Haika Lawere wa 'Mbezi Garden' apewa Talaka

Haika Lawere wa 'Mbezi Garden' apewa Talaka

Anaandika MUME (Phares Magesa):

Watu wengi kwa muda mrefu zaidi ya miaka 4 sasa wamekuwa wakiuliza maswali katika baadhi ya posts zangu mama wa watoto hawa mbona hawamuoni ? kwenye picha nyingi ukiacha chache chache sana za matukio muhimu au labda hata kwenye posts za mama yao pia labda baadhi ya watu nao wanauliza/wanajiuliza swali kama hilo .

Ukweli upo hivi;

Mwaka 2001 Phares Magesa na Haika tulioana na ndoa ilifungwa katika Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), mtaa wa Ally Khan, Upanga karibu na DIT au Regency Hospital, sherehe ya harusi baadae ilifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na watu takribani 1,000 wakati ule, sherehe ilifana sana MC alikuwa FomaFoma.

Wakati namuoa Haika alikuwa ni Mwanafunzi anasomea Shahada ya kwanza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na akamaliza vizuri licha ya kuwa kwenye ndoa akiwa mwanafunzi, na tukiwa ndani ya ndoa nikamshauri asiridhike na elimu aliyoapata na nikamruhusu akasome Shahada ya Uzamili, akaenda Salford University, Uingereza nako pia akamaliza vizuri masomo yake na kwa neema ya Mungu baada ya hapo tukajaliwa watoto wazuri watatu, wawili wa kiume Paxton na Haris na mmoja wa kike Princess.

Mungu amekuwa mwema sana kwetu ametusaidia sana kwa kutuwezesha kufanya kazi na biashara zetu kila mmoja kwa bidii, maarifa, nidhamu na kujituma kwa hali ya juu na kufanikiwa kadri Mungu alivyotujalia.

Baada ya kuwa katika ndoa kwa miaka 21, yaani 2001 hadi 2022 Mahakama ya Mwanzo, Kawe, Kinondoni ilihitimisha shauri la talaka lililokuwa mahakamani hapo kwa takribani mwaka mmoja na kuanzia 2022 kila mmoja akawa huru na kwa sasa tunashirikiana vizuri kulea watoto wetu (Co-Parenting) na tunashukuru Mungu kwa yote.

Ushauri kama hakuna sababu ya msingi ya kuachana na mwenza wako, sishauri wanandoa wowote hasa kama mkiwa na watoto kufikia kirahisi uamuzi wa kuvunja ndoa ni mpaka pale itakapokuwa hiyo ndio njia salama na ya lazima kwa mustakabali mwema wa pande zote tatu yaani Mke, Mme na Watoto.

Usiingie kwenye ndoa kwa nia ya kutaka kuonekana na wewe umo au kwa nia ya ku trend, pia usiachane na mtu kwa sababu hizo hizo.

Mbarikiwe wote mlio kwenye ndoa zidumu na mnaotaka kuingia pia ndoa zidumu,tumtangulize Mungu na kujali famlia zetu.
Ahmad Issa Michuzi on Instagram: "Msikilize kijana huyu Haris Phares Magesa ambaye ni mto wa Nguli wa mambo ya 'IT' kitaifa na Kimataifa @pmagesa akishangaa wanaofeli mitihani ya @nectatz,@nactvet haris_with_one_r_"
View attachment 3561971
Exactly
 
Mm kama mtu niliyefanyia kazi hayo maswala nakukatalia mpaka kesho ukweli ni kwamba hao wanaomwamini yesu ni waumini pia wa Mali kuliko utu.
Masaki, mwenge na kwingine Kuna wajane wengi kuliko mbagala na kwingine unajua sababu
Kuna upande watu wanaoana na kwingine wanao.
Fanya research
Hiyo sensa ya Wajane WEngio MASAKI NA MWENGE kulko kwenu hapo Mbagala kibonde maji na kwa mbiku sababu mbona zipo wazi.
MASAKI mtaa mmoja una nyumba kumi , kwenu Kibonde maji ni nyumba moja ya kupanga , yaani ukingia uani kuna wapangaji 15n na choo kimoja cha nje, hivyo mtaa ukiwa na wajane wawili Masaki ni sawa na nyumba moja ya Kwenu madongo poromoka.
 
Usiogope ndoa, cha muhimu ni kama upo na mali nyingi na unataka kulinda mali zako ikiwa ndoa itavunja basi cha kufanya ni tafuta mwanasheria na ujifunze kitu kinaitwa prenuptial agreement kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Kisha mweleweshe mtarajiwa (mke mtarajiwa) kuhusu hiyo Pre-nuptial Agreement, kisha atasaini.

Binafsi, mtazamo wangu, sioni ubaya kugawana mali na mtu ambaye nimezaa nae (it's for the sake of our children), hata ikifika point tumeshindwana na haiwezekani tena, basi ni ishu ya kutuliza mihemko na kukaa chini mkaongea na makubaliano yakafikika, kisha mkagawana.
So, unataka ukae na mtu 20-yrs halafu mkiachana unataka asipate kitu? Daah sio fair at all.

Tanzania hakuna "Prenuptial Agreement" au Prenups. Tanzania sio Marekani.
Do your homework. Hakuna prenups Tanzania. Soma sheria ya ndoa vizuri mkuu. Hakuna pre Agreement yeyote inayokuwa valid mara baada ya ndoa yenu, iwe ya kiserikali, kidini au kimila.
 
Mosha alikuwa mjanja, Mosha mali nyingi aliziweka kwenye makampuni ambayo mkewe aliyakuta. Mosha kaokoa mali kibao kupigwa pasu. Usipojua kuficha mali ukiwa kwenye ndoa za mitego, zitaibiwa kwa talaka.

Hili somo mzee wangu akishanieleza sana. Talaka ni wizi, ni ufilisi wa wazi. Talaka inakutoa upepo. Unapoteza mali kwa mujibu wa sheria. Unapigwa pasu jasho lako ulilotoa kwa miaka mingi. Mali yote uliyochuma ukiwa na nguvu inaondoka, inakuwa sio yako tena na wengine wanaenda kuila. Kama una 100 basi unabaki na 40. Tragedy of miscalculation
Aisee ulipata darasa zuri Toka kwa Mzee,safi sana
 
Sema wameachana kisomi sanaaa..

sema mambo ya ndoa ukiwaza sana na ukiona mambo yake power inakata aisee
Sikia kwa watu mkuu yasiksukute sie wengine siku 31 zilikuwa nyingi tukachapalapa nakuacha kodi ya mwaka nkasema bora abaki na kodi kuliko mambo yageuke mbelen tuanze kuulizana umechuma ngapi napata ngapi woii

Ahimidiwe Mungu alienipa nguvu ya kufanya maamuxi mapemaaaaaaa
Kunikomboa na magonjwa ya shinikizo la damu nk mbelen
 
Sikia kwa watu mkuu yasiksukute sie wengine siku 31 zilikuwa nyingi tukachapalapa nakuacha kodi ya mwaka nkasema bora abaki na kodi kuliko mambo yageuke mbelen tuanze kuulizana umechuma ngapi napata ngapi woii

Ahimidiwe Mungu alienipa nguvu ya kufanya maamuxi mapemaaaaaaa
Kunikomboa na magonjwa ya shinikizo la damu nk mbelen
Sasa hivi ndoa zimekuwa kama uwanja vita kinpindi kile kule Baghdad 😂😂 Hujui kesho mwenzako anaweza amka na kichaa gani na maamuzi yepi
 
Hawa watto wamesoma FEZA , ni wanafunzi bora Tanzania na pia ni wapo vyuo vikubwa Ulaya kuiwakilisha Tanzania.
Mama yao ni mmilii wa Mbezi Garden , wamegawana na mume baada ya kuachana lakini ni muhimu sana kwa wanaume kuwa makini na hizi ndoa za kuoana mkiwa chuo, unakuta binti ni bikra ama wewe ndio mwanaume wa pili kupita hapo, ikifika siku DUNIA IKAMFUNGUKIA mnaachana maana atakutana na fupi, ndefu, nyembamba na nene.
Kulingana na maelezo yako basi mambo ya wananwake magumu sana. (Unakuta ni bikra au wewe ndio mwanaume wa pili). Sasa uwe wa ngapi ndio salama?!
 
Back
Top Bottom