Haki wanayoitaka Watanzania ni Maji safi na salama, Huduma bora za afya, miundombinu ya barabara, Elimu ya uhakika,na usalama wa Chakula

Nigrastratatract

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
865
1,000
Ukiwa Genius lazima ugundue kuwa watanzania wanataka huduma bora za afya, maji safi na salama, elimu bora, miundombinu imara ya uhakika tofauti na hapo tusidanganyane

Demokrasia wakati nina njaa ni kunitapeli

Demokrasia wakati sijahudumiwa vizuri hospitali ni kunipaka pipi mdomoni

wananchi tunataka Mapambano dhidi ya Rushwa wizi wa mali za umma na ufisadi yaendelee maana haya yanadhorotesha misingi ya utawala bora
.Wanasiasa wasipoamini katika misingi ya kuwahudumia na kuwatumikia wananchi na kufuja mali za umma wataliangamiza Taifa
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,816
2,000
Kuna watu wana njaa na wanakaliwa na madikteta. Uchague kati ya maisha kama ya Korea Kaskazini au Demokrasia na njaa.
 
Jun 8, 2018
63
150
Inaonekana mama akizungumzia democracy unaumia sana. Kazi unayo baba. Never and never again should a nation go back to............

Malizia mwenyewe bwana usijifanye hujui.😄😄😄😄
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,725
2,000
..ni aibu kwamba miaka 59 tangu tupate uhuru bado kuna Watz hawajapata haki ya msingi kama kupata maji safi na salama.
 

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
5,183
2,000
Kweli kabisa, hayo ndiyo mahitaji halisi ya watanzania. Kushogeshwa ni hitaji binafsi la wanasiasa uchwara kama lisu.
 

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
556
1,000
Wafungwa Marekani wanapata yote unayoyasema lakini hawana uhuru kwa sababu ni wafungwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom