Taarifasahihi
Senior Member
- May 24, 2019
- 170
- 157
Yaani siku hizi Delivery Note ni nyaraka ya taarifa ya manunuzi? kweli??taarifa za manunuzi (Delivery Note )
Yaani siku hizi Delivery Note ni nyaraka ya taarifa ya manunuzi? kweli??taarifa za manunuzi (Delivery Note )
Hahahaaaa........ Alitaka kusema invoice!Yaani siku hizi Delivery Note ni nyaraka ya taarifa ya manunuzi? kweli??
Kati ya jamaa wa serikali hii ambao siwaelewi ni huyu DC. Mkurupukaji mnoHivi huyu jamaa hajamsikia Rais kasema nini? kwani mafuta ya kula yanatumika wakati wa Ramdhan tu baada ya hapo sawa kupandisha. mafuta yameanza kupanda bei kabla ya Ramadhan na hakuna mtu anakulazimisha kununua kitu kwa bei ya juu duka hili limekushinda nenda duka jingine biashara yoyote ni demand and supply ndio ina control bei, acheni siasa katika biashara
Umejuaje mkuu kama alitaka kusema invoice? Labda useme alitakiwa kusema Invoice, pengine maskini wa Mungu inawezekana hata hajui tofauti kati ya Invoice na delivery Note!!Hahahaaaa........ Alitaka kusema invoice!
Jambazi anaweza kumkemea nani,atulie tu tunamalizana nae siku si nyingiMkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amewajia juu wafanyabiashara waliopandisha bei ya mafuta ya kula wilayani humo na kutoa saa 24 kujitafakari kabla hajazinguana nao.
Sabaya ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 20, 2021 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la kituo cha mabasi Bomang'ombe wilayani Hai baada ya wananchi kumlalamikia juu ya kupanda kwa bei ya mafuta ya kula kutoka Sh22,000 kwa lita tano hadi kufikia Sh34,000 katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mmoja wa wananchi hao, Neema Meena alimweleza mkuu huyo wa wilaya mafuta ya kula lita tano yamefikia Sh34,000 huku sukari nayo ikipanda kutoka Sh2,000 hadi kufikia Sh3,000 kwa kilo jambo ambalo alilodai kuwapa wananchi wakati mgumu.
Malalamiko hayo yaliungwa mkono na wananchi karibu wote waliopata nafasi ya kuwasilisha kero zao, wakidai hivi sasa wanalazimika kutumia mafuta ya ng'ombe kupikia na wengine walidai kunywa uji wa futari bila sukari.
Akijibu malalamiko hayo, Sabaya amesema hakuna tatizo la upungufu wa mafuta nchini isipokuwa wapo wafanyabiashara wakubwa aliodai hawazidi watano waliokula njama na kukubaliana kupandisha bei ya mafuta ili kupata faida kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
"Ninafahamu wala sio wengi (wafanyabiashara) hawazidi watano na walinunua Alizeti yote kutoka kwa wakulima kwa bei ya chini ya soko wakaiweka kwenye container (makasha) na wanaendelea na uzalishaji isipokuwa wamekubaliana wote wahodhi soko na kupandisha bei ya mafuta," amesema.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa saa 24 hadi kufikia kesho Jumatano Aprili 21, 2021 saa 9 alasiri kwa wafanyabiashara wa jumla kukabidhi nyaraka zinazoonyesha bei waliyonunua mafuta hayo ili kujiridhisha na bei waliyonunulia na wasipofanya hivyo, atatangaza bei elekezi na ambaye hataifuata atazinguana naye.
Kwa taarifa yako ni RC mtarajiwa.Anatafuta kiki ya kuondokea huyo hana lolote jina lake lipo kwenye blacklist. Too late
RC mtarajiwa huyo atakumaliza wewe kwanza kabla hujammaliza mkuu!Jambazi anaweza kumkemea nani,atulie tu tunamalizana nae siku si nyingi
Dada magu utakua uko sober ya kulala njaaRC mtarajiwa huyo atakumaliza wewe kwanza kabla hujammaliza mkuu!
Mafuta ya kula yalishapanda bei siku nyingi sana. Kwa wanaopita njia ya kati, maeneo ya Shelui vilipo viwanda vya kukamua mafuta ya kula ya alizeti, bei tunayouziwa ni sh 25,000/ kwa gallon ya lita 5.Mafuta Dar nanunua 38000 kwa lita 5 hiyo 22000 bei ya mwaka gani?
Alizeti imepanda bei sanaMafuta ya kula yalishapanda bei siku nyingi sana. Kwa wanaopita njia ya kati, maeneo ya Shelui vilipo viwanda vya kukamua mafuta ya kula ya alizeti, bei tunayouziwa ni sh 25,000/ kwa gallon ya lita 5.
Sasa huyu Sabaya atuonyeshe hayo ya kwake ya sh 22,000/. Asitafute msamaha, Mama analo jina lake, ni kati ya watu wanaotakiwa kuwekwa benchi, hilo halina ubishi. Ni muda tu.
kabisa, kwanza tuko kwenye soko huria, ndiyo maana tume ya kudhibiti bei ilishakufa. Halafu kila mbuzi anakula kadri ya urefu wa kamba yake. Ndiyo maana kuna Korie,Mafuta ya korie safi azania being rahisi tu.hujalazimishwa kula alizeti.alizeti ipo juu