Haki haitendeki, tumeamua kusimama na #FreeMaxenceMelo

Haki haitendeki, tumeamua kusimama na #FreeMaxenceMelo

Heshima kwenu Wakuu,



Japo kwa maapizo ya waliomshikilia hakuna dalili, lakini iwapo kufikia saa saba (7) mchana wa leo, Maxence atakuwa bado hajafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka, tutafahamishana hatua inayofuata.

[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
View attachment 446473

Hivi sasa ni saa nane na dakika saba vipi tayari amefikishwa mahakamani au bado?
 
Freedom of expression ipo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18.

Swali la kujiuliza hao Polisi waliomkamata Max Melo na kumweka kwenye sero zao kwa zaidi ya saa 24 ambapo ni kinyume cha sheria za nchi, swali la kujiuliza hao Polisi wamepewa kiburi na nani hadi waione Katiba ya nchi yetu kama 'rubbish' fulani?!

Those who are in power, free Maxence Melo without any conditions.
 
huu utawala mwisho wake utakuwa mbaya sana. Tunakoelekea siko kabisa
 
0fd68d745c86936c5f1b4516702d1a3d.jpg
 
Heshima kwenu Wakuu,

Tumefuatilia kwa karibu kutoka kwa Jopo la Mawakili Wasomi, ndugu jamaa na marafiki ambao, wamekuwa katika jitihada za Kisheria na kiungwana, kujua makosa ya Maxence na kumuwekea dhamana ili awe huru. Majibu tuliyopata yanaonyesha kile anachofanyiwa ndugu yetu hakina na wala hakifuati kifungu cha Sheria yoyote katika Sheria za nchi ya Tanzania.

Waliomshikilia wanaonekana kuongozwa kwa maelekezo na nguvu kubwa isiyomithilika wala kudhibitika hata kwa Katiba ya nchi. Mathalani leo ni siku ya pili Maxence ameshikiliwa bila kufikishwa mahakamani, alipaswa ahojiwe ndani ya saa nne (4) toka awekwe kizuizini lakini kahojiwa jana jioni karibu baada ya saa zaidi ya 28, hadi sasa mawakili wake hawajapewa hati ya mashtaka hivyo hawajui kashikiliwa kwa kosa gani na lini atafikishwa mahakamani. Na waliomshikilia wanajiapiza kuwa Mawakili hata waende mahakama kuu, Maxence hatapelekwa mahakamani mpaka wao wapende!

Na kama Maxence kashikiliwa kwa kosa linalohisiwa kwamba ni kwa kukataa kutoa taarifa za faragha za baadhi ya watumiaji wa JamiiForums.com, basi nayo itakuwa ni usiginaji wa Sheria maana kesi ya hilo suala tayari iko mahakamani na Maxence yuko nje kwa dhamana.

Kufuatia hayo yanayoendelea, katika hatua ya awali leo, wale wote tunaoguswa na kile anachokisimamia na kukipigania Maxence tunaombwa kuanzia sasa kuungana kwenye kampeni maalum kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, Instagram, WhatsApp) inayoendeshwa chini ya [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]. Picha maalum kwa ajili ya kampeni imeambatanishwa hapo chini.

Wale mtakaotumia lugha za kigeni e.g Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kireno, n.k kumbukeni kunakili mashirika ya Kimataifa hasa yale yanayoshughulikia masuala ya habari, haki za waandishi wa habari, haki za binadamu na utawala bora.

Na pia kwa wale tunaolenga kufikisha masikitiko yetu kwa vyombo vya ndani, tumieni lugha ya staha kumueleza Rais Magufuli, Waziri Mwigulu Mchemba, IGP Mangu, Kamanda Sirro, na DCI Wambura.

Japo kwa maapizo ya waliomshikilia hakuna dalili, lakini iwapo kufikia saa saba (7) mchana wa leo, Maxence atakuwa bado hajafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka, tutafahamishana hatua inayofuata.

[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
View attachment 446473
[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
 
Imani yangu ni kwamba kila litendekalo hapa duniani Mungu amekwisha andaa hukumu yake ambayo inaweza kutekelezwa hapa duniani au Mbinguni. [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
 
Hivi hashtag ina maana gani wakuu.

[HASHTAG]#freemaxdemello[/HASHTAG]
 
Pelekeni malalamiko balozi za nje has a zile nchi wahisani kama Sweden,Denmark,EU,USA,Norway nk.
Rais wetu mpendwa niliyekupigia kura 25/10/2015 tukiamini utaliongoza taifa letu kwa kufuata sheria na haki za binadamu ninakuomba umuachie huru Max,taifa letu limepata sifa mbaya sana vyombo vya habari vya kimataifa vimeandika sana juu ya suala la Max.
Pambana na umasikini ,rushwa,ufisadi,madawa ya kulevya,ukosefu wa ajira,usipambane na Uhuru wa kujieleza,Uhuru wa kupata habari na demokrasia.
 
Jaman katiba inavunjwa kwanini? Tuachieni kijana wetu jaman, Arusha hapa tutainda makundi maaulum ya kupinga unyanyasaji huu
 
Back
Top Bottom