Haiba ya Kinana na CCM

Haiba ya Kinana na CCM

Wakuu Ritz na chama njooni hapa mje kusaidia kujibu hizi shutuma alizotupiwa huyo jangili wenu

Kila siku tutakuwa tunajibu vitu vilevile mbona nyie makamanda akili zenu zimekuwa pungufu kiasi? Yaani yamekuwa yaleyale ya babu tukilala EPA tukiamka EPA anasahau kuwa mmoja wa viongozi wenzake ni wakili mwandamizi kwenye kesi za EPA; njooni na mpya; mnataka mpaka tembo wetu watoe ushahidi kwamba mh.Kinana sio jangili ndio muamini?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hiv haya Maswali Walisahau kumuuliza Kikwete alipokuwa France sijui angejibu vp hapa.
 
Kila siku tutakuwa tunajibu vitu vilevile mbona nyie makamanda akili zenu zimekuwa pungufu kiasi? Yaani yamekuwa yaleyale ya babu tukilala EPA tukiamka EPA anasahau kuwa mmoja wa viongozi wenzake ni wakili mwandamizi kwenye kesi za EPA; njooni na mpya; mnataka mpaka tembo wetu watoe ushahidi kwamba mh.Kinana sio jangili ndio muamini?

Chama
Gongo la mboto DSM

aliyekuroga keshakufa
 
hapa pagumu mkuu.Hata mimi sigusi.atajibu Mzee mwenyewe.

Nimekuona una busara ndugu, mambo mengine sio ya kichama, ni mtu binafsi na udhaifu wake, tatizo kuna wengine wanakurupuka kutetea kila kitu kisa tu aliyetuhumiwa ni mwanachama mwenzao, mwisho wanaishia kukifanya chama chote kionekane kichafu kwa uchafu wa watu binafsi ndani ya chama.
 
Kwenye gazeti la Mwananchi la leo kurasa ya 9 kuna habari yenye kichwa cha habari "basi la Mtei lataifishwa kwa kubeba wahamiaji haramu"..
Kinana kampuni yake imesafirisha meno ya tembo.. hakuna hatua yeyote iliochukuliwa.. Ndo kwanza mwenyewe ameula kwa kupewa ukatibu Mkuu ccm.. Baci la Mtei limekamatwa na wahamiaji limetaifishwa.. Na mmiliki wa basi hilo hata hakuwapo wala kujua kama basi lake limefanya hivyo..!
Double standard.. Unless wakubali kwamba ujangili ndo part of their policies..
 
Kwa hiyo katika ajali za Barabarani ni kosa la waziri wa usafirishaji pia? Kinana ni Msafi

wizara ya usafirishaji siyo mali ya waziri hivyo hawezi kuwajibishwa kwa kosa la ajali inapotokea barabarani.anae wajibika ni yule anae sababisha hiyo ajali.kampuni iliyosafirisha meno ya tembo ni mali ya Kinana.kampuni iliyosafirisha haijachukuliwa hatua yoyote na serekali ya ccm.Kinana mwenyewe hajachukuwa hatua zozote kwa watumishi waliyosafirisha shehena hiyo zaidi ya kukili kuwa kampuni ni mali yake.kitendo cha Kinana kushindwa kumchukulia hatua yoyote mtumishi wake ambaye amemwajiri yeye mwenyewe kinaonyesha kuwa Kinana alikuwa anafaham kinacho fanyika ni kitu gani kama siyo muhusika moja kwa moja.
 
hapa pagumu mkuu.Hata mimi sigusi.atajibu Mzee mwenyewe.

Toka nianze kuona michango yako.. leo ndo nimeona comment yako ambayo imewakilisha ur true opinion.. Mambo mengine kuyapinga haimaanishi u ain't loyal kwa ur party..
 
chama na watendaji wote sio wasafi atakuja kuwa kinana wa juzi tu ambaye amewekwa hapo ili biashara ifanyike vizuri na kwa urahisi
 
Kila siku tutakuwa tunajibu vitu vilevile mbona nyie makamanda akili zenu zimekuwa pungufu kiasi? Yaani yamekuwa yaleyale ya babu tukilala EPA tukiamka EPA anasahau kuwa mmoja wa viongozi wenzake ni wakili mwandamizi kwenye kesi za EPA; njooni na mpya; mnataka mpaka tembo wetu watoe ushahidi kwamba mh.Kinana sio jangili ndio muamini?

Chama
Gongo la mboto DSM

ukiona jambo linajirudiarudia ujue kuwa majibu yanayotolewa ni ya kisanii.
 
ukiona jambo linajirudiarudia ujue kuwa majibu yanayotolewa ni ya kisanii.

Kila kitakochosemwa mtapinga kwasababu mna ajenda zenu naona iliyobaki tupate tembo wa kutoa ushahidi hapo ndio roho zenu zitatulia

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kila kitakochosemwa mtapinga kwasababu mna ajenda zenu naona iliyobaki tupate tembo wa kutoa ushahidi hapo ndio roho zenu zitatulia

Chama
Gongo la mboto DSM

tunaendelea kupinga kwa sababu mnaendelea kutudanganya.swala la kuwaleta tembo kuthibitisha kuwa Kinana siyo jangiri ni la mtuhumiwa mwenyewe kwani siyo kazi ya mlalamikaji kumpangia mtuhumiwa shahidi wa kumtetea.
 
imeandikwa na bart mkinga.

Hivi karibuni kampuni ambayo kati ya wamiliki wake ni-abrahaman kinana, katibu mkuu wa ccm, ilihusika na usafirishaji wa pembe za ndovu kinyume na sheria za nchi, kinyume na sheria za kimataifa.
-
vyombo vya habari viliripoti kuwa kinana mwenyewe alikiri kuwa kampuni yake ilihusika na usafirishaji wa shehena hiyo haramu lakini kampuni haikujua kuwa shehena ile ilikuwa ya biashara haramu.
-
kwa mtazamo mpana, kashfa hii na utetezi wa kinana, kweli unatosha kumsafisha kiongozi mkuu huyu wa chama tawala na kashfa hii? Hivi kampuni wakala wa usafirishaji mizigo husafirisha mzigo wowote bila ya kujiridhisha kuwa mzigo unaosafirishwa ni mzigo uliotajwa kwenye nyaraka za usafirishaji? Mara nyingi katika biashara, mtoa huduma huwa na wateja wake wa muda mrefu na wale wa mara moja. Kutokana na kushamiri kwa biashara haramu ya pembe za ndovu, je, kampuni hii ya usafirishaji wa bidhaa haramu inayomhusisha kiongozi mkubwa wa chama tawala, imesafirisha mizigo ya aina hii mara ngapi bila ya kukamatwa? Wamiliki wa mizigo hiyo haramu waliichagua kampuni ya mheshimiwa huyu kwa bahati mbaya au kulikuwa na sababu maalum ya kuichagua kampuni hii?
-
swali jingine la kujiuliza, kumiliki kampuni inayosafirisha bidhaa haramu, japo inawezekana kinana ni mmiliki tu wa kampuni na asiwe mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni, je, hiyo pekee yake inaweza kuwa ni sababu tosha ya kumwona mh. Kinana ana usafi wa kuongoza chama ambacho kinadai kipo kwenye hatua ya kujisafisha?
-
ccm kama chama cha siasa na chama tawala, kinapojiangalia kwenye kioo cha kujitathmini kinajiona ni chama cha namna gani, wakati viongozi wake wakuu majina yao yanatajwatajwa kwenye biashara chafu? Kwenye mambo kama haya, ndipo tunaposhangaa umakini wa ccm.
-

Katika hali ya kawaida kabisa kama nchi inaendeshwa na watu wanaochukia kwa dhati kabisa kabisa ufisadi, ubadhirifu na hujuma ya aina yoyote katika taifa; kampuni husika na wamiliki wake pamoja na chombo kilichohusika kusafirishia bidhaa haramu (contraband); wanastahili kukamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kuhujumu uchumi wa taifa.

Kwa bahati mbaya sana Tanzania sio nchi ya aina hiyo!! Watawala wetu wanahusika kikamilifu katika kupanga, kusimamia na kuwalinda wahalifu ( fully embedded) katika kila aina ya uchafu wa aina hiyo!! Na hawako tayari kujitia kitanzi wala kumfunga kengele paka shingoni!!

