Hahahaa GAZETI BORA LA MWANANCHI

Hahahaa GAZETI BORA LA MWANANCHI

Gazeti la Mwananchi limepigwa marufuku kuandika mazuri ya CCM, maana leo CCM imeshinda kata 22, wameshindwa kusema hilo badala yake wanaandika CCM IMEPOTEZA VITI VINNE.....tatizo la akili ya kushikiwa........KAMA AMBAVYO VI CDM VITAKAVYOKUJA KUPAMBANA HAPA KUISHAMBULIA THREAD HII....MOODS MSIIUNGANISHE POPOTE TUONGEE KWA UHURU....

acha dharau wewe mtoto wa kike.!
 
Hebu tusahau kidogo kuhusu
ratio kati matokeo ya CCM na CDM kwa vile tunapoteza muda tu CDM
wamechemka. Hivi nguvu yote ile M4C bado tunajadili na kupoteza muda
humu JF. Let them die while they are moving.

mbona unawasha indicator ya kushoto halafu unakata kulia?
 
Gazeti la Mwananchi limepigwa marufuku kuandika mazuri ya CCM, maana leo CCM imeshinda kata 22, wameshindwa kusema hilo badala yake wanaandika CCM IMEPOTEZA VITI VINNE.....tatizo la akili ya kushikiwa........KAMA AMBAVYO VI CDM VITAKAVYOKUJA KUPAMBANA HAPA KUISHAMBULIA THREAD HII....MOODS MSIIUNGANISHE POPOTE TUONGEE KWA UHURU....
Ni ukweli usiopingika vyombo vyetu vya habari vyote vimekaa kiushabiki sana. Honey unakosea unapo sema VICHADEMA, tayari nawe unakua umetanguliza dhihaka dhidi ya chadema. Tuangalie ni maneno yapi ya kuyatamka ili kama kujengana tujengane.
d
 
Kaseme maneno hayo mbele ya SLAA na MBOWE kama hujapigwa mawe na wana wa Redbrigade. Yaani nguvu yote ile ya M4C, Viongozi wote wa kitaifa kuzungukia kata zote kwa kambeni huku CCM wakisimama majukwaani wagombea wenyewe, mwisho wake wanaibuka na nyongeza ya viti 3 tu, Acha kabisa kuongea wewe, tathmini za kukuwa kisiasa huwa hazipimwi kichovu hivyo.

CCM wana zaidi ya miaka 50 ya uzoefu wa kampeni na kudhibiti nafasi zao kwa rushwa, ubabe na kila aina ya uovu. CDM wana uzoefu wa kushindana usiozidi miaka 20. CCM wana back-up ya TLP, CUF, NCCR-MAGEUZI nk. bado wananyang'anywa viti na CDM.
Tanbihi: Uzee unaambatana na kupoteza uwezo kwa baadhi ya misuli na viungo kutofanyakazi ipasavyo. Hatimaye, huja natural death

DARASANI (std 3)
MWALIMU: Sisiem alikuwa na ng'ombe 29. Jioni akagundua kuwa kuna ng'ombe 22 tu. Je amepata au amepoteza?
MWANAFUNZI: Amepoteza.

nb: Hata Rome haikujengwa siku moja.
 
Honey K pole sana mbona husemi gazeti lenubla Uhuru na Habari leo?????
 
Last edited by a moderator:
Gazeti la Mwananchi limepigwa marufuku kuandika mazuri ya CCM, maana leo CCM imeshinda kata 22, wameshindwa kusema hilo badala yake wanaandika CCM IMEPOTEZA VITI VINNE.....tatizo la akili ya kushikiwa........KAMA AMBAVYO VI CDM VITAKAVYOKUJA KUPAMBANA HAPA KUISHAMBULIA THREAD HII....MOODS MSIIUNGANISHE POPOTE TUONGEE KWA UHURU....

Unafahamu kitu kinachoitwa 'news angle'?
 
Kaseme maneno hayo mbele ya SLAA na MBOWE kama hujapigwa mawe na wana wa Redbrigade. Yaani nguvu yote ile ya M4C, Viongozi wote wa kitaifa kuzungukia kata zote kwa kambeni huku CCM wakisimama majukwaani wagombea wenyewe, mwisho wake wanaibuka na nyongeza ya viti 3 tu, Acha kabisa kuongea wewe, tathmini za kukuwa kisiasa huwa hazipimwi kichovu hivyo.

Vilaza wa CCM kaazi kweli kweli...Kuanzia mawaziri hadi wanachama. Hawajui hata historia ya darasa la 3 sembuse hesabu....chezea namba wewe? yaani 29 - 7 Unashangilia?? kupoteza? Sasa kama una Minus badala ya kuadd unategemea by 2015 utakuwa umepoteza vingapi? Pole.
 
