Haki ya nani kwa walichonifanyia NECTA kwenye matokeo yangu ya Form VI siwezi kuwasahau

Ilitakiwa ulipomaliza form four na grade nzuri usingepoteza mda kusoma A-level. Ungechukua zako diploma ya kozi yeyote unyoipenda, sasaiv ungekuwa unamalizia na kupata fursa ya kusoma degree. Ona Sasa umepiga bashite la PCM
Vilaza weng wanaiogopa A level...tutembee kifua mbele sis tulioipasuaga na moja zetu
 
Aliyezungusha kweli na akawa na uchungu wa kuzungusha angekuwa kajifungia analia. Hongera kwa kufaulu
Hahahah yani kapost kwambwebwe kabisa
matokeo yangu yalivotoka sikuzungusha lakin ilikua nimsiba mzito, nakumbuka kesho yake niliamua kutoka matembez kubadilisha mawazo nilivorudi nilikuta nyumbanzima wameenda kunitafuta sababu ya hofu kua ntakua nimeenda kujinyonga
 
Vilaza weng wanaiogopa A level...tutembee kifua mbele sis tulioipasuaga na moja zetu

Acha sifa! Walio na ONE kama wewe wameajiriwa na Diamond Platnumz aliyeishia la Saba B.

Walio na ONE wakasoma PhD zao marekani wameajiriwa na Bakhressa ambaye hata historia ya kusoma kwake haijuilikani 😭😭
 
Ilitakiwa ulipomaliza form four na grade nzuri usingepoteza mda kusoma A-level. Ungechukua zako diploma ya kozi yeyote unyoipenda, sasaiv ungekuwa unamalizia na kupata fursa ya kusoma degree. Ona Sasa umepiga bashite la PCM
Nimecheka kama mazuri vile et bashite la PCM watu mna mambo 😅
 
Nashindwa hata kusalimia Wajumbe!

Mwaka 2018 nikiwa nimetulia Naandalia Kideo ghafla napigiwa Simu na Classmate wangu ananiambia Mgodi umeshatema ingia Mtandaoni uangalie matoleo, Jinsi nilivyokuwa najiamini nilimjibu kuwa Mimi siingii Mtandaoni kuangalia Matokeo bali ninaingia kuconfirm Matokeo kwani Matokeo yangu ninayajua.

Baada ya kuingia Mtandaoni nilijikuta naangusha kicheko tu baada ya kujiona nimeigegeda One ya XIV O-Level nilijiona kweli mimi najua.
Nimeingia A-Level kwa mbwembwe kama zote nikijiona wazi kuwa ninakwenda kupiga Kijiti chengine.
Nilisoma sana usiku na mchana lakini cha ajabu leo naingia kwenye Mfumo kuangalia Matokeo yangu ya Kidato cha Sita nilichoona sikuweza kuamini! Yani nimezungusha kama sijawahi kusoma.
Mimi si wakupata Sifuri.

Kila nikikumbuka kujaza Fomu ya Mkopo kwa mbwembwe na kuipeleka Posta nikiwa najiamini kwa PCM yangu niliamini kwa 100% kuwa Mkopo nitapewa! Lakini mambo hayapohivyo, Nimekula Zero na hela ya kuhangaikia Mkopo imeliwa.

Kwa nilivyosoma NECTA walipaswa kunipa angalai D D D na sio FFF zote.
Umejiunga JF 2016,ulikuwa form two!!!!!
Hii chai
 
Mi mwenyewe nimefeli kabla ya exam nilitukana sana watu Kama mmi ndo genius full mbwembwe matokeo yameniumbua leo naona Aibu kutoka nje mdomo umeniponza
 
Mi mwenyewe nimefeli kabla ya exam nilitukana sana watu Kama mmi ndo genius full mbwembwe matokeo yameniumbua leo naona Aibu kutoka nje mdomo umeniponza

Yani toka saa 5 mchana leo nimekomaa na TV naangalia LFCTV sijatoka nje kwa stress
 
Back
Top Bottom