Haki sawa

Haki sawa

Hpn nae amezidi ss akiwa na familia nyumba itaoza au anakujaribu ili adeke jaman kwa mme

Nami nikafikiri hivyo, wapo wawili tu kazi ndogo ndogo zimemshinda, vipi familia ikiongezeka, ataweza kweli. Nakuwa na wasiwasi, baadhi ya malezi wanayopewa baadhi ya dada zetu si mazuri, hawafundishwi maisha, bali tamthilia tu.
 
Malez pia yanachangia wazaz wetu walikuwa wanajituma sana na kulikuwa zamani hakuna wafanyakaz na wazee wa zamani walikuwa wanazaa sana na shamba wanaenda
 
Wanawake wa siku hizi ni hatari tupu.

Jana nimenuniwa mwenzenu.

Kisa eti alikuwa busy na sikumsaidia.Cha kushangaza ni kuwa kulikuwa na shughuli mbili;
1. Kuosha sufuria 3, sahani 2, bakuli 1, mwiko, upawa na vijiko.

2. Kwenda kununua nyama buchani umbali wa m.150 toka nyumbani kwetu.
Nikamwambia zote zake.

Kanuna mpaka Leo.
Hahahahaaaaa.....
Wajibu wa Mke ni nini? Dada zangu haki sawa zinawapeleka kombo.

Kuweni makini.

Umemzoesha ,wenzio tunafanyiwa na vya ziada.Kama kweli anakupenda atafanya majukumu yake bila kukununia
 
Juzi ilikuwa pasaka jamani, hapakuwa na ofisi wala chochote. Kupika kg. 1 ya mchele na nusu ya nyama inahitaji kusaidiwa??? Mazingira ya kusaudiwa yako wazi kbs na hayana utata. Wewe unachotetea ktk scenario hii ni nini hasa? Mrsleo.

Unajua wale watu wanaosema mtu ajitambue kwanza ili aweze kujua ataoa/kuolewa na mwenza wa aina gani hawakukosea. Kama umelelewa kwa mfumo wa kupika na kuosha vyombo ni kazi za mwanamke na ni dharau kwa mwanaume ulitakiwa uoe mke mwenye itikadi hiyo. Lakini kama dhana nzima ya ndoa ni kusaidiana sioni kwa nini ukatae kwenda buchani wakati mwenzio anafanya kazi zingine. Kwanza ukitemebelea bucha nyingi hapa tz wateja wengi ni wanaume. Baba ndiye anapeleka kitoweo nyumbani, mama anapika. Lakini wewe kwa kuwa ni mkeo alikutaka uende buchani ukaona unadhalilishwa kwa kuwa unamchukulia ni wa hadhi ya chini na wewe wa hadhi ya juu.

Kama siku zote huwa anafanya hizo kazi bila malalamiko ila siku hiyo moja alikutaka umsaidie na akanuna hukutakiwa kuja JF kutuonya wanawake bali ulitakiwa uje kuomba msaada wa kuelimishwa kuhusu hiyo hali na namna ya kuboresha mahusiano yako na mkeo. Sasa muache aendelee kununa na wewe uendelee kulaumu haki sawa na kutunisha msuli uone utakavyokuwa na ndoa nzuri.

Wanaume wanaoona wamezidiwa au hawapendi kufanya kazi za nyumbani huwa hawaoi, wanaajiri wasaidizi kwa makubaliano ya kuja asubuhi na kuondoka jioni, au kuja mara 2 kwa wiki au kukaa hapo hapo nyumbani. Mwanaume anayeoa kwa sababu hii ni sawa na mwanamke anayeolewa ili kutafuta nafuu ya maisha. Matarajio yao yasipofikiwa ndoa inaanza kuyumba.

Kumsaidia mwenzio hasa mke shughuli zake za nyumbani ni njia ya kuonyesha upendo na kujali tu wala haina uhusiano na haki sawa. Kibinadamu tu haileti picha nzuri mwenzi wako tena siku ya mapumziko anahangaika na kazi za nyumbani we umelala au unaangalia tv au uko busy na JF na mitandao mingine ya kijamii.
 
I love you ICHANA. Well said.

Umeona ee? Humu kuna wanawake na wanaume wanaokuunga mkono na wanaokupinga. Sasa tofauti hii ya mitazamo ndo ilitakiwa ikupe picha ulitakiwa kuoa mwanamke mwenye mtazamo upi na si kutaka kuchukua samaki aliyekauka ukamkunje. Badala ya kufuarahia maisha ya ndoa mnatumia robo 3 ya umri wa ndoa kuvutana kuhusu tabia. Ukipata wa kufanana nae kuna nafuu flani hivi.
 
kazi gani hizo za kukosa kupumzika au uchoke asubuhi hivyo? Tena wako wawili zao, loh. Tusitetee tu, mara nyengine tunazidi.

Kama mwanamke hawezi kuchoka asubuhi tena wakiwa wawili tu na mumewe basi ina maana si kawaida. Hivyo hatutakiwi kumhukumu bila kujaribu kujua ni nini kilijiri ndani yake. Inawezekana kwa sababu za kibaolojia alikuwa off-mood, au jana yake alichoka na bado akaamka na uchovu, au alijihisi kupungukiwa na upendo wa mumewe akawa anataka assurance au attention. Wengi wetu hatupendi kuchukua muda kutafakari mienendo ya wenzetu. Tunakuwa tu wepesi kuokota mawe na kuanza kuwapiga!!
 
Hoja zako zimejibiwa ktk comments zako. Asante kushiriki.
 
Umeona ee? Humu kuna wanawake na wanaume wanaokuunga mkono na wanaokupinga. Sasa tofauti hii ya mitazamo ndo ilitakiwa ikupe picha ulitakiwa kuoa mwanamke mwenye mtazamo upi na si kutaka kuchukua samaki aliyekauka ukamkunje. Badala ya kufuarahia maisha ya ndoa mnatumia robo 3 ya umri wa ndoa kuvutana kuhusu tabia. Ukipata wa kufanana nae kuna nafuu flani hivi.

Nothing is perfect my dear. Inawezekana anayesapot akawa na blind spot nyingine kubwa tuu. Niliyazingatia yote ya msingi kuoa na wala sijuti. Uvumilivu, maongezi na kupendana na msingi wa maisha bora.
 
Kama mwanamke hawezi kuchoka asubuhi tena wakiwa wawili tu na mumewe basi ina maana si kawaida. Hivyo hatutakiwi kumhukumu bila kujaribu kujua ni nini kilijiri ndani yake. Inawezekana kwa sababu za kibaolojia alikuwa off-mood, au jana yake alichoka na bado akaamka na uchovu, au alijihisi kupungukiwa na upendo wa mumewe akawa anataka assurance au attention. Wengi wetu hatupendi kuchukua muda kutafakari mienendo ya wenzetu. Tunakuwa tu wepesi kuokota mawe na kuanza kuwapiga!!

U r very positive towards the women's perfection. Think of the other side of the coin.
 
Nothing is perfect my dear. Inawezekana anayesapot akawa na blind spot nyingine kubwa tuu. Niliyazingatia yote ya msingi kuoa na wala sijuti. Uvumilivu, maongezi na kupendana na msingi wa maisha bora.

Kama unajua uvumilivu, maongezi na kupendana ndo msingi usingekuja kumshtaki mwenzio jf na kejeli nyingi na ubabe. Ungeonyesha huo uvumilivu na upendo na maongezi asingechukua begi na kutaka kwenda kwao. Ila yeye alivitilia maanani akarudisha begi ndani.
 
Contradiction....
Limekugusa sanaaa???? Same type???
 
Back
Top Bottom