Hakika Tuache Kupeana Mikono Tunaposalimiana-Yamenikuta

mweeeeeeeeeee......mtoa mada ushantisha sasa...daaah...binadamu wa sikuhzi sijui wanaelekea wapi...hawakukuibia kitu kweli?ukute ndo njia yao mpya ya kuiba........???pole sana aiseee...
 
Kwanza pole kwa msukosuko huo ndugu yetu. Hata mimi juzi nilikua Iringa na rafiki yangu, tukawa tunatoka mitaa ya sokoni kuelekea stendi ya mabasi, mara ghafla wakatokea vijana watatu wakaonekana kumfaham sana rafiki yangu maana walianza kumchangamkia sana kwa maswali mengi.
Ikabidi nimsubiri na badae nikaona kama muda unaenda nikaamua kumstua.
Asalaalee! Kumbe walikua washampumbaza akawa kama haelewi kinachotokea ila wale vijana wakaanza kunilalamikia kua nampeleka wapi jamaa yao (yaani yule rafiki yangu).
Kuepusha mengi nikampeleka pemben nikamuuliza kilichompata akasema hakumbuki ila bahati nzuri hawakumwibia.
Kwa kweli tuwe makini sana kwa sasa kuna wizi kwa njia ya kupumbaza.
 
Bahati yako we Bubu Msemaovyo inavyoonekana UMEAGA KWENU vizuri ndo maana ukaanza kusikia kizunguzungu la sivyo wangekwapua hadi nauli. Pole mkuu ila huo wezi upo sana, kuna mmama alinijaribu na mimi kwenye ATM za pale Ubungo sheli akaambulia patupu na makofi nikamchapa
 
Last edited by a moderator:
kuna mahali huyo jamaa alikosea katika mtiririko ukagutuka....hypnotization ilitaka kufanyika...pole
Ebu tufafanulie mkuu, isije ikawa tukawa tunaogopa kusalimina na waku tikihisi wanchokifanya ni "hypotization"... binafsi sieliwi hiyo hypnotization ikojeikoje?
 
Pole sana Bubu Msemahovyo!!! Nataka na wengine wajue kuwa hata siku moja usikubali eti mtu anakusimamisha anakuuliza maswali, wengi wao ni kama hao uliokutana nao leo. Huwa natoka baru tu, siangalii wala sisikii maana Tz imeharibika sasa!! Nilikutana na binti mmoja maeneo ya fulani Dar analia sana nikamuuliza kulikoni akasema alikutana na watu wakamsemesha mwishowe akatoa kila kitu. Kwa hiyo alikuwa analilia simu yake.

Ili ujue kuwa mambo yameharibika zaidi ya ulivyosema, basi asilimia kubwa ya mabinti siku hizi huwa wanapiga ukunga wa uongo barabarani hukuwakijifanya wametapeliwa kwa mbinu hiyo hapo juu na kuhitaji msaada. Asilimia kubwa ni waongo pasee
 
Wanasalimianaje wao?

hawapeani mikono, bali wanainamisha vichwa tu wakiwa umbali wa kama mita moja kutoka kwa mmoja, au nayo wahuni hawa watatafuta namna ya kupumbaza watu??
 
Kwanza pole kwa msukosuko huo ndugu yetu. Hata mimi juzi nilikua Iringa na rafiki yangu, tukawa tunatoka mitaa ya sokoni kuelekea stendi ya mabasi, mara ghafla wakatokea vijana watatu wakaonekana kumfaham sana rafiki yangu maana walianza kumchangamkia sana kwa maswali mengi.
Ikabidi nimsubiri na badae nikaona kama muda unaenda nikaamua kumstua.
Asalaalee! Kumbe walikua washampumbaza akawa kama haelewi kinachotokea ila wale vijana wakaanza kunilalamikia kua nampeleka wapi jamaa yao (yaani yule rafiki yangu).
Kuepusha mengi nikampeleka pemben nikamuuliza kilichompata akasema hakumbuki ila bahati nzuri hawakumwibia.
Kwa kweli tuwe makini sana kwa sasa kuna wizi kwa njia ya kupumbaza.

Hata Iringa Mjini! Nilizani ni jiji DSM tu, Mungu unilinde na hao matapeli, kwa kuwa ni mungwana kwa watu wenye shida.
 
Tafuta the science of hypnosis au kama una rafiki daktari umuulize kuhusu hypnosis kwenye psychiatry then you will realise that at times you do not know everything. By the way, uchawi na mambo mengine spiritual huwa science haiwezi sana kuyaeleza ila pia science cannot refute them so be cautious when uttering matters in public.

mkuu arinaswi nakushukuru kwa namna ulivyomweleza huyo jamaa, mie kaniudhi hadi nikakosa subra,big up
 
Last edited by a moderator:
Leo asubuhi nimeteremka kituo cha Palm Beach, nikatoa nauli yangu kwa konda Tsh 2000/= Wakati nikisubiri change mbele yangu nawaona watu wawili wakiniangalia sana. Nikapokea change yangu na wakati nikiiweka mfukoni mmoja wao ananisemesha Nipe mia tano ya gazeti, kisha "Habari yako, za siku nyingi huku akinipa mkono. Nikampa mkono. Akaendelea kuniuliza "Vipi uko makao?" Wakati akiniuliza kama niko makao huku kanishikilia mkono ghafla nilianza kusikia kizunguzungu na kusikia kichefu chefu, nikajihisi akili zinaanza kama kuniruka. Hakika nilichofanya ni kutoka mbio nikiwa hoi ndani ya sekunde. Jamani nadhani itafika muda hatutasalimiana kwa kupeana mikono. Haya yamenikuta leo asubuhi.

Pole sana, lakini baada ya kukimbia hali yako iliendeleaje, I mean ilikuchukua muda gani akili kurudi kawaida?
 
Hata Iringa Mjini! Nilizani ni jiji DSM tu, Mungu unilinde na hao matapeli, kwa kuwa ni mungwana kwa watu wenye shida.

Brother, siyo Iringa na Dar peke yake bali hata Mwanza wapo maana walinikosakosa siku moja.
 
Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom