Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 16,095
- 24,323
Anaandika MUME (Phares Magesa):
Watu wengi kwa muda mrefu zaidi ya miaka 4 sasa wamekuwa wakiuliza maswali katika baadhi ya posts zangu mama wa watoto hawa mbona hawamuoni ? kwenye picha nyingi ukiacha chache chache sana za matukio muhimu au labda hata kwenye posts za mama yao pia labda baadhi ya watu nao wanauliza/wanajiuliza swali kama hilo .
Ukweli upo hivi;
Mwaka 2001 Phares Magesa na Haika tulioana na ndoa ilifungwa katika Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), mtaa wa Ally Khan, Upanga karibu na DIT au Regency Hospital, sherehe ya harusi baadae ilifanyika ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na watu takribani 1,000 wakati ule, sherehe ilifana sana MC alikuwa FomaFoma.
Wakati namuoa Haika alikuwa ni Mwanafunzi anasomea Shahada ya kwanza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na akamaliza vizuri licha ya kuwa kwenye ndoa akiwa mwanafunzi, na tukiwa ndani ya ndoa nikamshauri asiridhike na elimu aliyoapata na nikamruhusu akasome Shahada ya Uzamili, akaenda Salford University, Uingereza nako pia akamaliza vizuri masomo yake na kwa neema ya Mungu baada ya hapo tukajaliwa watoto wazuri watatu, wawili wa kiume Paxton na Haris na mmoja wa kike Princess.
Mungu amekuwa mwema sana kwetu ametusaidia sana kwa kutuwezesha kufanya kazi na biashara zetu kila mmoja kwa bidii, maarifa, nidhamu na kujituma kwa hali ya juu na kufanikiwa kadri Mungu alivyotujalia.
Baada ya kuwa katika ndoa kwa miaka 21, yaani 2001 hadi 2022 Mahakama ya Mwanzo, Kawe, Kinondoni ilihitimisha shauri la talaka lililokuwa mahakamani hapo kwa takribani mwaka mmoja na kuanzia 2022 kila mmoja akawa huru na kwa sasa tunashirikiana vizuri kulea watoto wetu (Co-Parenting) na tunashukuru Mungu kwa yote.
Ushauri kama hakuna sababu ya msingi ya kuachana na mwenza wako, sishauri wanandoa wowote hasa kama mkiwa na watoto kufikia kirahisi uamuzi wa kuvunja ndoa ni mpaka pale itakapokuwa hiyo ndio njia salama na ya lazima kwa mustakabali mwema wa pande zote tatu yaani Mke, Mme na Watoto.
Usiingie kwenye ndoa kwa nia ya kutaka kuonekana na wewe umo au kwa nia ya ku trend, pia usiachane na mtu kwa sababu hizo hizo.
Mbarikiwe wote mlio kwenye ndoa zidumu na mnaotaka kuingia pia ndoa zidumu,tumtangulize Mungu na kujali famlia zetu.