Dawa pekee ya kulitibu taifa letu kutokana na saratani mbaya ya aina hii ni mapambano katika maana na mantiki zote za neno hilo. Aluta continua; mapambano yaendelee kwa manufaa ya vizazi vyetu vijavyo.
 
tunaendelea kupinga kwa sababu mnaendelea kutudanganya.swala la kuwaleta tembo kuthibitisha kuwa Kinana siyo jangiri ni la mtuhumiwa mwenyewe kwani siyo kazi ya mlalamikaji kumpangia mtuhumiwa shahidi wa kumtetea.

Kama hoja ni ushahidi mh. Kinana aliweka wazi pamoja ya kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki; wao kama wakala wa kusafirisha mizigo hawahusiki kukagua mzigo hilo ni jukumu la mamlaka husika; wanaopaswa kuulizwa ni wafanyakazi wa mamlaka zinazohusika waliofanya ukaguzi wa mzigo; msafirishaji anachopatiwa ni vielelezo au documents zinazoonyesha ni vitu gani vimo ndani ya kontena; na Kinana pamoja na kuwa ni mmoja wa wamiliki yeye hausiki na daily operations za kampuni ni kitu gani hapo ambacho umeshindwa kuelewa?
 
Imeandikwa na Bart Mkinga.

Hivi karibuni kampuni ambayo kati ya wamiliki wake ni-Abrahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, ilihusika na usafirishaji wa pembe za ndovu kinyume na sheria za nchi, kinyume na sheria za kimataifa.
-
Vyombo vya habari viliripoti kuwa Kinana mwenyewe alikiri kuwa kampuni yake ilihusika na usafirishaji wa shehena hiyo haramu lakini kampuni haikujua kuwa shehena ile ilikuwa ya biashara haramu.
-
Kwa mtazamo mpana, kashfa hii na utetezi wa Kinana, kweli unatosha kumsafisha kiongozi mkuu huyu wa chama tawala na kashfa hii? Hivi kampuni wakala wa usafirishaji mizigo husafirisha mzigo wowote bila ya kujiridhisha kuwa mzigo unaosafirishwa ni mzigo uliotajwa kwenye nyaraka za usafirishaji? Mara nyingi katika biashara, mtoa huduma huwa na wateja wake wa muda mrefu na wale wa mara moja. Kutokana na kushamiri kwa biashara haramu ya pembe za ndovu, Je, kampuni hii ya usafirishaji wa bidhaa haramu inayomhusisha kiongozi mkubwa wa chama tawala, imesafirisha mizigo ya aina hii mara ngapi bila ya kukamatwa? Wamiliki wa mizigo hiyo haramu waliichagua kampuni ya mheshimiwa huyu kwa bahati mbaya au kulikuwa na sababu maalum ya kuichagua kampuni hii?
-
Swali jingine la kujiuliza, kumiliki kampuni inayosafirisha bidhaa haramu, japo inawezekana Kinana ni mmiliki tu wa kampuni na asiwe mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni, je, hiyo pekee yake inaweza kuwa ni sababu tosha ya kumwona Mh. Kinana ana usafi wa kuongoza chama ambacho kinadai kipo kwenye hatua ya kujisafisha?
-
CCM kama chama cha siasa na chama tawala, kinapojiangalia kwenye kioo cha kujitathmini kinajiona ni chama cha namna gani, wakati viongozi wake wakuu majina yao yanatajwatajwa kwenye biashara chafu? Kwenye mambo kama haya, ndipo tunaposhangaa umakini wa CCM.
-
nakwambia kwa ccm,yanayooneka mauvu mbele ya uma,kwao ni sifa kubwa,yaani hao wanahangaika nalaana za mwlm.wewe angalia tu safu yao ya uongozi utaona majambazi na majizi yote ndiyo yaliyoshinda kwa kishindo.sasa kinana akisafirisha hizo pembe za ndovu ndo kwanza anazidi kuwa juu ndani ya chama.
 
Naamini hizo pembe za ndovu ni biashara za ccm ndiyomaana mpaka sasa hakuna hatua iliyochukuliwa.
 
Back
Top Bottom