Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,832
- 2,790
Leo asubuhi nimeteremka kituo cha Palm Beach, nikatoa nauli yangu kwa konda Tsh 2000/= Wakati nikisubiri change mbele yangu nawaona watu wawili wakiniangalia sana. Nikapokea change yangu na wakati nikiiweka mfukoni mmoja wao ananisemesha Nipe mia tano ya gazeti, kisha "Habari yako, za siku nyingi huku akinipa mkono. Nikampa mkono. Akaendelea kuniuliza "Vipi uko makao?" Wakati akiniuliza kama niko makao huku kanishikilia mkono ghafla nilianza kusikia kizunguzungu na kusikia kichefu chefu, nikajihisi akili zinaanza kama kuniruka. Hakika nilichofanya ni kutoka mbio nikiwa hoi ndani ya sekunde. Jamani nadhani itafika muda hatutasalimiana kwa kupeana mikono. Haya yamenikuta leo asubuhi.