Haki haitendeki, tumeamua kusimama na #FreeMaxenceMelo

Mwigulu Nchemba nafikiri anapitia huku, analichukuliaje hili la sheria kuvunjwa na chombo anachokiongoza?
Tungependa kusikia neno kutoka kwake.
 
Hadi sasa polisi bado hawajafanikiwa kupata wanachotaka kutoka kwa Maxence Melo na wasaidizi wetu wawili.

Ningeelewa zaidi kuhusu lengo la polisi kama wangekuwa wanao wataalam wa teknohama ambao pengine wangeweza kuwasiaidia katika kutafuta khasa ni nani alietoa tarifa za ubadhifilu wa mafuta kule bandarini na taratibu za kifisadi hapa JF.

Lakini tangu kuanzishwa kwa JF miaka 10 ilopita JF imekuwa imara na itaendelea hivyo labda kama polisi na vyombo vya dola Tanzania watataka kupanda ndege kila mara kuitafuta JF na wasiipate server ilipo mahala fulani hapa duniani.

Serikali kupitia polisi kama chombo chake cha kutekeleza sheria ya mtandao, inapaswa kufikiria mara mbili juu ya njia wanayotumia kutaka kuinyamazisha JF kwani hata baadhi ya wanachama hapa ni watumishi wa serikali kwa majina halisi na wengine ni kwa majina bandia.

Wale wote wanaolalamika kwamba taarifa zilizotolewa kupitia JF kuhusiana na shughuli zao za ufisadi wanapaswa kujiuliza kwanini iwe wao na sio watu wengine?

Jeshi la polisi wana budi kumuachia Maxence Melo na wasaidizi wake na kuacha kuisumbua Jamii Media.

Jeshi la polisi lijikite zaidi katika shughuli za uchunguzi mahiri kama ule wa miili ya wale binadamu walokutwa wametupwa mtoni na hadi leo hakuna autopsy wala DNA tests zilizofanywa.

Huu ni wakati sasa wa jeshi letu hata kutumia mbinu za kutafuta watalaam wengi ambao wengine wapo hapahapa JF ili kulisaidia taifa katika kujiletea maendeleo katika Nyanja mbalimbali.

Pia ni wakati wa sasa wa serikali kufikiria upya juu ya ukosoaji ambao upo zaidi katika kuchagiza shughuli zake katika kuliletea mandeleo taifa hili badala ya kukesha na maombi na namna ya kuifunga na kuifutilia mbali JF.

Ningependa kulishauri jeshi la polisi kwamba njia wanayotumia kuinyamazisha Jamii Forums haitafanikiwa kwasababu Jamii Forums haina servers nchini Tanzania wala barani Afrika.

Hii ni sambamba na baadhi ya sisi wanachama hapa ambao wengine ni wataalam wa mitandao na nyanja zingine mbalimbali, lakini tupo kila mahala hapahapa duniani.

Polisi imwachie Maxence Melo na wasaidizi wake wawili ambao imewachukua leo kwa mahojiano zaidi.
haya mapolisi mbona yanasumbua ....yakuwa kama hayajala toka jana....kama yanaweza yaende kuwakamata na waanzilishi wa facebook...alafu siyapendi mapolisi kama kipolo cha dona
 
Inasikitisha Sana,ibara ya 18 inavunjwa mchana kweupe,Facebook ,instagram kuna matusi nabkuchafuana sana wakati JF moderation ipo...[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
 
#freemaxencemelo#

14cef5a214a5a8afbe2eccd1f116b30a.jpg
 
Heshima kwenu Wakuu,

Tumefuatilia kwa karibu kutoka kwa Jopo la Mawakili Wasomi, ndugu jamaa na marafiki ambao, wamekuwa katika jitihada za Kisheria na kiungwana, kujua makosa ya Maxence na kumuwekea dhamana ili awe huru. Majibu tuliyopata yanaonyesha kile anachofanyiwa ndugu yetu hakina na wala hakifuati kifungu cha Sheria yoyote katika Sheria za nchi ya Tanzania.

