Haja Ya Kuwepo Wawakilishi Wa Zanzibar Kwenye Balozi..

Choveki,

Siyo kwamba wanaweza kufanya referendum na kupindua matokeo kama walivyomnyang'anya Seif urais wa Zanzibar? Mimi sioni tatizo ya CCM kupata simple majority bara, not even Unguja.Kazi iko Pemba huko.Labda Muungano uendelee Tanganyika na Unguja, Pemba wende zao ati yakhee!

Au hata watu wa Unguja hawataki muungano nao?

Now this is where Nyerere's vision becomes a reality.Wkijitenga Zanzibar kesho itakuwa Unguja na Pemba wanajitenga.Keshokutwa Kwaani sijui na Michenzani wanataka kuwa na rais na jamhuri zao, mwishowe kila baba mwenye wake wawili naye anatangaza jamhuri lol!
 
Choveki,

Siyo kwamba wanaweza kufanya referendum na kupindua matokeo kama walivyomnyang'anya Seif urais wa Zanzibar? Mimi sioni tatizo ya CCM kupata simple majority bara, not even Unguja.Kazi iko Pemba huko.Labda Muungano uendelee Tanganyika na Unguja, Pemba wende zao ati yakhee!

Au hata watu wa Unguja hawataki muungano nao?

Now this is where Nyerere's vision becomes a reality.Wkijitenga Zanzibar kesho itakuwa Unguja na Pemba wanajitenga.Keshokutwa Kwaani sijui na Michenzani wanataka kuwa na rais na jamhuri zao, mwishowe kila baba mwenye wake wawili naye anatangaza jamhuri lol!


matusi sasa haya, tena matusi ya nguoni.

hii ndio siasa mnayotumia kuwatisha wazanzibari wasidai haki zao ooh mkituacha hamtobaki salama mtaanza kulana wenyewe kwa wenyewe. haya ni maneno ya kutujenga hofu ila ss tushawaelewa vya kutosha.

tanganyika kuna wachagga na wahaya na wengine na kuna malalamiko chungu nzima lkn siamini kuwa wakivunja muungano wachaga watataka kuunda chagga enpire yao au wasukuma watataka kuunda empire yao.

hayo yamepitwa na wakati tofauti zetu si kubwa za kiasi cha kufikiria kugawana visiwa hilo lijulikane, na wazanzibari wengi wanaamini hofu na hali hii tulionayo wanaileta wenzetu wa bara makusudi ili tuung'ang'anie muungano.

ss tatizo sio muungano tatizo muungano huu tulionao sio adilifu basi.

tukae tuuzun gumze na pasiwepo kuoneana.
 
Nijuavyo mimi tokea kuundwa kwa Bunge la Muungano hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini, 'SHERIA YOYOTE INAYOHUSU MAMBO YA MUUNGANO, ILIHITAJI TWO THIRD YA WAJUMBE KUTOKA ZANZIBAR NA TWO THIRD YA WAJUMBE KUTOKA BARA'ili ipite. Lakini sasa SHERIA YOYOTE YA MUUNGANO INAHITAJI TWO THIRD YA WAJUMBE WOTE WA BUNGEili ipite.
Kama wajumbe wote wa sasa ni 320, na wajumbe kutoka Zanzibar hawazidi hata 70, je hata Wazanzibar wakiikataa sheria ndani ya Bunge si itapita tu coz hawa Wabara tayari wao wapo two third ya wajumbe wote wa Bunge. Muungano gani huu zaidi ya mauzauza!
wenye kujua zaidi forums hapa tupeni ukweli plz


A day will come
 
Ninachotaka kuwaambia wanaJF ni kuwa muungano si kulazimishana au ubabe, ukweli utakuja onekana siku moja. Sisi muungano wetu una kasoro nyingi na fukuto ni kubwa sana, tunachofanya ni ku delay kuuvunja, ila utakuja vunjika tu.

