HAI: DC Sabaya amewajia juu wafanyabiashara waliopandisha bei ya mafuta ya kula wilayani humo na kutoa saa 24 kujitafakari kabla hajazinguana nao

Hivi huyu jamaa hajamsikia Rais kasema nini? kwani mafuta ya kula yanatumika wakati wa Ramdhan tu baada ya hapo sawa kupandisha. mafuta yameanza kupanda bei kabla ya Ramadhan na hakuna mtu anakulazimisha kununua kitu kwa bei ya juu duka hili limekushinda nenda duka jingine biashara yoyote ni demand and supply ndio ina control bei, acheni siasa katika biashara
Kati ya jamaa wa serikali hii ambao siwaelewi ni huyu DC. Mkurupukaji mno
 
Atawanyang'anya leseni za kufanyaia biashara ,nauliza anayo hayo mamlaka wakati ajira hamna na wakati serikali inashauri watu kujiajiri, haya mamlaka ya kuwatisha wafanya biashara kuwanyang'anya leseni anayapata wapi?
 
Hivi Mkuu wa Wilaya ndio mamlaka ya kutoa leseni za biashara? Kama sio, mamlaka ya kuzifuta anatoa wapi?

Amandla...
 
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amewajia juu wafanyabiashara waliopandisha bei ya mafuta ya kula wilayani humo na kutoa saa 24 kujitafakari kabla hajazinguana nao.

Sabaya ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 20, 2021 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la kituo cha mabasi Bomang'ombe wilayani Hai baada ya wananchi kumlalamikia juu ya kupanda kwa bei ya mafuta ya kula kutoka Sh22,000 kwa lita tano hadi kufikia Sh34,000 katika kipindi cha mwezi mmoja.

Mmoja wa wananchi hao, Neema Meena alimweleza mkuu huyo wa wilaya mafuta ya kula lita tano yamefikia Sh34,000 huku sukari nayo ikipanda kutoka Sh2,000 hadi kufikia Sh3,000 kwa kilo jambo ambalo alilodai kuwapa wananchi wakati mgumu.

Malalamiko hayo yaliungwa mkono na wananchi karibu wote waliopata nafasi ya kuwasilisha kero zao, wakidai hivi sasa wanalazimika kutumia mafuta ya ng'ombe kupikia na wengine walidai kunywa uji wa futari bila sukari.

Akijibu malalamiko hayo, Sabaya amesema hakuna tatizo la upungufu wa mafuta nchini isipokuwa wapo wafanyabiashara wakubwa aliodai hawazidi watano waliokula njama na kukubaliana kupandisha bei ya mafuta ili kupata faida kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

"Ninafahamu wala sio wengi (wafanyabiashara) hawazidi watano na walinunua Alizeti yote kutoka kwa wakulima kwa bei ya chini ya soko wakaiweka kwenye container (makasha) na wanaendelea na uzalishaji isipokuwa wamekubaliana wote wahodhi soko na kupandisha bei ya mafuta," amesema.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa saa 24 hadi kufikia kesho Jumatano Aprili 21, 2021 saa 9 alasiri kwa wafanyabiashara wa jumla kukabidhi nyaraka zinazoonyesha bei waliyonunua mafuta hayo ili kujiridhisha na bei waliyonunulia na wasipofanya hivyo, atatangaza bei elekezi na ambaye hataifuata atazinguana naye.
Jambazi anaweza kumkemea nani,atulie tu tunamalizana nae siku si nyingi
 
Mafuta Dar nanunua 38000 kwa lita 5 hiyo 22000 bei ya mwaka gani?
Mafuta ya kula yalishapanda bei siku nyingi sana. Kwa wanaopita njia ya kati, maeneo ya Shelui vilipo viwanda vya kukamua mafuta ya kula ya alizeti, bei tunayouziwa ni sh 25,000/ kwa gallon ya lita 5.

Sasa huyu Sabaya atuonyeshe hayo ya kwake ya sh 22,000/. Asitafute msamaha, Mama analo jina lake, ni kati ya watu wanaotakiwa kuwekwa benchi, hilo halina ubishi. Ni muda tu.
 
Sabaya ana bahati mbaya kwani kapangiwa wilaya ambayo ina jimbo alilokua akiliongoza mwenyekiti wa Chadema.

Yanayomtokea yeye yatampata yeyote atayekwenda Hai akajaribu kumchallenge ndg.Mwenyekiti.

Too bad for him.
 
Pale wakati unapoenda na mtu na sio mtu kwnda na wkt...
Yero jiandae dawa ishawekw kwny crying tulia sio mda utadungwa. Acha kurukaruka
 
Mafuta ya kula yalishapanda bei siku nyingi sana. Kwa wanaopita njia ya kati, maeneo ya Shelui vilipo viwanda vya kukamua mafuta ya kula ya alizeti, bei tunayouziwa ni sh 25,000/ kwa gallon ya lita 5.

Sasa huyu Sabaya atuonyeshe hayo ya kwake ya sh 22,000/. Asitafute msamaha, Mama analo jina lake, ni kati ya watu wanaotakiwa kuwekwa benchi, hilo halina ubishi. Ni muda tu.
Alizeti imepanda bei sana
 
Back
Top Bottom