Waliomshikilia wanaonekana kuongozwa kwa maelekezo na nguvu kubwa isiyomithilika wala kudhibitika hata kwa Katiba ya nchi. Mathalani leo ni siku ya pili Maxence ameshikiliwa bila kufikishwa mahakamani, alipaswa ahojiwe ndani ya saa nne (4) toka awekwe kizuizini lakini kahojiwa jana jioni karibu baada ya saa zaidi ya 28, hadi sasa mawakili wake hawajapewa hati ya mashtaka hivyo hawajui kashikiliwa kwa kosa gani na lini atafikishwa mahakamani. Na waliomshikilia wanajiapiza kuwa Mawakili hata waende mahakama kuu, Maxence hatapelekwa mahakamani mpaka wao wapende!

Na kama Maxence kashikiliwa kwa kosa linalohisiwa kwamba ni kwa kukataa kutoa taarifa za faragha za baadhi ya watumiaji wa JamiiForums.com, basi nayo itakuwa ni usiginaji wa Sheria maana kesi ya hilo suala tayari iko mahakamani na Maxence yuko nje kwa dhamana.

Kufuatia hayo yanayoendelea, katika hatua ya awali leo, wale wote tunaoguswa na kile anachokisimamia na kukipigania Maxence tunaombwa kuanzia sasa kuungana kwenye kampeni maalum kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, Instagram, WhatsApp) inayoendeshwa chini ya [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]. Picha maalum kwa ajili ya kampeni imeambatanishwa hapo chini.

Wale mtakaotumia lugha za kigeni e.g Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kireno, n.k kumbukeni kunakili mashirika ya Kimataifa hasa yale yanayoshughulikia masuala ya habari, haki za waandishi wa habari, haki za binadamu na utawala bora.

Na pia kwa wale tunaolenga kufikisha masikitiko yetu kwa vyombo vya ndani, tumieni lugha ya staha kumueleza Rais Magufuli, Waziri Mwigulu Mchemba, IGP Mangu, Kamanda Sirro, na DCI Wambura.

Japo kwa maapizo ya waliomshikilia hakuna dalili, lakini iwapo kufikia saa saba (7) mchana wa leo, Maxence atakuwa bado hajafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka, tutafahamishana hatua inayofuata.

[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
View attachment 446473

Kwanini kesho tusikutane hapo nje ya hicho kituo alichoshikiliwa @maxenceMelo
 
Huyu jamaa ni wa kumpigania kabisa kama watanzania, hatuwezi kukaa tunaangalia nchi wanajiamulia mambo bila kufuata sheria. Walianza siku za nyuma polepole, sasa hivi hadi wanakamata watu bila kutoa sababu kwa nini kakamatwa. Wanatufanya tuanze kuhisi hadi ya Ben Saa 8 kama ni ya kweli.

Sio tu mitandaoni, inabidi kujazana mahakamani na mabango kabisa hadi waelewe.
 
Waliomshikilia wanaonekana kuongozwa kwa maelekezo na nguvu kubwa isiyomithilika wala kudhibitika hata kwa Katiba ya nchi. Mathalani leo ni siku ya pili Maxence ameshikiliwa bila kufikishwa mahakamani, alipaswa ahojiwe ndani ya saa nne (4) toka awekwe kizuizini lakini kahojiwa jana jioni karibu baada ya saa zaidi ya 28, hadi sasa mawakili wake hawajapewa hati ya mashtaka hivyo hawajui kashikiliwa kwa kosa gani na lini atafikishwa mahakamani. Na waliomshikilia wanajiapiza kuwa Mawakili hata waende mahakama kuu, Maxence hatapelekwa mahakamani mpaka wao wapende!

Ubaya ni kwamba hakunaga mwenye hati miliki ya Dunia maana hata Yesu aliondolewa na Binadamu Bila kujua kuwa Baba yake anauwezo kuliko wao.
Hayo maneno yanaumiza sana! Maana huko nikuzika ndoto ya Nchi ya Viwanda mchana kweupe kabisa. Je hayo kwa masilahi ya nani?

[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom