Siku ya Sheria: Rais Magufuli azindua Mahakama inayotembea, Mfumo wa kieletroniki wa kuratibu mashauri! Asema uongozi wake hauingilii Mihimili mingine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,745
139,523
Maadhimisho hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.

Rais Magufuli ameshawasili katika viwanja vya ukumbi huu na sasa anapewa maelezo kuhusu mahakama inayotembea.

Mahakama inayotembea itaanza kutoa Huduma katika mikoa ya Dar Es Salaam na Mwanza, Mahakama hii iko ndani ya gari ambalo lina vifaa vyote vya Mahakama. Thamani ya gari hili ni zaidi ya sh 470 milioni.

Sasa mh Rais Magufuli anakata utepe kuzindua rasmi Huduma za mahakama inayotembea..Ameingia ndani ya gari hilo na anapewa maelekezo ya namna kesi zitakavyoendeshwa ndani ya mahakama hiyo.

Rais Magufuli na msafara wa majaji wanaingia ukumbini tayari kuanza rasmi kwa shughuli hii.



Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia(WB)
Mwakilishi wa benki ya dunia sasa anatoa salamu za benki hiyo kwa mahakama. WB ndio iliyofadhili magari yatakayotumika kama mahakama inayotembea.



HOTUBA YA JAJI MKUU

Nashukuru Rais Magufuli kwa kukubali wito wa kuwa mgeni rasmi. Wananchi wanapaswa kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi badala ya kushinda mahakamani kutafuta haki. Hivyo mwaka huu Mahakama inajikita katika kuhakikisha inatoa haki kwa wakati kwa kuipeleka Huduma karibu zaidi na wananchi.

Nawataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Mahakama katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati. Mheshiwa Rais, naomba Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali aweke Sheria zote mitandaoni yaani Serikali Mtandao ili wananchi wawezi kujisomea kwa wakati wao zile sheria ambazo wana maslahi nazo.

Huduma bora za Haki zinategemea mchango mkubwa wa Wananchi.Wananchi wanapaswa kufuata taratibu, kutokutoa rushwa, pia kufika Mahakamani kufahamu Sheria.Kabla ya kufungua kesi, Wananchi wanashauriwa kufahamu taratibu ambazo kesi itapitia

Siku hizi Mahakama zinaweza kusikiliza mashauri kupitia 'Video Conferencing'.Hii inawezesha kuendesha kesi kisasa kwa kuwasikiliza mashahidi walio nje ya Mahakama. Mwaka jana kwenye moja ya kesi, shahidi alisikilizwa akiwa Ufaransa

Niombe Mpiga chapa Mkuu wa Serikali afanye jukumu la kuziweka Sheria zote mtandaoni ili kuwarahisishia Wananchi kuzisoma Sheria hizo

Mfumo huu umeunganishwa na mfumo wa usimamizi wa mashauri, na hakuna kesi yoyote inayoweza kusahiliwa bila kulipa ada. Tangu tumejiunga na mfumo huu wa malipo maduhuri yameongezeka

Mifumo mingine inayofanya kazi kwa sasa ni kutumia mfumo wa kusikiliza mashauri kwa video, shauri linaweza kusikilizwa Mtuhumiwa akiwa mahabusu au gerezani.Desemba 5, Mahakama Kuu ilimsikiliza Shahidi akiwa Ufaransa

Mahakama Kuu iliwekewa Sera ya kutakiwa kusikiliza mashauri na kutolea maamuzi ndani ya miaka 2 tangu kufunguliwa kwake. Mahakama Kuu pia imejiwekea sera kuwa kila Jaji anatakiwa kusikiliza angalau wastani wa mashauri 220 kwa mwaka

Kwa kuzingatia idadi ya Majaji 66 waliokuwepo hadi Desemba 2018, mzigo wa kila Jaji ulikuwa ni kubeba wastani wa mashauri 568, idadi ambayo ni kubwa sana ikilinganishwa na wastani waliopangiwa kwa kila Jaji mashauri 220

Mahakama ina changamoto mbalimbali ambazo Mahakama inakutana nazo ikiwemo mashauri ya kodi ambayo usikilizwaji wake hucheleweshwa sana katika bodi za rufaa za TRA. Mfumo mzuri wa usikilizaji mashauri uko katika sekta ya ardhi.

Idadi ya Majaji katika Mahakama Kuu kwa sasa ni 73, kwa kuzingatia mashauri ya mwaka jana, wastani wa mashauri kwa Jaji umepungua kutoka 568 hadi 513. Hivyo Mbeshimiwa Rais, bado mzigo ni mzito

Kwa mwaka 2018 Mahakama za Hakimu Mkazi, Mwanzo na Wilaya zilikaguliwa na matokeo ya ukaguzi ni mashauri ya nidhamu yamependekezwa yafunguliwe dhidi ya maafisa 4, Maafisa hao walibainika kuvunja taratibu na Maadili

Mpango wa kusambaza nyaraka za kimahakama kupitia mpango wa Posta mlangoni umeanzishwa Machi 2018 na unatekelezwa ili Wananchi wote waliokuwa na kesi Mahakamani na zikaisha waweze kuletewa nakala za hukumu milangoni mwao

Mahakama inayotembea ina dhana inayomaanisha Mahakama ktk ngazi fulani inahamisha shughuli zake na kuzitolea sehemu fulani ktk mamlaka yake. Mfano, Mahakama ya Rufaa inapohamisha shughuli zake kutoka Dar kwenda vituo mbalimbali

Mahakama hii ni gari maalumu lenye sehemu 2. Chumba cha Hakimu kitakuwa na meza ya Hakimu, meza ya Karani na ya wadahawa. Kutakuwa na Runinga, Kompyuta, Kabati la majalada, Vyombo vya kurekodia, vipaza sauti na chumba cha faragha

Kwa awamu ya kwanza (Pilot study), yamenunuliwa magari mawili yatakayotoa huduma mikoa ya Dar na Mwanza .

Kwa Dar: Kinondoni kituo kitakuwa Bunju, Ilala kitakuwa Chanika, Wilayani Temeke kitakuwa Buza na Kibamba kwa Ubungo

Kwa mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Ilemela kituo kitakuwa Buhongwa na Igoma. Kwa Wilaya ya Nyamagana kituo kitakuwa Buswelu

Namshukuru Spika Ndugai na waziri Kabudi kwa namna wanavyosaidia katika kupitisha bajeti za Mahakama.



HOTUBA YA SPIKA WA BUNGE

Nikushukuru Jaji Mkuu kwa kunialika pamoja na wabunge wenzangu. Nimeleta salam nyingi kutoka Dodoma

Wenzetu wana siku ya Sheria, nikawa najiuliza sisi kwanini hatuna siku ya Bunge? Lakini kabla ya hiyo nikajiuliza hatuna siku ya serikali.

Jana kulitokea king'ora, kuangalia hivi wabunge wote hawapo, kumbe tuna wanariadha wengi. Waziri Mkuu naye hakuwepo, kuangalia hivi Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye yuko mgongoni anatimua.

Wiki iliyopita tulipata mgeni, mgeni huyo ni bundi, nikawa najiuliza hawa bundi wapo mpaka mahakamani au ni mimi tu spika! Ila alikuwa wa mchana hana madhara. Nachotakata kuwaambia ni kwamba wabunge tuko salama.

Maswali ni mengi sana kuhusu Mahakama za kutembea,ilikaa kamati kujiridhisha na maswali yakaibuka mfano mahali pa kujisaidia, cell za kufungia. Afrika hakuna nchi yenye mahakama inayotembea, labda Bangladesh. Kabla ya kupitisha muswada huo wabunge walitaka waende wakajifunze, tuliona inawezekana.

Uhuru wa Mahakama tunapenda tuone unaheshimiwa pale bungeni na sehemu nyingine. Bunge halitaingilia na endapo watakengeuka basi Jaji mkuu atukumbushe ili turudi kwenye mstari.

Niwapongeze kwa mfumo huu wa kielektronic wa kuratibu mashauri. Zamani ilikuwa usumbufu sana, ulikuwa huna kazi nyingine wewe kila siku unahudhuria mahakamani.Wengine hawakupenda kabisa mashauri yao kupelekwa Mahakamani kwasababu ya usumbufu huo. Sasa hivi mambo yatakuwa safi

Baada ya hayo niwashukuru na kuwapongeza.



HOTUBA YA RAIS MAGUFULI

Waheshimiwa Jaji Mkuu na viongozi wengine, yaliyozungumzwa ni mengi sana. Jaji mkuu ame-quote Mwl Nyerere kuwa 'Kulalamika lalamika sio vizuri' nikajiuliza yeye alikuwa analalamika au? Amezungumza mengi, zikiwepo changamoto

Nimekuwa nikifurahi sana kupata mialiko yenu, ingawa mimi sio mwansheria ila nimekuwa nikipenda sheria. Sheria ni muhimu katika ustawi wa jamii kwa ujumla,ii ni mara ya 4 tangu.

Tuko hapa kuazimisha siku ya sheria, pia ndio mwanzo wa kuanza mwaka mpya wa Mahakama. Mwanzo wa mwaka ni nafasi ya kutathmini mambo mbalimbali.

Tupo hapa tumekaa kwa amani kwasababu zipo sheria zinazotulinda.

Sheria zipo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ninyi ni mashahidi kuwa siku hizi kabla mtu hajaanzisha mradi ataangalia sheria zinazomuongoza, hii mtaona inaleta ustawi wa uchumi.

Nimefurahi kumuona Spika, amezungumzia kuhusu bundi, lakini hajazungumzia fisi zinazozunguka Dodoma. Awapeleke viongozi wa dini bundi hawatarudi tena.

Naipongeza Mahakama kwa mafanikio katika kupunguza idadi ya kesi, Mahakama inastahili pongezi katika eneo hili.

Kadhalika ujenzi wa miundombinu na kushughulikia rushwa ya watumishi mahakamani mnastahili pongezi. Pia ongezeko la mapato katika idara ya Mahakama kumenitia moyo.

Mwaka jana nilisaini hati ya idhini kuanzisha ofisi ya DPP iliyo huru kiutendaji. Hivyo kwa ujumla mwaka uliopita ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa mahakama na sekta ya sheria.

Kwa upande wa changamoto, kuna ucheleweshaji wa kesi na utolewaji wa nakala za hukumu bado ni tatizo. Suala la kuchelewesha upelelezi kwa kesi zilizoko mahamani bado ni tatizo pia

Suala la upungufu wa watumishi liko katika kila sekta kuanzia Polisi, Afya, Elimu nk na ili kuitatua changamoto hii kitu muhimu ni uwezo. Hivyo kutokana na uwezo halisi wa uchumi wetu changamoto hii inahitaji muda ili kuitatua. Naomba Mahakama iwatumie watumisi hawa waliopo kufanya kazi kwa ufanisi mpaka mambo yatakapokaa sawa.

Najua kuna Mahakimu kwa mujibu wa Katiba wameteuliwa na Mahakama kufanya kazi za Ujaji. Naomba muwapangie kesi, nimeona wana kesi sita.

Nawaomba watumishi wa Mahakama kuchapa kazi na kujiendeleza kitaaluma, pia nawaomba mtafsiri maamuzi kwa kiswahili.

Nawashukuru World Bank kwa namna wanavyoifadhili Mahakama, namshukuru Mwakilishi wa WB nchini kwa ushirikiano unaotupa.

Nawaomba Majaji na Mahakimu kumtanguliza Mungu mbele katika kutoa haki.

Nawaomba wapelelezi kukamilisha upelelezi kwa wakati. Mtuhumiwa anakamatwa na vidhibiti bado mnapeleleza, wakati mwingi mwizi mnakuta kafungwa alivyoiba shingoni, sasa hapo mnapeleleza nini, au mnataka kujua wakati anaiba alikuwa amelala au kasimama.

Wanasheria pia wana mtindo wa kushirikiana na hatimaye kumpora haki asiye na hatia. Kwa mfano wakili wa mshtakiwa na yule wa mashtaka wanaweza kula njama na kuumiza upande mmoja.

Mheshimiwa Jaji Mkuu, changamoto zote nimezichukua na nitazifanyia kazi japo hali bado. Katika serikali anayoiongoza kamwe sitawaangusha.

Mimi sijawahi kuliingilia Bunge wala muhimili wa Mahakama, Majaji mkatende kazi bila woga.

Saa nyingine Bungeni wanakutukana unaishia kuzima TV unaenda mahali pengine‬

Sijaingilia Muhimili wa Mahakama hata kama wanaenda kule kukushtaki wanasahau hata kifungu namba 46 cha Katiba ibara ya 46...ndio uhuru‬

Mahakama iangalie uwezekano wa Mahakama inayotembea moja kushughulikia kesi za mirathi na wajane tu.

