Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
- Thread starter
- #21
SEHEMU: 14
ILIPOISHIA:
"Mama nilikuwa kwa ma mdogo na pia nilipitia kwa kaka Lyasi."
"oooh kumbe ulikuwa na safari ndefu hawajambo wote?"
"Wazima wa afya njema."
"Mhu wanasemaje?"
"Wanakusalimia ila mama ma mdogo amenituma kesho niende kwa dada Cathy."
"Wapi? Dar?"
"Ndiyo mama."
"kuna nini tena?"
"Sijui amesema atanijulisha hiyo kesho kutwa."
"Mimi sina tatizo mjulishe na baba yako tu nisije nikaulizwa."
Jioni baba yake aliporudi alisubiri mpaka usiku baada ya chakula cha usiku ndipo alipomweleza. Lakini baba yake alisema ameisha pata taarifa la muhimu awahi kurudi.
"Mume wangu mwache mtoto akapumzike hata wiki ili aone na jiji."
"Na kazi za hapa?"
"Na akiolewa atafanya nani?"
"Mpaka akiolewa."
"Lazima tujifunze kukaa peke yetu ili akiolewa tusiwe wakiwa."
SASA ENDELEA…
"Haya kaa hata mwaka mzima."
"Hapana baba siku mbili tu siendi kukaa nimetumwa na ma mdogo."
"Ahaa kumbe haya mama uende salama."
Siku ilipotimu Sundi alikwenda Dar kwa dada yake Catheline, alipata siti ya dirishani upande wa siti ya watu wawili. Alikaa na mwanamke mmoja makamo ya dada yake mkubwa anayefuatwa na Cathy na yeye ameolewa Dar na ndiye alikaa na Cathy na kuolewa mikononi mwake.
Baada ya kusalimiana kila mmoja alipenda kuongea na mwenzie, kabla ya basi kuondoka yule dada wa jirani na Sundi alinunua gazeti na kusoma. Lilikuwa gazeti la udaku baada ya kusoma kwa muda alilikunja, ndipo Sundi na yeye alipoomba kusoma.
Yule mama alimpa na kuanza kusoma, alilisoma gazeti lote na kukutana na kitangazo kilichokuwa kukusema kuwa kuna mganga anayeweza kuokoa ndoa za watu. Kuimalisha ndoa zinazoyumba hata kumrudisha mke au mume aliyehasi nyumba yake.
Baada ya kusoma alijikuta akiguna kitu kilichomfanya yule mama wa jirani yake kuhoji:
"Vipi mdogo wangu unaguna nini?"
"Yaani unajua dada waganga wa kienyeji waongo sana."
"Kwa nini unasema hivyo mdogo wangu?"
"Eti wanawadanganya watu wana uwezo wa kuokoa ndoa za watu, hivi kweli duniani kuna dawa ya kubadili tabia ya mtu?"
"Mmmh kweli hakuna mdogo wangu."
"Sasa kama sio uongo ni nini?"
"Sikiliza mdogo wangu dawa zipo za kumfanya mwanaume atulie ndani au aachane na tabia chafu."
"Lakini kwa upeo wangu mdogo japo sijakuwa sana japo sijaolewa lakini naamini dawa ya mapenzi ni wewe mwenyewe."
"Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia, lakini mdogo wangu ukiona hivyo ujue Simba kazidi inabidi amloge mtu na pale hakuna mapenzi zaidi ya mmoja kugeuzwa ndondocha."
"Unazidiwa vipi na wewe unafanya yote kwa mumeo ikiwa tabia mpaka kauli njema."
"Mdogo wangu unajua ndoa ni jumba lililo na pande mbili yaani nje na ndani aliye nje anatamani kuingia ndani na walio ndani wapo wanaofurahia kubakia lakini wengine kwao kama jehanamu wanatamani kutoka na waliotoka hawataki kurudi tena na wengine waliotoka kwa uzembe wao ndio hao huenda kwa watalamu kama hawa na kuwapa dawa ambazo huwarudisha ndani. Vilevile wapo walio nje ambao wanatamani kuingia ndani lakini bahati hiyo hawa ndio huenda kwa wataalamu kama hawa ambao huwasaidia."
"Una amini zinasaidia?"
"Zinasaidia sana mdogo wangu."
"Mmh. Siamini."
"Bado mdogo ukikuwa utayajua haya unaweza kuwa unayafanya yote haya tabia nzuri au kauli tamu kama kinanda lakini mumeo akawa ndani hakai lazima utajua uangaike vipi kuiokoa ndoa yako hasa pale unapompenda mumeo na kutokutaka ndoa yako ivunjike."
"Wewe unaamini vipi?"
"Mimi ninaye kuelezea hivi yamenikuta," kauli ile ilimfanya Sundi ajiweke vizuri kupata kisa kingine kabla ya kumfikia dada yake. Kabla ya kuongea alitulia tuli kwa muda kisha alitoa kitambaa kwenye mkoba wake na kufuta machozi ikionyesha machozi yalikuwa yakimtoka kisha kwa sauti ya upole alisema:
"Mdogo wangu katika maisha yako usipoteze muda wako."
"Kivipi dada?"Sundi alimuuliza huku akiwa amemkazia macho.
"Mdogo wangu wakati ukuta na ukitimu hugota na vilevile hakuna marefu yasiyo na ncha na ngoma ikivuma sana hupasuka."
"Dada yangu yote uliyosema nimetoka kapa."
"Ni kweli lakini unakuwa na wakubwa hawakukosea kusema kuwa uyaone."
"Ni kweli dada yangu na sisi wadogo hujifunza kupitia ninyi wakubwa zetu mlio tutangulia."
"Ni kweli kabisa, ila nakuomba chondechonde mdogo wangu usiipige teke tunu uliyopewa na Mungu hasa huu uzuri wako ukajiona huwezi kuufuja kwa kuolewa na kutaka kuponda maisha...
Mimi mdogo wangu enzi zangu nilikuwa ni utatanishi kwa wanaume si kwa wanaume hata mwenyewe nilijijua ni mzuri. Nilikataa kuolewa kwa kujua ndoa ni utumwa na kujifuja. Hata elimu niliiona haina mpango kwa kuendekeza starehe.
Na siku zote mdogo wangu jiepushe na kuzionja starehe za kidunia zitakupoteza na kuona ndio maisha kumbe unapotea. Nilikuwa sishikiki enzi zangu lakini ipo siku nilibakia kama nyani mzee wanaume wakawa wananikimbia hapo ndipo nilikimbilia kwa wataalamu na kubahatika kupata bwana kwa vile sikuwa na uwezo wa kumshawishi mtu.
"Mmh ilikuwaje dada yangu mpaka kufikia hivyo?"
"Ni hivi baada ya siku moja kupata dhahama ambayo ni Mungu aliyeokoa maisha yangu. Siku hiyo nakumbuka vizuri ilikuwa baada ya kutoka hospitali na kusimama mbele ya kioo na kuiangalia sura yangu iliyopoteza haiba sikuwa mimi tena wa miaka ile iliyopita niliyekuwa nikitumia muda mwingi kwenye kioo lakini sasa uso wangu hauna tofauti na kibaka aliyekwapua mkoba kwenye kituo cha basi.
Sasa hivi mdogo wangu nimekuwa adui mkubwa na kioo kuna kipindi huuogopa uso wangu kwa kujiona nimekutana na kiumbe cha ajabu. Uso wangu nimekuwa kama dudu la kutishia watoto vikojozi.
Kila aliyeniona muda huu hawezi kuamini kuwa ni mimi mtu niliye kuwa tishio kwa wanawake wenzangu ni gari gani litakalopita bila kusimama na kuniulizia ninakwenda wapi kutembea kwa miguu kutaka mwenyewe.
Leo hii uso wangu umekuwa kama ubao wa shabaha ambao umebondeka kwa wale wenye shabaha ambao upiga nje ya duara mdomoni maskini sikuwa na meno ya kuchekea ambayo siku za nyuma nilicheka muda wote tena nilionyesha meno yangu matatu ya dhahabu na mwanya wangu mwembamba ulioongeza uzuri wangu.
Sikuwa radhi kuolewa raha za dunia ningezifaidi saa ngapi kwanza mwanamke mzuri kama mimi sikuumbwa ili nifungwe ndani kama mfungwa. Nilijua Mungu aliniumba ili nile raha za dunia na kutembea mitaani kuonyesha uwezo wake wa uumbaji, nikikaa ndani nani ambaye ataniona.
Halafu nivae nguo ndefu hayo maumbile niliyoumbwa nayo nani atayaona tena sikuvaa nguo nzito nilivaa nguo za wanaita za trans palent zilizo onyesha mpaka ndani. Wapo walionikufuru nilijua wananionea gere kwa sababu hawakuwa na maumbile wala sura ya mvuto kama yangu.
Lakini sasa imebakia simulizi na majuto ya nafsi na kuusemea moyo wangu ningejua lakini ni wakati huo. Hapo nyuma nilikuwa kimbelembele kuonekana mbele ya macho ya watu kwa sababu nilikuwa nikijiamini kwa kila kitu. Hata wanawake wenzangu walijua kwa kunisifia bila aibu wala choyo, ukiona mwanamke mwenzio anakusifia ujue wewe ni mzuri ni nadra mwanamke mwenzio kukusifia hata uwe mzuri vipi.
Najua una shauku mdogo wangu kuyajua ila nakuomba kupitia simulizi hii iwe fundisho kwako hata kwa mashoga zako sipendi kosa langu lirudiwe na mtu mwingine, kisa hiki ambacho kilinifanya nitake kujiua zaidi ya mara mbili.
Kwa jina mdogo wangu naitwa Konsolata nimezaliwa miaka 32 iliyopita ni mtoto wa nne katika familia ya watu watano nikiwa ni mmoja wa watoto wa kike wa famili ya mzee Jonasani na mama yangu Magdalena.
Kwanza lazima nimshukuru Mungu kwa kuzaliwa familia iliyompokea Bwana.Wazazi wetu walikuwa wacha Mungu wazuri sana. Lakini ilikuwa tofauti na sisi watoto wao kwenda kanisani ilikuwa mbinde au kusingizia tunakwenda kanisani kumbe kwenye mambo yetu.
Siku zote tulijua ukimuona mtu anamfuata sana Mungu ujue maisha ya kidunia yamemshinda hasa wazee ambao wakiona wamekaribia kufa hapo ndipo humrudia Mungu.
Pamoja na wazazi wetu kuwa wacha Mungu tulikuwa hatukosi kwenye matamasha hasa kumbi za starehe majira ya usiku kwa kutoroka.
Baada ya kumaliza kidato cha sita nilibahatika kwenda chuo kikuu, kwa kweli kwa upande wangu nilikuwa kama mfungwa aliyefunguliwa kifungoni kwa kupata muda wa kufanya mambo yangu ambayo wazazi wangu walikuwa wakinibana.
Nilikutana na shoga yangu ambaye tulikuwa tunakaa naye chumba kimoja kwa kweli mwanzo mavazi yake yalinishinda yalikuwa ya nusu uchi alinishangaa mimi kuvaa nguo ndefu kama mtawa.
"Konso utakatifu gani huo?"
"Kwa nini unasema hivyo?"
"Mavazi gani hayo yaani umbile kama lako ningekuwa nalo mimi kila mtu angelisoma namba Mungu amekupa ili uutangaze uwezo wake wa uumbaji ukilificha usije shangaa siku moja ukasikia umekuwa mremavu kwa kushindwa kuvitangaza..kwanza unajijua wewe mzuri."
"Nitajijuaje mwenyewe."
"Ina maana kote uliko soma hukuwahi kusifiwa?"
"Hiyo hali nimeisha izoea."
"Basi Konso wewe ni mzuri chuo kizima yaani ningekuwa kama wewe mbona wangenikoma."
Suzy msichana ambaye alionekana ni mjanja kuliko mimi starehe kwake kilikuwa kitu cha kawaida eti hata wazazi wake walilijua hilo kwa kumuachi kujirusha la muhimu akili yake ilikuwa ikichaji.
Ushawishi wa Suzy haukuwa mkubwa kwa sababu hata mimi starehe nilikuwa nazipenda lakini ndio hivyo ni nilikuwa kwenye geti kali. Kwa kweli nilijikuta naungana na Suzy kwenda kwenye kumbi za starehe usiku. Huku nako Suzy alikuwa na rafiki yake wa kiume na mimi alinitafutia rafiki yangu.
Basi mdogo wangu mabwana tulio wapata walikuwa na pesa za kumwaga, ilifikia hatua ya kusafiri nje ya mkoa kwenda kwenye miji ya starehe. Ajabu bwana wa Suzy alifanya mapinduzi kwa kunitangazia dau kubwa kwa kuwa mimi nilikuwa mzuri kuliko Suzy kibaya niliyekuwa natembea naye ni rafiki yake na pesa alikuwa akitoa yeye.
Yule bwana alisababisha mimi na shoga yangu tuwe maaduni na kuwa kama chui na paka hata kufikia hatua ya kutengana chumba na kununiana hatukuwa tukiongea ulikuwa uhasama mkubwa.
Yule bwana aliyefahamika kwa jina la Afidh Bantu au kama alivyokuwa akipenda kujiita 'Bishanga'. Aliamua kunihamisha shule na kunipangishia uswahilini lakini sehemu ya watu wenye uwezo.
Aliniwekea kila kitu ambacho ni muhimu kwa kweli nilijikuta nayasahau maisha ya chuo na kuishi maisha ya starehe ya kila wiki lazima tutoke kwenye kumbi za starehe. Bishanga aliniambia niache kusoma kwa kuwa anataka kunioa na kunipa maisha mazuri.
Nilikubali kuacha shule bila wazazi wangu kujua niliamua liwalo na liwe hata kama wakijua watasema mwisho watalala. Bishanga alikuwa tayari kuwalipa kiasi chochote cha gharama ya masomo yangu kuanzia chekechea.
Niliishi na Bishanga kwa mwaka mmoja nikiwa sijui kupika wala kufua, niliishi kama malkia na yeye aliniita malkia wake. Kwa kweli kila sehemu tuliyokwenda walimuuliza amenitoa wapi malaika ambaye hawaamini kama nimezaliwa bali nimeshushwa kwa uzi wa buibui.
Sehemu zote nilikuwa nakwenda naye katika mavazi ya ajabu ya nusu uchi nilipomgomea alisema kama Suzy.
"Lazima niutangaze utaalamu wa Mungu kwa utundu alioufanya kukuumba nina imani siku aliyo kuumba aliacha shughuli zote na kukuumba kwa utundu wa hali ya juu."
Mwanzo nilikuwa naona kazi lakini nilikuja kuyazoea na kuona kutembea uchi au nusu uchi ni jambo la kawaida. Pamoja na kuwa na pesa nyingi lakini nilikuwa sijui kazi ya Bishanga. Siku moja tukiwa tumelala majira ya saa saba za usiku nyumba yetu ilivamiwa na askari.
Afidh Bantu pamoja na mimi tulichukuliwa juujuu na kupelekwa polisi usiku huohuo, kwa upande wangu sikujua tumechukuliwa kwa sababu gani. Huko nyuma tuliacha nyumba kwenye upekuzi mzito.
Tulipofika polisi tulitenganishwa kila mmoja aliwekwa sehemu yake, tulilala palepale hadi asubuhi. Kesho yake majira ya saa saa tano tulitolewa kwa dhamana na rafiki zake na Bishanga, walikuwa na watu wenye pesa.
Mpaka tunarudi nyumbani sikujua jana yake tulichukuliwa na polisi kila nikimuuliza anasema achana nayo. Pamoja na kukaa kimya bado nilikuwa kwenye maswali mazito juu ya kuvamiwa na jeshi zito la Polisi na siraha nzito na mbwa kama jambazi au mhaini.
Jioni ya siku ile Bishanga alinieleza kuwa tatizo lake ni zito kwa hiyo anatakiwa kuondoka nchini usiku ule, nilijiuliza ni tatizo gani linalo mkimbiza nchi.
"Sasa utarudi lini?"
"Kwa kweli haijulikana ikiwezekana kuonana majaliwa."
"Ooh! Mungu wangu na mimi itakuwaje?"
"Sina jinsi itanibidi nikuache kwa sababu tatizo lenyewe limetokea ghafla."
"Mimi nitaishi vipi kwa kuwa wewe ndiye umeniachisha shule?"
"Siwezi kukuacha kwenye hali mbaya bali nitakuachia pesa nina imani itakutosha kununua nyumba na gari moja dogo na za kutumia kwa miaka mwili."
"Kiasi gani."
"Milioni 50 ila ndani ya nyumba hii unatakiwa kuanzia kesho uondoke nyumba si mali yetu tena nimeiuza ili kupata nauli na pesa ya kukuachia."
Nilitamani kulia kwa kujua sasa ndipo wakati wa kuadhirika mtoto wa kike kwa sababu Afidh Bantu alikuwa amenizoesha vibaya sana. Sikuwa na jinsi nilimuagia palepale kwa sharti hatakiwi kusindikizwa na mtu.
Baada ya Bishanga kuondoka nilirudi kwenye chumba changu ambacho nilikuwa bado sijakirudisha. niliyaanza maisha mapya nikiwa peke yangu niliwaza kurudi nyumbani lakini nilijiuliza nitawaeleza nini. Niliamua maisha yangu yatakuwa mbele kwa mbele sirudi nyuma.
Kama pesa nilikuwa nayo ya kuishi maisha yoyote ninayotaka, nilisimama mbele ya kioo kuthibitisha uzuri wangu, kweli nilithibitisha mimi mzuri tena sana. Nilikuwa nikiona fahari kusimama kwenye kioo kwa muda mrefu kwa kuuangalia uzuri wangu.
Basi mdogo wangu nilichukua muda wa mwezi mmoja na kuolewa na bwana mmoja wa kiarabu. Kwa kweli ilikuwa harusi kubwa sana ambayo nina imani mpaka Mungu ananichukua haitatokea. Bwana huyu pesa alikuwa nayo alikuwa akimiliki magari na vituo zaidi ya kumi vya mafuta jijini.
Mwanzo ndoa niifurahia kwa kuona napendwa na ndugu na jamaa wa mume wangu. Lakini ndoa ilinitumbukia nyongo kwa kujiona nipo kizuizini. Yaani nilikuwa mimi na ndani, ndani na mimi. Kwa kweli ndoa niligundua ni utumwa haina nafasi ya kujitawala.
Nilijifikilia kama pesa ninayo tatizo nini maisha ya kufungwa yalinishinda na kuamua kuomba talaka japo mume wangu alinipenda sana. Lakini nilimlazimisha kunipa na kumtishia asiponipa atanipea mahakamani.
Mume wangu hakuwa na jinsi alinipa talaka baada ya talaka niliapa sitaolewa tena na mwanaume nitaishi maisha yangu kwa kumchagua mwanaume atakaye kubali masharti yangu.
Mdogo wangu ujinga mzigo nilijiona mzuri na kusahau kuna wazuri wengi wanao hangaika kwa waganga bila mafanikio lakini mimi nilijiona mimi ndio mimi, nisiye kubali kubabaishwa na mwanaume yeyote kwa kujijua wanaume wananigombea kama mpira wa kona.
Niliyaanza maisha yangu kwa staili nyingine kwa kila jioni kwenda kwenye kumbi za starehe na kurudi nyumbani majira ya usiku wa manane. Siku moja nikiwa kwenye moja ya kumbi za starehe nilimuona kijana mmoja ambaye nilivutiwa naye.
Itaendelea...