Ninakubali na sikatai kabisa mkuu.Na vipi hizi taharuki,Kwa sababu kila kukicha ni yupo wapi?yupo wapi? Na inafika hatua watu wanasema na yeye ni kama harakaharaka,je hata kama wananchi wanapaswa kujua ni kwa style hii?
Ni kweli watu wanajitaji kujua kiongozi wao wanayemwamini yuko wapi?
Sikatai kabisa,jee ni sawa kuja na maneno yeny ukakasi kama hao wanaosema “NA YEYE WAMEONDOKA NAYE.
Hivi wakuu
Kiranga na
Mwaka wa Mbele mzaweza kuniambia,kwamba Mzee Imma atakuja na kusema mimi nipo hapa,au swali lingine ni kwamba mnataka afanye kitu gani ili kujua kama yupo.
Anyway Tuseme hivi,kwa mfano
Mwaka wa Mbele na
Rebeca 83 kwa uelewa wenu ikiwa mimi ninawauliza ETI WAKUU YUPO WAPI?
Mtanijibu vipi?
Kwa lengo la kueleweshana
Habari ya Asubuhi.
Kuna msemo wa Kiingereza "Nature abhors a vacuum".
Kwenye physics tuliosoma tunajua hakuna vacuum ya kweli, there are always virtual particles popping up to fill any vacuum.
Hivyo hivyo, kwenye mambo ya information, ulimwengu hautaki ombwe la habari.
Ukiwa katika position ya kutoa habari, halafu ukaificha habari, ukaacha kukawa na vacuum ya habari, watu hawakubali kuwe na ombwe la habari. Watatunga habari zao za kweli au uongo na kujaza hilo ombwe.
Serikali ina wajibu wa kumtoa Nchimbi aongee na watu, ajibu maswali.
Ila, inaonekana haitaki kufanya hivyo kwa sababu Nchimbi labda kuna vitu amelazimishwa kufanya, kuna wengine wanasema ameteswa, kuna wengine wanasema ... mambo yanayosemwa ni mengi na namna pekee ya kupata uhakika hata kwamba Nchimbi yupo hai na hajauawa, ni Nchimbi kuwekwa mbele ya watu ajibu maswali.
Lakini serikali haitaki kufanya hivyo. Na hilo linaonesha serikali inaficha kitu haina uwazi.
Na hivyo, kudai Nchimbi ajitokeze ni kudai uwazi katika uongozi wa Tanzania. Hili suala ni zaidi ya Nchimbi.
Tumeweka precedent mbaya ya Makamu wa Rais kujiuzulu kwa tweet, halafu anapotea.
Na hata hatujui kwamba tweet ni yake kweli.
Sasa mtu akimuua Rais akamzika kwa siri, halafu akatuma barua ya Rais kujiuzulu, bila ya sisi kumuona Rais, tutawezaje kukataa kuwa Rais hajajiuzulu kama tushakubali Makamu wa Rais kujiuzulu kwa tweet bila ya yeye kuonekana, bila hata ya kuthibitisha hiyo tweet imetumwa kweli na Makamu wa Rais?
Kuuliza Nchimbi yuko wapi si chanzo cha taharuki, chanzo cha taharuki ni Nchimbi kutoonekana. Sasa kwa nini unashangaa watu wanaouliza Nchimbi yuko wapi na kuona wanaleta taharuki lakini hushangai Nchimbi haonekani, hatujui hata kama kajiuzulu, hatujui hata kama yupo hai, huoni hilo ndilo chanzo cha taharuki?
Yani unamshangaa vipi mtu anayesema Samia kajamba, na kuona analeta taharuki, lakini humshangai Samia mwenyewe aliyejamba kama chanzo cha taharuki?
Nchimbi, kama yupo hai, anatakiwa kuongea na wananchi ili.
1. Watu wajue yupo hai, yupo na hali gani na hajauawa.
2. Watu wajue kajiuzulu kweli na hajafichwa tu.
3. Watu wajue ile barua iliyosambaa aliandika yeye ama la.
4. Watu wajue sababu za kweli za kujiuzulu kwake.
5. Watu wapate sababu za kumuhoji kwa kina, kumuwajibisha na kujua wategemee nini mbele.
Haya yote ni sehemu za haki za kikatiba za Watanzania, kwa nini watu wakidai haki zao za kikatiba unaona ni taharuki?