Haka kamvua na kiwinta vinakukumbusha nini?

DN mimi bwana kipindi hiki nilipokuwa shule ya msingi.............mmh nilikuwa sipendi kukanyaga maji maji au matope, kwenda shule duh kazi ya ziada ilihitajika. nilikuwa na boot zangu maalum for such days with my stockings (uchepechepe ulikuwa unaniudhi sana, sasa ndo nikiona na uchafu uchafu dizain duh hata msosi sitaki kabisa coz when am eating i would recall that) hahaaa but I looked lovely with my speicial boots n stockings lol!!!

hapo ndio kasheshe, yaani vidume vyote huo ndio ulikua muda wa kucheza chandimu, kuangua matunda nk. i remember nilikua napiga boli balaa kwa hiyo mvua haikunisumbua

mabadiliko yalikuja nipoanza kuangalia wadada kwa jicho la tatu, hapo mvua turned from fun to ******** ==== balaaaaaaaaaaa
 
Noname, umenifurahisha na signature yako, nimeipenda lol!

"I’m a woman who knows no defeat, for there is no ground to fall, as I chooses to stand, Despite my trembling knees, I conquer my fate. I am a woman who creates her own destiny"
 
..Mi nakumbuka mahindi ya kuchoma kule kijijini kwetu. Mida hii umejikunyata unachochea moto na mahindi kibao ukitoka hapo unanuka moshi unapiga kata ya maji ya kunywa unatafuta pa kumalizia usiku.
 
Tehe tehe inanikumbusha wakati niko darasa la pili miaka ya 80 mwanzoni pale Sumbawanga, mvua ilikuwa ikinyesha mwalimu wetu wa Mwandiko alipenda sana kutuambia tuunganishe madawati, yaani rows zote tatu tunaziunganisha tunakuwa tumekaa km kwenye fremu moja mithili ya yale ma benchi marefu ya kanisani. Niliipenda sana style hiyo sababu upande wa kulia kwangu walikuwa wanakaa wasicha watupu watatu, nawakumbuka wawili, mmoja alikuwa akiitwa LILIAN, Mwingine MONICA, acha bana walikuwa watoto wazuri ajabu (tehetehetehe). ile tukiunganisha madawati tu wananiweka katikati yao, basi kale kajoto na kule kunifinya finya mara wanitekenye daaaaaaaaaaaaah niliipenda sana ile style. walikuwa marafiki zangu wakubwa sana tukitaniana sana, lkn wao hawakujua kwamba nilikuwa nawahusudu mbaya!! ingawa nilikuwa na oly 8 yrs hahahahahah mpaka leo nawakumbuka. Huyu Monica alikuwa mweupe kama papai ana meno meupeeee, dimpo za kufa mtu na nywele ndefu akisuka only twende kilioni wakati ule kulikuwa hakuna kulemba. Huyu LILIAN alikuwa ana weusi wa NYOKA, ana ng'aa balaa halafu alikuwa ana kaalama shavuni hivi ka duara. Nilipenda kuwaita wachumba zangu lkn bahati mbaya tulikuwa bado watoto wadogo sana. Baadaye darasa la tatu nilihama mkoa. Kila mvua inyeshapo na kiubaridi kama hiki sichelei kuwakumbuka hawa friends wangu!!!!

Niambie Lily yuko wapi na Monny yupo wapi kwani nahisi umewamiss sana
 
hahaaaa B siku hizi mbona chokest jamani..........those old good days aaah wacha bana

B speed ya net inanikwaza (miss u)


hawa SEACOM B usiajali......ngoja nitafute miwani yangu sasa kuna sehemu pananitatiza zioni vizuri
 
Niambie Lily yuko wapi na Monny yupo wapi kwani nahisi umewamiss sana

dah kaka its 28 yrs sijawaona nikikutana nao ntafurahi mno, kuna jamaa mmoja tulisoma nae, nilibahatika pata namba yake nikampigia akashangaa sana hakuamini, ntampigia tena ataniambia wapo wapi ntakujuza
 
Nyumba yetu ilikuwa inavuja na tulikuwa tunatumia kibatari na mnajua tena mpakani mwa kENYA NA TZ kuna baridi sana.
 
Haaa Sisi wa mikoani tunakula kuku tu. Huku Mwanza jua lilishaanza kukamua mwanawane.
 
Back
Top Bottom