Nyumba yoyote iliyojengwa kwenye foundation ya hewani, ni lazima ije anguka tu siku moja, lakini iliyojengwa mwambani hudumu milele!

Chukua tano zako mkuu
 
Mtu wa pwani......

niliwahi sikia kuwa TANGANYIKA walikuwa hawana KITI KTK UMOJA WA MATAIFA,nasikia baada ya muungano wakafanya mazingaombwe na kuwapokonya kiti chetu wa-ZANZIBAR na kukitumia wao,ingawa sina uhakika wa hili.naamini JF wapo wanaolijua hili,hebu tuwekeeni data.

Hayo maneno siyo sahihi mkuu wangu Engineer. Ukweli wenyewe huu hapa:
Tanganyika and Zanzibar
Tanganyika was admitted on 14 December 1961, and Zanzibar was admitted on 16 December 1963. The two countries were unified to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar on 26 April 1964, later changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964, and have since been represented as one member.

habari zaidi nenda:
http://child-un.org/dmdocuments/UN_Flags.html#Tanganyika_and_Zanzibar
 
Iwapo inatokea siku muafaka ukifanikiwa, je CUF wanampango gani kuhusiana na wawakilishi wa SMZ kwenye balozi nje?!

SteveD.
 
ndio pale tunaposema hatuna haja na huu unaioitwa muungano(maana hawa wenzetu ni mapaketi matupu)mawazo yao yote eti wazenj ni kidogo
 
Nitakubaliana na hoja tu... kama kwenye balozi kubwa na zile kweli strategic na hazizidi kumi... lakini ati kwa kila balozi then huo ni upuuzi.
 
Nina hofia sana uhai wa Muungano hasa pale bara tunapojaribu kufumba macho ktk maswala muhimu ya muungano huu. Na kibaya zaidi ni pale Wazanzibar wanaposhindwa kutumia akili na kuhoji mambo muhimu badala yake wanatumia tofauti zetu kama binadamu kuuandika Muungano...
Kuna sababu kubwa sana Muungano huu ulitakiwa kuwepo hasa baada ya Zanzibar kupata Uhuru..Kuna makosa makubwa yalifanyika na kina Shamte kukubali kumrudisha Sultan kama mtawala, na hata consitution ya nchi kuitaja Zanzibar kama 'an Arab states'..(Arab - Zanzibar).
Shamte kukubaliana Kenyatta kuhusiana Mombasa iwe part of Kenya na mengine mengi makosa ambayo yalikuwa sababu kubwa ya Mapinduzi, Mapinduzi ambayo yalikuj onekana kama tishio la kuingia Ukommunist nchini na yakadumu kwa mwezi mmoja tu kabla Karume hajachukua madaraka na udikteta wake ulionekana wazi na mapema...Mfululizo wa mabo haya unaonyesha wazi jinsi Zanzibar ilivyokuwa lege ktk Utawala na ulinzi wa Uhuru wa wananchi wake.

Muungano ulikuwa lazima na kusema kweli hadi leo pamoja na matatizo yote Wazanzibar wanashindwa kuonyesha kuridhika na Mapinduzi au mabadiliko yaliyokuwa lazima.. jambo ambalo linazidi kujenga hofu na wasiwasi zaidi kwamba wapo watu wenye agenda inayo address zaidi Uhuru wa Zanzibar kama nchi badala ya matatizo ya Uhuru huo kwa Wazanzibar..
 
Kitila,
nakuunga mkono...watanganyika hawadadisi kabisa haki zao ndani ya Muungano. Kwa mfano:-

..kwanini Tanzania Bara inalipa mishahara ya SMZ wakati waalimu wetu wanacheleweshewa malipo?

..kwanini SMZ haichangii ktk gharama za uendeshaji wa vyombo vya Muungano?

..kwanini wabunge wa Zanzibar wanachukua posho, wanashiriki na kupiga kura, ktk vikao vinavyojadili masuala ya Tanzania Bara?

..kwanini wazanzibari wanaendelea kuajiriwa/kuteuliwa ktk nafasi zisizo za Muungano?

