Hakimu mkazi au resident magistrate ni nani?

Resident magistrate? Hapa hakuna elimu ya Civics wala ya sheria inayohitajika kujibu hili swali.
Ni kiingereza tu.
Mimi nadhani ni kutokana na kuwa huko nyuma kutokana na upungufu wa majaji wa mahakama kuu na ile ya rufaa majaji walilazimika kuzunguka mkoa mmoja hadi mwingine kwenda kutoa hukumu.. Yani unakuta jaji anatoka Mbeya kwena Iringa, Mwanza kwenda Shinyanga ili kutoa hukumu hivyo kuwafanya majaji wawe 'non resident magistrates'. Sasa kutokana na mashitaka kuwa mengi na kuchelewa kutolewa hukumu mahakama ikaamua ianzishe mahakama yenye uwezo wa kushughulikia baadhi ya mashauri ambayo sio lazima yashughulikiwe na majaji ndio wakaamua kuwe na hakimu wa kudumu wa eneo husika atayesikilisha mashauri madogo madogo na yale makubwa yangemsubiri jaji, Huyo hakimu wa kukaa eneo hilo nadhani ndio wakaamua wampe jina la resident magistrates yanii hakimu anakaa eneo lake la kazi hivyo kuwa hakimu mkazi.
 
Hili swali linapaswa kujibiwa na mtu yeyote aliyesoma Civics Form Two na kuendelea. Kabla yakukujibu naomba kujua wewe umefikia level ipi ya elimu? Kama umevuka form two basi kuna shida kwenye mfumo wa elimu yetu.
Mi nilpata A civics form 2 na 4 lakini sijui kwanini inaitwa hivyo sababu nilkuwa napenda masomo ya sayans hasa pcm..ukisema hivyo inamaana hata mimi nikimfata lawyer nikamuuliza kwanini gari ikifunga breki unasukumwa mbele akishindwa nimwambie kuna tatizo kwenye elimu yetu...jibu kama unajua kwanini hakimu mkazi kisutu?
 
Hakuna kitu kama mahakama ya mkoa kwenye mfumo wa sheria zetu. Mfumo wa mahakama unaanzia 1. Mahakama ya Mwanzo. 2. Mahakama ya Wilaya. 3.Mahakama ya Hakimu Mkazi. 4.Mahakama Kuu, na 4. Mahakama ya Rufaa.
Mahakama ya mafisadi ipo wapi hapo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mi nilpata A civics form 2 na 4 lakini sijui kwanini inaitwa hivyo sababu nilkuwa napenda masomo ya sayans hasa pcm..ukisema hivyo inamaana hata mimi nikimfata lawyer nikamuuliza kwanini gari ikifunga breki unasukumwa mbele akishindwa nimwambie kuna tatizo kwenye elimu yetu...jibu kama unajua kwanini hakimu mkazi kisutu?
Hata haihitaji kusomea sheria. Sisi tulifundishwa Form Two habari za mihimili ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.
Mfumo wa mahakama Tanzania wa Tanzania Bara unaanzia Mahakama ya Mwanzo. Hii ni mahakama ya ngazi ya chini. Inaweza kughukulika na mashauri ya kisheria kwenye kata au tarafa. Mashauri ambayo thamani yake haizidi elfu 50.(Japo busara pia inatumika). Hakimu wake anaitwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo au PCM kwa maana ya Primary Court Magistrate.
Mahakama inayofuata ni Mahakama ya Wilaya. Hii mahakama unspoken rufaa kutoka mahakama za mwanzo ndani ya Wilaya husika. Pia hupokea mashauri ambayo yanathamani zaidi ya shilingi elfu hamsini yasiyozidi laki mbili na nusu. Hakimu wake anaitwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya lazima awe walau na degree ya Sheria.
Mahakama ya Hakimu Mkazi inafuatia. Hii mahakama imepewa hadhi juu kidogo ya Mhakama ya Wilaya na inaweza kuthikiliza kesi ambazo thamani yake inazidi kidogo kiwango cha zile za wilaya. Hushughulikia mashauri ya ndani ya mkoa au Kanda. Hakimu wake anaitwa Hakimu Mkazi (idadi yao inategemea na mahitaji). Mara nyingi inaongezewa jina la mahali ilipo.
Mahakama inayofuata ni Mahakama Kuu. Hii inapokea rufaa kutoka Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi. Pia hushughulikia mashauri ya jinai kubwa kama mauaji au kesi ambazo thamani yake ni kuanzia laki tano (busara). Mahakama kuu ni moja japo inafanya kazi kwa kanda. Hivyo haijalishi kosa lilopotendeka ila popote ndani ya Tanzania Bara shauri linaweza kufunguliwa. Kiongozi wa Mahakama hii anaitwa Jaji na anateuliwa na Rais.
Mahakama ya juu kabisa ni Mahakama ya Rufaa kwa Tanzania Bara. Kiongozi wa Mahakama hii ni Jaji Mkuu. Nayo inashughulikia rufaa kutoka Mahakama Kuu.
Huo ndiyo mfumo wa Mahakama ya Tanzania Bara. Kwa upande wa Zanzibar wao mfumo ni Tofauti kidogo japo. Hiyo ni knowledge ya Form Two.
 
mkuu unaonekana ulikua mchoyo sana wa material ya kusoma wakati upo shule....
Kwa nini unafikiri hivyo? Bahati nzuri sikuwa na material binafsi zaidi ya vitabu vya shule. Past papers nilikuwa naletewa kuwasolvia maswali.
 
Hata haihitaji kusomea sheria. Sisi tulifundishwa Form Two habari za mihimili ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.
Mfumo wa mahakama Tanzania wa Tanzania Bara unaanzia Mahakama ya Mwanzo. Hii ni mahakama ya ngazi ya chini. Inaweza kughukulika na mashauri ya kisheria kwenye kata au tarafa. Mashauri ambayo thamani yake haizidi elfu 50.(Japo busara pia inatumika). Hakimu wake anaitwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo au PCM kwa maana ya Primary Court Magistrate.
Mahakama inayofuata ni Mahakama ya Wilaya. Hii mahakama unspoken rufaa kutoka mahakama za mwanzo ndani ya Wilaya husika. Pia hupokea mashauri ambayo yanathamani zaidi ya shilingi elfu hamsini yasiyozidi laki mbili na nusu. Hakimu wake anaitwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya lazima awe walau na degree ya Sheria.
Mahakama ya Hakimu Mkazi inafuatia. Hii mahakama imepewa hadhi juu kidogo ya Mhakama ya Wilaya na inaweza kuthikiliza kesi ambazo thamani yake inazidi kidogo kiwango cha zile za wilaya. Hushughulikia mashauri ya ndani ya mkoa au Kanda. Hakimu wake anaitwa Hakimu Mkazi (idadi yao inategemea na mahitaji). Mara nyingi inaongezewa jina la mahali ilipo.
Mahakama inayofuata ni Mahakama Kuu. Hii inapokea rufaa kutoka Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi. Pia hushughulikia mashauri ya jinai kubwa kama mauaji au kesi ambazo thamani yake ni kuanzia laki tano (busara). Mahakama kuu ni moja japo inafanya kazi kwa kanda. Hivyo haijalishi kosa lilopotendeka ila popote ndani ya Tanzania Bara shauri linaweza kufunguliwa. Kiongozi wa Mahakama hii anaitwa Jaji na anateuliwa na Rais.
Mahakama ya juu kabisa ni Mahakama ya Rufaa kwa Tanzania Bara. Kiongozi wa Mahakama hii ni Jaji Mkuu. Nayo inashughulikia rufaa kutoka Mahakama Kuu.
Huo ndiyo mfumo wa Mahakama ya Tanzania Bara. Kwa upande wa Zanzibar wao mfumo ni Tofauti kidogo japo. Hiyo ni knowledge ya Form Two.
Huu uelewa unatakiwa u-update mkuu.

Sheria ishafanyiwa mabadiliko siku nyingi.

Siku hizi kuna Mahakimu wenye Shahada ya Sheria wapo hata kwenye Mahakama za Mwanzo.

Pia thamani ya kusikiliza kesi za Madai Mahakama za mwanzo imepanda mpaka milioni 20 au 30 hivi. Hivyo hivyo kuna mabadiliko kwenye Mahakama ya Wilaya pia.

Kwa hiyo update knowledge yako mkuu.
 
Nilikuwa nauliza kuhusu ile mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, hivi mpaka inaitwa jina hilo hivi huyo Hakimu ni mwenyeji /mkazi wa maeneo hayo au kuna sababu nyingine?
Ni ngazi ya kimahakama katika mfumo wa mahakama za Tanzania kutoka chini kama ifuatavyo,Mabaraza ya usuruhishi,mahakama ya mwanzo,mahakama ya wilaya ,mahakama ya hakimu mkazi,mahakama kuu na juu kabisa mahakama ya rufaa au rufani.Mahakama ya hakimu mkazi ni mahakama kama ya wilaya ambayo imekasimiwa madaraka ya kuendesha kesi ambaxo zingepaswa kuendeshwa na mahakama kuu.Hakmu mkuu mkazi anaitwa principal magistrate.
 
Hawa jamaa wana kihede hede.. Wanazikimbilia kesi alafu utasikia wanalalmika kuwa hawana uwezo wa kuzisikiliza.. If so kwa nini hizo kesi zisianzie mahakama kuu moja kwa moja ili mshitaki na mshitakiwa wapewe haki yao upesi? A law reform is needed here.
Ni utaratibu wa kisheria mkuu Commital proceeding ni lazima kesi itajwe pale kosa lilipofanyika hata kama mahakama haina mamlaka ya kuisikiliza.Unaiandaa kesi na kumuandaa mtuhumiwa ili kesi sasa ipelekwe kwenye competent court.
 
Hawa jamaa wana kihede hede.. Wanazikimbilia kesi alafu utasikia wanalalmika kuwa hawana uwezo wa kuzisikiliza.. If so kwa nini hizo kesi zisianzie mahakama kuu moja kwa moja ili mshitaki na mshitakiwa wapewe haki yao upesi? A law reform is needed here.
Ni utaratibu wa kisheria
 
Yule hakimu wake anaishi ndani ya jengo hilo la mahakama,
ndo maana inaitwa mahakama ya makazi kisutu,
yaani mahakama ya hakimu mkaaji wa mule mule ndani ya mahakama ya kisutu
 
Huu uelewa unatakiwa u-update mkuu.

Sheria ishafanyiwa mabadiliko siku nyingi.

Siku hizi kuna Mahakimu wenye Shahada ya Sheria hata kwenye Mahakama za Mwanzo.

Pia thamani ya kusikiliza kesi za Madai Mahakama za mwanzo imepanda mpaka milioni 20 au 30 hivi. Hivyo hivyo kuna mabadiliko kwenye Mahakama ya Wilaya pia.

Kwa hiyo update knowledge yako mkuu.
Hiyo ilikuwa Form Two Mkuu miaka hiyo.
 
Back
Top Bottom