John Kachembeho
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 560
- 386
Wale walioenda shule vizuri wanatambua theory maarufu ya Kuhn's theory of scientific revolution. Kuhn anaamini hakuna nadharia nzuri itakayodumu duniani milele. Zitakuja nadharia kwa wakati wake, zitafanya kazi kwa muda na kadri mahitaji ya watu yatakavyobadilika hiyo nadharia itashindwa kukidhi vilivyo hivyo kutokea migongano, wengine kutokubali kuendelea kuitumia na wengine kutaka ibaki itumike. hiki kipindi huitwa crisis stage. Ikitokea nadharia ikakataliwa au ikashindwa kuleta matunda yatarajiwayo nadharia nyingine hujitokeza. Wakati umefika sasa wa kuona kuona nadharia inayohusu demokrasia ya magharibi imeshindwa. Nadharia hii haijawahi kuitoa nchi yeyote ile duniani kutoka katika umasikini. Badala yake madharia hii imezidi kuzifukarisha nchi masikini zenye kuifuata huku nchi zilizokuwa masikini zikaikataa nadharia ya demokrasia ya magharibi zimepiga hatua kubwa. Tuache ku kremu mambo ya mihimili ambayo hayana tija na ustawi wetu. Tujenge mfumo wenye kuheshimu watu na kumfanya kila mmoja wetu awajibike kufikia lengo awe anataka au hataki.Maslahi mapana ya walio wengi yawekwe mbele. Tukikopi kutoka kwa Machiaveli kiasi na mengine kwa Rouseau tutafika. Kukremu mambo yasiyo kichwa wala miguu kama kasuku huku tukibana pua, tutabaki si kuwa masikini milele bali pia wajinga wa kutupwa!
Umenikumbusha post yangu ya siku za nyuma;
Uendeshaji wa TAZARA sasa wakabidhiwa kwa Mchina
Watakuwa surprised zaidi wakigundua kuwa hakuna nchi iliyowahi kuhama kutoka umaskini kwenda utajiri kwa kupractice demokrasia tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, watashangaa zaidi wakigundua nchi zilizohama toka umaskini kwenda utajiri hazikuruhusu full demokrasia na uhuru kamili wa habari. Ajabu nyingine ndani ya Africa yetu hii hii nchi karibu zote zenye unafuu wa kimaendeleo kutoka misri na jamaa zake wote wa kiarabu hadi Africa ya kusini zimeeendelea katika kipindi zikiwa hazina demokrasia. Having said that, simaanishi demokrasia ni kitu kibaya au haifai, ni vile tu hatujui matumizi sahihi ya demokrasia katika maendeleo. Kwa wengi wetu demokrasia ni kupeana Zamu za kutawala....Then What????
Angalia nchi zenye demokrasia zaidi africa kwa sasa
- Sierra Leon.
- Tanzania. ...
- Senegal. ...
- Lesotho. ...
- Benin. ...
- South Africa. ...
- Namibia. ...
- Botswana.
Halafu angalia nchi zenye uchumi mzuri zaidi africa (By GDP) kwa data za 2015
- Nigeria
- Africa kusini
- Misri
- Algeria
- Angola
- Morroco
- Libya
- sudan
- Kenya
- Ethiopia