Najua kuna changamoto kwenye kesi za uvuvi haramu,Mimi wakati nipo Wizara ya uvuvi wakati tunashughulikia wavuvi haramu, hii ‘mobile court’ ilifanya kazi nzuri kule Mwanga‬. Tukawashika wavuvi haramu nakumbuka mmoja alikuwa Diwani wa CCM, akafungwa papo hapo miezi sita. Nilifurahi kweli

Kule kulikuwa na makaburi yamechibwa yakafukiwa yanawekewa misalaba na jina la marehemu linaandikwa, ukifukua ndani unakuta kuna makokoro‬

------------

> Viongozi wote, yaliyozungumzwa ni mengi na hotuba ya Jaji Mkuu imelezea mengi na mwishoni akatoa nukuu ya Nyerere kuwa kulalamika sio kuzuri.Nikawaza alikuwa anatoa taarifa au alikuwa analalamika. Ila nikuambie ujumbe umefika

> Hii ni mara yangu ya nne kushiriki maadhimisho haya na nashukuru kwa kunialika kwenye maadhimisho haya. Nimefurahi kwa kuwa mimi mwenyewe napenda sana Sheria

> Maadhimisho haya yanaonesha ni mwanzo wa mwaka wa Mahakama. Ni mwaka wa kutathmini yaliyopita mwaka jana. Niipongeze Mahakama kwa mafanikio mliyoyapata mwaka jana, pana mabadiliko mengi sana, mmefanya kazi nzuri

> Licha ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Mahakama bado kuna changamoto nyingi na Jaji Mkuu umezitaja. Nimezisikia na nimezipokea, na ndiyo maana ulipomaliza hotuba yako nimekuomba nakala ya hotuba yako niipitie tena

> Matatizo ya ucheleweshaji kesi, ushahidi na kutotolewa kwa nakala ya hukumu na wananchi kujichukulia Sheria mkononi bado yapo. Mathalani, mwaka jana Mahakama ilifuta kesi 1986 kwa ucheleweshaji wa upelelezi. Hizi ni changamoto

> Jaji Mkuu amezungumza kuhusu upungufu wa Wafanyakazi na Watumishi, najua Jaji Mkuu lazima azungumze. Lakini ukweli unaeleweka, kila sekta, kila mahali kuna upungufu sio Polisi, sio Walimu hata kwenye Majeshi ni hivyohivyo

> Upungufu wa Wafanyakazi ni changamoto, ila unafanyaje wewe ndio kiongozi. Kuitatua changamoto kikubwa kinachohitajika ni uwezo. Kwa sasa 'payroll' ya Watanzania ni zaidi ya watu Laki 5, na ni baada ya kupunguza Watumishi hewa

> Ni lazima niseme ukweli kuwa, changamoto hii haiwezekani kutatuliwa siku moja kutokana na hali halisi ya uwezo wa nchi. Niwaombe na nikuombe Jaji Mkuu wakati tunatafuta njia mbadala, tutumie wale waliopo kikamilifu

> Ushauri mwingine, kwenye Mahakama najua kuna Mahakimu wanaoteuliwa chini ya kifungu cha Sheria namba 173. Hawa Mahakimu huwa wanapewa na wanaweza kusimamia hata kazi za majaji, tujiulize tumewatumiaje kwa kipindi kilichopita?

> Serikali itaendelea kuunga mkono shughuli zote zinazofanywa na Mahakama na ndio maana tunajaribu kushiriki kutatua changamoto. Tangu tulipokutana mwaka jana, tumeweza kuteua Majaji wa Rufaa 8 na Majaji wa Mahakama kuu 27

> Nitoe wito kwa Wizara, Taasisi na Idara kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu Sheria mbalimbali zinazosimamiwa. Pia nitoe wito kwa Sheria kutafsiriwa kwa Kiswahili

> Viongozi wa dini Wanafahamu vizuri kuhusu amri za Mungu tangu enzi za akina Mussa zinavunjwa mpaka leo. Tunazivunja wote inawezekana hata wanaozihubiri nao wanazivunja. Hivyo Sheria zitaendelea kuvunjwa

> Wapelelezi kapelelezeni haraka. Umeona kitu kipo unaenda kupeleleza nini? Mtu kashikwa kaiba na kidhibiti anacho, labda kafungiwa shingoni. Bado unataka kukapeleleze! Unataka ukapeleleze alivyoiba alikuwa ameinama au amelala?

> Saa nyingine Mahakamani mnamwambia Hakimu upelelezi bado unaendelea, kumbe unamchelewesha, ukimwambia ujue utafungwa zungumza sasa. Lawama wanapewa Mahakimu na Majaji kwamba wamechelewesha kazi, aliyechelewesha wala hatajwi

> Lakini pia Wanasheria siku zote huwa kuna pande 2. Mwanasheria wa utetezi na upande mwingine. Wanazungumza kesi itakavyoenda usiku, vipengele vya kumfunga mtuhumiwa wanaviruka makusudi ili Mwanasheria wa kujitegemea ashinde

> Niwaombe wote kwa upole, tukazingatie maadili ya kazi zetu, ukienda Mahakamani kesi bado upelelezi unafanyika, zinafutwa. Ndio maana kesi zaidi ya 800 zimefutwa kwa kuwa zimekaa muda mrefu Mahakamani na nyingine zina ushahidi

> Ila tumeanza vizuri, ndio maana sijazungumza niliyozungumza mwaka jana na inawezekana wengi walitegemea nitazungumza lakini sizungumzi ng’oo Kwasababu ninaona kuna mabadiliko

> Wasajili wa Mahakamani nanyi mna dhambi zenu ndogo ndogo ambazo mnazielewa, kazirekebisheni. Saa nyingine mnachagua Jaji gani apelekewe kesi. Huyu anapelekewa yenye mashiko, huyu anapelekewa yenye shuruba

> Serikali ninayoiongoza kamwe haitawaangusha. Nafahamu zipo changamoto ndogondogo za baadhi ya Watendaji kuingilia mambo ya Mahakama. Nanyi mtoe maamuzi vizuri msiingiliwe, saa nyingine mnaingiliwa kwasababu ya hasira za watu

> Lakini ninafahamu mipaka ya kila chombo ni muhimu, lazima izingatiwe. Na sisi huwa tunawasiliana vizuri, na nimejitahidi katika uongozi wangu kutokuingilia muhimili wowote

> Saa nyingine Bungeni wanakutukana unaishia kuzima TV unaenda mahali pengine. Sijaingilia Muhimili wa Mahakama, hata kama wanaenda kule kukushtaki wanasahau hata kifungu namba 46 cha Katiba ibara ya 46...ndio uhuru

> Wapo akina mama wanaohangaika na mirathi, suala ambalo ni changamoto. Hilo Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi mkalishughulikie. Wajane wanapata shida sana, mtu anafiwa na mirathi inachukua miaka, saa nyingine wanaochukua si wahusika

> Hata kama ni kuwa na ‘Mobile court’ ya kushughulikia wajane tu kwenye suala la mirathi, mkalishughulikie. Nimuombe Mheshimiwa Bella atafute magari mengine, ili lingine liwe la kushughulikia kero za akina mama suala la miradhi

> Wakati nipo Wizara ya uvuvi tunashughulikia wavuvi haramu, hii ‘Mobile court’ ilifanya kazi nzuri kule Mwanga. Tuliwashika wavuvi haramu, nakumbuka mmoja alikuwa Diwani wa CCM, akafungwa papo hapo miezi 6. Nilifurahi kweli

> Sasa kesi zikienda hivyo ndio safi, na uvuvi haramu ukapungua. Kule kulikuwa na makaburi yamechibwa yakafukiwa yanawekewa misalaba, ukifukua ndani unakuta kuna makokoro
 
Karibu!

Maadhimisho hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere.

Up dates;
Wageni mbalimbali wameshaingia ukumbini akiwemo Spika Ndugai pamoja na viongozi wa dini.
Mawakili na wadau wa sheria nao wamejazana kwa wingi ukumbin

Viongozi wa vyama vya siasa Chadema, Cuf, UDP na Chauma wanaonekana hapa, nawaona Mzee Cheyo, Lipumba na Dovutwa wakijadiliana jambo.i.
Hivi huyu JAMAA anafanya kazi saa ngapi? kila wiki lazima uzinduzi na MATIVII. Rais anatakiwa akae na kuwaza namna ya kuisaidia Nchi kwa kujenga fikra.
 
Karibu!

Maadhimisho hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere.

Up dates;
Wageni mbalimbali wameshaingia ukumbini akiwemo Spika Ndugai pamoja na viongozi wa dini.
Mawakili na wadau wa sheria nao wamejazana kwa wingi ukumbin

Viongozi wa vyama vya siasa Chadema, Cuf, UDP na Chauma wanaonekana hapa, nawaona Mzee Cheyo, Lipumba na Dovutwa wakijadiliana jambo.i.
Prof Lipumba sasa hv kafikia level sawa na Dovutwa😀😀

Kiongozi gani wa chadema yupo hapo? Lisu?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom