

Na hizi zinazojitahidi kutoka umaskini sasa;
1.Thailand
2. Rwanda

Homework hii ikikushinda nitakufanyia hapahapa.

Ukimaliza Homework yako jitahidi kumeza ukweli mchungu kwamba katika uongozi wowote namna nzuri ya kukwama kufikia maamuzi ni kumsikiliza kila mtu, ndio hivyo!
 
(li)pumba tupu
 
Please tuwekee hukumu hizo kwa ajili ya elimu
Sina soft copy. Zipo hard copy kwa wakili fulani. Nilizisoma huko kwani nina maslahi nazo. Moja ililetwa hapa ikiwa soft copy ambayo ndio wananchi wa kimara jaji aliwapa ushindi. Sina utaalamu wa kufukua uzi wa zamani. The same facts ikaja na kesi nyingine maeneo ya mail moja, wakataka kutumia kesi ya watu wa Kimara kama rejea, Jaji wa hiyo kesi ya pili akagoma na kuchukua msimamo tofauti na wananchi wakaambiwa wamevamia barabara. Mimi nakubaliana na tafsiri ya sheria ya jaji wa pili hata kama ni chungu kwa wananchi. Ya kwanza ni Proches Tarimo na wenzake. Ya pili ni Manson Shaba na wenzake. Tumia hizo kufukua mitandaoni. Mimi ni born before computa
 
Sina soft copy. Zipo hard copy kwa wakili fulani. Nilizisoma huko kwani nina maslahi nazo. Moja ililetwa hapa ikiwa soft copy ambayo ndio wananchi wa kimara jaji aliwapa ushindi. Sina utaalamu wa kufukua uzi wa zamani. The same facts ikaja na kesi nyingine maeneo ya mail moja, wakataka kutumia kesi ya watu wa Kimara kama rejea, Jaji wa hiyo kesi ya pili akagoma na kuchukua msimamo tofauti na wananchi wakaambiwa wamevamia barabara. Mimi nakubaliana na tafsiri ya sheria ya jaji wa pili hata kama ni chungu kwa wananchi.

Naomba citation nitazitafuta
 
Naomba citation nitazitafuta
Nime edit post yangu kuweka majina ya Wadai. Full citation sina. Kesi ya kwanza ni Proches Tarimo na wenzake. Kesi ya pili ni Manson Shaba na wenzake. Zote zimeamuliwa na mahakama kuu-Land Division, majaji tofauti
 
Angalau ungekuwa unafahamu tu maana ya kukremu tungepata mjadala wa maana sana. Kukremu hakuvuki hatua ya kumbukumbu, kukremu hakwendi kwenye application kama unafahamu Bloom taxonomy learning. Nimesema umepitwa na wakati kwa kutoa mifano kamaa lengo letu ni maendeleo. Kukosoa mawazo nikuyaheshimu, asiyekosoa huyo ndio hayaheshimu, I see what you were trying to insinuate, we are calling them red herring. Mengine uliyoyasema huyafahamu vizuri, hasa ya Azimio la Arusha. Ungekuwa kweli ni mfuasi wa demokrasia usingedharau hizo unazoziita theory za Azimio la Zanzibar, MKUKUTA na MKURABITA. Naona unayapenda sana maneno ya 'ethics na logic', nakuombea Mungu siku moja uwezekuyafamu vyema ili uyatumie ipasavyo. Hauna haja ya kuji confuse na maneno maneno " 'scientific theories'. Revolution/evolution of science is one thing, while logic, philosophy and ethics are each, another thing all together" kama unataka kujifunza na kushiriki katika mjadala wa maana. Angalau unaweza ukayatumia ili nawe moyoni mwako ujisikie wa maana. Karibu tujadiliaane.

Hasira za nini? Hoja ya msingi ni kuwa hamtaki Demokrasia na Utawala wa Sheria. Elimu yangu binafsi huwezi kuijua, naijuwa mwenyewe. Sipo hapa kuuambia ulimwengu lolote kuhusu elimu au uwezo wako wa kufikiri, sina haki wala nia ya kuingia kwenye aina hiyo ya malumbano.
 
Na bila democracy hakuna maendeleo ndiyo maana africa ya kusini inarudi nyuma baada ya kuingia madictators.

Afrika kusini imeyumba baada ya kuingia kwenye full democracy mkuu, nchi ile iliendelea enzi za ukandamizaji na ubaguzi wa rangi.
 
