Haja Ya Kuwepo Wawakilishi Wa Zanzibar Kwenye Balozi.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haja Ya Kuwepo Wawakilishi Wa Zanzibar Kwenye Balozi..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Dec 4, 2007.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wana JF, je kuna haja ya kuwepo wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwenye balozi zetu nje ya nchi? Naomba tujadiliane kama ilivyo jadi yetu hapa.

  Source link: IppMedia.

  --Miye nilijua kutokana na kiwango cha utalii visiwani ningelitegemea hawa wawakilishi wapo tayari, na naona kuna haja kubwa ya wawakilishi kutoka Zanzibar kuwepo, ila wawe wataalam wa mambo yao na isitokee likawa jambo la uwakilishi tu kwa nia ya kujaza nafasi..


  SteveD.
   
 2. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #2
  Dec 4, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ndio sisi wengine tunaamini kwenye muungano wenye serikali tatu.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kitila, naomba ufafanue zaidi, kwa ajili ya uelewa wa wengi ambao hatujui haya mambo kiundani, ahsante.


  SteveD.
   
 4. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2007
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kwa nini kila siku lazima Zanzibar waje na jambo jipya ? Ni kitu gani special kitachohitaji mzanzibar kukizungumzia kuhusu zanzibar . Mimi naamini ya kuwa maofisa wabalozi wanachohitaji ni proper training ya kuweza kulitangaza taifa letu kikamilifu ! Na ikiwezekana serikali iwape tour kwenye vivutio vyetu vya kitalii.

  The point sio mtu lazima atoke zanzibar au atoke bara , bali tunahitaji marketer mzuri atakayeweza kusell product yetu " utalii" Mimi nimekaa Tanzania bara miaka yote lakini ukiniambia nizungumzie mbuga za selous ziwezi kwa sababu sijafika huko . Kitu ninachojiuliza jee tukiruhusu hawa wanzanzibar waitangaze zanzibar tutegemee nini huko mbeleni ? Nina hakika watasema ya kuwa unguja inatakiwa itangazwe na waunguja ....kwa hiyo waunguja wawe na mtu wao ! Huu ni ujinga ni lazima hawa wawakilishi watambue serikali aioperate kwa kuangalia sura au rangi ya mtu bali kwa kuangalia masuala ya taifa.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kuwepo kwa wawakilishi wa Zenj katika Balozi, hakumaanishi kuwepo kwa serikali tatu.
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Je sasa hawapo?
   
 7. m

  mwenekapufi Member

  #7
  Dec 4, 2007
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wazenj ni walalamishi sana. Kwani hao mabalozi 5 hawatoshi kuwawakilisha? Maana ukichukulia population yao ni ndogo kwa ratio labda watakuwa over representing. Wanadekezwa sana.Wapige kitabu kwanza.
   
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Dec 4, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Walalamisha au wadadisi wa haki na maslahi yao? Kwa ujinga wangu, wanzibari wanatuzidi sana sisi wa bara kwa habari ya uelewa wa kisiasa.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Dec 4, 2007
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Kitila,
  nakuunga mkono...watanganyika hawadadisi kabisa haki zao ndani ya Muungano. Kwa mfano:-

  ..kwanini Tanzania Bara inalipa mishahara ya SMZ wakati waalimu wetu wanacheleweshewa malipo?

  ..kwanini SMZ haichangii ktk gharama za uendeshaji wa vyombo vya Muungano?

  ..kwanini wabunge wa Zanzibar wanachukua posho, wanashiriki na kupiga kura, ktk vikao vinavyojadili masuala ya Tanzania Bara?

  ..kwanini wazanzibari wanaendelea kuajiriwa/kuteuliwa ktk nafasi zisizo za Muungano?

  ..kwanini watanzania bara wanalazimika kutumia passport kuingia wanapokwenda Zanzibar, lakini Wazanzibari wanaingia Tanzania Bara kama msalani?

  ..kwanini wazanzibar wanaruhusiwa kupiga kura ktk chaguzi zetu lakini sisi haturuhusiwi kupiga kura ktk chaguzi zao?

  ..kwanini machangudoa kutoka Bara wanafukuzwa Zanzibar, lakini mashoga toka Zanzibar hawafukuzwi wanapoweka makazi huku Bara?
   
 10. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hii ndoa ya Muungano...kaaziii kweli kweli.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mzalendo that is a good question! Unajua kuna wakati mwingine ukianza kuwasikiliza wajinga unaweza kuwa unaumiza kichwa. Suala la Ushirikiano wa Kimataifa ni suala la muungano, kwa hiyo hakuna mahali ambapo Tanganyika au Zanzibar zinawatumishi wake kwenye balozi za nje. Sasa hivi ukiangalia make up ya balozi zetu utaona kwa asilimia ya uwakilishi wafanyakazi watangayika ni wachache kuliko wazanzibar, wapo hata mabalozi kutoka Zanzibar. Sasa sijui hoja hii inatoka wapi, au ndio ule ule mdomo mrefu!
   
 12. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huu muungano inabidi uangaliwe upya, tukiamua kuendelea nao basi tuwe na serikali tatu, ya bara, ya visiwani na ya muungano; vinginevyo tutakuwa tunaahirisha matatizo tu.
   
 13. D

  Dotori JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2007
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tunaelekea pabaya. Nadhani mabalozi wachaguliwe on merits kwani wana kazi kubwa kuitangaza Tanzania hasa wakati wakati huu ambapo tuna advocate Economic Diplomacy. Kugawa ubalizo by virtue of proportional representation tutakuwa tunakosea. I think five ambassadors out of thirty plus embassies is more than a fair share for this little island.
   
 14. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Zanzibar kama wanahitaji kuwa na wawakilishi zaidi uwekwe mpango kamambe ili wawalipie mishahara n.k. kutoka bajeti yao ya serikali ya mapinduzi na tuache kutumia hovyo pesa za walipa kodi kwa uchu wa madaraka.

  Hivi sasa serikali ya Zanzibar ina wawakilishi wengi sana per head katika serikali na sina uhakika kama kweli wote wanahitajika kulipwa pesa nyingi hivyo bila kazi za kueleweka.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160

  Kwa Taarifa tu:
  Hakuna tena utaratibu wa kuingia Zenj kwa passport, Wabara wanaruhusiwa kupiga kura ili mradi tu awe ameishi Zenj zaidi ya miaka mitano, na Hao Machangudoa wamejaa tele na wanafanya kazi zao bila bughuza.
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  as long as kuna serikali mbili .....zanzibar lazima kila siku watakuja na jipya
  kwa sababu it doesnt make sense kuwa nchi mbili ziungane zifanye serikali mbili, ilitakiwa iwe moja au tatu!
  kwa manufaa na kuwaridhisha watanzania wote, mie ningependekeza serikali tatu na si moja.
   
 17. Gigo

  Gigo JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2007
  Joined: Aug 6, 2006
  Messages: 455
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  wako sawa...They Are so creative!!!
   
 18. Gigo

  Gigo JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2007
  Joined: Aug 6, 2006
  Messages: 455
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Nilisha wahi kusema... serikali moja..Mabunge mawili...
  La sivyo..Hili wazo ni sawa...!!
   
 19. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2007
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  nadhani hapo ni kutafuta mgongano katika balozi, mathalani
  -huyo mwakilishi wa zanzibar ubalozini atakuwa anaripoti kwa nani?
  - kama tayari kuna muwakilishi wa zanzibar ubalozini sas balozi atakuwa anawakilisha tanzania, tanzania bara au tanganyika?
  - je mshahara wa huyo muwakilishi utatoka katika fungu gani?

  ninavyofahamu mimi katika baadhi ya balozi wapo maafisa kutoka zanzibar lakini wanafanatambulika kama maafisa wengine wa ubalozi wanaotokea bara yaani maafisa wa ubalozi wa tanzania.
   
 20. _SiDe_

  _SiDe_ Member

  #20
  Dec 7, 2007
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wakuu haya yote yamo kwenye matatizo ya Muungano wetu, tokea miaka hiyo hadi sasa kuna kilio ya kuwa hakuna usawa katika Muungano, tume lukuki zimeundwa na watu kuchukuwa chao just kufunika kombe mwanaharamu apite, hakuna hata tume moja iliosikilizwa. Wakati umefika sasa wa kuja na KATIBA mpya na then MUUNGANO mpya. Na ikiwezekana hata kuku wa Tz ajue details za Muungano huo achilia raia wa Tz!
  muungano huu sio kabsaa, Tatu sio mbili. Mazungumzo ya Nahodha na EL kuhusu kero za Muungano sawa CUF na CCM, hayana mwisho. Wao watazungumza na wengine watafuatia kuzungumza.
  yangu macho tu!
   
Loading...