..kwanini watanzania bara wanalazimika kutumia passport kuingia wanapokwenda Zanzibar, lakini Wazanzibari wanaingia Tanzania Bara kama msalani?

..kwanini wazanzibar wanaruhusiwa kupiga kura ktk chaguzi zetu lakini sisi haturuhusiwi kupiga kura ktk chaguzi zao?

..kwanini machangudoa kutoka Bara wanafukuzwa Zanzibar, lakini mashoga toka Zanzibar hawafukuzwi wanapoweka makazi huku Bara?

Kwa minajili hii...Zanzibar ndiyo inaitawala Tanganyika na maoni yangu kama ni uhuru basi Tanganyika ndio tunautaka!
Yani sasa tukaliwe kichwani hadi lini?
Ndugu zangu wa Zenji hamkuwaambia ukweli.
Juzi hapa Obama kawaambia ukweli wamarekani kwenye debate hapa...Akasema wazi kuwa marekani wasijidai eti kusema wana mafuta.
Nilipofika hapa USA ndiyo kauli niliyokuwa nikisikia kutoka kwa wananchi wengi wazungu...Tena wale wenye mielekeo ya kibaguzi...Ooh tuna mafuta nk.
Obama akawaambia kuwa USA ina consume mafuta asilimia 25 ya world reserve kwa mwaka...Na hapa USA kuna 3% peke yake a oil reserve ya dunia...Sasa hapo si ni sawa na jaribio la kumlisha tembo mwenye njaa pipi gololi?
Mlishawaambia wa Zenji kuwa wana mafuta...Na kwahiyo mnapouza uhuru wote huu na wao wanajiuliza inakuwa vipi..Na ndio maana wawakilishi wao wakaja juu kuwambiwa kuwa hawana mafuta.
Sasa kama ni kweli hawana mafuta...Tupeni uhuru wetu na wao wapeni huo wao wanaodai hawana.
 
Choveki,

Siyo kwamba wanaweza kufanya referendum na kupindua matokeo kama walivyomnyang'anya Seif urais wa Zanzibar? Mimi sioni tatizo ya CCM kupata simple majority bara, not even Unguja.Kazi iko Pemba huko.Labda Muungano uendelee Tanganyika na Unguja, Pemba wende zao ati yakhee!

Au hata watu wa Unguja hawataki muungano nao?

Now this is where Nyerere's vision becomes a reality.Wkijitenga Zanzibar kesho itakuwa Unguja na Pemba wanajitenga.Keshokutwa Kwaani sijui na Michenzani wanataka kuwa na rais na jamhuri zao, mwishowe kila baba mwenye wake wawili naye anatangaza jamhuri lol!

Mheshimiwa Pundit. Be sensible!!
 
Nijuavyo mimi tokea kuundwa kwa Bunge la Muungano hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini, 'SHERIA YOYOTE INAYOHUSU MAMBO YA MUUNGANO, ILIHITAJI TWO THIRD YA WAJUMBE KUTOKA ZANZIBAR NA TWO THIRD YA WAJUMBE KUTOKA BARA'ili ipite. Lakini sasa SHERIA YOYOTE YA MUUNGANO INAHITAJI TWO THIRD YA WAJUMBE WOTE WA BUNGEili ipite.
Kama wajumbe wote wa sasa ni 320, na wajumbe kutoka Zanzibar hawazidi hata 70, je hata Wazanzibar wakiikataa sheria ndani ya Bunge si itapita tu coz hawa Wabara tayari wao wapo two third ya wajumbe wote wa Bunge. Muungano gani huu zaidi ya mauzauza!
wenye kujua zaidi forums hapa tupeni ukweli plz


A day will come

Muungano na uendelee. |Lakini usanii Laa. Tuko macho.
 
Mada inapoletwa katika ukumbi huu watu wajadili ukweli na sio ushabiki wa kisiasa kama alivyofanya

'kwanini watanzania bara wanalazimika kutumia passport kuingia wanapokwenda Zanzibar, lakini Wazanzibari wanaingia Tanzania Bara kama msalani?' hivyo wewe upo katika sayari gani? unamini watu kutoka bara wanaingia kwa passport? tokea lini mambo hayo au ulikuwa umekufa umeacha mambo hayo ya passport na sasa umefufuka kujaulizia mambo kama yamebadilika una ndoto ile ile ya zamani?

Ama kweli wewe ni yebo yebo yaani kiatu kisicho na thamani maana hata haya maneno yako yako ya aina hii.
unasema 'kwanini wazanzibar wanaruhusiwa kupiga kura ktk chaguzi zetu lakini sisi haturuhusiwi kupiga kura ktk chaguzi zao?' jibu kwa kura inayopigwa ni ya Rais wa Tanzania ambaye anahusika Tanzania nzima.

..'kwanini machangudoa kutoka Bara wanafukuzwa Zanzibar, lakini mashoga toka Zanzibar hawafukuzwi wanapoweka makazi huku Bara?' nani kakwambia kama machangudoa wanafukuzwa? unakubali habari zilizoandikwa katika magazeti bila ya wee mwenyewe kufanya utafiti? unajua hao machangudoa waliokuwa wameandikwa kwamba wamefukuzwa unajua kilichotokea? kwa taarifa yako anayefanya biashara hiyo alifukuzwa lakini sasa amezurudi tena kwa ari mpya na nguvu mpya na kwa ajili ya kuogopea kuugusa muungano biashara inaendelea kama kawaida. sijui mwanao kama hayumo aktika kundi hilo maana kuna wasichana wengi sana wadogo.

tatizo viongozi wa zanzibar wameogopa kumfukuza maam gogo ambaye anaathiri jamii yetu kwa kiasi kikubwa na sio jamii ya wazanzibari tu bali ni jamii ya kitanzania maana kwa taarifa yako au for infomation mama gogo ni mwanamke anayetokea huko Arusha amekodi mkoa nyumba mkoa wa kaskazini unguja kwenye beach anachukua watoto wadogo wenye umri wa miaka kuanzia 14 hadi 25 kutoka Arusha, Mwanza na Morogoro na kuwaleta zanzibar na kuwauza kwa wazungu na biashara hiyo inafahamika sana na ilipoandikwa watu wa bara wamekuja juu na kaundika uchambuzi kuwa suala hilo sio la wabara pekee bali hata wanaume wa zanzibar ni malaya lakini hawajajua athari inayopatikana. sasa serikali nayo imekaa kimya kwa kuogopa kuwakera mabwana zao huko bara eti wakiwafukuza watahatarisha muungano lakini akina baba nakutahadharisheni watoto wenu wadogo wanaokuja huku kufnaya kazi katika majumba ambao wapo mikononi kwa mama huyo wapo hatarini katika maambukizo ya ukimwi.

mimi ninaeesema haya nimeshayashuhudia na kumuona huyo mama na kumhoji mambo kadhaa na nimeweka mkono chini maana biashara hii inafanya na vigogo wakubwa wa huko bara wanaletwa huku kwa ajili ya bussines. inauma sana kuona watoto wanafanywa ni biashara lakini ndio maambo kama hayo ikiandikwa watu wanakuja juu.

kuhusu mashoga waliopo huko bara ambao ni wazanzibari nakuomba dada yangu au kaka yangu tema mate chini kwanza usikufuru hata kidogo tuombe toba kwa Mungu unajua kama siku hizi mashoga na tabia ya usagaji haipo visiwani tu? unajua kama mchezo huu upo kila pahala? unajua joseph na john ambao mmoja anatokea ilala na mwengine kariakoo hapo bongo wapo zanzibar na wanatesa kuliko hata shoga mkubwa anayeitwa sabri bachan? unajua kama hao ni vijana wadogo kutoka dar wapo zanzibar lakini kama utawaona huwezi kuamini kama ni wanaume mpaka uwasogemee tena wamevuka mipaka maana mashoga wa zanzibar pamoja na ushoga wao hawathubutu kuvaa nguo za kike wakiwa nje lakini hao joseph na john wanavaa vimini na ukitaka kuhakikisha nakuommba tembelea zanzibar na uende moja kwa moja sehemu moja inaitwa kwa raju halafu kaa kaa pale utawaona wakiingia lakini uwe makini maana unaweza ukadhania ni asha na janet
 
The two countries were unified to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar on 26 April 1964, later changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964, and have since been represented as one member.