Na bila democracy hakuna maendeleo ndiyo maana africa ya kusini inarudi nyuma baada ya kuingia madictators.
Hivi South Africa ya ubaguzi wa rangi na South Africa ya sasa ipi ina democrasia?

Kisha jiulize kwanin South Africa ya kipindi cha Makaburu ndio iliyopiga hatua kubwa kiuchumi na sasa wanashuka?democrasia na maendeleo ni vitu viwili tofauti.
 
(li)pumba tupu

Kwani unaweza kusoma mkuu???
Ningeweza kukuwekea hapa reference za kusoma ujue ukweli lakini najua huwezi kusoma chochote kinachozidi page moja.

Jibu basi swali hili rahisi, Katiba ya Marekani iliandikwa na watu wangapi??
 
Mafuta sio maendeleo.Mafuta ni kichocheo cha maendeleo. Kabla haijawahuru mwaka 1814 Norway tayari ilikuwa inajitosheleza. Zaidi asilimia 90 ya wananchi wake walikuwa wakiishi rural areas na walikuwa wazalishaji wazuri wa bidhaa za kilimo na ufugaji. Mfumo huu haukujengwa na demokrasia ndugu yangu. Norway ilikuwa na Muungano na Sweden kabla hawajawa 'independent'. Ukipiga jicho haraka haraka dunia nzima ukiacha scandnavian countries ambazo hata nazo zina historia yake na tamaaduni zake na hata pia aina ya demokrasia yake ni tofauti, they are social democrats, dunia nzima hakuna nchi iliyochomoka kutoka umasikini kwa kufuata mfumo wa demokrasia. Demokrasia kwanza haiwezi kushamiri kwenye umasikini. Demokrasia ni hatua inayokuja baada ya maendeleo ya kiuchumi. Demokrasia huimarisha maendeleo ya kiuchumi lakini si kuleta maendeleo ya kiuchumi. Taratibu za kidemokrasia haziko favourable kwa ukuaji wa uchumi katika nchi masikini. Mfumo wa demokrasia unapoteza muda na focus sana. Ili kupata maendeleo inatakiwa ifanyika kama Mungu alivyofanya na hata mataifa makubwa ya Marekani, uingereza, Ujerumani, China na mengine yenye power. Umba 'maendeleo' halafu ndipo watu waje kuanza kubishana. Pengine hata Mungu angewauliza wanadamu nini akiumbe na nini asikiumbe, labda mpaka hii leo dunia ingekuwa haijakamilika.
Asingeweza kuwauliza kwa maana aliwaumba wa mwisho baada ya kuumba vitu vyote ......ikawa jioni ikawa asubuhi; siku ya sita. Mwa. 1:26-
 
Na bila democracy hakuna maendeleo ndiyo maana africa ya kusini inarudi nyuma baada ya kuingia madictators.
Ukitaka kuona umuhimu wa democrasia soma historia ya ulaya kabla na baada ya democrasia. Angalia walivyopata maendeleo ya kasi baada ya kuwaangusha watawala wa kifalme na kuleta demokrasia. Usipokuwa na demokrasia unaweza kuleta maendeleo ya haraka kwa muda mfupi lakini hayawezi kuwa maendeleo ya kudumu kwani yataharibika yote na kurudi kubaya zaidi ya mwanzo.
 
Tujifunze pia kupitia Dubai, imewezaje kuendelea kwa kasi sana katika kipindi kifupi??
Nini nafasi au mchango wa Demokrasia???

Mtazamo wangu mimi, katika nchi maskini na fukara zinahitaji individuals watakaokuwa "Masterminds" wa mchoro mzima wa maendeleo, waweke misingi ikibidi kwa mkono wa chuma na kisha baada ya misingi hiyo sasa waziache jamii zao katika mikono ya demokrasia ya wengi wape!
 
Hivi South Africa ya ubaguzi wa rangi na South Africa ya sasa ipi ina democrasia?

Kisha jiulize kwanin South Africa ya kipindi cha Makaburu ndio iliyopiga hatua kubwa kiuchumi na sasa wanashuka?democrasia na maendeleo ni vitu viwili tofauti.

Kwahiyo enzi za Makaburu wananchi weusi wa SA ambao ni majority walikuwa na maendeleo kuliko sasa?
 
Back
Top Bottom