Kabla hujatoa tamko kama hilo hadharani ongelea vigezo vilivyotumika na uonyeshe jinsi ambavyo aliyekuwa na vigezo hivyo kumshinda Messi alidhulumiwa. Kwa taarifa ni kuwa vigezo ni pamoja na kufunga magoli, kutoa pasi za mwisho kupata goli, kutokupoteza pasi na kucheza vizuri kwa ujumla. Na vigezo hivi vinatumika KILA MECHI ndio maana kila mechi kuna "man of the match". Sasa ndugu yangu, hao kina Robben, Muller, au Rodrigues walikuwa "man of the match" mara ngapi? Yeye Messi alikuwa man of the match mara 4 katika fainali hizo. Ni mchezaji yupi aliyemzidi Messi kuwa "man of the match"? Kama hakuna nadhani HAKUNA HOJA ya kuhoji ushindi wa Messi. Kwa wale wenye kumbukumbu wakati fainali kama hizi zilipofanyika Korea na Japan aliyeshinda uchezaji bora alikuwa GOLIKIPA Oliver Khan wa Germany. This was IN ADDITION to being the best goalkeeper. Hakufunga goli hata moja na nchi yake haikuchukua ubingwa waliochukua ubingwa walikuwa Brazil. Tena mbaya zaidi ile mechi ya finali Khan alifanya uzembe na kusababisha goli la kwanza lakini kwa vile overall alicheza vizuri katika mashindano bado tuzo yake aliipata. Hakupata Ronaldo de Lima wala Rivaldo ambao walikuwa na magoli mengi na nchi yao ikatwaa kombe. Wala hakuwa Ronaldinho ambaye wakati ule alikuwa star kwenye timu ya Brazil. Wengine wanadai CNN, BBC, etc wameponda tuzo ya Messi. Sio misimamo ya hizo TV station bali ni baadhi ya watu waliotoa maoni yao kwenye hizo Tv stations. Ni kama hapa JF , mtu hawezi kusema kuwa JF wameponda tuzo ya Messi kwa vile wewe umeiponda.