Haiba ya Kinana na CCM

Haiba ya Kinana na CCM

Hata akishuka malaika kutoka mbinguni kuja kukuelimisha kuhusu ubaya wa msukule wako unaojitahidi kuusafisha hutamuelewa.Endelea kuusafisha msukule wako nayo ni demokrasia.

Dhambi ya udhanifu ndio inayokudumaza! Huyo malaika angeshuka kukuelemisha wewe kwanza unahitaji sana msaada akili yako kidogo inaonekana haipo barabara

Chama
Gongo la mboto DSM
 
chama na Ritz mpaka sasa mmeshindwa kujadili kwa kugusa ingalau mzizi wa mada na kujikita kwenye hoja. Mna mbwelambwela tu kwa maneno ya kuokoteza ili kukwepa hoja za msingi.

Naomba mnijibu haya acheni porojo.

1. Je haiba ya kinana kwenye raslimali za nchi hasa pembe za ndovu ina faa kutiliwa mashaka?! Kama 'ndio' ni kwa nini na kama jibu ni 'sio' ni kwa nini?

2. Kutaifishwa kwa basi la Mtei kwa kubeba wahamiaji haramu huku kampuni ya katibu wa chama nayo ikikamatwa na nyara haramu na yeye kukiri kuwa kampuni ni yake huku mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa dhidi yake ni double standard yenye kulindana au siyo?

Mkuu Mohamedi Mtoi
Usijifanye kama mtu zobe; naamini pamoja na kuwa umejiweka sana karibu na tutusa bado akili yako ina weledi wakuelewa mambo; tuanze na kampuni ya Kinana; labda kwanza ningekushauri ujifundishe namna kampuni za wakala wa mizigo zinavyofanya kazi; hii itakusaidia sana kupata fikra bora kabla hujajikita kwenye malumbano; kwa ufupi tu si jukumu la wakala kukagua kilichomo ndani; wewe msafirishaji ndiye unaye saini declaration ya kutaja unasafirisha mzigo gani; zipo mamlaka husika TRA na kitengo cha bandari wao ndio wanaokagua mzigo na kuweka seal kwenye kontena; kama ni kesi Kinana atakuwa shahidi upande wa mashtaka.
Wafanyakazi wa basi la Mtei wanahusika kwa asilimia 100% na hujuma hizo; walijua fika wanasafirisha wahamiaji haramu; walitakiwa kuviarifu vyombo husika; hata wewe siku ukiona basi la Mlalo limepanda wadigo 20 utajiuliza kulikoni hutakaa kimya; sembuse basi liliojaa waethiopi?
Mkuu naona huna hoja ya msingi zaidi ya kuokoteza hapa na pale kutoka Tanzania Daima; wakili wako Lissu anajua misingi ya sheria jaribu kumuuliza.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo katika ajali za Barabarani ni kosa la waziri wa usafirishaji pia? Kinana ni Msafi

Eti na wewe umejibu. Haya ndiyo majibu ya mashabiki wa ccm. Ungetegemea ccm wenyewe wakija majibu yataridhisha lakini yakitolewa chumba kizima kinanuka harufu ya kutokuwa makini, kutojali na kutojua uhalisia wa mambo.
Haya! kanyaga twende. Kinana msafi.
 
Mkuu Mohamedi Mtoi
Usijifanye kama mtu zobe; naamini pamoja na kuwa umejiweka sana karibu na tutusa bado akili yako ina weledi wakuelewa mambo; tuanze na kampuni ya Kinana; labda kwanza ningekushauri ujifundishe namna kampuni za wakala wa mizigo zinavyofanya kazi; hii itakusaidia sana kupata fikra bora kabla hujajikita kwenye malumbano; kwa ufupi tu si jukumu la wakala kukagua kilichomo ndani; wewe msafirishaji ndiye unaye saini declaration ya kutaja unasafirisha mzigo gani; zipo mamlaka husika TRA na kitengo cha bandari wao ndio wanaokagua mzigo na kuweka seal kwenye kontena; kama ni kesi Kinana atakuwa shahidi upande wa mashtaka.
Wafanyakazi wa basi la Mtei wanahusika kwa asilimia 100% na hujuma hizo; walijua fika wanasafirisha wahamiaji haramu; walitakiwa kuviarifu vyombo husika; hata wewe siku ukiona basi la Mlalo limepanda wadigo 20 utajiuliza kulikoni hutakaa kimya; sembuse basi liliojaa waethiopi?
Mkuu naona huna hoja ya msingi zaidi ya kuokoteza hapa na pale kutoka Tanzania Daima; wakili wako Lissu anajua misingi ya sheria jaribu kumuuliza.

Chama
Gongo la mboto DSM
Kawadanganye watoto
 
Kama hoja ni ushahidi mh. Kinana aliweka wazi pamoja ya kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki; wao kama wakala wa kusafirisha mizigo hawahusiki kukagua mzigo hilo ni jukumu la mamlaka husika; wanaopaswa kuulizwa ni wafanyakazi wa mamlaka zinazohusika waliofanya ukaguzi wa mzigo; msafirishaji anachopatiwa ni vielelezo au documents zinazoonyesha ni vitu gani vimo ndani ya kontena; na Kinana pamoja na kuwa ni mmoja wa wamiliki yeye hausiki na daily operations za kampuni ni kitu gani hapo ambacho umeshindwa kuelewa?

Kwa hiyo wewe na akili yako mmekubaliana na huu utetezi na mko confortable kabisa kuwa tukae kimya tu kuwa kinana hausiki katika hili? Hata jambazi siku ya kwanza kusomewa mashitaka huwa anakana tuhuma lakini baadaye unasikia ameswekwa segerea miaka 30, hivyo si jambo la ajabu kwa mwizi(jangili) mzoefu pia kukana tuhuma kwa mara ya kwanza lakini upekenyuzi ukifanywa na independent investigator mtakuta mambo ya aibu tupu!
 
Fanyeni huo uchunguzi wenu; lakini mpaka sasa hivi hakuna kinachomuunganisha Kinana na kontena taratibu za usafirishaji zipo wazi; na hilo ndilo tunalolisimamia.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Imeandikwa na Bart Mkinga.

Hivi karibuni kampuni ambayo kati ya wamiliki wake ni-Abrahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, ilihusika na usafirishaji wa pembe za ndovu kinyume na sheria za nchi, kinyume na sheria za kimataifa.
-
Vyombo vya habari viliripoti kuwa Kinana mwenyewe alikiri kuwa kampuni yake ilihusika na usafirishaji wa shehena hiyo haramu lakini kampuni haikujua kuwa shehena ile ilikuwa ya biashara haramu.
-
Kwa mtazamo mpana, kashfa hii na utetezi wa Kinana, kweli unatosha kumsafisha kiongozi mkuu huyu wa chama tawala na kashfa hii? Hivi kampuni wakala wa usafirishaji mizigo husafirisha mzigo wowote bila ya kujiridhisha kuwa mzigo unaosafirishwa ni mzigo uliotajwa kwenye nyaraka za usafirishaji? Mara nyingi katika biashara, mtoa huduma huwa na wateja wake wa muda mrefu na wale wa mara moja. Kutokana na kushamiri kwa biashara haramu ya pembe za ndovu, Je, kampuni hii ya usafirishaji wa bidhaa haramu inayomhusisha kiongozi mkubwa wa chama tawala, imesafirisha mizigo ya aina hii mara ngapi bila ya kukamatwa? Wamiliki wa mizigo hiyo haramu waliichagua kampuni ya mheshimiwa huyu kwa bahati mbaya au kulikuwa na sababu maalum ya kuichagua kampuni hii?
-
Swali jingine la kujiuliza, kumiliki kampuni inayosafirisha bidhaa haramu, japo inawezekana Kinana ni mmiliki tu wa kampuni na asiwe mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni, je, hiyo pekee yake inaweza kuwa ni sababu tosha ya kumwona Mh. Kinana ana usafi wa kuongoza chama ambacho kinadai kipo kwenye hatua ya kujisafisha?
-
CCM kama chama cha siasa na chama tawala, kinapojiangalia kwenye kioo cha kujitathmini kinajiona ni chama cha namna gani, wakati viongozi wake wakuu majina yao yanatajwatajwa kwenye biashara chafu? Kwenye mambo kama haya, ndipo tunaposhangaa umakini wa CCM.
-

Kali zaidi ni yale majibu ya Padri Slaa kuhusu kushawishiwa na Mushumbusi na kujichotea milion 140 za Saccos ya Kaskazin
 
Back
Top Bottom