Mambo yanaanzaga hivo hivo taratibu mpka mnajikuta na kiti kimoja.Ningekuwa mimi ni sisiemu ningechukua tahadhari
 
hapana, let us be objective, he has a point!Sio hangover, anasema ukweli ulio wazi. This type of reporting is not that much welcome. mimi naipenda CDM (sio mwanachama) lakini mwananchi inaonyesha bias ya hali ya juu, which is not a good reputation for a respectable newspaper like Mwananchi!

Wewe inaonekana hujui maana ya objectivity. Kwani gazeti hilo limeandika uongo upi? Si kweli kwamba CCM imepoteza kata tano? Habari haiwezi kuwa CCM YASHINDA KATA 22 maana hapo awali ilikuwa imeshikilia kata 27. Kupoteza kata tano ndiyo habari yenyewe.

Lakini kingine huandiki habari ili tu kufurahisha watu, unatazama na upepo wa soko ulivyo. Habari za CCM haziuzi magazeti kwa sasa.Watu wananunua sana habari za mabadiliko.
 
sijakiona kibaya kwa mwananchi,ukitumia sana akili kufikiria utaona habari za CCm haziuziki, ebu yatazame magazeti ya UHURU,HOJA hata HABARI LEO kama yanauzika kihivyo au waulize wauza magazeti watakuambia kuhusu hilo! wanachofanya mwananchi ni BIASHARA na siyo fadhila.na habari nyingi nzuri za CHADEMA zinauzika kuliko za Chama chochote kile hapa Tz.
 
Wewe inaonekana hujui maana ya objectivity. Kwani gazeti hilo limeandika uongo upi? Si kweli kwamba CCM imepoteza kata tano? Habari haiwezi kuwa CCM YASHINDA KATA 22 maana hapo awali ilikuwa imeshikilia kata 27. Kupoteza kata tano ndiyo habari yenyewe.

Lakini kingine huandiki habari ili tu kufurahisha watu, unatazama na upepo wa soko ulivyo. Habari za CCM haziuzi magazeti kwa sasa.Watu wananunua sana habari za mabadiliko.

Actually, habari ambayo inalinda heshima ya gazeti kutoonekana liko biased ingeweza kuwa CCM yapoteza kata 5. hii itamshtua mtu, lakini CDM imepata kata 5 kati ya 27 is no news to many who are not that analytical, maana watu wanaofuatilia wanajua kuwa vacant wards zilikuwa 27, then you win 5 is no news at all kwa chama kama CDM! Ingelikuwa ADC, SAUT, DP that would have been news!
 
Ungekuwa ndani ya sekratariat ya CCM ungekuwa na mtazamo kama huo huo, unajiulizaimekuwaje tupoteze hivi viti vinne? Sidhani kama ungeshangilia!!
Ila kwa wewe mnazi unaona kama umesemwa, huyu mwandishi ni CCM damu kwa sababu anawakumbusha kwamba msipokuwa makini next time viti vingine vitazidi kupungua. Tusizoee kubweteshwa.
 
Ukifuatilia vizuri utagundua kwamba Mwananchi wako sahihi.

pamoja na hilo,
MOJA YA VITU VINAVYOCHANGIA USHINDI WA CCM NI PAMOJA NA DAFTARI LA KUPIGA KURA. TANGU 2009/2010 KWA NINI DAFTARI HALIFANYIWI MABORESHO? SI SAHHI KUSEMA KUWA WATU WALIOTIMIZA MIAKA 18+ NI WENGI KUKIWEZESHA CDM KUSHINDA LAKINI NI UKWELI PIA WATANZANIA WENGI HAWAKUJIANDIKISHA MIAKA HIYO CHINI YA 2010. KWANINI KWASABABU WATU HAWAKUONA UMUHIMU WA KUPOTEZA MUDA, KUOTA JUA KUJIANDIKISHA, KUPIGA KURA ILI HALI WAKIJUA CCM NDIYO WATAKAO SHINDA KWA VYOVYOTE VILE. IKUMBUKWE PIA KWAMBA VYOMBO VYA DOLA NA MFUMO MZIMA WA CHAGUZI ZETU SIYO HURU NA NI PENDELEO KWA CHAMA TAWALA. RUSHWA INAHALALISHWA NA MWENYE KITI WA CHAMA, RAIS NDANI YA CHAGUZI ZAO, WAO KWA WAO...!? UNATEGEMEA NINI WATU HAO HAO WANAPOKUWA WANASHINDANA NA WATU WENGINE WA VYAMA TOFAUTI NA KATIKA HALI YA SASA YA KUTAKA KUAMINISHA WATANZANIA KWAMBA VYAMA VISIVYOTAWALA SI CHOCHOTE??? TAFAKALI KABLA YA HATUA
 
Halafu viongozi wa chama walikuwa wanasema hivi?

[TABLE="width: 1"]
[TR]
[TD]
15576bfe7aec7bba1aaebbfa06505951_normal.jpeg
[/TD]
[TD]Zitto Zuberi Kabwe (@zittokabwe)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]27/10/2012 11:25
Rombo kufunga kampeni za Udiwani kata ya Nanjarareha. #CHADEMA twaelekea kushinda zaidi ya nusu ya viti tunavyogombea nchi nzima. Fired up
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Kaseme maneno hayo mbele ya SLAA na MBOWE kama hujapigwa mawe na wana wa Redbrigade. Yaani nguvu yote ile ya M4C, Viongozi wote wa kitaifa kuzungukia kata zote kwa kambeni huku CCM wakisimama majukwaani wagombea wenyewe, mwisho wake wanaibuka na nyongeza ya viti 3 tu, Acha kabisa kuongea wewe, tathmini za kukuwa kisiasa huwa hazipimwi kichovu hivyo.
 
Hilo unalotaka, la kushinda viti 22 limesemwa la lugha nyingine usiyoitaka, tena kwenye sentensi ya kwanza. Story yenyewe hii hapa:

LICHA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kunyakua viti 22 kati ya 29 vya udiwani katika uchaguzi uliofanyika juzi, chama hicho tawala kimepoteza kata nne kilichokuwa kinazishikilia kabla ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huo ulifanyika kuziba nafasi zilizoachwa wazi na madiwani walioondoka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo vifo.
Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha kwamba katika Kata 29, Chadema wameshinda katika kata tano na kukifanya kuongeza madiwani watatu. TLP na CUF kila kimoja kimepata kata moja.
Kabla ya uchaguzi huo, Chadema kilikuwa na Kata mbili za Rombo na Mvomero ambazo kimefanikiwa kuzitetea na kuongeza nyingine tatu, ambazo ni Mlangila (Ludewa), Ipole (Tabora) na Daraja Mbili (Arusha) ambazo awali, zilikuwa zikishikiliwa na CCM.
TLP kilitetea kiti chake katika Kata ya Vunjo (Kilimanjaro) wakati CUF kilitwaa Kata ya Newala ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na CCM.
CCM kimetetea viti vyake vingine vilivyobaki ambavyo ni Msalato (Dodoma), Bang'ata (Arumeru Magharibi), Mletele (Songea), Mwawaza (Mjini Shinyanga), Lwezera (Geita), Bugarama (Kahama) na Bagamoyo mkoani Pwani.
Viti vingine ni Mnero na Miembeni (Nachingwea), Myovizi (Mbozi), Mpapa (Momba), Mahenge (Ulanga), Vugiri (Korogwe), Tamota (Lushoto), Makata (Liwale), Mpepai (Mbinga), Kiloleli (Sikonge), Miyenze (Tabora), Karitu (Nzega), Lubili (Misungwi), Kilema Kusini (Moshi), Nanjara/Neha (Rombo), Lokokona (Nanyumbu) na Kitangiri (Newala).
Katika Kata ya Rwezera, Misango Jeremiah alishinda baada ya kupata kura 1,309 dhidi ya wapinzani wake, Ibuga Mussa (Chadema) aliyepata kura 933 na Mussa Mtagala (CUC) aliyepata kura 317. Uchaguzi huo ulifanyika kujaza nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo, Anatory Mkufu kufariki dunia kwa ajali ya gari Februari 23, mwaka huu.

Kilimanjaro
Katika Kata ya Kilema Kusini, Joseph Rubega wa TLP alishinda kwa kura 1,044 wakati Peter Temu (CCM) alipata kura 797 akifuatiwa na Serafine Mbuya (Chadema) kura 736 na Paul Shirima wa DP kura 13.
Katika Kata ya Nanjara Reheha, Rombo, Frank Salakana (Chadema) alishinda kwa kura 2,370 na kumshinda mpinzani wake pekee kutoka CCM, Dismas Silayo aliyepata kura 1,128.

Lindi
Katika Kata ya Mnero Miembeni, Gervas
Ungele (CCM) alipata kura 818 wakati Jumanne Ali (CUF) alikuwa wa pili kwa kura 611 na Sinji Ali (Chadema) alipata kura 138.

Mbozi na Momba
Katika Kata ya Myovizi, Mbozi Cosmas Nzowa (CCM) alipata kura 1,726 huku Musa Mtakati (Chadema) akipata kura 1,498.
Katika Kata ya Mpapa, Momba, Nolatico Simbeye (CCM) alishinda kwa kura 903 na mpinzani wake, Ladius Kasonso (Chadema) alipata kura 310.

Morogoro
CCM kilishinda katika Kata ya Mahenge kwa Mark Asenga, kupata kura 710 , dhidi ya Baltazar Kizee (Chadema) aliyepata kura 444.
Katika Kata ya Mtibwa, Mwakambaya Edward (Chadema), alishinda kwa kura 3,096 na Musa Kingu (CCM) alipata kura 1,372.


Arusha
Kata ya Daraja Mbili, iliyokuwa ikishikiliwa na CCM kabla ya diwani wake, Bashiri Msangi kufariki dunia ghafla mapema mwaka huu, Chadema kiliibuka na ushindi baada ya mgombea wake, Prosper Msofe kupata kura 2,193 dhidi ya Philip Mushi wa CCM aliyepata kura 1,324. Mgombea wa CUF, Zani Hassan Zakaria alipata kura 162, William Msuyakura (TLP) alipata 42, Mohamed Msuya wa NCCR Mageuzi alipata kura 22.
Uchaguzi huo, unafanyika wakati bado kuna viti sita vya
udiwani katika Manispaa ya Arusha, vikiwa wazi. Madiwani watano kati yao walitimuliwa na Chadema na diwani mwingine wa Kata ya Sombetini, Alphonce Mawazo alijiondoa CCM na kujiunga na Chadema.

Vurugu CCM
Kuhusu vurugu za wanachama wa UVCCM kutwangana hadharani na suala la rushwa katika uchaguzi, Nnauye alisema CCM kinasubiri ripoti kuhusiana na vurugu pamoja na madai ya kukithiri kwa rushwa wakati wa chaguzi za chama hicho.
Katika uchaguzi wa ngazi mbalimbali ikiwamo uwakilishi wa Nec wilaya, mikoa, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na ule wa Vijana (UVCCM) suala la rushwa lilichukua nafasi kubwa.
Nnauye alisema mpaka sasa ofisi yake haijapokea malalamiko kuhusiana na chaguzi hizo... "Ingawa malalamiko yote hupelekwa sekretarieti ya maadili ya uchaguzi ya chama, lakini pia huwa ninapata taarifa isipokuwa kwa sasa hakuna malalamiko yoyote."
Juu ya kuzuka kwa vurugu baada ya uchaguzi wa UVCCM alisema suala hilo linasubiri ripoti ya matukio ambayo yamejitokeza katika uchaguzi na baadaye tathmini itafanywa.
Aliwataka makada wanaolalamikia kukithiri kwa rushwa katika chaguzi za chama hicho kufuata utaratibu wa chama badala ya kukimbilia majukwaani.
Habari hii imeandikwa na Salum Maige (Geita), Venance George (Morogoro), Mussa Juma na Moses Mashalla (Arusha), Stephano Simbeye (Mbozi), Christopher Lilai (Nachingwea), Daniel Mjema (Moshi) na Gadius Rwiza (Dar).
 
The headline and news is true but the method used is spin.

Wana CDM wengi waliaminishwa na viongozi wao kama chama kitashinda nusu au zaidi ya viti vilivyokuwa wazi. Ndiyo maana kabla ya matokeo walikuwa wanapiga kelele sana. Ninaamini wengi walipigwa na mshangao baada ya kupata news kama chama kimeshinda viti vitano tu.

Wana CCM wengi walikuwa na wasiwasi kuwa chama kitapoteza viti vingi kutokana na kelele zilizokuwa zinapigwa na wana CDM, kwa hiyo matokeo haya kwao ni kama ushindi.

Labda tu swali kwa wana CDM, Je, kama CCM hii inayosemwa imechoka bado inaweza kuaminiwa na watu wengi na kupewa kura ukilinganisha na CDM inayosema iko active na M4C imesambaa nchi nzima. Tatizo ni nini au spin tu ni nyingi badala ya uhakika wa hali halisi ya kisiasa.

Kumalizia tu, hivi ni kweli kata zote alizopiga kambi katibu mkuu wa CDM wakati wa kampeni zote zimebaki CCM.
 
Furaha ya CCM inatokana na kutarajia maumivu makubwa sana awali.Ni sawa na Familia ya watu 27 ikakumbwa na ugonjwa mkali wa kipindupindu ambapo mwenye kaya akategemea kupoteza familia nzima. Kipindupindu kikipita akagundua kati ya watu 27 wamekufa watano tuu kama uwezo wake wa kufikiri mdogo atasheehekea badala ya kuhuzunika na vifo vitano. Hiyo ndio CCM bwana. Nape anasimama kifua mbele kujisifu kuwa pamoja na "kipindupindu" kikali wamekufa watano tuu na kukikebehi kuwa hakikuwa lolote au chochote. Sisi wengine wenye utu tunasema poleni wafiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom