Haiba ya Kinana na CCM

Haiba ya Kinana na CCM

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Imeandikwa na Bart Mkinga.

Hivi karibuni kampuni ambayo kati ya wamiliki wake ni-Abrahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, ilihusika na usafirishaji wa pembe za ndovu kinyume na sheria za nchi, kinyume na sheria za kimataifa.
-
Vyombo vya habari viliripoti kuwa Kinana mwenyewe alikiri kuwa kampuni yake ilihusika na usafirishaji wa shehena hiyo haramu lakini kampuni haikujua kuwa shehena ile ilikuwa ya biashara haramu.
-
Kwa mtazamo mpana, kashfa hii na utetezi wa Kinana, kweli unatosha kumsafisha kiongozi mkuu huyu wa chama tawala na kashfa hii? Hivi kampuni wakala wa usafirishaji mizigo husafirisha mzigo wowote bila ya kujiridhisha kuwa mzigo unaosafirishwa ni mzigo uliotajwa kwenye nyaraka za usafirishaji? Mara nyingi katika biashara, mtoa huduma huwa na wateja wake wa muda mrefu na wale wa mara moja. Kutokana na kushamiri kwa biashara haramu ya pembe za ndovu, Je, kampuni hii ya usafirishaji wa bidhaa haramu inayomhusisha kiongozi mkubwa wa chama tawala, imesafirisha mizigo ya aina hii mara ngapi bila ya kukamatwa? Wamiliki wa mizigo hiyo haramu waliichagua kampuni ya mheshimiwa huyu kwa bahati mbaya au kulikuwa na sababu maalum ya kuichagua kampuni hii?
-
Swali jingine la kujiuliza, kumiliki kampuni inayosafirisha bidhaa haramu, japo inawezekana Kinana ni mmiliki tu wa kampuni na asiwe mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni, je, hiyo pekee yake inaweza kuwa ni sababu tosha ya kumwona Mh. Kinana ana usafi wa kuongoza chama ambacho kinadai kipo kwenye hatua ya kujisafisha?
-
CCM kama chama cha siasa na chama tawala, kinapojiangalia kwenye kioo cha kujitathmini kinajiona ni chama cha namna gani, wakati viongozi wake wakuu majina yao yanatajwatajwa kwenye biashara chafu? Kwenye mambo kama haya, ndipo tunaposhangaa umakini wa CCM.
-
 
Kinana angekuwa chadema angefukuzwa ila kwa vile yuko ktk kundi la wahuni ataendelea kutamba.ccm siku zao zinahesabika
 
Wakuu Ritz na chama njooni hapa mje kusaidia kujibu hizi shutuma alizotupiwa huyo jangili wenu
 
Last edited by a moderator:
Nyerere aliwahi kuserma hivi Mke wa Kaissari hatakiwi KUTUHUMIWA.

Lakini Tanzania sio tu anatuhumiwa, bali anashikwa LIVE akimeng'enywa lakini bado Kaissari anaendelea naye!
 
Hivi Kinana anatuona Watanzania wote ni Ngumbaru kama wanachama wa CCM? Si rahisi kwa kampuni ya usafirishaji wa mizigo kusafirisha mzigo wasioujua;

kwanza ni kwa nia ya kuuthaminisha ili waweze kutoza gharama halisi kutokana na thamani wa kile wanachokisafirisha, pia katika karne hii ya Ugaidi wa kutisha duniani, ni lazima kukagua kile unachokisafirisha ili kisije kikawa ni silaha za kigaidi ambazo kama zitakamatwa na Mataifa kama Marekani, kitakutia matatizoni mmiliki wa kampuni inayotumika kusafirishia huo mzigo.

Leo hii huyu jamaa anakuja na Ngonjera ambazo ni wenye akili finyu tu ndio wanaoweza kuziamini eti hakujua anachokisafirisha! Kwa hiyo kuna siku atakuta anasafirisha hata viungo vya Albino! Huu si Uzembe wa bahati mbaya, jamaa ni lipiga dili sana la meno ya ndovu.

Eti jana nilimsikia yule kamanda wa polisi Radio One akidai kwamba polisi wanachunguza mwenye ule mzigo, wakati wanayo kampuni iliyousafirisha ambayo inamjua waliyefanya naye biashara ya kumsafirishia mzigo wake huo! Kweli nchi hii, Wonders shall never end!

Hii ndiyo serikali ya chama cha akina Nape Jeetu Patel bana!
 
Kwa hiyo katika ajali za Barabarani ni kosa la waziri wa usafirishaji pia? Kinana ni Msafi
 
Watu kama hawa ni kuweka sheria za kuwanyonga tu, period!
 
Mtandao wa Kuuza pembe za ndovu unawahusisha wakubwa wengi wa CCM kama mwenyekiti alimteua Kinana akijua kashfa hii ina maana na yeye amebariki Meli za Kinana ziendelee kufanya kazi ukumbuke meli haijashikwa mara moja na hivi tuulize Kinana toka kijana amekuwa mtumishi wa serikali lini mwenzetu alipata mapesa hadi kufikia kuwa na meli za kusafirisha mizigo dunia nzima Utoh uko wapi jamani
 
Hivi Nape ameshampata baba yake?akifanya upelelezi wa kina akagundua baba yake ni Kinana atatuambia au atahama ccm?
 
Nchi hii ni ya ajabu sana. Cha kushangaza Kinana hajawahi hata kuhojiwa na polisi kuhusiana na shehena ile ambayo ilikadiriwa kwa ni TEMBO 320 waliouliwa. Hata kumchunguza na kumuhoji ilikuwa ngumu. Je tuko serious kwenye kulinda rasilimali zetu kwa style hii. Mbaya zaidi kuna wimbi kubwa sana la wanajeshi wetu kutumika kwenye hii biashara na wengine wakitumia magari ya majeshi yetu, Je tembo watasalimika hadi 2015???

Chadema ileteni hii ishu ya katibu mkuu wa chama kujihusisha na ujangili kwa wananchi ili tumuhukumu sisi wenyewe maana dola yote ameiweka mfukoni. Pia wasomali wa Al-shabaab wanatuhumiwa kuongoza mtandao wa uwindaji wa tembo, na Kinana ni msomali, what a coincidence...
 
Wachafu wauaji laana maccm, Nape na maccm hapo mnasemaje? maana ulishasema mnywa gongo siyo mpaka akamatwe nayo mkononi, ajivue gamba mwenyewe.
Ingieni kiundani na mje na maadili, siyo kuongea mambo ya chekechea oh Slaa ana kadi yetu, oh CDM ni ya kaskazini....bla bla
 
Watanzania huwaga tunasifiwa tu wakarimu lakini ukarimu wetu inabidi utafutiwe jina jingine,hivi kweli ni binadam mwenye ukarimu gani na akili timamu anaweza akavumilia kuona vinavyoendelea tz? pesa ya kampeni inatafutwa kwa kuuza wanyama tena hai,mara epa,kagoda,meremeta halafu hao hao wezi wakisimama majukwaani eti wanashangiliwa na kujiita wakombozi! jamii inahitaji elimu wasichukulie kila kitu ni propaganda za kisiasa,inauma sana ukiyaona maisha wanayoyaishi huko vijijini na wengi wao ukuwakuta wamevalia kofia na t-shirt za kijani huku wanaonekana kukata shauri na maisha,tuwapeni elimu wananchi ili wamjue adui wao mkubwa na mchango wao wenyewe unaompa jeuri kuendelea kuwafukarisha,watu kama hawa ata mkiwafunga gerezani haitasaidia bali ingependeza mtu kam kinana na wenzake kunyongwa mpaka kufa tena hadharani wote waone,INAUMA SANA
 
he is an elephant dentist by profession

i wonder if nowadays elephants chew bubble gums or take candy sweets and chocolate bars
 
Hivi Kinana anatuona Watanzania wote ni Ngumbaru kama wanachama wa CCM? Si rahisi kwa kampuni ya usafirishaji wa mizigo kusafirisha mzigo wasioujua; kwanza ni kwa nia ya kuuthaminisha ili waweze kutoza gharama halisi kutokana na thamani wa kile wanachokisafirisha, pia katika karne hii ya Ugaidi wa kutisha duniani, ni lazima kukagua kile unachokisafirisha ili kisije kikawa ni silaha za kigaidi ambazo kama zitakamatwa na Mataifa kama Marekani, kitakutia matatizoni mmiliki wa kampuni inayotumika kusafirishia huo mzigo.
sio kuwa anatuona bali ndivyo tulivyo mkuu.
Angalia hapa, Mohamedi Mtoi ametoa maelezo ambayo sio mapya machoni na masikioni mwa watz na ni ushahidi tosha comconvict mtu yeyote duniani, tumefanya nini juu ya hili mbali na kuendelea kukikumbatia hiki chama chao?? Inasikitisha lakini hakuna jinsi
 
Imeandikwa na Bart Mkinga.

Hivi karibuni kampuni ambayo kati ya wamiliki wake ni-Abrahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, ilihusika na usafirishaji wa pembe za ndovu kinyume na sheria za nchi, kinyume na sheria za kimataifa.
-
Vyombo vya habari viliripoti kuwa Kinana mwenyewe alikiri kuwa kampuni yake ilihusika na usafirishaji wa shehena hiyo haramu lakini kampuni haikujua kuwa shehena ile ilikuwa ya biashara haramu.
-
Kwa mtazamo mpana, kashfa hii na utetezi wa Kinana, kweli unatosha kumsafisha kiongozi mkuu huyu wa chama tawala na kashfa hii? Hivi kampuni wakala wa usafirishaji mizigo husafirisha mzigo wowote bila ya kujiridhisha kuwa mzigo unaosafirishwa ni mzigo uliotajwa kwenye nyaraka za usafirishaji? Mara nyingi katika biashara, mtoa huduma huwa na wateja wake wa muda mrefu na wale wa mara moja. Kutokana na kushamiri kwa biashara haramu ya pembe za ndovu, Je, kampuni hii ya usafirishaji wa bidhaa haramu inayomhusisha kiongozi mkubwa wa chama tawala, imesafirisha mizigo ya aina hii mara ngapi bila ya kukamatwa? Wamiliki wa mizigo hiyo haramu waliichagua kampuni ya mheshimiwa huyu kwa bahati mbaya au kulikuwa na sababu maalum ya kuichagua kampuni hii?
-
Swali jingine la kujiuliza, kumiliki kampuni inayosafirisha bidhaa haramu, japo inawezekana Kinana ni mmiliki tu wa kampuni na asiwe mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni, je, hiyo pekee yake inaweza kuwa ni sababu tosha ya kumwona Mh. Kinana ana usafi wa kuongoza chama ambacho kinadai kipo kwenye hatua ya kujisafisha?
-
CCM kama chama cha siasa na chama tawala, kinapojiangalia kwenye kioo cha kujitathmini kinajiona ni chama cha namna gani, wakati viongozi wake wakuu majina yao yanatajwatajwa kwenye biashara chafu? Kwenye mambo kama haya, ndipo tunaposhangaa umakini wa CCM.
-
majibu ya wanamagamba ni kwamba,yale hayakuwa meno ya tembo ni plastic
 
Back
Top Bottom