Haki ya nani ogopa kitu inaitwa "KUFUMANIWA"

Nyetk

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,648
1,696
Nilikuwa na timu ya wenzangu kikazi mikoa ya kusini - Lindi na Mtwara kwa siku mbili, sasa tukiwa tunarejea Dar usiku wa kuamkia tarehe 3 August 2012 tuliingia Dar tumechelewa kidogo (kama majira ya saa tano hivi usiku). Wenzangu wakapendekeza kuegeshe mahali fula tupate chakula kabisa kabla gari haijatusambaza kila mtu kwake. "Good idea!", wote tuliunga mkono. Hapo tulishaingia mitaa ya Keko, na mwenzetu mmoja mwenyeji wa mitaa hiyo akatuongoza hadi "National Hotel".

Wow! tukakuta kikundi cha promotion ya bia ya "Windhoek" wakiwa jukwaani. tukakaa, tukaagiza chakula. Meza ya jirani yetu palikuwepo watu watatu: wanaume wawili na kabinti kamoja, na mmoja wao alionekana anatawala meza kwa jinsi alivyokuwa anazimwaga windhock. Mkuu wa meza ndo alionekana anamawasiliano ya karibu na yule binti pekee kwenye meza.

Ghafla akaingia kwa kasi binti/mama mmoja kabeba mtoto mgongoni (anayeonekana si mtoto wa kubebwa na mamaye mgongoni kwa ukubwa wake katika hali ya kawaida), na ndipo picha ikaanza. Akaenda moja kwa moja kwa mkuu wa meza na kumshushia valangati!

"Unafanya nini hapa?" Jamaa kimya, kaduwaa!
"Nakuuliza unafanya nini hapa?" Kamwasha kibao!
"Mbona hunijibu, unafanya nini hapa?" Kibao kingine cha nguvu zaidi; jamaa bado kimya tu. Yule mama akachukua glasi ya pombe ya yule binti aliyemkuta mezani akamwagia mumewe yote. Jama kimya tu utadhani yupo kwenye friji!
"Wewe nakupigia tangu saa kumi na mbili jioni hupokei unajua nakupigia kwa sababu gani? Mbwa wee!" Kibao kingine! Yule rafiki wa mkuu wa meza kaamka, anamtuliza huyo mama.
"Shemeji, huyu anamwaga ofa hapa, ebu muulize nyumbani ameacha hata elfu moja, mbwa huyu?" Kibao kingine - na jamaa amekaa tu kwenye kiti! "Mshenzi mkubwa! Badala ya kuwaza mambo ya maeneleo unakaa kuwaza ujinga tu!" (Hii sentesi ya mwisho aliirudia mara nyingi).

Picha iliendelea kwa muda na wakati wote jamaa yuko kwenye kiti. Huyu mama mtoto pamoja na vurumai zote alionyesha kufanya kwa stara kubwa bila kupiga makelele, ila alikuwa anaongea kwa sauti ya chini bila kuvuruga amani ya wasiohusika (ku-attract attention); hakumtukana wala kumpiga yue binti aliyemkuta na bwana wake (ingawa huyo binti aliepaniki sana), kitu kilichonipa kufikiri kuwa huyu mama mtoto kimsingi si mtu mkorofi kwa asili. Hatimaye yule kijana mwingine akawatuliza na akamudu kuwashawishi wakaondoka wote.

Jina la mfumaniwa halikujulikana ila yule rafiki yake alikuwa anatajwa na mfumaniaji kwa jina la Mwita.

MY TAKE:
Wadau, najua kesi za namna hii na kuzidi ni za kawaida sana kwenye jamii, hata mimi nimeshuhudia senema nzito kuliko hii. Ninachojiuliza ni kwamba, ni nini huwa kinatokea kwa wamaume kisaikolojia wanapokuwa wamefumaniwa hata wakose uwezo wa kujitetea hata kwa ku-act au kudanganya???? Leo nashuhudia rafiki ya "Mwita" anapigwa makofi sita, anamwagiwa pombe na kutukwanwa "mbwa" mara sita, "mshenzi" mara nyingi, "mpumbavu" mara nyingi..... na binti ambaye kwa mwonekano si mmbabe (alikuwa anaonekana mpole sana kwa kweli) na njemba haiwezi hata kujibu kivyovyote?

Najua wanaume wenzangu wengi mmekumbwa na balaa la kufumaniwa; na akinadada/mama wengi mmewafumania/mmewabamba waume zenu na wanaume daima walikuwa wapole. Ebu mwagikeni; ni nini huwa kinawafanya wanaume wawe hivi?
 
Duuuh hiyo story noooma! Kwanza namsifu huyo maama kwa ustarabu alio onesha hasa kwa huyo dada , ingekuwa mwanamke mwingine hapo pange chimbika na huyo dada reception lazima ingegeuzwa garage!

Duuuuuuuh! Huyo baba ametia haibu sana kwenda kutafuta heshima bar wakati home hakuna kitu, ni funzo kwetu!

Linapokuja swala lafumanizi wanaume ujanja huwa tunakosa kabisa, kwanza ujue fumanizi ni kitu cha kushitukiza kwa hiyo lazima uwe mdogo kama piriton sababu huwa ni fedheha na haibu.

Na ukifumaniwa unajiona mdogo kiasi kwamba wa kikwambia ingia kwenye ndoo unaingia,una kuwa mtu wa kufata maelekezo.

Fumanizi nomaaaaa!
 
Mkuu ruttashobolwa you said it all. Wallahi nawambia hakuna fedheha kama kufumaniwa; to be honest mwenzenu yalishan'kuta zamani kabla sijafunga pingu zangu! It is the most humiliating experience ever na hupaji kabisa ujasiri wa kujenga hoja coz akili ina-cease kufanya kazi. Nadhani zile adrenal glands zinatoa hormone inaufanya ubongo usinyae hivyo uwe defenceless! Simshangai huyo jamaa pamoja na kwamba ni rafiki ya "Mwita" akawa so impotent!

It is a very interesting story though, mkuu Nyetk.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ukifumaniwa ni lazima uwe mdogo maana unakuwa huna haki..
Omba uwe na mke mstaarabu, ukiwa na mke mcharuko wee... Utakoma, atafunga mtaa mzima hadi aibu
 
Huyo aliyefumaniwa ameiaibisha jinsia ya kiume.Kawaida mwanaume huwa haonekani kwenye fumanizi watu wanakuta simulizi tu kuwa jamaa alikuwepo hapa na hata hatujui amepoteaje.Mimi nilishafumaniwa na mpenzi wangu miaka hiyo na mbaya zaidi alikuwa ni Sajenti jeshini,alipofika tu cha kwanza ilikuwa ni kuirusha meza na kumwaga vinywaji vyote.Basi kabla hata meza haijafika chini mimi nilikuwa tayari naishilizia mtaa wa pili,bora tukayamalize nyumbani kuliko mbele za watu bana....
 
Tz just ni ukio la kush2kiza mtu hajategemea kwahiyo anapata butwaa..
 
hahahaaaaaaa, heri muabishane mkiwa wenyewe kuliko kutiana aib mbele za watu, kuwapa story lol,
Huyo aliyefumaniwa ameiaibisha jinsia ya kiume.Kawaida mwanaume huwa haonekani kwenye fumanizi watu wanakuta simulizi tu kuwa jamaa alikuwepo hapa na hata hatujui amepoteaje.Mimi nilishafumaniwa na mpenzi wangu miaka hiyo na mbaya zaidi alikuwa ni Sajenti jeshini,alipofika tu cha kwanza ilikuwa ni kuirusha meza na kumwaga vinywaji vyote.Basi kabla hata meza haijafika chini mimi nilikuwa tayari naishilizia mtaa wa pili,bora tukayamalize nyumbani kuliko mbele za watu bana....
 
cha kusikitisha ni kua kaenda na mtoto wake..kwa hiyo hilo varangati mtoto alikua analishuhudia LIVE yaani...its sad
 
Mkuu ruttashobolwa you said it all. Wallahi nawambia hakuna fedheha kama kufumaniwa; to be honest mwenzenu yalishan'kuta zamani kabla sijafunga pingu zangu! It is the most humiliating experience ever na hupaji kabisa ujasiri wa kujenga hoja coz akili ina-cease kufanya kazi. Nadhani zile adrenal glands zinatoa hormone inaufanya ubongo usinyae hivyo uwe defenceless! Simshangai huyo jamaa pamoja na kwamba ni rafiki ya "Mwita" akawa so impotent!

It is a very interesting story though, mkuu Nyetk.

Asante Dr. Naona umeamua kutazama kitaalamu zaidi

Mkuu ukifumaniwa ni lazima uwe mdogo maana unakuwa huna haki..
Omba uwe na mke mstaarabu, ukiwa na mke mcharuko wee... Utakoma, atafunga mtaa mzima hadi aibu

Nakwambia jamaa alikuwa zadi ya mdogo! Anamwagiwa pombe, anatukanwa mbwa lakini anapotezea tu, hahahahaaaa!

Hakuna chochote ila basi tu ndo inakuwa hivyo!

Mkuu hujasomeka kabisa. Yaani unataka kusema kufumaniwa siyo issue?

Huyo aliyefumaniwa ameiaibisha jinsia ya kiume.Kawaida mwanaume huwa haonekani kwenye fumanizi watu wanakuta simulizi tu kuwa jamaa alikuwepo hapa na hata hatujui amepoteaje.Mimi nilishafumaniwa na mpenzi wangu miaka hiyo na mbaya zaidi alikuwa ni Sajenti jeshini,alipofika tu cha kwanza ilikuwa ni kuirusha meza na kumwaga vinywaji vyote.Basi kabla hata meza haijafika chini mimi nilikuwa tayari naishilizia mtaa wa pili,bora tukayamalize nyumbani kuliko mbele za watu bana....

Duh! mkuu haiwezekani, lazima bibi yako alikuwa mchawi! Unathubu kumwibia mjeshi?

Tz just ni ukio la kush2kiza mtu hajategemea kwahiyo anapata butwaa..

Mana'ke ni "thunderbolt!"

Mamndenyi! Nakuvutia pumzi.

Mamndenyi aliwakutaje chumbani na kamera kabisa mukuu? Amenitumia picha moja kabla hamjavaa kabisa!

cha kusikitisha ni kua kaenda na mtoto wake..kwa hiyo hilo varangati mtoto alikua analishuhudia LIVE yaani...its sad

Afu toto lilikuwa linaonekana kubwa tu, kama miaka miine-mitano. Muda wote wa valangati lilikuwa linavunga limelala mgongoni mwa ***** coz halikutoa kichwa nje. Usikute walipanga na ***** si unajua tena sanaa ya kujaribu kupata sympathy ya watu?
 
yasikie kwa mwenzio jaribu na wewe u "prove" ujue kinatokeaga nin!
 
Mi nikifumania nitamcheka tu mwenza wangu na kumuuliza ujanja woote ndo akili yako imeishia hapa? Nitaondoka na kumuacha hapo akishangaa, naenda kumsubiria home.

Nikifumaniwa, yaani kama imefika hatua ya ku-cheat ina maana its over! Tunapeana talaka ya mdomo hapo hapo, nguo watanichukulia wapambe.
 
Kama ni mwana ume unaye mpenda kweli huwezi kucheka lazima ukasirike. Na utakacho kifanya ni vigumu kutuambia kwani utashangaa umefanya!

Si mchezo!
Mi nikifumania nitamcheka tu mwenza wangu na kumuuliza ujanja woote ndo akili yako imeishia hapa? Nitaondoka na kumuacha hapo akishangaa, naenda kumsubiria home.

Nikifumaniwa, yaani kama imefika hatua ya ku-cheat ina maana its over! Tunapeana talaka ya mdomo hapo hapo, nguo watanichukulia wapambe.
 
Sijawahi kupata hiyo kasheshe. Nimekuwa mpenzi wa program ya DSTV inaitwa Zone Reality - Cheaters! Nimeona jinsi gani temperature nifikia lethal! Usiombee kufumania au kufumaniwa! Nomaaa
 
Back
Top Bottom