Haki huinua Taifa na kuleta upendo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Usiku huu nimeshindwa kuomba! Nimejikuta nikitokwa na machozi! Si machozi ya huzuni wala si machozi ya furaha! Ni machozi ya mshangao nikimshangaa Mungu! Nilikuwa nikitaka kuwaombea baadhi ya viongozi akiwemo Rais mpya wa Zambia! Ilipofika zamu yake nihimizwa moyoni kuwa niangalie kwanza taarifa za Zambia kabla sijaomba! Macho yangu yamekutana na taarifa iliyonigusa.

Taarifa hiyo imenifanya nishindwe kuendelea kuomba kutokana na mshangao. Macho yangu yameshuhudia Rais Hakainde Hichilema akimuapisha Naibu Kamishina Generali wa Jeshi la Magereza nchini Zambia! Hichilema alipokuwa Kiongozi wa Chama cha Upinzani, alikamatwa na kutupwa Gerezani. Alifunguliwa Mashtaka ya ugaidi/uhaini. Alipokuwa Gerezani, wakati Wakuu wengi wa vyombo vya dola wakimnyanyasa, kulikuwa na kijana mmoja Afisa wa Jeshi la Magereza aliyeamua kutenda haki. Katika mazingira yale magumu yule Afisa Magereza alijitofautisha na wengine waliokuwa 'wanauabudu' mfumo kandamizi!

Sasa Hichilema ndiye Rais wa Zambia! Amempandisha cheo yule kijana kuwa Naibu Kamishina Generali wa Jeshi la Magereza, cheo kinachofuata baada ya Kamishina Generali. Kabla ya kumuapisha, Rais Hichilema alisimulia mazingira magumu ya Gerezani. Simulizi yake ndiyo iliyoniliza! Kwa kiasi ninaelewa maana ya kuwekwa nyuma ya kuta. Ingawa sikuwahi kulala Magereza, lakini nimelala katika Mahabusu za Polisi. Nililala Central Police Dar es Salaam na nililala Kituo cha Polisi Kirumba, Mwanza. Pia, nimekuwa nikipata taarifa za mahabusu wa kisiasa kutoka sehemu nyingi nchini na kuwapazia sauti.

Natamani ujumbe huu uwafikie Askari wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza nchini Tanzania. Hivi wanaelewa kuwa hao wanaopita mikononi mwao kama watuhumiwa, mahabusu au wafungwa siku moja baadhi yao wanaweza kuwa wakuu wao? Wakijua hivyo watakuwa na utu katika kutimiza majukumu yao! Ukiamka kesho, hakikisha ujumbe huu anasoma kila aliye Askari katika Majeshi tajwa, kuanzia mdogo hadi mkubwa. Wakuu wanaoshika nafasi za utukufu katika Wilaya, Mikoa, Wizara na hata Ikulu wasiache kusoma nao wasome!

Wekeni ujumbe huu kwenye magrupu yenu ili kila mtu ausome. Hivi utamuangaliaje yule uliyemnyanyasa endapo ndiye atakayekuja kuwa kiongozi na mkuu wako kesho baada ya mapambazuko? Hivi utajisikiaje Kama yule uliyemsingizia na kumbambikia Kesi endapo ndiye atakayekuja kuwa na mamlaka juu yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Ni wachache sana wenye moyo kama wa huyo kijana aliekuwa askari magereza wa Zambia, hapa kwetu CCM imetapakaa kila mahali kujaribu kufanya hivyo halafu yatokee ya Zambia panahitajika muujiza mkubwa sana, kwetu ni rahisi zaidi kushinda mgombea asiekubalika na wengi kuliko yule anaekubalika na wengi.
 
Ndiyo sababu hawa genge la wahuni maccm wanahofia sana Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi kwa kuwa wanajua fika ndiyo vitasababisha kuwa Kiama cha hawa majambazi.
Ni wachache sana wenye moyo kama wa huyo kijana aliekuwa askari magereza wa Zambia, hapa kwetu CCM imetapakaa kila mahali kujaribu kufanya hivyo halafu yatokee ya Zambia panahitajika muujiza mkubwa sana, kwetu ni rahisi zaidi kushinda mgombea asiekubalika na wengi zaidi ya yule anaekubalika na wengi.
 
Wekeni ujumbe huu kwenye magrupu yenu ili kila mtu ausome. Hivi utamuangaliaje yule uliyemnyanyasa endapo ndiye atakayekuja kuwa kiongozi na mkuu wako kesho baada ya mapambazuko?

Hivi utajisikiaje Kama yule uliyemsingizia na kumbambikia Kesi endapo ndiye atakayekuja kuwa na mamlaka juu yako?
 
Hivi utamuangaliaje yule uliyemnyanyasa endapo ndiye atakayekuja kuwa kiongozi na mkuu wako kesho baada ya mapambazuko? Hivi utajisikiaje Kama yule uliyemsingizia na kumbambikia Kesi endapo ndiye atakayekuja kuwa na mamlaka juu yako?
😂😂😂😂😂

Mkuu BAK ...

some dreams are nightmares... Em amka ... kunywa maji kwanza. Kisha tuendelee..

Mama yuko safiii... Twende nae.
 
Ni wachache sana wenye moyo kama wa huyo kijana aliekuwa askari magereza wa Zambia, hapa kwetu CCM imetapakaa kila mahali kujaribu kufanya hivyo halafu yatokee ya Zambia panahitajika muujiza mkubwa sana, kwetu ni rahisi zaidi kushinda mgombea asiekubalika na wengi zaidi ya yule anaekubalika na wengi.
tanzania Mungu atutazame kwa jicho la pekee
 
Itabidi tuombe muujiza wa Mungu atubadilishie Katiba, kwani kubadili sura za watu pekee nimeona hakutoshi.
Hili la katiba ni mwiba ukiowakwama CCM shingoni. Dunia nzima inawashangaa ni kwanini hawaitaki na Denmark ameanza kujitoa kimahusiano nao.
 
Huko chadema mna tenda haki?! Kwa nini kila anayegombea na Mbowe uenyekiti hua mnamfukuza chamani? Yaani nyinyi mnataka mfanyiwe haki ila nyinyi kutenda haki hamtaki maajabu sana hayo.

Any way hamieni Zambia sasa.
 
Ukidai katiba unapewa kesi ya ugaidi!
Ukifungua kesi ya kupinga tozo unafunguliwa kesi ya kuambiwa wewe sio raia!
Hakuna haki, hakuna usawa hakuna amani ya kweli, Tuzidi kumuomba Mola wetu afanye 'wepesi hasa kwa haya makatili'.
 
Kama nia yako ,ni kumuongelea Gaid Mbowe.Sio hivyo.HHH ni MTU mwaminifu kabisa ,na mkweli.Mbowe ni Gaidi kabisa.Na si mkweli
 
Kwa wenye UFINYU WA AKILI TU kama ZWAZWA wewe.
Kama nia yako ,ni kumuongelea Gaid Mbowe.Sio hivyo.HHH ni MTU mwaminifu kabisa ,na mkweli.Mbowe ni Gaidi kabisa.Na si mkweli
 
Back
Top Bottom