Haki ya nani kwa walichonifanyia NECTA kwenye matokeo yangu ya Form VI siwezi kuwasahau

Rajab_Omar

JF-Expert Member
May 15, 2016
16,475
27,168
Nashindwa hata kusalimia Wajumbe

Mwaka 2018 nikiwa nimetulia Naandalia Kideo ghafla napigiwa Simu na Classmate wangu ananiambia Mgodi umeshatema ingia Mtandaoni uangalie matoleo, Jinsi nilivyokuwa najiamini nilimjibu kuwa Mimi siingii Mtandaoni kuangalia Matokeo bali ninaingia kuconfirm Matokeo kwani Matokeo yangu ninayajua.

Baada ya kuingia Mtandaoni nilijikuta naangusha kicheko tu baada ya kujiona nimeigegeda One ya XIV O-Level nilijiona kweli mimi najua. Nimeingia A-Level kwa mbwembwe kama zote nikijiona wazi kuwa ninakwenda kupiga Kijiti chengine.

Nilisoma sana usiku na mchana lakini cha ajabu leo naingia kwenye Mfumo kuangalia Matokeo yangu ya Kidato cha Sita nilichoona sikuweza kuamini! Yani nimezungusha kama sijawahi kusoma.
Mimi si wakupata Sifuri.

Kila nikikumbuka kujaza Fomu ya Mkopo kwa mbwembwe na kuipeleka Posta nikiwa najiamini kwa PCM yangu niliamini kwa 100% kuwa Mkopo nitapewa! Lakini mambo hayapohivyo, Nimekula Zero na hela ya kuhangaikia Mkopo imeliwa.

Kwa nilivyosoma NECTA walipaswa kunipa angalai D D D na sio FFF zote.
 
Dah, pole mku kubaliana na hali tu maana still bado una nafasi ya kusonga mbele ,una uwezo wa kwenda ku apply diploma kwa kutumia chet cha 4m4 na chuo utafika, maana wapo watu weng wamepotia njia hii wapo makazin
 
Ilitakiwa ulipomaliza form four na grade nzuri usingepoteza mda kusoma A-level. Ungechukua zako diploma ya kozi yeyote unyoipenda, sasaiv ungekuwa unamalizia na kupata fursa ya kusoma degree. Ona Sasa umepiga bashite la PCM
 
Muda wote uko jukwaa la Liverpool special na kurandaranda kwenye thread ya Manchester united ulitegemea ufaulu Form VI tena PCM???

Pole sana dogo nitafute kuna kitu chamsingi nikwambie
 
dah,pole mku kubaliana na hali tu maana still bado una nafasi ya kusonga mbele ,una uwezo wa kwenda ku apply diploma kwa kutumia chet cha 4m4 na chuo utafika,maana wapo watu weng wamepotia njia hii wapo makazin

Kwa Matokeo haya nahisi kama Mungu ananiambia Wewe Kenge pambana na Mambo mengine kusoma sio Fani yako waachie wasomaji 😭
 
Ilitakiwa ulipomaliza form four na grade nzuri usingepoteza mda kusoma A-level. Ungechukua zako diploma ya kozi yeyote unyoipenda, sasaiv ungekuwa unamalizia na kupata fursa ya kusoma degree. Ona Sasa umepiga bashite la PCM

Si nilijiona Kipanga nikahisi A-Level nitateremka Kitonga tu! Kumbe O-Level nilibahatisha 😭
 
Muda wote uko jukwaa la Liverpool special na kurandaranda kwenye thread ya Manchester united ulitegemea ufaulu Form VI tena PCM???

Pole sana dogo nitafute kuna kitu chamsingi nikwambie

Nyumbu wacha Roho mbaya 😭
 
Back
Top Bottom