Hivi wewe unafahamu hili? Sasa jee? Zanzibar ni Nchi au La. (samahni kurejesha mdahalo uliopita)
 
Ndio sisi wengine tunaamini kwenye muungano wenye serikali tatu.

yani kwenye balozi wawepo wajumbe wa serikali ya mapinduzi na serikali ya tanganyika balozi ndio anakua wa serikali ya muungano.

Mimi binafsi sioni kabisa sababu ya kukumbatia huu muungano Serikali ya mapinduzi ifanye tu ku declare kua wao ni serikali huru na wanavunja muungano rasimi.sasa sijui wanashindwa nini?
 
yani kwenye balozi wawepo wajumbe wa serikali ya mapinduzi na serikali ya tanganyika balozi ndio anakua wa serikali ya muungano.

Mimi binafsi sioni kabisa sababu ya kukumbatia huu muungano Serikali ya mapinduzi ifanye tu ku declare kua wao ni serikali huru na wanavunja muungano rasimi.sasa sijui wanashindwa nini?
Wewe Bwana. Sasa nini kinagomba hapo. Kwani Ubalozi ni wa Tanganyika?
Hivi wewe hufahamu kuwa SMZ ni Serikali huru?
 
Huyo Mama aliyetoka Arusha kama kweli anaendesha Dangulo la watoto wadogo hakuna haja ya kusubiri serikali ya Muungano ifanye kazi..Chukueni nguvu mnayoitumia hapa kupinga Muungano kuwakilisha hoja hii ambayo haipendezi hata kidogo.Isiwe sababu kuwa mama huyo katoka Arusha, mambo anayoyafanya ni uchafu mtupu unaotokana na KUIGA, uhalifu unaopfanywa nchi za nje ktk kujipatia fedha kirahisi..
Mhalifu hana rangi wala asili ni jambo baya linalotakiwa kukomeshwa.
Vijana wa Kizanzibar, wake kwa waume haya ndio maswala mnayotakiwa kuyapiga vita kwa nguvu zote bila kujali mtu huyo anatoka wapi. Wapo pia Wataliani ambao wanafanya binashara chafu za madangulo na ukusanyaji wa unga kutoka nnchi za Asia na South America...Hawa wote wanatakiwa kukomeshwa na sauti zetu zitasikika kwa urahisi zaidi. Tuyakemee mabaya yote yanayofanywa na viongozi, serikali, chama watu binafsi, na kadhalika kabla hatuja utazama Muungano kuwa ndio sababu ya machafu haya.
 
Samahani kama hili limeisha ulizwa! Hivi balozi anayetoka Zanzibar anawakilisha nchi gani, Tanzania au Zanzibar? Kama akiwepo anayetoka Tanzania anaonekana kuwa anawakilisha bara tu hadi panahitajika mwakilishi wa Zanzibar basi na pale anapokuwepo mZanzibari inabidi awepo mwakilishi wa JMT ambayo ni ya watanganyika! Au hata pale atakapokuwepo mZanzibari bado patatakiwa kuwepo mwakilishi wa nchi ya Zanzibar?

Hii ni kutafuta ulaji tuu na kutuingizia gharama zisizo na sababu. Balozi ateuliwe kwa uwezo na si ametokea wapi. Kama mandate yake ni kuangalia maslahi ya nchi ya unguja na hafanyi hivyo, atemwe bila kujali anatokea wapi!
 
Back
Top Bottom