Ukosefu wa umeme na maji ya uhakika. Tujitafakari, tujiongeze kitaalamu

Nov 6, 2016
52
141
UKOSEFU WA UMEME NA MAJI KATIKA DUNIA YA SASA YENYE TEKNOLOJIA LUKUKI, TUJITAFAKARI VIZURI

Na Comrade Ally Maftah

Nawapongeza sana viongozi wote wasaidizi wa Dr Samia kwa jitihada mbalimbali za kuimarisha ustawi wa Taifa letu,

Rai yangu kuhusu ukatikaji wa umeme na maji ni kwamba wahusika waongeze nguvu zaidi katika kufikiria njia mbadala za uzalishaji wa huduma hizi muhimu kwa uchumi na ustawi wa Taifa kwa kushirikisha wajuzi wa Teknolojia.

Kuna uwezekano kwamba upungufu wa umeme na maji unatokana na uzalishaji duni wa huduma hizi, upotevu wa nishati/ mali katika usambazaji, njia duni za usambazaji uharibifu wa miundombinu ya uzalishaji na usambzazi wa huduma hizi.

NAWASHAURI VIONGOZI WETU

1. Tuongeze ubunifu katika uzalishaji wa huduma hizi kwa kutumia teknolojia endelevu, tusiogope kuiga kutoka kwa wenzetu walio mbali kwenye utoaji wa hizi huduma mfano -: walioweza kubadili maji ya baharini kuwa maji safi, walioweza kubadili maji ya chooni kuwa maji safi.

Tupunguze uwezekano wa upotevu wa mali hizi kabla hazijawafikia wateja -: Mipango ya ujenzi wa nchi yetu iendane, tutapunguza uwezekano wa uharibufu wa miundombinu hii pindi tunapotengeneza miundombinu mipya

2. Tuwadhibiti wahujumu na waharibifu wa miundombinu na mali katika sekta hii-: kuna watu wanahujumu hii miundombinu na mipango kwa maslai yao wenyewe. hawa watu wapo kuanzia ngazi za chini mpaka juu zaidi na mbaya zaidi kuna kundi la wanufaika pia nao ni wahujumu alafu wao ndio wa kwanza kulalamika.

3. Tumuunge mkono Dr Samia kwa vitendo, Tusimuhujumu Rais wetu mwenye mapenzi makubwa sana na Taifa letu.

Ndimi Comrade Ally Maftah
IMG-20240209-WA0000.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom