Hadthi : Sundi

Hadthi : Sundi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
Image may contain: 1 person, text and close-up


HADITHI: Sundi
MTUNZI: Ally Mbetu
SEHEMU: 01

SUNDI

Ndoa ni jumba lililo na pande mbili yaani nje na ndani.Aliye nje anatamani kuingia ndani na walio ndani wapo wanaofurahia kubakia na kutotamani kutoka nje lakini wengine kwao kama jehanamu wanatamani kutoka na waliotoka hawataki kurudi tena na wengine waliotoka kwa uzembe wao huenda kwa watalamu kuwapa dawa ambazo huwarudisha ndani.Vile vile wapo walio nje ambao wanatamani kuingia ndani lakini bahati hiyo hawana.Nao huangaika kwa waganga wa kienyeji au makanisani kuombewa ili nao waingie ndani na ndiyo nikasema ndoa inamitazamo miwili nje na ndani Ili kuyajua yote unagana na mtunzi ALLY MBETU

*********
Sundi akikaa pembeni ya mama yake akiwa amesongwa na mawazo juu ya siri ya ndoa ambayo kila kukicha ilimchanganya. Ilikuwa ni muda wa wiki tatu toka ampate mchumba kanisani aliyemuahidi kumuoa. Lakini swali lilikuja mbona mawazo yake ya awali ya kuomba usiku na mchana kuolewa umemtumbukia nyongo.
Baada ya kupata tu mchumba mtu wa kwanza kumpa taarifa alikuwa mama yake mdogo ambaye ndiye aliyekuwa shoga yake mkubwa. Siri zote alimpelekea yeye kabla ya kumfikia mama yake au dada zake, mama yake mdogo alikuwa mfanya biashara na hakuwa na mume baada ya kuikimbia ndoa yake baada ya manyanyaso ya mume na wifi zake.
Ndiye aliyemsimamia kila kitu katika masomo yake na kumnunulia akitakacho bila kuhoji kina gharama gani. Kitu kilichofanya Sundi amuone mama yake mdogo ni zaidi ya mama yake bali rafiki. Baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja ambaye alimpenda kama alivyo mpenda.
Kijana yule alipofikia hatua ya kutaka kwenda kwao kujitambulisha, ndipo Sundi alipompelekea taarifa mama yake mdogo ili amsikie anasemaje. Siku hiyo alikwenda hadi kwa mama yake mdogo na kumueleza siri yake ya kupata mwenza.
Alimkuta mama yake mdogo akijiandaa kwenda kuoga baada ya kurudi kwenye shughuli zake za kutwa nzima. Mama yake alipomuona kwa uzoefu alimgundua mwanaye amekuja na kitu gani.
"Sundi mwanangu karibu.”
“asante mama.”
“Kwema?” alimuuliza huku akimtazama usoni.
Kwe,,,kwema ma' mdogo,” Sundi alibabaika kujibu.
“Hapana Sundi kuna kitu kunakusubumbua," mama yake alimwambia kwa sauti ya upole.
"Ma' mdogo umejuaje?"
"Mi' mkubwa ninajua mtu yupo katika hali gani pia we si mgeni kwangu."
"Ni kweli ma mdogo."
"Ehe una tatizo gani mwanangu kipenzi?"
"Ma' mdogo nimepata mchumba."
"Mchumba? Mmh, makubwa," kauli ile ilimshtua sana Sundi na kutaka kujua kwa nini mama yake mdogo amejibu vile.
"Ma' mdogo mbona unanitisha?"
"Sikutishi mwanangu mbona haraka sana?"
"Ma' mdogo miaka ishirini na tatu unaniona bado mdogo?"
"Tena sana."
"Ma' mdogo mbona da Monika kaolewa na miaka kumi na nane?" Sundi alimuuliza mama yake.
"Ni kweli dada yako kaolewa na miaka kumi na nane, lakini mwanangu ndoa mtihani ndoa ni vita ndoa ni jahanamu na ndoa ni pepo ya duniani."
"Una maana gani?"
"Mwanangu ndoa inahitaji ukomavu wa akili vilevile inahitaji bahati ya kuolewa na mwanaume akupendae mwenye mapenzi ya kweli mwenye utu moyoni mwake."
"Nina imani huyu niliyenaye ana mapenzi ya dhati kwangu."
"Hata mimi nilijua hivyo na kumuona baba yako mdogo ananipenda,lakini.."Ma mdogo alinyamaza na kuinama chini na kutulia kwa muda kiganja cha mkono wa kulia kikiwa juu ya paji la uso.
Alitulia kwa muda kitu kilichomshtua Sundi, lakini alikuwa mzito kumuhoji mama yake. Baada ya dakika kadhaa alisema huku mashavu yake yakiwa na michilizi ya machozi.
"Samahani mwanangu kwa hali iliyojitokeza, imenikumbusha miaka saba iliyopita nikiwa ndani ya ndoa yangu. Ndoa mwanangu ni kama jumba au ngome ambayo ina siri kubwa yaani nje na ndani, nikiwa na maana kuwa waliomo nje wanatamani kuingia ndani na waliopo ndani wanatamani kutoka nje.
Pia wapo waliotoka kwa makosa wanatamani kurudi tena ndani na waliopo nje hawataki kuingia ndani na wengine kama sisi yuliowahi kuwepo ndani hatutaki kurudi tena na wengine kama dada na mumewe wanaishi kama wapokwenye pepo ya dunia hawafikilii kutoka. Atatoka mmoja wao kwa kuchukuliwa na mauti kama walivyo apa mbele ya Mungu.
Mwanangu Sundi maisha ya dada yangu ambaye ni mama yenu na mumewe baba yenu ambaye ni shemeji yangu ndiyo yaliyonivuta na kutamani kuolewa. Kwa bahati nzuri nilibahatika kumpata mwanaume wa ndoto yangu mwenye hali nzuri kimaisha. Baada ya ndoa yangu iliyoacha simulizi midomoni mwa watu Eliza mimi niliyaanza maisha kama mke wa mtu..
Niliishi ndani ya jumba la kifahari kulala kitanda cha kifahari kutembelea gari la kifahari nilikula chakula nikitakacho na kujipamba kwa vito vyote vya gharama. Mwanangu na weupe huu nilikuwa kama malaika...
Ni kweli niliamini ndoa ni pepo ya duniani kwa maisha niliyoishi na mume wangu kwa kuonyesha mapenzi ya kweli na upendo ulioonekana dhahiri shairi. Nilipendeza machoni mwa watu mume wangu hakuwa mbaguzi wala kunihoji matumizi yangu.
Niliweza kufanya mambo mengi kwa siri bila kumjulisha, msiri mkubwa alikuwa mama yenu. Aliweza kuniwekea pesa na kufanikisha kuninunulia kiwanja ambacho aliwezesha kunijengea nyumba hii. pamoja na miladi yote unayo iona ni msaada wa mama yako. Basi mwanangu ndoa yangu ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu tu ikaanza vituko, pale baba yako mdogo alipoanza visa. Na yote ilikuwa ni kutokana kuchelewa kupata mtoto na kuonekana mgumba, mwanzo mume wangu alikuwa upande wangu na kuwa pamoja na mimi kunipa moyo.
Japo upande wa wazazi wake hasa mama mkwe na wifi zangu walimshauri aniache. Msimamo wake ulinifanya nijione kweli nimepata mume wenye mapenzi ya kweli. Lakini ndugu zake walianzisha kampeni ya kumtafutia mwanamke wa pembeni ili kumpatia mtoto na kupata njia ya kunitoa ndani.
Kweli dua baya nalo hupokelewa baada ya kufanya siri ile mume wangu alifanikiwa kumbebesha ujauzito mke wa pembeni. Hapo ndipo nilipoanza kuiona nyumba mbaya mume wangu akaanza dharau hata kukubali dada zake waninyanyapae,japo mwanzo aliwakataza na kuwaonya.
Uliandaliwa mpango kabambe yaani siku ya kujifungua ndiyo siku ya mimi kutolewa ndani. Nilivaliwa kanga za mafumbo na kuimbiwa nyimbo nyingi zenye kutia kichefuchefu. Yote nilivumilia na yote manyanyaso nilimweleza mama yako ambaye alinipa moyo.
Alinieleza maisha ya ndoa yana misukosuko ambayo yanahitaji ujasiri wa hali ya juu na kuwa na moyo wa chuma hasa kuzingatia hali yangu ya kuchelewa kupata mtoto. Alinieleza kuwa nimsikilize mume wangu ndiye aliyeniweka ndani na ndiye mwenye maamuzi yote.
Siku moja nilipata taarifa ambazo zingeweza kusimamisha mapigo ya moyo wangu pale mtu wangu wa karibu aliponiletea taarifa.
"Shoga una habari gani za mumeo?"
"Hata sina."
"Basi mafumbo yote ya wifi zako na dharau za mumeo leo nimezipatia jibu."
"Jibu gani tena,mbona unanitisha?"
"Basi kama huna moyo siwezi kukueleza."
"Shoga moyo ninao bila huo moyo leo nisingekuwa hapa."
"Basi shoga kumbe mumeo ametafutiwa kisichana na sasa kina mimba ya miezi sita."
"Usiniambie!" nilihisi kuishiwa nguvu na mwili kunitetemeka hali iliyomtisha shoga yangu na kutaka kuacha kunisimulia
"Basi shoga naona mambo sio mazuri moyo wako mwepesi"
"Sio mwepesi hata wewe ungeshtuka malizia tu shoga"
"Basi mpango uliopangwa ni kuwa akijifungua tu na wewe out tena sio siri nashangaa we ndio hujui kila mmoja anakuonea huruma kwa kitendo cha kinyama wanachotaka kukutendea"
"Mungu wangu yaani wameisha kuwa Mungu wa duniani wananihuku sawa Mungu ndiye anayejua yote namuachia yeye"
Huwezi kuamini mwanangu wakati huo sikuwa Eliza yule mwenye mvuto wa kimalaika bali nilikuwa nimebakia mfupa na ngozi.Hata haki yangu ya ndoa nilipewa pale alipopenda.Kweli nilikuwa nimechokwa na mume wangu kwa kuniambia nimepoteza mvuto.
Mabadiliko ya hali yangu ilinifanya niingiwe na wasiwasi kwa kutokuziona siku zangu kwa mwezi wa pili. Wakati huo mwanamke wa pembeni alikuwa amabakiza mwezi mmoja ajifungue.Majibu ya uchunguzi wa afya yangu yalionyesha kuwa nimenasa yaani mjamzito.
Sikuamini niliamini Mungu ameyakomboa maisha yangu kwa kulifanya lile ambalo kwa mwanadfamu haliwezekani.Taarifa nilimfikishia Mume wangu,kwa kweli alishtuka na kusema
"Muongo mkubwa"
"Yaani mume wangu badala ya kufurahi kwa Mungu kusikiliza kilo chetu wewe unasema uongo"
"Hiyo sio dawa safari ipo pale pale"
"Mume wangu ulikuwa na lingine au hili hili?"
"Baada ya kunifanya nikose amani kwa familia yangu sasa unataka kunigombanishja kabisa"
"Mume wangu kukugombanisha kivipi?"
"Kwa kuwaeleza uongo"
"Mume wangu inamaana vyeti hivi vinasema uongo?"
"Nitaamini vipi labda umemuhonga daktari ili kukuokoa"
"Mume wangu sikulazimishi kukaa na mimi hata kama utaniacha leo basi uelewe umeniacha na ujauzito wako"
"Siamini twende wote hospitali"
Niliongozana na mume wangu hadi hospitali na kuchukuliwa vipimo mbele ya mume wangu na majibu yalimfanya mume wangu ahudhunike,lakini akuomba msamaha nilijua ni kiburi na ubabe.Bila kutarajia nilimwambia neno ambalo lilinitoka mdomoni
"Mume wangu nenda ukawaambie wamlete huyo walio muandaa"
"Wamlete nani na kina nani?"
"Unawajua"
"Naona umenikosea adabu"
"Na nitakukosea sana ninyi si miungu watu"
Maneno yalimuingia mume wangu na hakutaka kusema neno,tulipofika nyumbani aliondoka bila kuaga.Hapo mimi roho iliniuma na kujikuta nalia peke yangu,moyo uliniuma sana na kujiona sina thamani tena.

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: Sundi
MTUNZI: Ally Mbetu
SEHEMU: 02

ILIPOISHIA:
Niliongozana na mume wangu hadi hospitali na kuchukuliwa vipimo mbele ya mume wangu na majibu yalimfanya mume wangu ahudhunike,lakini akuomba msamaha nilijua ni kiburi na ubabe.Bila kutarajia nilimwambia neno ambalo lilinitoka mdomoni
"Mume wangu nenda ukawaambie wamlete huyo walio muandaa"
"Wamlete nani na kina nani?"
"Unawajua"
"Naona umenikosea adabu"
"Na nitakukosea sana ninyi si miungu watu"
Maneno yalimuingia mume wangu na hakutaka kusema neno,tulipofika nyumbani aliondoka bila kuaga.Hapo mimi roho iliniuma na kujikuta nalia peke yangu,moyo uliniuma sana na kujiona sina thamani tena.
SASA ENDELEA...

Jioni akili ilinituma nirudi nyumbani kwa dada,nilibeba kila kilicho changu na kupakiza kwenye gari na kurudi nyumbani.Mama yako aliponiona alishangaa na kunihoji kulikoni
"Dada nimechoka mimi na shemejio basi"
"Hapana mdogo wangu maisha hayaendi hivyo utamfanya Mungu mjinga kwa kukupa kile ulichokiomba kwake kwa machozi ya damu"
Nilimueleza yote yaliyojili majira ya mchana,kabla ya kujibu alishusha pumzi na kusema
"Mdogo wangu nikikurudisha muda huu nitakuwa sikutendei haki pumzika kwanza.Ni kweli ndoa ni makubaliano ya mke na mume lakini matatizo yakizidi unatakiwa kupumzisha akili na kutafakali upya"
"Dada sina haja ya kutafakali lolote kwa upande wangu ndoa basi...dada nimenyanyapaliwa sana kuchelewa kwangu kupata mtoto nilifananisha na nguruwe kazi yangu kunenepeana bila faida...dada nashkuru nimerudi kwenye hali yangu ya mwili mdogo tena nikiwa mjamzito...
Mungu akijalia nikijifungua salama watamfuata mtoto wao na kulelewa na mama yake mpya"
"Mwanangu una ukweli gani na hayo unayosema?"
"Dada ni mimi tu nilikuwa sijui lakini kila mmoja anaelewa ninavyo nyanyapaliwa..uoni nilivyokwisha kwa ajili ya mateso ya ndoa"
"Ni kweli lakini mpango wao Mungu kaupangua na ukijifungua salama midomo itawashuka"
"Si leo wacha nipumzike kwanza niepukane na karaha za wanadamu huenda wakasababisha kuharibu mimba yangu kwa hasira"
"Pumzika mdogo wangu"
Siku ile nilipumzika kwa dada hata siku ya pili vile vile nilikaa kwa dada.Shemeji yeye alisema nipumzike pale mpaka mume wangu atakaponifuata kama hata kuja basi nitaaendelea kuwepo pale mpaka nitakapojifungua.
Siku ya tatu mume wangu alikuja na kuniomba nirudi kwangu,nilimkatalia na kumwambia
"Bado mwezi mmoja mkeo aingie ndani mimi wa nini mgumba tena tasa ninajekujazia choo bila faida"
"Mke wangu maneno ya watu yatavunja ndoa yetu wewe ni mke wangu tuliyeapa mbele ya Mungu kuwa kifo ndicho kitakachotutenganisha"
Siku zote dada alikuwa na maneno ya busara na mume wake,walinisihi nirudi kwangu na kumueleza mume wangu maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa.Japo sikuwa radhi nilikubali kurudi kwa mume wangu kwa shingo upande kutokana na kuwaheshimu dada na shemeji.
Nilirudi kwangu na kuyaanza maisha ya awamu nyingine wakati huo wifi zangu sikuwa na uelewano nao kwa kuwaona wao ndio wabaya wangu.Hapo awali kabla ya matatizo walikuwa marafiki zangu wakubwa kwa kuwapa chochote wakitakacho hata walichonyimwa na kaka yao.
Niliapa sitawapa kitu wataula wa chuya kwa uvivu wa kuchangu,hata walipokuja nyumbani walijichekeleza,nikuwa na mchangamfu nao.Mwezi mmoja baadae mke mwenza alijifungua mtoto wa kike,taarufa nilizipata kupitia kwa shoga yangu.
Mume wangu aliporudi nilimuuliza kuhusu kuletwa mke mwenzangu,uso ulimshuka hakuwa na jibu.Sikutaka kumuudhi sana niliachana na yale.
Siku zilikatika na kufikia siku ya kujifungua salama salimini na kujifungua na mimi mtoto wa kike.Mume wangu alifurahi na kuniomba msaha kwa yote yaliyotokea.Sikuwa na budi kumsamehe pamoja na wifi zangu ambao walikuja kuniangukia.
Niliyaanza maisha upya na mume wangu na mwanangu mpenzi niliyempa jina la dada yangu yaani mama yako Ester.Mwanangu Ester alikuwa vizuri kwenye afya njema.Hali yangu ya mwli ilirudi kama kawaida na kunawili na kunenepa kama mwanzo.
Baada ya miaka mitatu ambayo naweza kusema ilikuwa mizuri ambayo ilinifanya niifurahie ndoa yangu na kumsifu dada kwa yote aliyochangia kuiokoa ndoa yangu.Bila yeye ningekuwa labda nimeolewa na mwanaume mwingine.
Mwaka wa tatu nilishuka ujauzito na ambao uliongeza mapenzi kwa mume wangu.Na muda ulipotimu nilijifungua watoto mapacha wote wa kike.Ilikuwa furaha kwa familia yote iliyozidi kuongeza mapenzi kwa ndugu na jamaa wa mume wangu ambao walijua mimi ni mgumba.
Wanangu walikuwa vizuri na afya nje na wenye miili mikubwa.Na mimi hali yangu ya maisha ilikuwa kwa kumpelekea dada pesa ambazo ndizo alizoninunulia kiwanja pamoja na kusimamia ujenzi wa nyumba yangu.Baadae alinitafutia miladi kama kunitafutia fremu za maduka na kunifungulia maduka.
Huwezi kuamioni shemeji yako kila nilichomuomba alikuwa anihoji napeleka wapi au pesa atakazo niachia alikuwa haulizi pale ninapomwambia zimeisha.Niliweza kujitanua kimiradi ambayo ilisimamiwa na kaka yako Lyasi.
Mungu alizidi kumuonyesha mume wangu anapoamua hana mpinzani,pale aliponiongeza ujauzito baada ya miaka miwili baadae kitu kilichofanya mume wangu kuongeza mapenzi mazito na kuninunulia gari la kutembelea la kifahari.
Muda ulipokaribia wa kujifungua mume wangu hakuwepo alikuwa ametoka kikazi na kuniacha katika matayalisho yote muhimu ya kujifungua kwetu.Basi siku ilipotimu wifi zangu walisimama kidete na kunipeleka hospitali.
Muda ulipotimu nilijifungua salama mtoto wa kike mwenye afya njema.Nikiwa nyumbani baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kujifungua salama,mume wangun alipiga simu na kutaka kujua hali yangu
"Haloo my sweet"
"Haloo my Honey"
"Vipi"
"Safi"
"Umejifungua salama?"
"Salimini"
"Mtoto gani?"
"Wa kike"
"Ooh mkosi gani?"
"Mkosi wa nini?"
"Aaa..aa mke wangu unajua sikupenda kila mara ujifunguapo ninakuwa mbali nawe"
"Mmmh mume wangu yaani kuwa mbali nami wakati wa kujifungua ni mkosi"
"Aaa..aa unajua ni ulimi nilitaka kusema nina bahati mbaya"
"Pole mume wangu najua ni kuchanganyikiwa na furaha Mungu kaamua kukufungulia bomba la maji"
"Wanne wanatosha"
"Mimi sina neno ni wewe tu uliyekuwa na haraka ya watoto"
"Basi mke wangu nakuombea afya njema wewe na watoto wetu hasa huyo mgeni wetu"
"Amina mume wangu Mungu atazipokea dua zako"
Mume wangu alirudi baada ya siku tatu na kuja kujumuika na familia yake.Ilikuwa nifuraha isiyokifani ya kuungana na familia yake,Kwa kweli nilimshukuru mungu kwa maajabu aliyonifanyia ya kunipatia watoto mfurulizo na kuwafunga midomo walioona labda mtoto wa kwanza nilikuwa nimebabatisha.
Maisha yalikuwa mazuri na mimi mambo yangu yalizidi kuwa mazuri miradi yangu iliendelea vizuri na kaka yako Lyasi aliisimamia vizuri sana na muda ulipotimu wa kuoa nilimsimamia kila kitu ikiwa pamoja na kumpa moja ya nyumba zangu.
Basi mwanangu kweli maisha ya ndoa ni kama msumeno yanakata nyuma na mbele.Mwanzo nilijua wenye matatizo ni wanaume tu kumbe hata sisi wanawake tuna matatizo makubwa tena ya kutisha.
Huwezi kuamini mwaka mmoja wa ndoa ya kaka yako ilipitia mambo mazito yanayotisha na kukutisha tamaa akikueleza.Huwezi kumueleza chochote zaidi ya kumueleza amani ya maisha yake na furaha ya moyo wake ni kuivunja ndoa yake.
Japo ni dhambi kuivunja ndoa ya mtu lakini kwa hali ile ilikuwa haina jinsi kama kumkata kiungo mgonjwa wa kansa.Japo unampunguza kiungo lakini ndio pona yake.
Kwa kweli niliisimamia ndoa ya kaka yako na kuivunja kwa mkono wangu japo mama yako alijaribu kuiokoa bila mafanikio.Mambo aliyofanyiwa kaka yako na wifi yako yalikuwa hayafai kufanyiwa mwanadamu.
Ni kweli dini inatuziwia kuachana lakini kwa mtindo ule huwqezi kukubali kuona nyumba yako inateketea na kuiacha.Lazima utamwaga maji na kuizima ukikosa,ukikosa maji utatumia mchanga.
"Ma mdogo ni vitendo gani hivyo alivyo fanyiwa kaka ifikie kuwachukia wanawake wote"
"Kwa vile mwenyewe yupo siwezi kukueleza chochote utaona naongeza chumvi"
"Hapana ma mdogo nidokeze angalau kidogo"
"Sundi kaka yako hayupo mbali ukitoka hapa pitia kwake mara nyingi akitoka dukani huwa nyumbani kwake,tena ana mpango wa kuokoka"
"Mmmh makubwa,ehe lete habari"
"Tena ujue nimechanganya mada niliishia wapi?"
"Baada ya kupata mdogo wangu wa nne na mambo kuwa mazuri yaliyopelekea kaka kuoa"
"Oooh kweli unakumbukumbu na unanifuatilia kwa makini"
"Mama nisikufuatilie wakati nimo darasani na mtihani upo mbele yangu nisiposoma hapa leo,siwezi kusoma siku ya mtihani"
"Ni kweli mwanangu,basi ilipita mwaka toka nijifungue kumbe sina habari,kitendo changu cha kuzaa watoto wa kike kilimuudhi baba yako mdogo na wifi zangu.Ambao walianza choko choko zao tena pele waliposema..
Nitamzalia watoto wa kike mpaka lini nani atakuwa mrithi wa mali zake kama nitaendelea kumjazia mitoto ya kike.Kwa kweli hilo sikulijua mwanzo lakini siku zote sikio halilali na njaa.Kuna mtu alizikamata taarifa zingine.
"Shoga una mpya?"
"Ipi hiyo tena mpenzi?"
" Mambo yameanza upya"
"Yapi hayo?"
"Wanadamu kweli hawana shukurani yaani kila nikiwaangalia wifi zako siwamalizi"
"Kivipi mpenzi?"
"Yaani wameanzisha kampeni mpya ya kukutoa ndani"
"Ipi hiyo mbona kila kukicha maaduni wanaongeka yalabi"
"Ni hivi baada ya kufeli mpango wao wa kukutoa ndani wa kupata mtoto,sasa wamekuja na mpya eti umewajazia malaya nani atakuwa mrithi wa mali za mumeo.Imeanzishwa kampeni nyingine ya kutafuta mtoto wa kiume nje ya ndoa ili kukung'oa ndani"
"Mmmh makubwa"habari zile zilinishtua na kuninyima raha kila nikiwafikilia wifi zangu siwamalizi

Itaendelea
 
HADITHI: Sundi
MTUNZI: Ally Mbetu
SEHEMU: 03

ILIPOISHIA:
"Wanadamu kweli hawana shukurani yaani kila nikiwaangalia wifi zako siwamalizi"
"Kivipi mpenzi?"
"Yaani wameanzisha kampeni mpya ya kukutoa ndani"
"Ipi hiyo mbona kila kukicha maaduni wanaongeka yalabi"
"Ni hivi baada ya kufeli mpango wao wa kukutoa ndani wa kupata mtoto,sasa wamekuja na mpya eti umewajazia malaya nani atakuwa mrithi wa mali za mumeo.Imeanzishwa kampeni nyingine ya kutafuta mtoto wa kiume nje ya ndoa ili kukung'oa ndani"
"Mmmh makubwa"habari zile zilinishtua na kuninyima raha kila nikiwafikilia wifi zangu siwamalizi.
SASA ENDELEA...

"Basi ndio mpango wao na mumeo siku hizi kila akitoka kazini anaanzia kwa bi mdogo ndipo arudi kwako"
Nilijikuta moyo ukiniuma na kuona kila moyo ukitulioa wanaanzisha mapya kosa langu nini?Nilipanga baada ya kuondoka shoga yangu niende kwa dada kumueleza habari zile ambazo zilikosesha raha.Sikuamini wanangu leo wanaonekana machangudoa,kosa langu nini kuzaaa watoto wa kike.
"Basi shoga mpango uliokuwepo ndio huo kazi kwako kuipangua kama ulivyo wanyamazisha"
"Mimi sina uwezo ni uwqezo wa Mungu pekee hakuna anayejipangia"
"Lakini Mungu yupo pamoja nawe"
"Hata nisipo pata mtoto wa kiume bado Mungu yupo nami"
"Basi shoga ni hayo nami nakuombea Mungu upate mtoto wa kiume"
"Mmmh shoga hata mwaka ujaisha nibebe tena mimba wacha nipumzike,liwalo na liwe"
Baada ya shoga yangu kuondoka,mimi kiguu na njia mpaka kwa dada ambaye alishangaa kuniona
"Vipi mbona hivyo nikikuona upo hivyo najua mambo sio mazuri"
"Ma mdogo unamjuaje mtu akiwa kwenye mabadiliko maana mimi nilipokuja nilikuwa nimeyaficha moyoni"
"Mkubwa yoyote unapokuja jicho lake la kwanza usoni kwako kujua umekuja na heri au shari"
"Mmhu ikawaje?"
"Basi sikuwa na kumficha zaidi ya kumueleza ukweli,baada ya kunisikiliza asema
"Mdogo wangu jiepushe na maneno ya pembeni siku zote sio mazuri hata kama ni yakweli yeye yanamuhusu nini.Hebu fikilia mwenzio baada ya kukueleza yale yupo tuli,lakini wewe presha juu"
"Hapana pamoja yananiumiza lakini yana ukweli asilimia mia moja"
"Ndio maana nasema yakatae maneno ya pembeni siku zote huwa ya uchonmganishi.Hata kama ni ya kweli yeye yanamuhusu nini,kwani mwenendo wa mume wako unauonaje?"
"Japo anarudi kama kawaida lakini nimesikia kumbe huwa anawahi kurudi na kupitia kwa mwanamke wake"
"Mdogo wangu nakuomba hata kama ni jambo la kweli ambalo hulijui mkomeshe tena akome.Hata sisi waume zetu walikuwa na makosa yao lakini tuliziba masikio mpaka leo tupo nao"
"Sasa dada huoni kama mtu anaye kueleza ukweli ni mtu mzuri"
"Mdogo wangu huyo ni nyoka tena mwenye sumu kali unafikili ukiachika atakusaidia nini?"
"Sasa unanishauri nini?"
"Mpende mumeo kama ilivyo ada usikubali ya kuambiwa siku zote neno la kumabiwa linauma sana.Na siku zote mleta taarifa huongeza chumvi zionekane zinaukweli tena amezithibitisha kwa machjo yake.Jiepushe naye uwe naye kama rafiki lakini maisha yako aachane nayo"
"Sasa akija nimwambieje?"
"Akianza tu habari zake mwambie mbona shoga hizo habari ninazo kitambo.Hapo utakuwa umemkata maasni na kuona hila zake zimegonga mwamba"
Niliachana na dada na kurudi nyumbani nikiona pamoja na dada kunieleza yale,hakunisaidia lolote.Nilijua atanieleza cha maana kumbe kumuona muongo shoga yangu.Mbona ya mwanzo yote yalikuwa kweli ubaya upo wapi?
Siku hiyo mume wangu alichelewa kurudi,moyo uliniuma kwa kujua lazima alikuwa kwa mwanauke wake.Kibaya zaidi hata chakula alikataa kula kwa kusingizia ameshiba.Nilijikuta nalia peke yangu na kujikuta nakosa raha.
Lakini maneno ya dada kwa upande mwingine niliyaona yana maana kubwa,nilijiuliza bila shoga yangu nisingejua lolote na moyo wangu ungekuwa kwenye amani.Nilijiuliza maumivu ya moyo ninayo yapata ni kwa ajili ya maneno ya shoga yangu japo niliyaamini kwa asilimia mia.
Siku zilikatika mabadiliko ndani yalikuwa makubwa kwa kuelezwa kuwa nisiache chakula cha usiku.Na safari za kikazi zilikuwa haziishi.Kama kawaida shoga yangu hakuacha kuja kunipasuka moyo.Yaani nilipo muona moyo ulinilipuka na kutaka kujua kulikoni alipofika tu.
"Shoga mambo kila kukicha yanazidi kuwa mabaya"Mungu wangu kumkanusha nilitaka lakini sikujua ana habari gani.Nilipiga moyo konde na kumuuliza
"Mambo gani tena yailahi mbona mwaka huu nitakufa kwa kihoro"
"Yaani shoga wanaume watu wabaya sana"
"Kwa nini?"
"Kwanza shemeji yupo wapi?"
"Kazini"
"Kazini ofisini au kasafiri"
"Mbona unanitisha kulikoni?"
"Ndio maana nikasema wanaume ni wauaji tena wana sumu kali kama ya nyoka"
"Mbona sikuelewi?"
"Basi unajua juzi nilipokuja ukanieleza mumeo amesafiri,nilikubali lakini mtandao ulimkamata kumbe sasa hivi amehamia kwa bi mdogo tena ana tumbo la leo la kesho"
"Mmmh utani huo"
"Basi muda wote yupo na huyo mwanamke ambaye amempangia nyumba nzima,na sasa safari ziotazidi"
"Mungu wangu mbona nanyanyaswa hivi mtoto wake"
"Sikiliza Eliza nawe umezidi upole kama upo tayali nitakupeleka mpaka alipoi mumeo.Tena nitakusaidia kumfundisha adabu huyu mwanamke.Ndiyo tabia yake kuwachukua waume za wenzie"
"Yaani we niache hata nguvu zenyewe zimeyeyuka zote"
"Sasa nikusaidieje?"
"Ni hivi shoga nakuomba kuanzia leo lolote linalo muhusu mume wangu kama unaliojua liishie huko huko.Namba leo iwe mwanzo na mwisho"
"Ishakuwa hivyo?"
"Wewe si rafiki bali adui yangu,huwezi kila siku kuiniumiza roho naomba leo iwe mwisho nma kwangu nisikuone"
"Basi nisamehe"
"Nimekusamehe ila ushoga basi"Pamoja na kluniomba msamaha sikumkubalia zaidi ya kuuvunja urafiki rasmi japo moyo ulinisuta.
Mwanzo mume wangu alikuwa akiuniomba msamaha anapochelewa,lakini ikageuka hali ya kawaida.Hata kulala nje ikawa jambo la kawaida.Niliumia mtoto wa kike na kupoteza uzito mwilini kwa mawazo.
Nilijiuliza hivi wote wanapata misukosuko kama mimi,ina maana hata dada alivumilia matatizo yale.Basi lazima alikuwa na moyo wa chuma,nilijiuliza inamaana hiyo ndiyo ya wanaume wote.Nakumbuka tona niwe na dada sijawahi kumuona akipoteza uzito kama mimi inamaana moyo wangu ni dhaifu.
Haikuishia hapo nilipata taarifa ya juu juu kuwa mke mwenzagu amejifungua mtoto wa kiume kwa hiyo safari yangu imeiva.Niliyapuuza na kujua ndiyo yale yale ya shoga yangu niliyo yakataa,hayakunishtua moyo nilisubili nione waliyonitabilia.
Baada ya taarifa ile ilipita miezi mitatu,siku moja nikiwa na wanangu tukipata kifungua kinywa.Mara waliingia wifi zangu niliwakaribisha chai.Lakini hawakuonekana kunijali zaidi ya kusema
"Hukumu imetimia"
Nilishangaa kuwaona wakiingia chumbani kwangu kitu ambacho hakijawahi kutokea,toka niolewe na kaka yao.Nilitulia nione wanataka kufanya nini? Basi baada ya muda nilishangaa kuona vitu vyangu vikitolewa na kuhamishiwa chumba cha watoto
"Hey jamani mbona hivyo?"
"Utawala wako umekwisha uliruka ile na hii ruka"
"Mbona siwaeleweni"
"Utatuelewa"
"Naomba mtoke chumbani kwangu"
"Hiki si chumba chako tena sasa utalala na watoto"
Nilijikuta napandwa na hasira na kutaka kukamatana na wifi zangu niliogopa wangeniumiza kwa sababu walikuwa wengi.Nilikubali yaishe na kusubili nione mweisho wao kwa kuwaomba niondoe vitu vyangu mwenyewe.
Basi niliingia chumbani na kuondoa vitu vyangu muhimu na kuviamishia chumba cha watoto.Baada ya kuhamishishia nilisubili nione nini kinaendelea.Baada ya kuondoa vitu vyangu na kufanya usafi wa chumba.
Baada ya saa moja na nusu nilisikia sauti ya gari nje,Nilitulia sebuleni na wanangu ambao walikuwa bado hawajaelewa kitu.Nilimkumbuka shoga yangu pamoja na kumuona mmbea bado alikuwa na umuhimu kwangu.
Mara wifi zangu walitoka nje na kurudi na mizigo waliyoiingiza chumbani kwangu kikiwemo kitanda cha mtoto mchanga.Mara nilisikia "Karibu malkia wetu"
Mara aliingia mume wangu akiwa amempakata mtoto mchanga ameongozana na mwanamke mmoja aliyekuwa amevalia vazi la kitenge kuanzia chini mpaka kiremba.Sikusema kitu japo niliwaona wifi zangu walikuwa wamejiandaa kwa shari.
Sikunyanyua mdomo wangu niliwaangalia wafanye watakavyo,baada ya yule mwanamke wa mume wangu kuingia ndani.Wifi zangu waliingia jikoni na kuanza kumuandalia chakula cha mchana.Walikuwa wamekuja na vyakula vyao kabisa kazi ilikuwa kuingia jikoni na kupika.
Niliwachukua wanangu na kujifungia ndani na kuanza kulia nikisaidia na wanangu.Kilio cha wanangu kilinifanya ninyamaze na kuanza kuwabembeleza.Roho iliniuma na kuona la muhimu ni kuondoka kurudi nyumbani kwa kuwa sikuwa na mapungufu kwenye maisha yangu.
Nikiwa bado nimekumbatiana na wanangu nilishtushwa na mlango uliokuwa ukigongwa.Sikunyanyuka mpaka niliposikia sauti ya mume wangu.Nilinyanyuka huku nikifuta machozi na kwenda kufungua mlango
Nilipofungua malngo na kukutana na mume wangfu ambaye aliyaona machozi yangu na kuniuliza
"Sasa unalia nini?"
"Yaani umeamua kunifanyia hivyo mume wangu?"
"Kipi cha ajabu"
"Hakuna cha ajabu"
"Sasa kinacho kuliza?"
"Mume wangu unadiliki kunitoa chumbani mke wako wa ndoa na kumuingiza malaya ndani?"
"Basi huyo unaye muona malaya ndiye mwenye thamani kwenye familia"
"Thamani gani kuliko mke wako wa ndoa nimekuzaliwa watoto wangapi mume wangu leo umewaona si kitu?"
"Hivi wewe mwanamke ni nani aliyekuambia hapa nataka kufungua baa au grosary?"
"Una maana gani kusema hivyo mume wangu?"
"Nani amekwambie nina shida ya mitoto ya kike ndio mwanzo wa kugeuza kitua cha kulea watoto wasio na baba wala hakuna mrithi wa mali zangu"

Nini kitaendelea? Tukutane tena.
 
SEHEMU: 04

ILIPOISHIA:
"Kipi cha ajabu"
"Hakuna cha ajabu"
"Sasa kinacho kuliza?"
"Mume wangu unadiliki kunitoa chumbani mke wako wa ndoa na kumuingiza malaya ndani?"
"Basi huyo unaye muona malaya ndiye mwenye thamani kwenye familia"
"Thamani gani kuliko mke wako wa ndoa nimekuzaliwa watoto wangapi mume wangu leo umewaona si kitu?"
"Hivi wewe mwanamke ni nani aliyekuambia hapa nataka kufungua baa au grosary?"
"Una maana gani kusema hivyo mume wangu?"
"Nani amekwambie nina shida ya mitoto ya kike ndio mwanzo wa kugeuza kitua cha kulea watoto wasio na baba wala hakuna mrithi wa mali zangu"
SASA ENDELEA...

"Mume wangu nani aliyerkuambia mtoto wa kike arithi mali za wazazi wake"
"Mrithi siku zote ni mtoto wa kiume na ndiye aliyeniumiza kichwa na sasa amepatikana mama aliye mletea ndiye mwenye thamani kwangu"
"Mume wangu hata dini inakataza kudhini nje ya ndoa"
"Hiyo unajua wewe ni nani aliyekuambia yaliyoandikwa kwenye vitabu yanatoka kwa Mungu?"
"Leo hii usaliti wako umekufanya umsaliti Mungu,lakini kumbuka ghadhabu ya Mungu huwezi kuiziwia"
"Sasa tuachane na hayo,sikufuata kuhubiliwa injili hapa.Kilichonileta ni kukujulisha kuwa kuanzia leo mgeni ndiye atakaye kuwa na madaraka kweenye nyumba hii wewe utakuwa chini yake"
Yalikuwa maneno makali kama kuimeza shubiri au kuuchokonoa moyo wangu kwa mdenge.Nilipandisha pumzi na kujibu kwa sauti ya kilio
"Sa..sa.aa.awa"
"Huo ndio uamuzi kuanzia sasa na mambo yote utamfuata yeye na kukupangia"
"Sawa hakuna tatizo mume wangu"
Baada ya kuondoka nilirudi kitandani na kukianza kilio upya,safari ile sikusikiliza kilio cha watoto.Nililia mpaka uso na macho yakavimba,nilitoka hadi sebuleni na kukuta hali ya sebuleni imebadilishwa na kupangwa tofauti na nilivyo panga mimi.Tena wakisimamiwa na mwanamke wao.
Nilipopita nimeongozana na wanangu yule mwanamke alinibinulia mdomo na kutema chini.Sikujali niliwachukua wanangu hadi nje na kumuomba dereva anipeleke kwa dada.Lakini dereva alisema kuwa amekatazwa kusikiliza amri ya mtu yoyote zaidi ya mwanamke mgeni
"Mama wacha nikamuombe ruksa ya kukupeleka mjini"
"Hapana Salumu wacha tu tutapanda daladala"
"Hapana mama wacha nikachukue ruhusa nikupeleke kwa nini upande daladala wakati magari yapo?"
"Salumu we acha tu"
"Kwani mama imetokea nini?"
"Hakuna lolote"
"Sawa mama,au nikupeleke tu kwani hata nikikupeleka atanifanya nini?"
"Salumu nashukuru kwa msaada wako"
Niliagana na dereva wetu ambaye alikuwa kwenye maswali mazito yasiyo na majibu.Nilikwenda hadi kituo cha teksi na kukodi gari hadi kwa dada.Aliponiona alishtuka sana na kuniuliza kulikoni maana kila kukicha yanazuka mapya
"Mmmhu lete taarifa au shoga yako kayaleta mapya?"
Nilimueleza yote yaliyonisibu na kumfanya dada abakie kinywa wazi baada ya kutulia kwa muda alisema
"Yote ilikuwa lele sasa ndiyo ngoma kamili,yaani mumeo amefikia hatua hiyo,kwa hiyo amekufukuza?"
"Hapana"
"Ila?"
"Kwa hali ile sio lazima ufukuzwe"
"Sasa siukilkiza mdogo wangu suala hili ni zito,kabla ya kukushauri lolote kwanza kabisa muda huu bila kupoteza muda nenda kwao na mumeo uwasikilize wanasemaje ndipo nasi tutakuwa na kuyaongea"
"Sawa dada nimekuelewa"
Nilikodi gari jingine hadi kwa wazazi wa mume wangu,bahati nzuri niliwakuta wote.Waliponiona walinikalibisha na kunishangaa na hali niliyokuwa nayo.Bila kupoteza wakati niliwaeleza yote yaliyonisibu,walionyesha kushangazwa ha habari zile na kuniambia nipumzike ili wafanye utaratibu wa kumwota mume wangu.
Nilitulia uwani kwenye mkeka chini ya mti kumsubili mume wangu,baada ya muda mume wangu aliwasiri na kuitwa wote sebuleni na kuulizwa sababu ya kufanya niliyoyasema
"Wazazi wangu najua mnajua vizuri jinsi ninavyo umia na mrithi wa mali zangu.Kila kukicha mke wangu ananijazia mitoto ya kike anafikili mimi nataka kufungua baa, grosary au danguro"
Nilijikuta namkatisha kauli mume wangu baada ya maneno yake kunichoma
"Mume wangu ni maneno gani hayo yaani leo hii wanangu umewabashiria kuwa mabaa medi au machangudua kwa lipi hasa.Ina maana hawatasoma na kuwa na nyadhifa serikalini"
"Labda saerikali yako ya mabaa medi au machangudoa"
"Kweli mume wangu umenichoka,asante sana"
Baada ya kusema yale nilinyanyuka ili niondoke lakini baba mkwe alinirudisha na kusema
"Mwanangu katika siku umetukosea adabu ni leo au kwa sababu ya vijipesa zako,yaani umefikia hatua ya kuwaita wajukuu wangu mabaa medi na machangudoa..Siamini kitendo chako kinatuweka wapi mbele ya familia ya mkeo,watatujua sisi wote ni wahuni na familia yangu wote wahuni"
"Lakini baba wewe unasema hivyo suara hili hata mama anajua"
"Ndiye aliye kwambia uwaite wajukuu zangu mabaa medi na machangudoa...Eti mama Kijoki?"
"Mmmhu ..ha.a..pana we mtoto usinigombanishe na baba yako"
"Baba hili sio jambo la siri tulikubaliana kutafuta mtoto wa kiume iuli awe mrithi wangu"
"Yaani kweli nyinyi ni wapumbavu wa hali ya juu nani alikwambia mrithi wa mali ni mtoto wa kiume tu kama ukuzaa mwanaume mali yako inakwenda wapi?"
"Baba Kijoki usimlaumu mtoto ameisha kosa la muhimu ni kumkosoa ilki asirudie"
"Asirudie ni kama kuzaa nje ya ndoa amezaa na ni dhambi kumbwa kibaya zaidi ..Mwanangu Kijoki unadiliki kumfukuza mkeo wa ndoa kwenye chumba chake kwa ajili ya hawala wako...Umeidhalilisha ndoa yako kiasi gani..umemdhalilisha mkeo kiasi gani...umewakosea kiasi kikubwa wanao kiasi sijui wakikuwa utawaeleza nini na kauli yako chafu kama choo kisicho na uangalizi watu wanajisaidia ovyo bila mpangilio"
"Baba Kijoki ni maneno gani hayo mwanao amekosa hata ukisema nini maji yameisha mwagika hayazoleki"
"Mmmmh sasa nimeelewa kumbe mbaya ya mkwe wangu si mwanangu bali mke wangu...sasa ni hivi ngoja nimalize haya nina kazi na wewe yako yanakushinda unaingilia maisha ya mwanao"
"Baba Kijoki yamekuwa hayo?"
"Kwanza funga kopo lako chafu,na ukizidi nitakugeukia mwanamke mbaya usiye na haya.Kumbe wewe ndiye chanzo cha yote"
Kwa kweli nilijikuta najilaumu kwa kutofikisha matatizo yangu kwa baba baada ya kuona mama mkwe na wifi zangu wakinigeuka.Ilionyesha jinsi gani baba mkwe alivyo na msimamo thabiti juu ya ndoa.Mama mkwe aliufyata kama sio yeye
"Ni hivi nasema ukitoka hapa ukauondoe uchafu wako sitaki kuuona na hao dada zako wamekosa adabu kiasi gani kufikia hatua ya kuingia chumba cha wizi yao bila idhini yake...Kijoki ndivyo nilivyo wafunza kuishi kwa mtindo huo wa kukosa adabu...
Nasema hivi watarudi watanikuta leo watatafuta pa kwenda naona wamenisahau,hakuna hata mwenye mtoto wacha wa kike hata wa kusingiziwa.Huyo mume kwao kitendawili waolewe na nani kwa tabia zao mbaya" baada ya kusema yale alinigeukia mimi niliyekuwa nimewapakata wanangu
"Mama pole sana lakini nimeisha mjua mchawi wa ndoa yako,niliyasikia nakayadharau kumbe yalikuwa na maana yake.Leo ndio nimesaidi muvunja nchi ni mwananchi...Mwanangu rudi kwako nakuhakikishia nitakuwa na wewe muda wote"
"Asante baba kwa kuliona hilo,ni mengi sikujua kumbe yote ningeyaleta kwako"
"Mwanangu yote nayajua niliwaonya, kumbe walifanya mambo yao kwa siri sasa nasema kwanza sipendi kuongea mengi...mama niache niongee na hawa washenzi wa tabia kapumzike nje na wanao"
Nilitoka nje na kuwaacha mume wangu na wazazi wake kwenye kikao cha dharula.Baada ya nusu saa mume wangu aliondoka bila kuniaga.Nilitulia nisubili nini kilichoendelea,baada ya muda niliitwa na baba mkwe na kunieleza
"Ni hivi mama nimemtuma akarudishe vitu vyako ndani na kisha auondoe ule uchafu ili urudi chumbani kwako mama pole sana mwanangu...lakini kwa nini hukuja kunieleza na mapema?"
"Kutokujua baba"
Nilishinda ukweni mpaka jioni na kufuatwa na dereva wetu Salumu,aliyenichukua na kunirudisha nyumbani kwangu.Nilipofika ndani kwangu niligundua vitu vyangu vingi vimechukuliwa.Lakini sikujali sana.
Usiku wa siku ile nililala peke yangu mume wangu hakurudi,hiyo haikunishtua nilijua ni kawaida yake.Lakini niliona aibu kwenda kumueleza baba mkwe,ilionyesha kiasi gani mume wangu asivyoi nipenda amelazimishwa na baba mkwe vile vile ilionyesha jinsi nisivyo pendwa na familia ya mume wangu zaidi ya baba mkwe.
Siku ya pili nilirudi hadi nyumbani kwa dada na kumueleza nilipofikia.Dada alisema
"Unaona vitu vingine sisi kama sisi hatuwezi kuviamua kwa kuwa ni waolewaji hatuna uamuzi.Imeonyesha jinsi gani mkweo wa kiume alivyo na msimamo na jinsi gani mama mkwe wako alivyo adui yako namba moja"
"dada unafikili kuna ndoa hapo?"
"Inaweza kuwepo na isiwepo kwa kuwa umezungukwa na wabaya wako lakini kwenye haki ushindi huwa juu,Mungu atakusaidia utawashinda"
"Na dua letu lipokelewe"
"Amina"
Baada ya maongezi na dada nilirudi kwangu,nilimuuliza mlinzi wa nyumba kama mume wangu amerudi.Alinijibu hajamuona,siku ile nayo ilipita bila kumuona mtu yoyote si mume wangu wala ndugu wa mume.
Sikujali kwa kuwa pesa za matumizi dereva wetu aliniletea,lakini nilijiuliza kuna agenda gani ya mume wangu na hatma ya maisha yangu kwake.Nilikuwa naimani kwa kauli nzito ya baba mkwer basi angekuwa na uoga moyoni mwake.
Ilionyesha wazi alikuwa amedhamilia kufanya vile,kwa hiyo ni wazi sitakiwi na mume wangu kwa kuwa nimemjazia machanguzoa na mabaa medi.Niulijikuta nakosa amani moyoni mwangu,kama uvumilivu nimeonyesha wa hali ya juu kila mmoja atakili.
Imeonyesha sasa nalazimisha penzi au ndoa wakati sitakiwi,nikiangalia maisha yangu si mabaya ni ya kawaida tu nilikuwa na nyumba moja aliyonijengea mume wangu enzi ya mapenzi moto moto na nyingine niliyojenga kwa nguvu za dada.
Niliijiwa na wazo baya la kuondoka pale kwangu na kurudi kwetu na huo ndio mwanzo na mwisho wa ndoa yetu. Lakini maamuzi yalikuwa mazito,nililiangalia jumba lote nililoachiwa na watoto nikipatwa tatizo nani atanisaidia.
Nilijiuliza swali jingine kung'ang'ania pale nimeolewa au nimejioa na sina pa kwenda ni wazi mume wangu anajua sina pa kwenda ndio maana kaamua kuniachia jumba lile.

Itaendelea.
 
SEHEMU: 05

ILIPOISHIA:
Ilionyesha wazi alikuwa amedhamilia kufanya vile,kwa hiyo ni wazi sitakiwi na mume wangu kwa kuwa nimemjazia machanguzoa na mabaa medi.Niulijikuta nakosa amani moyoni mwangu,kama uvumilivu nimeonyesha wa hali ya juu kila mmoja atakili.
Imeonyesha sasa nalazimisha penzi au ndoa wakati sitakiwi,nikiangalia maisha yangu si mabaya ni ya kawaida tu nilikuwa na nyumba moja aliyonijengea mume wangu enzi ya mapenzi moto moto na nyingine niliyojenga kwa nguvu za dada.
Niliijiwa na wazo baya la kuondoka pale kwangu na kurudi kwetu na huo ndio mwanzo na mwisho wa ndoa yetu. Lakini maamuzi yalikuwa mazito,nililiangalia jumba lote nililoachiwa na watoto nikipatwa tatizo nani atanisaidia.
Nilijiuliza swali jingine kung'ang'ania pale nimeolewa au nimejioa na sina pa kwenda ni wazi mume wangu anajua sina pa kwenda ndio maana kaamua kuniachia jumba lile.
SASA ENDELEA…

Baada ya mashauri ya peke yangu ya siku mbili mfurulizo nikiwaza mambo mengi niliyojiuliza na kujijibu mwenyewe hatimaye nilipata jibu ambalo ndilo litakalo kuwa la mwisho bila kusikiliza ushauri wa mtu yoyote.
Ni kweli mashauri mengi huwa kama maji yanayo upoza moyo wa mtu,lakini basi sio kosa la makusudi.Nimefundishwa tusamehe saba mara sabini lakini sasa too much inatosha Mungu atanisamehe.
Nimeweza kuvumilia ndoa yangu mwaka wa sita sasa na kukubali kuyasahau yote,lakini kwa hili inatosha.Ilikuwa inawezekana kabisa maamuzi yangu ya kuondoka na kugoma kuriudi kwa mume wangu ingemfanya mume wangu aishi kwa uhuru mkubwa.
Kwa kuogopa mume wangu kulaaniwa na baba yake kwa ajili yangu,wakati kuna njia ya kuepusha mataizo ya kukubali yaishe kwa kumuachia mwenzangu mwenye mayai ya kiume sio mimi mwenye mayai ya machangudoa na mabaa medi.
Kupitisha uamuzi wangu ilikuwa ngumu kutoa maamuzi mazito,moyo uliniuuma sana.Nililia usiku mzima lakini nilimuomba Mungu aniusamehe kwa maamuzi yangu mazito hatakakuwa na suruhu kwa kuwa nimechoka nahitaji uhuru wa moyo wangu na faraha ya maisha.
Kama nimeikosa kwenye ndoa sidhani nje ya hapo itakosena,japo moyo uliniuma kwa kushindwa kutimiza ndoto yangu ya tangu utotoni kuishi na mume wangu na kutenganishwa na kifo au kila mmoja atembelee mkongojo.
Nibeba nguo zangu tu na kucha kila kitu,nilivyo beba vingi ni vya wanangu,lakini mimi nilibeba nguo chache kwa kujua suala la nguo kwangu sio tatizo.Vile vile kumuonyesha mume wangu sikufuata alivyo vifikilia kwa kufikili labda nyumba yake na magari yake pamoja na utajiri wake unaonifanya ning'ang'anie kwake.
Nilipanda gari hadi nyumbani kwa dada,kama kawaida dada alishtuka na kutaka kujua kulikoni maana ndoa yangu imekuwa inamuwerka roho juu.
"Mmhu mdogo wangu kulikoni maana kila nikikuona roho hunipaa"
"Nafikili umefika muda ukiniona roho yako inatua sio kupaa tena"
"Una maana gani kusema hivyo?"
Nilimueleza yote na uamuzi nilioamua kuuchukua,dada aliniangalia kwa jicho la huruma na kusema
"Kwanza lazima nikusifu ni mwanamke wa shoka lakini bado sijakubaliana na uamuzi wako"
"Kwa nini dada?"
"Umerudi kwa mkweo kumsikia naye anasemaje"
"Dada ndoa yangu imekuwa si ndoa bali ndoana"
"Najua lakini kwa msaada wa baba mkwe ulikuwa na nafasimkubwa ya kuiokoa ndoa yako"
"NI kweli kabisa uyasemayo,lakini mume wangu ameonyesha jinsi gani alivyo chukizwa na maamuzi ya baba yake ya kumfukuza mwanamke wake ndani na kuamua kumdharau baba yake kwa kumuondoa mkewe na yeye kuniachia nyumba"
"Tena ndiyo vizuri kurudi kwa mkweo kumueleza dharau aliyo ionyesha mumeo"
"Mama...ooh samahani dada nimechanganyikiwa mpaka nakuita mama"
"Sio mbaya kuniita baba kwa kuwa wazazi wetu hatunao..ehe"
"Dada hakuna mapenzi ya kulazimishana kwa sasa mume wangu hana mapenzi na mimi anaona aibu kumjazia machangudoa na mabaa medi utawaweka wapi? Kwa hali hiyo siwezi kumlazimisha mume wangu kwa shinikizo la baba mkwe"
"Ni kweli ulikuwa na uamuzi gani?"
"Dada sina jinsi zaidi ya kubwaga manyanga naomba usiingize mdomo wako kwa kuwa yoye umeyashuhudia kwa macho kama ameshindwa baba yake mkali kama pili pili kwanza hata yeye simuamini huenda lao moja hawezi kutoa mkwara mzito mwanaye asishtuke"
"Mmh kwa kweli mdogo wangu mpaka hapo uamuzi nakuachia mwenyewe,yaani kila nikikuangalia nakuonea huruma.Ukipata mwili kidogo matatizo yanajitokeza...mdogo wangu ndoa umekururua mwili.Mpaka hapo uamuzi nakuachia mwenyewe najua maisha hayatakushinda kwa kuwa ulijiandaa mapema"
Jioni shemeji mume wa dada aliporudi alielezewa na dada hakusita kunipa pole kwa yote yaliyonisibu na uvumilivu nilio uonyesha mwisha alimalizia kwa kusema
"Unajua umejitahidi na kuyafanyika kazi yote tuliyo kueleza na umeonyesha uvumilivu wa hali ya juu,ambao kwa dunia ya leo ni nadra.Umejitahidi vya kutosha kwa kweli ndoa yako imekuwa sawa na sikio la kufa lisilo sikia dawa na siku zote la kuvunda halina ubani na kila chenye mwanzo hakikosi mwisho"
Nilikaa kwa dada kwa muda wa wiki nzima huku nikijifikilia kama mume wangu akitokea na kuniomba radhi nitachukua uamuzi gani?japo moyo wangu haukuwa tayali kumsamehe na kuwa tayali kuishi maisha ya upeke kwa kujua heri maskini huru kuliko tajiri mtumwa.
Wiki ilikatika bila kuiona sura ya mume wangu,najua alipata taarifa za kuondoka kwangu hata kukataa kuipokea pesa aliyo nitumia kwa matumizi.Na jinsi nilipo muomba dereva asiniletee chochote atakacho pewa na mume wangu.
Baada ya wiki kuisha nilihamia kwenye nyumba yangu na kuyaanza maisha yangu mwenyewe.Japo yaliniwia vigumu kwa kuwa nilikuwa nimezoea kuishi chini ya mtu tena kwa amri.Amini usiamini yalikuwa magumu kwa kweli kama mume wangu angetokea kwa muda ule nilikuwa radhi kumsamehe na kurudi kwangu.
Nyumba niliiona kubwa kama bahari japo haikuwa kubwa kama ya mume wangu ambayo inaizidi yangu ukubwa mara nne.Lakini kwa mume wangu nilikuwa na matumaini huenda atatokea.Maisha yalikuwea machungu kila nilipomkumbuka mume wangu.
Nilitamani nimtafute na kumuomba msamaha ili turudiane hata kwa kukaa nyumba moja na mimi kuwa chini ya mwanamke wake. Lakini nilishangaa na kujiuliza ni moyo gani dhaifu nilio uonyesha kwa kipindi kifupi.
Lakini nilimuomba Mungu anipe ujasiri ili niweze kusahau mume wanmgu hasa ndoto za usiku ninapo ota nipo na mume wangu na nizindukapo usingizini hujikuta peke yangu. Hapo huumia mara mbili na kujikuta nalia peke yangu usiku.
Kilikuwa kipindi kigumu maishani na chenye maumivu makubwa na kuwa na mtihani mzito juu ya maamuzi yangu niliyojiapiza.Huwezi kuamini kila hodi iliyopigwa niuliomba awe mume wangu lakini wapi.Ile hali ilipozidi ilinifanya nirudi kwa dada kuomba ushauri.
"Mdogo wangu pole sana najua kiasi gani unavyoumia hii hali inatofauti kidogo na mwanao Chaty"
"Samahani ma mdogo kwani na da Cathy alifanya nini nakumbuka kuna kipindi alirudi nyumbani na kukonda kama mgonjwa wa tibii na kuna siku alinituma nipeleka barua kwa mumewe,huwezi kuamini sikukubali kumuacha shemeji kwa hali aliyokuwa nayo dada na kumlazimisha turudi wote..
Lakini baada ya kurudi kwa mumewe sasa hivi mzima wa afya njema tena amenenepa mpaka amechusha"
"Mwanangu ya mama yako mdogo nayo ni mazito ambayo nayo utayaelewa vizuri akikusimulkia mwenyewe"
"Utanipa nauri ya kwenda?"
"Hilo usihofu najua ukiyajuayote tana una bahati kila mmoja kwenye familia yetu anamitihani yake ya ndoa ndio maana nikasema maisha ya ndoa ni nje ndani.Wandani wanataka kutoka na waliotoka haweataki kurudi au waliotoka wanatamani kurudi tena,vile vile walio nje wanatamani kuingia takwa kwa kupitia kwa waganga wa kienyeji"
"Mmhu ma mdogo tuendelee maana yote nitasikiliza lakini yako naona mwisho wa matatizo"
"Usiseme hivyo zunguka kote kisha utachambua ndoa ni nini na utakuwa umejifunza kabla ya kuingia kwenye ulingo wa maisha"
"Sawa nimekuelewa..nini kilichoendelea baada ya kuongea na mama?"
"Mama yako aliniomba nijiweke bize ndio njia ya kumsahau mume wangu.Basi kuanzia hapo nilijishughulisha katika moja ya maduka yangu.Nilijikuta nakuwa bize muda wote na kurudi nyumbani nimechoka kama mtu aliye kunywa pombe...
Wanangu niliwatafutia mfanyakazi ambaye waliwalea vizuri kwa kuwapeleka shule ya kindagate kila asubuhi hata magari ya shulu yalijua tyulipo hamia na kuwapitia kila asubuhi.ubize wa kujishughulisha na shughuli za dukani.
Tulijikuta tunagawana majukumu na Lyasi kwa mimi kusafiri nje ya nchi kufuata mizigo ya biashara na kujikuta tunatanua biashara na mambo yalikwenda kama yalivyopangwa.Huwezi kuamini nilimsahau baba yako mdogo na akili yangu yote niliielekeza kwernye biashara.
Kwa nusu mwaka mambo yalikwenda vizuri na mimi kuwa mwenyeji wa baadhi ya nchi nilizofuata mzigo.Hali yangu ya kimwili na kiakili ilirudi kama zamani,nilinenepa na kupendeza.Siku moja baba yako mdogo alishangaa kunikuta dukani kwangu akiwa na mkewe.
Aibu iliwaingia na kuamua kuondoka bila kununua kitu,sikuwajali niliona ni aibu inawasuta lakini sikuwa na kinyongo na yeye wala mwanamke wake kwa kujua hawakujua walitendalo.Nami maisha yalizidi kuniyookea.Hapo ndipo kaka yasko alipopata mchumba na kuja kunieleza.
Nilimuhusina kuwa amlee mkewe asiwe baba yake mdogo kwa kuingilia kazi ya Mungu kwa kuwa tayali kuishi na mkewe kwenye hali yoyote ya uzima na ugonjwa ya raha na matatizo.Kwa kweli kaka yakoi aliunisikiliza.
Alifanikiwa kuoa binti mzuri wa sura lakini mwenye tabia mbaya hata matabishi yana afadhali.Kwa kweli na yeye alivumilia lakini hali ilizidi kuwa mbaya.Ilibidi niingilie niingilie kati kuivunja ndoa ya kaka yako kwa sababu kaka yako aliyofanyiwa yote alikubali mpaka kugeuzwa ndondocha.
Basi tuachane na habari za kaka yako ambazo najua leo utaweza kuzipata.Basi siku moja nikiwa kwenye shughuli zangu nilikutana na shoga yangu wa zamani.Ambaye hakuamini kuniona nipo kwenye hali ile nilijua al;itegemea kunikuta nimekwisha kama sio kubakia mfupa na ngozi kwa niliyotendewa na mume wangu
Aliponiona aliuonekana amepigwa na butwaa na kutoamini macho yake nilimzindua kwa kumwambia
"Usishangae shoga ni mimi yule yule wa zamani Eliza Kijoki"
"Mmmh siamini kweli Mungu mkubwa na hulipa dunia kabla ya mauti"
Kauli ile ilinishtua na kutaka kujua ina maana gani? na kutaka kuja kwa nini amesema vile
"Eliza yaani yote aliyokutendea mumeo yamemtokea puani"kauli ile ilinishtusha kwa kuogopa mzazi mwenzangu kukutwa na matatizo ambayo yataiathiri hata familia yangu kwa kujua malezi ya watoto ni wazazi wote
"Mungu wangu mume wangu amefanya nini tena?"
"Yaani we mtu wa ajabu unamuonea huruma mtu aliyekutenda vile?"
"Shoga eliza yaliyokuleta mengine hayakuhusu..amefanya nini?"
"Mbona amekubwa na aibu ya mwaka!"
"Aibu gani hiyo tena?"
"Mumeo kauziwa mbuzi kwenye gunia"
"Hebu niweke wazi umekuwa kama umetoka kwenye ngano za kiswahili"
"Mumeo alipewa mtoto si wake"
"Si wake una maana gani?"

Nini kitaendelea?
 
SEHEMU: 06
ILIPOISHIA:
"Mungu wangu mume wangu amefanya nini tena?"
"Yaani we mtu wa ajabu unamuonea huruma mtu aliyekutenda vile?"
"Shoga eliza yaliyokuleta mengine hayakuhusu..amefanya nini?"
"Mbona amekubwa na aibu ya mwaka!"
"Aibu gani hiyo tena?"
"Mumeo kauziwa mbuzi kwenye gunia"
"Hebu niweke wazi umekuwa kama umetoka kwenye ngano za kiswahili"
"Mumeo alipewa mtoto si wake"
"Si wake una maana gani?"
SASA ENDELEA…

"Kumbe alilea mimba na mtoto wa mwanaume mwenzake ambaye alikuwa gerezani kwa kufungwa miaka mitano na miezi sita.Baada ya kuondoka yule mwanaume kwa kufungwa.Huku nyuma ndipo alipoikutana na mumeo na kumbambikia ujaiuzito"
Habari zile zilifanya nihisi kama tumbo la kuharisha na kujikuta namuonea huruma mume wangu wadogo zake ambao ni wifi zangu na mama mkwe.Niliiona picha wakiwa mbele ya baba mkwe wakiomba msamaha huku wakifukuzwa kama mbwa.
"Vipi shoga naona umekwenda mbali?"
"Ni kweli habari hizi ni nzito nawaonea huruma watu wazima wameadhirika..ehe"
"Basi yule mwanamke nasikia nyumba yake ilikuwa ndio inamaliziwa kujengwa.Kwa bahati nzuri au sijui niseme yule mwanaume alitumikia kifungo kwa maka na nusu na kutoka baada ya kukata rufaa na kushinda.Si ndipo aliuporudi nyumbani na kumkosa mkewe na kuelezwa na wasamalia wema alipo.
Si ndipo aliupokwenda moja kwa moja kwa mumeo kwa ustaarabu aliomba mtoto wake na kumuachia mumeo yule mwanamke.Hapo ndipo mumeo na mwanamke wake walipoumbuka.
Mumeo hakukubali na kuamua kumshtaki yule bwana,kutokana na kuwa na pesa yule bwana alikamatwa na kuwekwa ndani.Baada ya yule kusulubiwa yule bwana bila kosa,ilibidi aseme ukweli wa mambo.Hapo ndipo yule bwana na yule mtoto na mumeo wakaenda kupima damu japo picha halisi ilionyesha mtoto si wa mumeo.
Vipimo vilikuwa vile vile mumeo si mtoto wake,hapo mbona liliwashuka.Nasikia shoga sikuwepo lakini waliofuatilia kwa karibu walipofika nyumbani yule mwanamke alifukuzwa kama mbwa.Sasa hivi kuna mtafaruku kati ya mama mkwe na baba mkwe juu ya yale yaliyotokea vile vile sasa hivi wifi zako na mumeo ni chui na paka"
"Hayo ni malipo ya duniani siku hizi malipo duniani ahera kwenda hesabu"
"Basi shoga kwa ufupi ni hayo mengine siyajui"
"Sawa shoga nashukuru kwa yote ila tusamehane kwa yote"
"Shoga mbona mimi nilikusamehe mapema nilijua ulikuwa umechanganyikiwa kwanza kusikuamini kukutata umetakata kiasi hiki.Nilijua umekuwa kama mpira wa malatasi uliochoka"
"KIla kitu kina kinapangwa na Mungu na si sisi wanadamu"
"Au umeisha pata mzee mwenzio?"
"Wala ni kulidhika na maisha na kuyasahau machungu"
Shoga yangu aliondoka na kuniacha na mawazo mazito kila nilichojiuliza kilikosa jibu.Nilikuta nikimuonea huruma mume wangu kwa yote yaliyo msibu kwa pigp mujarabu alilolipata kwa kuuziwa mbuzi kwenye gunia kumbe mbwa.Lakini siwahurumii sana kwa kuwa kila mchuma janga hula na wa kwao
Habari zile zilinifanya nikose raha hata sijui kwa nini ziliniweka kwenye hali ile.Hata hamu ya kufanya kazi ilinishinda na kuamua kurudi nyumbani mapema.Nikiwa nyumbani nikikumbuka walivyo nitenda familia ya mume wangu na aibu iliyowakuta,nilijua lazima kwa vile nyuso zao hazina haya watakuja kuniomba msamaha kama mwanzo.
Lakini niliuapia moyo wangu kuwa kata sitakubali kurudi kwa mume wangu hasa baada ya kuyazoea maisha ya upweke na uhuru iliojiwekea.Sikuwa radhi kuurudisha moyo wangu kifungoni tena ,wala kujiingiza kwenye mateso ya kujitakia.
Huwezi kuamini nililia kwa kuona nilionewa bila kusa na kuonekana sina thamani kwenye familia ya mume wangu.Mwanzo nilionekana mgumba,Mungu akawaumbua nimepata mtoto tena si mtoto bali watoto.Hawakuridhika wakatafuta sababu nyingine eti nimewajazia mitoto ya kike.
Lakini Mungu mkubwa amewaumbua sijui watanitazama vipi usoni.mmmh yangu yalikuwa macho na kusubili tuone.Kama atatafuta mwanamke mwingine sawa au atarudi kwangu,sikuwa radhi kugeuzwa Punda wa Dobi asiye na moyo wala masikio"
"Ma mdogo Punda wa Dobi yuko vipi?"Sundi aliuliza baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu akimsikiliza mama yake mdogo ambaye alimuona ni mwanamke aliyepitia mitihani ya ndoa inayokatisha tamaa na kumfanya aihofie ndoa yake.
"Mwanangu Punda wa Dobi ni hadithi moja niliisoma miaka mingi wala sikumbuki ni kitabu gani iliyomuelezea Punda mmoja aliyekuwa anafugwa na Dobi mmoja.Basi katika mji ile ule palikuwepo Simba mfalme wa nyika aliyekuwa na urafiki na bwana Sungura...
Basi Simba yule alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu na alipo pona alikuwa hana nguvu ya kuweza kuwinda wanyama wenye nguvu kwa kuwa bado hakuwa na nguvu.Basi mwanangu Simba yule alikuwa na hamu ya nyama na kumuomba Sungura aliyekuwa shahiba wake amtafutie nyama.
Sungura akamwambia kuwa kuna Punda mmoja wa Dobi anaye landa landa majiani.Sungura alimuahidi kuleta yule Punda kwa Simba na Simba itakuwa kazi lahisi ya kumkamata tu na kumla...
Basi Sungura alikwenda hadi kwa Punda yule ambaye alikuwa jike na kumueleza kuwa bwana Simba anampenda na anataka kumuoa.Punda wa Dobi alikataa kwa kumuhofia Simba anaweza kumrarua na kumla nyama.
Lakini Sungura alimuhadaa na kumueleza kuwa Simba sio anaye mfikilia ni mwenye mapenzi ya kweli na anataka kumuoa ili apate msaidizi hasa baada ya kuugua na kukosa msaidizi.
Punda bila kuelewa alikubali na kwenda na Sungura hadi kwa Simba,alipofika alimwacha Punda pembeni na kumfuata bwana Simba na kumueleza kuwa nyama tayali kazi kwake.Basi Simba alikwenda mpaka alipokuwa amesimama Punda na kumrukia.
Kwa kuwa hakuwa na nguvu Punda alimponyoka na kukimbia hadi kwao huku akiwa amekwaruzwa sehemu za mwili wake na kutoa damu.Sungura alimlaumu bwana Simba kwa uzembe alio uonyesha wa kupoteza kitoweo,lakini Simba alijitetea kuwa ni kutokana na ugonjwa hivyo nguvu zimepungua.
Alimuahodi kumletea tena Punda wa Dobi japo Simba alijua nyama amekwisha ipoteza.Basi Sungura alimuahidi kumletea tena na kumfuata.Alipofika kwa Punda na kumkuta akijikanda majeraha,Sungura alipofika aliangua kicheko kilicho mshangaza Punda wa Dobi na kuhojim kulikoni kumpeleka kwenye dhahama kama ile.
Sungura alimwambia kuwa yale ndiyo mapenzi ya Simba kutokana na kuwa na nguvu nyingi.Lakini alimuahidi kuwa safari hii hatatumia nguvu kama mwanzo.Basi bila kujua alikubali kurudi kwa Simba,wakati huo Simba alikuwa amajiandaa vizuri.
Basi Punda wa Dobi alipofika kwa Simba hakufanya makosa alimkamata vizuri na kumuua"Kufika pale Sundi alijikuta alkimuonea huruma Punda wa Dobi na kumchukia Sungura
"Jamani ma mdogo yaani Sungura ana roho mbaya amemponza mwenzake bila sababu"
"Basim mwanangu hiyo si hadithi kama unavyoisikiliza bali ni mafunzo ya maisha tunayo ishi wakina Sungura wapo wengi na sisi kina Punda nao tupo wengi tunapelekwa kwa Punda bila kujijua na kutolewa uhai"
"Ehe ma mdogo iliishia wapi?"
"Basi baada ya kumuua Punda wa Dobi Simba alimwambia Sungura amchomee moyo na masikio kwanza vitu anavyovipenda.Basi Sungura baada ya kuichoma ile nyama alikula moyo na masikio badala ya kumpelekea Simba...
Baada ya kuichoma ile nyama alimpelekea Simba ambaye alishangaa kukuta kwenye nyama hakuna moyo wala masikio.Simba alipo hoji moyo na masikio vimekwenda wapi walijibu kuwa,Punda yule alikuwa hana moyo wala masikio.
Simba alishangaa kusikia eti Punda wa Dobi alikuwa hana moyo wala masikio.Alikataa kwa kujua hakuna mnyama asdiye na moyo wala masikio.Hapo ndipo Sungura alipo mwambia Simba kuwa kama Punda wa Dobi angekuwa na moyo na masikio asinge asingerudi.
Huwezi kumkosa kumuua kisha arudi tena lazima alikuwa hana moyo wala masikio.Basi mwanangu mwanzo nilijua ni hadithi lakini sasa ndio nimeelewa kuwa hadithi ilikuwa na maana kubwa tena ilikuwa inanilenga mimi waziwazi"
"Inakurenga kivipi?"
"Mwanzo walinitenda kuwa sizai na kuamua kuondoka,baadae walikuja kuniomba msamaha na kurudi kama Punda wa Dobi aliyejeruhiwa na Simba.Kwa vile nilikuwa sina moyo wala masikio nilirudi kwa mume wangu..
Lakini yaliyonikuta siwezi kuyasahau mpaka naingia kaburini,leo hii waje tena kuniomba msamaha nikubali kama sio kufuata kifo kama cha Punda wa Dobi ni nini?...
Basi baada ya kukaa kwa wiki toka nipate habari zilizo ushtua moyo wangu za mume wangu kuuziwa mbuzi kwenye gunia.Nilipata ujumbe kutoka kwa dada kuwa ninatakiwa nikitoka kwenye shughuli zangu nipitie kwake.Nilitii amri baada ya shughuli zangu nilipitia kwa dada na kumkuta.
Dada aliniambnia ana mazungumzo na mimi,nilimkubalia na kusubili nilichoitiwa.Muda niliofika yalikuwa majira ya saa kumi na moja za jioni.Basi katika majira ya saa kumi na mbili kasoro niliitwa na dada sebuleni.Nilipofika nilishtuka japo si sana kumkuta baba mkwe baba ya mume wangu.
Nilijua ni yale yale niliyokuwa nayawaza baada ya kuzipata zile habari za kuumbuliwa mchana kweupe mume wangu.Nilipofika mbele ya baba mkwe nilisabahi na kukaa pembeni yake lakini kochi la pili.
"Karibu baba"
"Asante mwanangu,kwanza pole kwa yote"
"Nimepoa baba"
"Mbona mama yalitokea mambo kinyume siku ile hukuja kunieleza?"
"Baba nina imani kwa kauli kali uliyoitoa siku ile na mume wangu kuidharau.Sikuwa na haja ya kurudi"
"Kwa nini mama?"
"Baba mume wangu nilikuwa nampenda sana tena mapenzi ya dhati nikuwa tayari kumsahe kwa makosa yake.Mwanzoni nilimsamehe tena bila mashrti japo alilonitendea lilikuwa zito..
Nilirudi kwake na kuonyesha mapenzi mazito na kuyasahau yote ikiwepo na kuwasamehe wifi zangu na mama mkwe kwa kuwaonyesha mapenzi bila kuwabaguwa wala kuwawekea kinyongo.Kumbe ilikuwa wazi mimi sitakiwi.Wakatafuta ya kutafuta na kufanikiwa kunitoa ndani"
"Hapana mwanangu bado hujatolewa ndani"
"Kwa wewe mzazi wangu utasema hivyo hebu fikila toka siku ile ulipomuamuru mume wangu amtoe nda yule mwanamke wake mpaka leo hii sijamtia machoni kweli mimi ni mke wake wa ndoa au anakuheshimu wewe mzazi wake...
Baba mama mkwe wifi zangu na mume wangu hawanipendi hivyo siwezi kuishi kwa shinikizo lako.Je ukifa nani atakuwa mtetezi wangu.Baba akumulikae mchana usiku atakuchoma"
"Nimkweli mwanangu lakini umeo funzo amelipata sidhani atarudia upuuzi wake"
"Baba siwezi kuwa Punda wa Dobi kamwe"
"Mwanangu ile ni hadithi"
"Lakini iliyotolewa makususi kwetu wanadamu,wamenikosa mara mbili ya tatu ni mauti yangu siwezi kuyakimbilia mauti nayaona mbele ya macho yangu"
"Hapana mwanangu huu mguu ni wa mumeo anaomba umsamehe na kuyasahau yote ili muwalee wenenu"
"Baba nakuapia maisha ya ndoa mimi tena basi,kurudi kwa mume wangu au kwenye familia yako siwezi labda maiti yangu lakini nikiwa mzima navuta pumzi katu abadani"
"Hapana mama mrudie bwana Mungu wako msamehe mumeo amefanya makosa kama mwanadamu"

Itaendelea.
 
SEHEMU: 07
ILIPOISHIA:
"Lakini iliyotolewa makususi kwetu wanadamu,wamenikosa mara mbili ya tatu ni mauti yangu siwezi kuyakimbilia mauti nayaona mbele ya macho yangu"
"Hapana mwanangu huu mguu ni wa mumeo anaomba umsamehe na kuyasahau yote ili muwalee wenenu"
"Baba nakuapia maisha ya ndoa mimi tena basi,kurudi kwa mume wangu au kwenye familia yako siwezi labda maiti yangu lakini nikiwa mzima navuta pumzi katu abadani"
"Hapana mama mrudie bwana Mungu wako msamehe mumeo amefanya makosa kama mwanadamu"
SASA ENDELEA…

"Ni kweli,lakini sitarudi kwa mume wangu siwezi kuwa Punda wa Dobi mwambie amfaute mwanamke mwingine amuoe.Mwisho sipendi kuongea sana kwa vile nakuheshimu mzazi wangu naomba tuishie hapa naogopa kuropoka maneno mazito ambayo lazima yatakuvunjia heshima...
Sitaki mzazi wangu katika watu duniani nawaheshimu na sitawasahau na kukuona ni kiumbe wa pekee uliyejaliwa na Mungu,lakini umekosa familia baora yenye muongozo thabiti.Nisamehe kwa hilo mzazi wangu kamwambie katu abadani sitarudi kwake"
Maneno yangu yalimfunga mdomo baba mkwe alinyanyuka na kuondoka.Baada ya kuondoka dada alikuja kuniuliza nimefikia wapi,nilimueleza yote bila kuacha hata moja baada ya kunisikiliza aliniuliza
"Kwa hiyo mdogo wangu umeamua"
"Si mimi ila wao na kamwe siwezi kuwa Punda wa Dobi"
"Mmmh kwa hilo siwezi kukuingilia maamuzi yake usije sema bila wewe yasingenikuta"
Nilirudi nyumba nikiwa na hasira hata kuwa karibu na wanangu sikutaka japo sio kawaida yangu kulala bila kuonana na wanangu hata kama nimechoka vipi.Nilimuagiza mutumishi wangu wa ndani aniletee vidonge vya maumivu.Badala ya kimoja nilimeza vitatu na kujilaza hadi asubuhi.
Siku ya pili nikiwa ofisini alikuja mume wangu dukani mwangu na kuniomba tuongee.Sikutaka kumkatalia kwa sababu ni mazazi mwenzangu,vile vile sina kinyongo nae.Tulikwenda kwenye kibanda kinachouza vinywaji baridi na kutafuta meza ya pembeni iliyokuwa tupu na wakati ule watu hawakuwa wengi.
Baada ya kukaa niliyaanzisha maongezi kwa kujua mwanzo kwa mume wangu utakuwa mgumu.
"Ndio mume wangu za siku?"
"Nzuri hongera kwa hatua uliyofikia"
"Asante nashukuru"
"Vipi watoto hawajambo?"
"Buheri wa afya"
"Mke wangu najua nimekukosea mengi"
"Ni kweli"nilimjibu
"Mke wangu nakili makosa yangu mbele yako na kukubali adhabnu yoyote kwako ili mradi tu urudi kwako"
"Mume wangu najua ndoa yetu imefungwa mbinguni hakuna mwanadamu atakaye weza kuivunja..uongo kweli?"
"Ni kweli kabisa"alijibu mume wangu
"Lakini siku zote usipende pasipo penzi na usilazimishe mapenzi.Ni kweli kufanya kosa ni kosa na kurudia kosa ni kudhamilia.Na siku zote hitimisho la karibu ni tatu baada ya moja, mbili mwisho ni tatu"
"Una maana gani?"
"Kama leo nitakusamehe na kurudi kwako lazima tatu itakuwa mbaya zaidi ya yote"
"Una maana gani kusema hivyo?"
"Ya kwanza ulinitendea nikavumila na kukubali kurudi kwako ya pili ikawa mbaya zaidi ambayo nilikuwa sawa na kinyesi nisiye hitajika moyoni mwako wala usoni si mimi hata damu yako ambayo ameinyanya paa kwa kuwaona ni machangudoa na mabaa medi..
Leo hii unataka nirudi kwako ili unimalize kabisa mume wangu hata mimi amani ya moyo naitaka vile vile bado natamani kuishi japo sijui siku yangu lini kwa vile sijui siku yangu ya kufa bado nina hamu ya kuendelea kuishi"
"Mke wangu siwezi kukufanyia unayofikilia nimejifunza kutokana na makosa.Nitakuwa mume mwema na mwenye mapenzi kwako na kwa familia yangu"
"Yaani mume wangu una bahati yote ni kutokana na kuwa mzazi mwenzangu lakini bila hivyo kila nikikumbuka roho inaniuma kama moyo upasuke na maumivu yake ni makubwa.Yaani wewe ni mnafiki mkubwa leo hii ndio umeniona mzuri mzazi mwenzi kwa sababu umeumbuka..eeeeh
Basi kwa taarifa yako mimi kurudi kwako sahau kabisa moyoni kwako kwanza hunipendi nirudi kufanya nini si wewe familia nzima mnataka kuniambia baada ya kuumbuliwa ndoa mapenzi yenu yamekuja kwangu...
Nakuomba kuanzia leo unione kama mbingu na ardhi ila tutashilikiana kwa jambo lolote si mapenzi na ukinikuta na bwana muheshimu kama mume mwenzio"
"Mama jacky"
"Ndio mimi baba Jacky"
"Sikubali lazima utarudi kwa nguvu kwa hiyali"
"Jaribu uone"
Mume wangu aliondoka akiwa amefura,sikumuonea huruma kwa kuwa nilijua alitaka kunigeuza kuchaka cha kumalizia haja zake pale anaposhikika.Kuanzia hapo sikusikiliza la mtu,pamoja na kuwatuma hata wazee wa kanisa.
Niliwajibu kama mazazi wake alishindwa hakuna wa kusikiliza na kumalizia hadithi ya Punda wa Dobi ambnayo uliwaacha mdomo wazi na kukosa lakuongezea na kuniacha na maamuzi yangu.Basi mwanangu tokea siku ile maisha ya ndoa nayachukia walio ndani ya ndoa huwapo pole na wengine huwapa hongera kama ndoa ya dada na mume wake"
Baada ya maelezo yale ma mdogo alimalizia kumeleza Sundi
"Mwanangu Sundi ndoa ina mambo mengi ndoa ni bahati nasibu ule au uliwe ndoa ni vita ndoa ni mateso ndoa ni pepo ya duniani na ndoa vile vile ni jahanamu ya duniani..
Sio wote wamekosewa na waume zao tena imekuwa vizuri nikueleze makosa mengine huyafanya wanawake.Sipendi mwanangu umtende hivi mumeo pale anapokuwa ameonyesha mapenzi mazito kwako na kumnyanyasa kisa we mzuri na unatambua mumeo anakupenda
"Mmhu mama tena naomba unisimulie na kisa hicho maana kabla ya ndoa yangu nataka niwe nimejifunza mengi juu ya ndoa"
"Hiki kisa alinisimulia shoga yangu mwenyewe mwenyewe ambaye aliangaika kurudi kwa mumewe baada ya kufanya makosa ya kijinga pake alipojisahau eti kwa sababu anapendwa..
Na kurudi kwa mumewe jasho limemtoka tena kwa nguvu za kiza kwa kutumia njia za miti shamba.Japo karudi kwa mumewe lakini yale mapenzi ya mwanzo aliyokuwa akipewa na mume wake hayapo tena...
Alianza kunisimulia kama ifuatavyo naomba uwe makini maana nalo hili somo usije fanya makosa kwenye ndoa yako.Alianza kwa kusema kuwa.Akiwa na umri wa miaka kumi na nane alibahatika kuolewa na mwanaume ambaye alimpenda sana.
Kutokana na mapenzi mazito ya mume wake na ucheshi aliomuonyesha.Ilimfanya amzoee mume wake upesi na kumfanya ayainjoi maisha.Kwa muda mfupi aliweza kuyafurahia maisha ya ndoa..
Mumewe alikuwa ndiye mwalimu wake mkubwa wa kufunza maisha kwa vile alikuwa mtoto mdogo.Cha kwanza alimuonya kuwa karibu na mashoga wa mjini.Kwa kuwa wao wako mbele kuvuruga ndoa za watu zilizo tulia.
Basi kwa kweli maisha yalikwa mazuri mtoto wa kike alinenepa na kupendeza machoni mwa watu.Mume wake naye alikuwa mwepesi katika miezi miwili ya ndoa tu alishika ujauzito.Hapo mapenzi ya mume wake yaliongezeka.
Nilisahau kidodo mwanzo wa ndoa yao mume wake alimpeleka kwenye starehe za kila aina na kumbi mbali mbali za burudani pamoja na fukwe kwenda kupunda upepo.Basi baada ya muda alijifungua salama salimini mtoto wa kike.
Basi mume wake alifurahi sana na kipindi kile hakuwa na mazoea ya kukaa kwenye vikao vya kimbea.Basi kama ujuavyo wanaadamu wana hila walimtafuta taratibu kwa kutafuta urafiki wa lazima na yeye bila kujijua alijiunga nao.
Akiwa kwenye vikao vya umbea alisikia vitu vingi ambavyo hakuwahi kuvisikia na kujilaumu kwa kuchelewa kuyajua mambo ya kidunia.Basi alikuwa mjumbe mwisho wake akawa mwenyekiti wa kikao yaani kikao kile kilihamishiwa kwake.
Mumewe hali ile alimwambia kwa hatua kama ile si muda mrefu ndoa ataiona chungu au kuivunja ndoa kabisa.Lakini alimuhakikishia hakuna yale yanayoweza kuivunja ndoa zaidi ya kuelimishana maisha.
Sikumoja akiwa kwenye kikoa ma maongezi yamepamba moto mumewe alirudi na kuingia ndani.Aliona kazi kubwa kunyanyuka kwenda kutayalishia chakula mumuwe.Mumewe alisubili robo saa bila kumuona mkewe ilibidi amwite kwa sauti ya juu
"Mama Abdu..mama Abdu"
"Abeee"aliitikia huku akiwa amebinua mdomo,kitu ambacho shoga zake walikiona na kuhoji
"Kwani anakuitia nini anatuharibia maongezi yetu"
"Hata sijui"
"Mweleze akupe nafasi"
Basi alikwenda ndani amevimba kama unga wa ngano ulioumuliwa kwa hamira.Na alipofika kwa mume wake alisahau kama mume wake anatakiwa kutengewa chakula ale.Ajabu alipofika alimsimamia mbele yake na kumumuliza mumewe
"Unasemaje?"
"Leo sili?"
Kauli ile ilimuudhi na kutamani kumwambia mumewe aingie jikoni mwenyewe.Lakini alishindwa kufanya vile na wakati huo hakukuwepo na mahot port ya kuhifadhia chakula.Ilibidi awashe jiko la mchina na kumtengea chakula mumewe.
Na siku zote ilikuwa lazima wale pamoja yaani umsubili mumewe hadi arudi ndipo wale pamoja.Siku hiyo alitenga kisufulia kidogo ambacho hakikuchelewa kuchemka.
Alisonga ugari haraka haraka akiwa katikati ya maongezi alisikia kicheko nje cha umbea nusra auache ugari nikoni na kukimbilia umbea.Baada ya kumaliza kusonga ugali alikuwa amevimba nusra ya kupasuka.Alimtengea mumewe chakula haraka haraka na kutoka hata bila ya kumtengea maji ya kunywa wala kunawa.
Alipotenga mezani aligeuka na kuondoka kuwahi umbea,lakini alipofika mlangoni aliitwa na mumewe
"Mama Abdu"
"Nini?" alisahau hata kuitikia abeee mume wangu,alirudi akiwa amefura mara mbili na kumuuliza
"Unasemaje?"
"Mezani mbona hujamaliza"
"Kumaliza nini?"
"Mbona hakuna maji ya kunywa wala kunawa?"
"yaani hata maji nikisahamu huwezi kutenga"
"Naweza lakini bado hajafika mbali"
Aliyatenga maji akiwa amefura na alipomaliza kuyatenga hata bila ya kumwambia mume wangu karibu chakula alitoka.Mumewe lile aliliona hakutaka kupigizana naye kelele.Alikaa mezani na kula chakula cha mchana.
Alipofika kwa shoga zake alipokelewa na maneno ya kimbea
"Shoga umepitwa na mengi"
"Jamani si mnajua kuolewa"
"Kuolewa nini hata mende anamume"
"Alafu mumeo unamdekeza yaani hata kupika hawezi mbona wakwetu wanapika hata kutufulia nguo"
"Mmmmh nyinyi mna bahati"
Kama kawaida siku ya pili kikao kiliendelea kama kawaida na mama Abdu aliendelea kuwa mwenyekiti wa kikao.Kama kawaida wakiwa katikati ya kikao chao cha umbea mumewe mama Abdu alirejea toka kwenye mihangaiko yake.
Kama kawaida hakunyanyuka mpaka mumewe alipotoka nje baada ya kukaa ndani zaidi ya saa moja bila kumuona mumewe.Akiwa anaendelea na maongeze baada ya kupita zaidi ya nusu saa baada mumewe kuingia ndani mmoja wa shoga zake alimuuliza.
"Shoga leo mumeo hali?"
"Mikono anayo akisikia njaa atapika"
"Na kweli usimdekeze"mwingine aliongezea
Ndio baada ya saa moja mumewe alipotoka na kusimama mlango lakini alijifanya hamuoni na kuendelea na maongezi mpaka mmoja wa shoga zake aliposema
"Shoga moonee huruma kasimama kama yupo kwenye lindo"
Ndipo mama Abdu aliponyanyuka na kwenda kwa mumewe,alipofika alisimama mbele yake bila ya kusema neno wala kumsalimia.Mumewe alimuangalia juu mpaka chini kisha alitikisa kichwa na kusema
"Tusilaumiane"
"Kwa lipi"
Hakujibu neno aliondoka na kumwacha mkewe amesimama kama sanamu,baada ya kuondaka alirudi kwenye kikao chake.Amesemaje mbona mmetazamana kama mabubu.
"Eti ananitishia maisha"
"Kukutishia maisha!kivipi?"
"Eti amesema tusilaumiane"
"Msilaumiane kwa sababu gani?"
"Nilimuuliza kwa lipi?"
"Hakunijibu zaidi ya kunitizama kuanzia kuanzia juu hadi chini na kutikisa kicha na kuondoka"
"Mmmh makubwa"
"Kwani vipi?" mama Abdu alishtuka
"Jaribu kumuheshimu kidogo mumeo japo mkimya anaweza kuchukua uamuzi mbaya"
"Mbaya wa vipi?"
"Usije achika bure"
"Mmh asimtishe yaani na uzuri alionao akiachika hachukui hata wiki anaolewa"
Jioni ilipotimu kila mmoja alilia shida zake
"Mama Abdu kwa mambo sio mazuri naomba angalau nusu mchele"
"Mimi sukari japo robo ili wanangu kesho wapate ya chai kabla ya kwenda shule"
"Mmh na mimi mia tano nikanunue fungu la samaki"
Kila mmoja alimpa mahitaji yake na kuondoka na kumwacha peke yake.Mama Abdu alimuogesha mwanae na kuandaa chakula cha usiku kisha alipanda kitandani.
Mumewe aliporudi alimuamsha na kumuweka kitako na kumueleza
"Mke wangu unapokenda sipo nilikueleza mapema jiepushe na makundi hayo ya kimbea unaona sasa toka ujiunge umebadilika"
"Nimebadilika nimeota mkia au mapembe"
"Mke wangu rudia tabia yako hapo mwanzo haukuwa hivyo"
"Bwana eeh kama umeona tabia yangu mbaya mwite fundi selemala"
"Tusije laumiana"
"Bwana eeeh usinitishe nimechoka na vitisho vyako"
"Sawa"
Maelewano ndani ya ndoa yaliingia migogolo kila kukicha,watu wa pembeni walimjaza umbea na kumuona mumewe si mali kitu.Aliwaona mashoga zake ni wa maana kuliko mumewe.Siku moja kama kawaida mumewe aliporudi na kumkuta yupo katikati ya maongezi.
Alipita na kuingia ndani kama kawaida yake hakunyanyuka mpaka shoga zake waliposema
"Vibaya hivyo mama Abdu kasikilize mumeo"ndipo aliponyanyuka na kwenda ndani.
Alimkuta mumewe anasoma gazeti na kwenda moja kwa moja kumsimamia mbele bila kusema neno.Mumewe akusema kitu zaidi ya kuendelea kusoma gazeti ndipo mama Abdu kwa ukali alipo sema
"Umeniita kunifanya kama fenicha au nini?"
"Hivi mama Abdu mke wangu hata salamu siku hizi imekuwa shida,yaani hao mashoga zako ndivyo wanavyo ishi na waume zao?"
"Hiyo haikuhusu,sema ulichoniitia"

Itaendelea
 
SEHEMU: 08
ILIPOISHIA:

ILIPOISHIA:
"Ndivyo somo yako alivyo kufunda kuondoka bila ruksa ya mumeo?"
"Sasa baba Fatu yaani mwanao auawe anaangalia kisa kaolewa?" mama aliingilia kati.
"Kama kukimbia ungekimbia wewe nikukuvunja mkono mbona hukuondoka?"
"Kila mtu na mwili wake."
"Naomba kwanza mazungumzo na mwanao unyamaze kimya kama yalikushinda niachie mimi," mama Fatuma bibi Abdu alinyamaza kimya kwa kumjua vizuri mumewe kulianzisha hata mbele ya watoto humlamba mikwaju.
SASA ENDELEA…

"Najua siku zote watoto wa kike huwa waongo, sasa rudi kwa mumeo nitakuja jioni kusikiliza. Siamini mumeo kufanya yote uliyosema,” maneno yale yalimfanya akose raha na kujua kama baba yake atasikia tabia zake chafu basi lazima atamtolea radhi.
Mumewe aliporudi na kumkosa mkewe, hali ya ndani ilimuonyesha hakukuwepo na hali ya usafi ilionyesha wazi mkewe aliondoka asubuhi. Baada ya kuikuta nyumba kama alivyo ondoka asubuhi. Aliamua kumfuata mkewe kwao na alipofika mkewe alikuwa ndoa anapanga nguo. Aliposikia sauti ya mumewe akikaribishwa na baba yake nusra haja ndogo imtoke. Alisikia baba yake akimkaribisha:
"Ooho mzee, karibu sana tena umenipunguzia safari ya kuja huko."
“Asante baba,”
Baadaye mama Abdu aliitwa ili liongelewe lile jambo mbele ya wazazi wao ili tatizo lijulikane linatokana na nini. Walikusanyika wote mama Abdu akiwa pembeni ya mama yake kwa kuogopa kupokea kipigo toka kwa baba yake pale itakapobainika yeye ndiye chanzo cha matatizo.
Baada ya kukaa mzee Hasani Chuna babaye Fatuma.
"Ndiyo baba nimerudi na kumkuta mkeo na kushangaa kumkuta kwenye hali hii kibaya zaidi amerudi kwangu bila idhini yako. Ni mengi ameonge lakini raha ya jambo liongelewe kwa watu wote kuwepo. Kabla ya yote mama Abdul naomba uhadithie yote kama ulivyo tuambia ili mumeo aseme kweli ama si kweli," baba alisema kwa upole.
Hapo ikawa kazi kwa mama Abdu kusema uongo mbele ya mumewe, mdomo ukawa mzito kusema alibakia ameng’aa macho kama kibaka aliyekutana na polisi.
"Mama ongea nina kusikiliza mbona umegeuka bubu ghafla na muda mfupi ulikuwa unaongea."
"Lakini baba Fatu aongee nini wakati amekwisha kueleza."
"Mama Fatu unanitafuta nini au wewe ndiye uliyemtuma mwanao akose adabu kwenye nyumba yake," lilikuwa dongo ambalo liliambatana na ukweli lililomfunga mdomo na kumwacha mama Abdu ajitetee mwenyewe.
Ilikuwa kazi nzito kama kumeza kaa la moto, lakini mzee Hasani Chuna alitumia busara zake kumaliza ugomvi ile na mama Abdu alirudi na mumewe. Mama Abdu aliishi kwa kumuogopa baba yake kama vile mume wangu na familia yake.
“Hapo ndio ujue matatizo ya kindoa yanafanana japo si kwa asilimia mia, lakini kuna baadhi ya mambo yanafanana, Basi amani ilirudi kwenye ndoa ya mama Abdu na mumewe, pamoja na kuiheshimu ndoa yake lakini hakuacha kuonana mara moja na shoga zake ambao walimjaza maneno. Ikiwa pamoja na kumwambia atafute bwana wa nje kwa kuwa bwana yake ana kisichana kimoja.
Aliwasikiliza lakini aliogopa kwa kujua akirudi kwa baba yake lazima mume wake atasema ukweli hapo ndio utakuwa mwanzo wa kutolewa radhi na baba yake.Aliyasikiliza na kuyaweka kiporo. Kama ujuavyo kila kiumbe kilichoumbwa kinachopumua kitakufa, basi kwa mapenzi ya Mungu baba yake mama Abdu mzee Hasani Chuna alifariki baada ya kuugua ghafla.
Mama Abdul alipata pigo maishani kwa kumtegemea baba yake kama muongozi wa maisha yake japo kuna mambo alikuwa anamkosesha raha kama maamuzi yake mwenyewe. Lakini hakuwa na
jinsi kwa kuwa alimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi.
Baada ya msiba kwisha mama Abdu alirudi kwake na kuyaanza maisha bila kuwa na ngome kuu yaani baba yake mzazi. Alikaa kwa muda wa miezi miwili na kujikuta anarudi kwenye kikao chake cha umbea.
Siku moja akiwa kwenye kikao chake ambacho alikirudisha nyumbani kama mwanzo mumewe aliporudi alikwenda kumtayalishia chakula kama kawaida kama kawaida ikiwa pamoja na kumkaribisha mumewe alitoka kwenda kwenye kikao chake. Mumewe baada ya kula alinawa kwa vile alikuwa na haraka alitoka hadi mlangoni na kumwita mkewe ambaye hakuonyesha hali yoyote ya kuchukia. Kitu kilichomfanya mume wake asiwe na wasi wasi tena na vikao vile.
"Unasemaje mume wangu?"
"Natoka kidogo ila leo nitachelewa kurudi chakula usiniwekee."
"Sawa mume wangu, utachelewa sana?"
"Tuna kikao inategemea naweza hata kuwahi ila ni dharula nikichelewa usije sema sijakwambia."
"Hakuna tatizo mume wangu kazi njema."
"Asante na wewe ubakie salama."
Waliagana na kurudi kwenye kikao cha umbea alipofika walimuuliza juu juu na kutaka kujua kaitiwa nini.
"Aah! Amesema atachelewa kurudi hata chakula nisimuwekee."
"Mmh,"mmoja wa shoga zake aliguna.
"Mbona umeguna?"aliuliza mama Abdul
"Nisijesema nikaonekana mmbea."
"We niambie kuna umuhimu gani kuwa watu wangu wa karibu na ukweli msiniambie?"
"Unajua hatupendi kuingilia mapenzi yenu."
"Mbona mnaniacha njia panda kuna umuhimu gani kuniambia."
"Unajua mumeo japo mkimya lakini mwingi wa mambo, sisi tunajua lakini tumekuwa kimya."
"Jamani mnajua nini juu ya mume wangu?"
"Ana kitoto kigori tena nasikia ana mpago wa kukioa na wewe kukumwaga, kwa nini achelewe kurudi. Hata kama ingekuwa kweli shughuli kwa nini asile chakula cha usiku na wewe, lazima atakuwa amekula nyumba ndogo kazi kwako," mmoja wa shoga zake alichomekea.
"Tena namshangaa kuna watu wanammezea mate utautumia ujana wako kaburini, shauri zako sema sasa hivi tule pesa."
Kauli ile ilimfanya mama Abdu akose raha na kuondoka kikaoni na kwenda ndani na kujifungia na kuanza kulia. Hakuamini jinsi anavyo mpenda mumewe na kuwa muaminifu wa ndoa yake kumbe mumewe anamzunguka.
Siku ile alilia sana ndani na kumuona kumbe mume wake ni chui aliyejivisha ngozi ya kondoo. Siku ile hata hamu ya kula hakuwa nayo hata kuoga hakuwa na haja ya kuoga alipanda kitandani na kukumbatia mto huku akilia.
Mumewe alirudi majira ya saa nne kasoro alishangaa kumuona mkewe mashavu yana michirizi ya machozi na kutaka kujua kulikoni, lakini mkewe alianza kulia safari ile kwa sauti ya juu kidogo kitu kilichomshtua mumewe.
"Mke wangu umekumbwa na nini?"
"Naumwa tumbo, alisingizia uongo.
"Twende hospitali."
"Hapana litatulia."
"We si Mungu jiandae twende hospitali."
"Hospitali siendi naumwa mimi sio wewe usinilazimishe."
"Mke wangu mbona majibu yako kama yamejaa shari?" mumewe alishtuka.
"Unafikiri unayofanya sijui."
"Nini tena mke wangu?"
"Kama unipendi si bora unipe talaka."
"Kwa lipi kubwa nililokufanyia?"
"Kumbe una mwanamke nje ndio maana umechelewa kurudi na umekataa kula kwa kuwa umekula kwa huyo mwanamke."
"Hiyo imeanza lini yaani leo ndio niende kwa huyo mwanamke na kula kwake, mke wangu jiepushe na maneno ya pembeni wameona tumetulia wanachokonoa tena."
"Sasa leo ulichelewa wapi?"
"Tena mke wangu kikao chetu kimechukuliwa na vyombo vya habari vya televisheni kesho angalia kwenye mkutano wetu."
"Mmh, haya."
"Usijibu kwa shingo upande, ukweli ndio huo."
Mama Abdul alirudi matawi ya chini na kwenda kuoga na mumewe na kupata chakula cha usiku pamoja na kupanda kitandani kulala.
Mashoga zake hawakuchoka kumchokonoa bila kujijua huku wakimkuwadia wanaume wa nje. Na yeye bila kujielewa alijikuta akiisaliti ndoa yake alipotoka nje ya ndoa. Kwa kuwa alikuwa hajaonja penzi la nje pale alipokutana na mwanaume aliyemaliza ujuzi wote kwenye mwili wake.
Alijikuta akichanganyika na kumuona mumewe si mali kitu mwanaume asiyejua mapenzi. Aliyaona mapenzi matamu kuliko kitu chochote dunia na kutaka kila siku akutane kimwili na bwana wa pembeni.

Itaendelea
 
SEHEMU: 09

ILIPOISHIA:
"Sasa leo ulichelewa wapi?"
"Tena mke wangu kikao chetu kimechukuliwa na vyombo vya habari vya televisheni kesho angalia kwenye mkutano wetu."
"Mmh, haya."
"Usijibu kwa shingo upande, ukweli ndio huo."
Mama Abdul alirudi matawi ya chini na kwenda kuoga na mumewe na kupata chakula cha usiku pamoja na kupanda kitandani kulala.
Mashoga zake hawakuchoka kumchokonoa bila kujijua huku wakimkuwadia wanaume wa nje. Na yeye bila kujielewa alijikuta akiisaliti ndoa yake alipotoka nje ya ndoa. Kwa kuwa alikuwa hajaonja penzi la nje pale alipokutana na mwanaume aliyemaliza ujuzi wote kwenye mwili wake.
Alijikuta akichanganyika na kumuona mumewe si mali kitu mwanaume asiyejua mapenzi. Aliyaona mapenzi matamu kuliko kitu chochote dunia na kutaka kila siku akutane kimwili na bwana wa pembeni.
SASA ENDELEA…

Taratibu akaanza kumdharau mumewe hata kutojisikia kufanya naye mapenzi. Hali ya nyumba ilikosa usafi kitu kilichomfanya mumewe aingie kazi ya kufanya usafi. Alimuonya mkewe kwa mabadiliko yale yana mwisho mbaya.
Lakini yaliingilia sikio la mkono wa kulia na kutokea mkono wa kushoto. Alijiingiza katika unywaji wa pombe kitu ambacho kilimkela mumewe. Hali ile ilimfanya mumewe apeleke malalamiko kwa mama mkwe. Lakini jibu lilikuwa mtajuana wenyewe kwa kuwa Fatuma ni mtu mzima.
Siku moja mama Abdu alirudi amelewa na kutapika ndani, mumewe alipo jaribu kumpiga hakukubali alimshika sehemu za siri kama sio majirani kuwahi kuamua angemuua mumewe. Tokea siku ile alifanya mambo kama amejioa.
Ilikuwa kila siku anatoka usiku wa manane na kurudi alfajiri japo mumewe alimuonya, siku moja alimweleza ukweli.
"Mke wangu usifikiri hiyo tabia uliyo ianza itakupeleka pema ina mwisho mbaya, kwa nini hujionei huruma. Hivi huoni maisha ya mama yako nikikuacha utaadhirika jirekebishe bado una nafasi moyoni mwangu."
"Bwana eeh katika wanaume na wewe mwanaume hebu niache uone nitavyo papatikiwa na wanaume kama pande la nyama kwenye mamba wenye njaa kali."
"Haya narudia tena tusije laumiana."
Upole wa mume wake aliutumia vibaya na kumfanya bushoke kunywa pombe aliona haitoshi akaanza kuingiza wanaume ndani. Hapo ndipo mume wake alipoona too much, hukuwepo Malaika wako alikuwepo.
Siku hiyo aliwafumania chumba chake cha kulala mkewe akiwa na mwaname. Waswahili walisema kimya kingi kina mshindo mkuu. Bwana yule alimkamata mgoni wake na kumpa kipigo kizito kilichomfanya apoteze fahamu akiwa amevunjika mbavu mbili na kuvunjika taya.
Wakati mumewe akimshikisha adabu mgoni wake mkewe alimsaidia yule mgoni na kumtia meno ya mgongo mumewe. Baada ya kushikisha adabu mgoni alimgeukia mkewe na yeye kwa kutaka kupima maji alimvaa ili amshike sehemu za siri kwa kujua kila siku ni jumapili.
Aliambulia kifuti cha mdomoni kilichomfanya apoteze meno ya mbele matatu, hakukubali alijinyanyua ili ajaribu bahati yake nyingine. Mumewe akiwa na ghadhabu alimsahau kama mkewe na kushushia kipigo kizito kwa kusanya makosa yote ya nyuma.
Mama Abdu alikimbizwa hospitali akiwa hajiwezi akiumwa kila kona ya mwili. Baada ya vipimo alionekana ameumia sehemu za mbavu na taya lake lilikuwa limeyumba na kufungwa waya.Mgoni wake ilibidi awekewe chuma kwenye mbavu.
“Mwanangu lazima uelewe cha mtu mavi na uchungu wa mke aujuae mume na uchungu wa mume aujuae mke.Sio umejiona unapendeza unachukua wanaume za watu yatakukuta yaliyomkuta mama Abdu na hawala yake.
Basi mama Abdu amekaa hospital zaidi ya miezi mitatu bila kumuona mumewe wala shoga zake. Mama yake ndiye aliyekuwa akihangaika hospitali peke yake. Siku moja baada ya miezi miwili na nusu, alishangaa kumuona mumewe hospitali.
Alidhania labda huruma imemuingia kumbe baada ya kidonda alimuongezea msumali wa moto pale alipompelekea talaka palepale kitandani. Fatuma mama Abdu alilia na kumuomba msamaha mumewe ambaye baada ya kumpa talaka aliondoka bila kusema kitu."
Maneno yale yaliufanya mwili wa Sundi usisike na kumuonea huruma mama Abdu.
"Jamani mama baada ya kumpa kipigo kizito na talaka juu!"
"Siku zote mwanangu kilanga haliliwi wala hawekewi matanga."
"Mhu, ikawaje?"
"Basi baada ya miezi mitatu ndipo alipotoka hospital akiwa na sura kama ukuta uliokosa lipu. Meno ya mbele hakuwa nayo hata tembea yake ilikuwa ya upande upande kama kasa.
Baada ya kutoka hospitali alikutana na dhahama nyingine nyumbani pale mama yake alipo mfukuza na kwambie aende kwa wale waliomponza na sio kwake kwa kuwa kula yake haijui hawezi kumfuga mtu kwenye matatizo ya kujitakia.
Sio wote duniani wamchukia mwanadamu wapo wasamalia wema wasiopenda kuona wenzao wakiadhirika. Alitokoe shoga yake ambaye walisoma naye na kumpa hifadhi, baada ya wiki alimpeleka kwa mtaalamu wa miti shamba na kuhakikishiwa kurudi kwenye nyumba yake.
Aliagizwa anunue vitu vya kutengenezea kafara la kurudisha ndani, kwa vile alikuwa hana pesa aliuza vitu vyake kama nguo na mapambo yake na kuweza kufanikisha kafara. Baada ya kafara iliyofanyika saa tisa za usiku makaburini kwa kuzika vitu na vingine kupasua njia panda.
Baada ya wiki alielezwa aende kwa mumewe, ilikuwa siku ya jumapili siku ambayo alijua mumewe aendi kazini. Siku hiyo alipewa kizizi cha kutafuna na kunuiza maneno ya kumfanya mume wake apoe kama maji mtungini na kuyasahau yote waliyoyazika makaburini.
Pamoja na kuhakikishiwa lakini alijikuta akimuogopa mumewe kama Simba. Alimuomba Mungu mpango wake ufanikiwe kama mambo yatakwenda kinyume atakuwa mgeni wa nani. Kwa hali aliyokuwa nayo.
Njiani aliwaza jinsi alivyokimbiwa na ma mashoga zake hasa baada ya kumwingiza mkenge na kumkimbia hata sura zao hakuziona hospitali. Alikumbuka kauli ya mtalaka wake kuwa wale mashoga zake ni sawa na mashetani ambao hukuingiza kwenye matatizo humkimbia na kukuacha mwenyewe bila msaada.
Mama Abdu akiwa anajutia nafsi yake, moyo ulianza kumdunda na mapigo yalikwenda kwa kasi na kufanya ahisi kizunguzungu na kuamua kukaa chini kwa muda baada ya kuikaribia nyumba ya mtalaka wake.
Alimuomba Mungu ampe ujasiri ili aweze kwenda kwa mumewe na kuweza kusamehewa kwa kuwa na yeye ni kiumbe dhaifu mwenye kutenda makosa. Alijinyanyua chini alipokuwa amekaa na kwenda kwa mumewe.
Nyumba ilikuwa mlango wazi alikwenda hadi mlangoni na kusimama kabla ya kuingia alijiuliza atamwambiaje mtalaka wake akimuuliza amefuata nini? Huku akitetemeka alibisha hodi na kupokelewa na sauti ya kiume toka ndani ikisema:
"Ingia."
Aliingia ndani na kumkuta mtalaka wake akiwa amejipumzisha kwenye kochi akisoma gazeti la michezo la siku ile. Kwa woga alijikuta akikaa chini baada ya kukaribishwa, jeuri yote ilimuisha na kuyeyuka kama mbonge la mafuta juu ya kikaango cha moto.
"Aaah, mama Abdu hebu nyanyuka kaa kitini," mama Abdu alinyanyuka na kukaa kitini akiwa amejikunja kama ndege aliyemwagiwa maji.
"Jisikie huru kwa kuwa yote ulijitakia utamlaumu nani?"
"Ni kweli mume wangu...ooh samahani mtalaka wangu...kinywa cha mtu kinanuka lakini maneno hayanuki...naomba unisamehe mume wangu nipo chini ya miguu yako kiburi si maungwana leo dunia imenifunza," aliyasema yale aliwa amepiga magoti huku akilia japo masharti ya mganga alimwambia yeye akifika asiongee neno lolote mpaka mume wake atakapo msemesha.
Mumewe alimnyanyua na pale chini na kumketisha juu ya kiti na kumfuta machozi na kumweleza kwa lugha ya upole:
"Mama Abdu mke wangu haya niliyajua mapema yote ulifanya ilifikia hatua ya kunipiga kunitukana haikutosha ikafikia hatua ya kutoka nje ya ndoa yote nilivumilia, mke wangu ulivuka mipaka baada ya kuniona nimefumbia macho sio kwa sababu nilikuwa nakupenda sana au umenizidi kinguvu hata utawala wa ndani..
Haikutosha ukajigeza popo makalio yupo juu unajisaidia ili kinyesi kiruke juu ni nani aliyewahi kufanya hivyo zaidi ya kujipakaza kama ulivyofanya.Wako wapi waliokuwa wakikudanganya?"
"Hawapo."
"Nililijua mapema nilikukanya na kukuonea huruma na kujua una mwisho mbaya na ndio huu."
"Nakubali nimekosa mume wangu nisamehe na kuyasahau yote ili nirudi kwenye nyumba yangu."
"Fatuma nimekusamehe lakini sitakusahau na uelewe mapenzi yale hayapo tena utaishi kama mke wangu na si mke bwangu kipenzi."
"Usifanye hivyo mume wangu."
"Umejitakia, karibu kwa mara nyingine kuanzie tulipoishia."
Basi mwanangu huo ukawa mwanzo wa mama Abdu kurudi nyumba, sasa hivi wana mwaka wa nne toka warudiane na sasa hivi wana mtoto wa pili wa kiume. Umegundua au umejifunza nini katika matukio haya mawili ya kwangu na Fatuma mama Abdul?"

Itaendelea.
 
SEHEMU: 10

ILIPOISHIA:
"Mama Abdu mke wangu haya niliyajua mapema yote ulifanya ilifikia hatua ya kunipiga kunitukana haikutosha ikafikia hatua ya kutoka nje ya ndoa yote nilivumilia, mke wangu ulivuka mipaka baada ya kuniona nimefumbia macho sio kwa sababu nilikuwa nakupenda sana au umenizidi kinguvu hata utawala wa ndani..
Haikutosha ukajigeza popo makalio yupo juu unajisaidia ili kinyesi kiruke juu ni nani aliyewahi kufanya hivyo zaidi ya kujipakaza kama ulivyofanya.Wako wapi waliokuwa wakikudanganya?"
"Hawapo."
"Nililijua mapema nilikukanya na kukuonea huruma na kujua una mwisho mbaya na ndio huu."
"Nakubali nimekosa mume wangu nisamehe na kuyasahau yote ili nirudi kwenye nyumba yangu."
"Fatuma nimekusamehe lakini sitakusahau na uelewe mapenzi yale hayapo tena utaishi kama mke wangu na si mke bwangu kipenzi."
"Usifanye hivyo mume wangu."
"Umejitakia, karibu kwa mara nyingine kuanzie tulipoishia."
Basi mwanangu huo ukawa mwanzo wa mama Abdu kurudi nyumba, sasa hivi wana mwaka wa nne toka warudiane na sasa hivi wana mtoto wa pili wa kiume. Umegundua au umejifunza nini katika matukio haya mawili ya kwangu na Fatuma mama Abdul?"
SASA ENDELEA…

"Mmh hapo nimeona mashoga walivyo wabaya kwenye mahusiano ya watu."
"Ni tukio gani linalo fanana na langu?"
"Ni mmoja apatapo mtu wa pembeni na kudharau wa ndani."
"Na kingine?"
"Sidhani zaidi ya hivyo maana wewe hukusamehe ila mume wa mama Abdu amesamehe."
"Kuna kitu kunafana kuliko vyote bado hujakisema."
"Kipi hicho ma mdogo?"
"Kuhusu wazazi wa kike kuingilia ndoa za watoto wao na wazazi wa kiume kusimama kidete kuokoa ndoa za watoto wao."
"Mmh, kweli kabisa yaani aliyo yafanya mama yake na ba mdogo ndivyo alivyo fanya mama yake Abdu."
"Basi mwanangu umeona visa viwili vya ndoa vilivyo kwenda na kuishia, mimi nilikuwa ndani baada ya kutoka nje nilirudi tena ndani lakini nilipotoka mara ya pili sikutaka kurudi tena na nimetoka si kwa kupenda bali kulazimishwa na watu.
“Tofauti yangu na Fatuma mama Abdu yeye mwenyewe alilazimisha kutoka na alipotoka ndipo alipojua umuhimu wa ndani baada ya kuwa nje na kufanya kila njia na kurudi ndani. Kwa njia yoyote ambayo nina wasiwasi alikuwa radhi hata kupoteza roho ya mtu arudi ndani, ndio maana nikasema ndoa ni nje ndani.
Wa ndani wanataka kutoka nje wa nje kama wewe wanataka kuingia ndani, kila mmoja inategemea ataokota kalata gani galasa au turufu kama dada yeye aliokota turufu ila mimi niliokota galasa ambalo lilinitoa kapa ya mapenzi na kunifanya niyachukie na kuwaonea huruma wote walio kwenye ndoa na kuwaonea wivu wenye mapenzi kama dada na mumewe.
Wote wangeishi kama dada na mumewe hata ugonjwa wa UKIMWI kwenye ndoa usingekuwepo. Nina imani hata mume wa mama Abdu ningempata kama mimi mbona ningenenepa mpaka mnipasuke. Basi mwanangu nenda na kwa kaka yako umsikie najua na yeye anayake hasa ukimwambia unataka kuolewa.
Sundi baada ya kuongea na mama yake mdogo alimuaga na kuelekea kwa kaka yake ambaye alikuwa hakai mbali sana ni mwendo wa dakika arobaini na tano. Kwa vile alikuwa karibu na barabara alipanda gari na kwenda moja kwa moja kwa kaka yake.
Alipofika lijikuta akikosa raha baada ya kumkosa kaka yake kwa kukuta mlango umefungwa. Alipogeuka aondoke ili aelekee barabarani, mlio wa gari nyuma ulimshtua na alipogeuka alikutana na kaka yake.
"Ooh bibie yaani unakuja bila taarifa."
"Nimekuwa mwanamke wako unaogopa kufumaniwa."
"Mmh tuachane ukiongea hayo yananipa kichefuchefu."
"Tena leo naona utatapika."
"Kwa nini unasema hivyo?"
"Teremka tutaongelea hapa nje."
"Basi tangulia ndani,"Lyasi alimrushia mdogo wake ufunguo na kugeuza gani. Alimkuta ameisha ingia ndani na kumkuta akiwa ameshikilia chupa ya maji na kujimiminia kwenye bilauli na kupiga funda mbili za maji na kutulia kisha alizungumza:
"Bro ulipitia wapi au umeisha pata wifi nini?"
"Mdogo wangu yaani usikumbushe jambo hilo kwa muda huu sipendi kulisikia kwenye masikio yangu yaani kwa muda huu namchukia kila mwanamke duniani."
"Siku zote nikikuuliza utaki kuniambia nikimuuliza ma mdogo au mama wanasema nikuulize mwenye kwa kuwa kila mmoja analiongelea vizuri lililomkuta na sio kuongelewa na mtu kwa kuwa mtu mwingine huweza kuongeza chumvi au kusahau mambo mengine."
"NI kweli mdogo wangu niliongea mwanzo na sitapenda kulirudia kwa sababu unikumbusha machungu na kufanya kila nimalizapo kuhadithia huchimbua chuki upya na kuwachukia wanawake wote japo sio wote wenye tabia mbaya kama za mke wangu."
"Ni kweli kaka hata mimi sipendi uwe kwenye hali hiyo ila ni kwamba, nimekuja hapa kukueleza nimepata mchumba lakini kabla ya kuolewa kuna makosa ambayo amefanya na wifi yangu kwa bahati mbaya au makusudi hivyo basi lazima nijiepushe japo sijui nitapata mume kama ba’ mdogo au baba mzazi ili niweze kuishi na mume wangu bila karaha japo mama mdogo kaniambia ndoa ni kama jumba lenye sehemu mbili nje na ndani wa ndani wanataka kutoka na wa nje anataka kuingia.
Yaani wa ndani wanataka kutoka nje na wengine kama sisi tulio nje tunataka kuingia ndani na wapo kama wewe na ma’ mdogo waliotoka hawataki kurudi ndani na wapo kama dada Cathy ambao walitaka kutoka lakini waliomba usiku na mchana na kurudi kwenye ndoa yao.
Na mpaka leo wapo kwenye ndoa na wapo kama wazazi wetu toka waingie kwenye ndoa awafikilii kutoka na wanafanya wote tutamani kuishi kama wao. Kwa hiyo kaka yangu naomba uniambie yote usifiche hata moja."
"Kwa kweli mdogo wangu wamesema kisu kimegusa mfupa siwezi kukukatalia japo hata mama anajua nilimkatalia kurudia yaliyonikuta zaidi ya ma mdogo, Lakini najua unataka kuingia dunia mpya ambayo mimi mwanzo niliiona ni maji mafupi au walioshindwa walijidekeza na kushindwa kuhimili vishindo ambavyo vinazuilika.
Mwanzo nilijiuliza wao wameweza wana nini na mimi nishindwe nina nini siku zote nilimlaumu mama mdogo kwa uamuzi aliochukua wa kuyachukia maisha ya ndoa, lakini mimi ni tofauti kidogo. Nawachukia wanawake na kuwaona ni waongo wakubwa tena wauaji.
Basi mdogo wangu baada kuanza kazi ya kusimamia miradi ya mama kwa kweli kipindi kile sikujua nini kinaendelea kwenye ndoa yake. Ilikuwa siri yake na mama kumbe ilikuwa inawaka moto mzito ambao kweli haikufaa kusikia wakati ule.
Kwa kuwa nikuwa ndio nimemaliza masomo yangu ya kidato cha sita na matokeo yangu hayakuniwezesha kunipatia kazi au kujiunga na chuo kikuu. Nilipopewa mradi wa ma mdogo nilisimamia hasa pale aliponiambia niufanye kama ajira yangu na sio mali ya mama.
Kwa kuwa masuala ya biashara nilikuwa nayajua kwa muda mfupi niliweza kuinyanyua kazi yangu. Kwa ubunifu wangu ulisababisha duka lipanuke na kuwa kubwa. Nilishauri ma’ mdogo tufungue maduka mengine mawili madogo wadogo sehemu za karibia na watu hasa kuuza vitu muhimu kwa matumizi ya kila siku kama mchele maharage na vitu vyote muhimu.
Hakuamini jinsi lililovyopokewa hasa pale tulipopunguza bei tofauti na maduka mengine. Siku zote ukitaka faida ndogo utapata watu wengi na kufanya upate faida zaidi kwa muda mfupi. Kwa miezi sita niliweza kuyapanua yale maduka na kuuza kwa jumla na rejareja.
Ma mdogo aliniamini na kuniachia madaraka yote ikiwa pamoja na kunilipa mshahara mzuri, tena zaidi ya wale walioajiliwa na kunizidi elimu. Ma mdogo alikataa hela zangu nisizitumie zaidi ya kuziweka benki mpaka hapo nitakapoanza kujitegemea.
Kama ujuavyo kila mwanaume anahitaji mwenza hata mwanamke vilevile anapofikisha muda wa kufanya hivyo. Siku moja nikiwa katika mizunguko yangu ya kutoka duka moja kwenda jingine. Nilikutana na msichana mmoja niliyesalimiana naye kwa ucheshi, alikuwa binti mzuri sio siri mdogo wangu aliugusa moyo wangu ghafla.
Nilichana naye na kuendelea na mihangaiko yangu, ilipita kama wiki nikakutana naye tena nikiwa naingia dukani yeye anatoka. Nilisalimia na kupita ili niingie, nilishangaa kusikia nikiitwa nyuma:
"We kaka," mara ya kwanza nilisikia lakini sikujua kama naitwa mimi mpaka aliporudia mara ya pili, hapo niligeuka na kuuliza huku nikiwa nimeshikilia kifuani pangu.
"Nani! mimi?"
"Eeeh ndiyo,"nilirudi kidogo kumsikiliza.
"Unasemaje ma’ mdogo?"
"Kama sikosei hii ni mara ya pili kuonana na wewe ni wiki imepita," alisema huku ajinyonganyonga na kuniangalia usoni kwa macho yake maregevu vidole vikiwa mdomoni.
"Ni kweli."
"Nimevutiwa na wewe."
"Asante."
"Asante tu haitoshi au haukuvutiwa na mimi?"
"Naweza kuvutiwa lakini mrembo kama wewe lazima utakuwa na mtu kukupenda wewe sawa na kutafuta mateso ya kunitakia."
"Mmh, ni kweli lakini sivyo unavyofikiria..najua uko bize na maisha la muhimu naomba namba yako ya simu tutawasiliana."
Sikusita nilimpa namba yangu ya simu ambayo aliiandika kwenye simu yake iliyokuwa ya bei mbaya dukani bila laki saba huchukui. Aliiandika namba yangu kwenye simu yake kisha aliibeep ya kwangu.
Baada ya kuibeep simu yangu niliziona namba zake kisha alikata simu.
"Niandike mpenzi nani..ooh sorry kaka nani?"
"Lyasi na wewe mrembo nani?"
"Waridi."
"Nimekubari jina lako linafanana na wewe kabisa hongera wazazi wako pia aliyekuchagulia jina bila kumsahau mwenyezi Mungu kwa kukupa upendeleo," nilimmwagia sifa.
"Asante..bai tutawasiliana," baada ya kusema vile aligeuka na kuondoka na kuniacha niingie dukani kuangalia maendeleo ya biashara.
Siku ile majira usiku saa tano kama kawaida yangu nilikuwa nimeisha panda kitandani kulala. Nilishtushwa na sauti ya simu iliyokuwa ikiita pembeni ya kichwa, nilishtuka nilipoichukua wakati naangalia ni nani simu ilikatika.
Nilipoangalia nilikita missed calls zipo tatu ikionyesha nilikuwa nimepitiwa na usingizi mzito. Nilipoangalia ni nani aliyepiga nilikuta ni Waridi. Niliamua kumpigia lakini nilishangaa badala ya kupokelewa ilikatwa.
Nikiwa najiuliza kwa nini amebeep zaidi ya mara tatu kwa nini hataki kupokea mara simu iliita tena nilipoangalia nilikuta ni Waridi kabla ya kuipokea nilijiuliza mbona amekata kisha kapiga niliamu kuipokea.
"Haloo."
"Lyasi ndio nini au kukupenda nimefanya makosa?"mmh makubwa yameisha kuwa hayo, nilishtuka.
"Mbona sikuelewi?"
"Utanielewa nini wakati kuna mtu mmemkumbatia pembeni?"
"Wala sikuelewi na lawama zako siwezi kuzizuia hisia zako lakini nilikuwa kwenye usingizi mzito."
"Muongo lazima utakuwa unajitetea lazima utakuwa na mtu umpendae zaidi yangu," yule binti alizidi kumwaga lawama.
"Bahati mbaya sina mtu ninaye mpenda zaidi ya mama yangu."
"Ina maana hata mpenzio hutapenda kama mama yako."
"Ni hapo nitapompata kwa sasa mwenye nafasi hiyo ni mama yangu na nitakapo mpata na yeye atakuwa na nafasi yake pengine kumshinda mama yangu."
"Unanidanganya Lyasi kijana mzuri kama wewe ukose mwanamke."
"Labda wewe Waridi una mpenzi wako."
"Haki ya Mungu mimi sina mpenzi huwezi kuamini nitamani niwe karibu yako lakini nawaogopa wazazi."
"Ipo siku kama kweli usemayo huenda sasa hivyo mzee kapitiwa na usingizi unanikoga."
"Lyaaasi maneno gani hayo au kwa vile nimeonyesha nakupenda, ndio tabu ya wanaume ukionyesha unampenda anakuona malaya asante nashukuru," sauti ya upande wa pili ilionyesha Waridi akilia kisha alikata simu.
Yaani nilijikuta nampenda yule binti bila kujielewa na kuingiwa na huruma, nilipigia simu muda uleule simu iliita bila kupokelewa, ilionyesha jinsi gani maneno yangu yalivyo muumiza. Nikaona kuna umuhimu wa kumtumia ujumbe mfupi wa kumbembeleza na kumtaka radhi.
Baada ya kumtumia Waridi alipiga simu na kuipokea.
"Haloo."
"Mbona Lyasi unaninyanyasa hivyo au kosa langu kukupenda?"
"Waridi naomba yote yaliyopita tuyasahau siku zote mapenzi yametawaliza na maneno matamu."
"Lyasi naomba kukuuliza swali."
"Uliza."
"Una rafiki wa kike?"
"Sina."
"Upo tayari kunioa?"
"Ni mapema sana Waridi kukujibu kwa kuwa mimi na wewe hatujuani."

Nini kitaendelea?
 
SEHEMU: 11

ILIPOISHIA:
"Ipo siku kama kweli usemayo huenda sasa hivyo mzee kapitiwa na usingizi unanikoga."
"Lyaaasi maneno gani hayo au kwa vile nimeonyesha nakupenda, ndio tabu ya wanaume ukionyesha unampenda anakuona malaya asante nashukuru," sauti ya upande wa pili ilionyesha Waridi akilia kisha alikata simu.
Yaani nilijikuta nampenda yule binti bila kujielewa na kuingiwa na huruma, nilipigia simu muda uleule simu iliita bila kupokelewa, ilionyesha jinsi gani maneno yangu yalivyo muumiza. Nikaona kuna umuhimu wa kumtumia ujumbe mfupi wa kumbembeleza na kumtaka radhi.
Baada ya kumtumia Waridi alipiga simu na kuipokea.
"Haloo."
"Mbona Lyasi unaninyanyasa hivyo au kosa langu kukupenda?"
"Waridi naomba yote yaliyopita tuyasahau siku zote mapenzi yametawaliza na maneno matamu."
"Lyasi naomba kukuuliza swali."
"Uliza."
"Una rafiki wa kike?"
"Sina."
"Upo tayari kunioa?"
"Ni mapema sana Waridi kukujibu kwa kuwa mimi na wewe hatujuani."
SASA ENDELEA….

"Tujuane kivipi wakati kila mmoja wetu amekuwa muwazi kwa mwenzake au kwa upande wako unanidanganya?"
"Siwezi kukudanganya nikudanganye kwa faida ya nani kama sitaki kuna mtu wa kunilazimisha?"
"Hapana, unajua Lyasi moyo wa kupenda huwa hauna subira huona kila dakika unaweza kuporwa ukipendacho."
"Ni kweli na jambo zuri halitaki haraka kwa vile wote hatuna watu basi tupange mambo yetu kwa utaratibu na kulifanya lipendeze zaidi."
Huwezi kuamini tuliongea zaidi ya masaa matano mpaka usiku mzito, hata sijui aliweka simu yake kiasi gani cha pesa, akili yangu ilinifanya niamini kweli ananipenda. Siku ya pili hata kuamka niliamka muda umekwenda sana.
Kuanzia hapo mapenzi yangu na Waridi yalikuwa mazito, alinipenda nikajua napendwa. Nina imani hata wewe mdogo wangu ulikuwa mmoja wa watu waliomsifia Waridi na kuniona nimepata bara na pwani yaani sura umbile na tabia.
Nilijikuta naingia kichwakichwa bila kupima urefu wa maji kwa kuyaona yametulia kwa kujua maji ya mafutini kumbe wee acha. Kama kawaida nilitambulishwa kwao kwa vile kwetu tayari alikuwa anafahamika. Wazazi wake walinipokea kwa mikono miwili na kukubali nimuoe mtoto wao, kwanza nilishangaa mama yake aliponiuliza:
"Baba umempa nini mpaka Rose amekubali kuolewa?"
"Kwani vipi mama?"
"Hata katika watu waliokuwa hawataki kuolewa yeye wa kwanza nashangaa kwako kawa kama mbwa kwa chatu."
"Mama kila shetani na mbuyu wake," kumbe lile swali lilikuwa na siri nzito nyuma.
"Na kweli mwanangu."
Ndoa iliandaliwa ambayo ilikuwa kubwa baada ya ma mdogo kunifanyia kufuru. Baada ya ndoa alinikabidhi nyumba hii aliyojengewa na mumewe. Basi mdogo wangu kama waswahili wasemavyo utamu wa ngoma uingie ucheze, basi mdogo wangu nikaingia kucheza.
Mwanzo kwa kweli ulianza vizuri japo baada ya kumuo tu alitaka mfanyakazi wa ndani. Nilifanya alivyotaka na kumwekea mfanyazi wa ndani. Alimweka aliyemtafuta mwenyewe sikuwa na shaka na hilo kwa ni yeye aliyetaka mfanyakazi aweje au atoke wapi ilimuachia yeye.
Maneno ya kuwa wajapo nyumbani hawamkuti mke wangu mwanzo niliyapuuza. Lakini siku moja nilipata taarifa kuwa mke wangu ameonekana kwenye hotel majira ya mchana akipata chakula cha mchana na jamaa yake ambaye alikuwa mtu wake kabla ya kwenda South na muda ule alikuwa amerudi.
Siku zote sikupenda kusikiliza maneno ya pembeni baada ya kuhusiwa na mama kuwa nikipenda kusikiliza maneno ya pembeni naweza kuivunja nyumba yangu hata kama yana ukweli. Nilimuuliza kwa upole juu ya kutokukaa nyumbani.
"Mume wangu lini ulirudi hukunikuta?" kwa kweli nilikosa jibu kwa kuwa sijawahi kurudi nyumbani na kumkosa.
"Sikiliza mke wangu sipendi tuvunjiane heshima tulipoamua kuwa pamoja tuliamua kuachana na yote au siyo?"
"Ni kweli mume wangu."
"Basi nakuomba umefanya hujafanya naomba jambo hili lisirudiwe tena," nilitoa onyo ili kumtia woga hata kama amefanya aache.
"Mume wangu watu wameishaanza kulichokonoa penzi letu hata mwaka bado usipo kuwa makini tutaachana wakati tunapendana."
"Na mimi sipendi itokee hali hiyo."
Basi kuanzia siku ile nilikuwa narudi nyumbani ghafla na kumkuta mke wangu nyumbani. Nilijua yote yale ni ya wambea, ilifika hatua hata ya kuwachukia ndugu zangu mlipokuwa mkifika nyumbani roho iliniuma basi nilishindwa kuwafukuza.
Siku moja nilikwenda hospital nikuwa najisikia maralia nilishangaa kukutana na mke wangu akitoka kwa daktari. Aliponiona alishtuka lakini sikumuonyesha kushtuka.
"Vipi mbona upo hapa?" nilimuuliza.
"Na..sumbuliwa naa kichwa ..ooh tumbo."
"Mbona majibu mawili lipi sahihi?"
"Tumbo."
Sikutaka kumuuliza limemuanza saa ngapi kwa kuwa ni mkewangu niliamini yale si maeneo ya kumuuliza, nilimuulizia kuhusu kupata matibabu.
"Vipi umepata matibabu?"
"Ndi.i.yo."
"Utanisubiri tuondoke pamoja."
"Hapana utanikuta nyumbani na wewe mbona upo hapa?"
"Sijisikii vizuri nimekuja kuangalia damu ili nijue tatizo."
"Sawa utanikuta."
Niliachana naye na kuingia ndani nilimkuta daktari akiwa ameshika kichwa akionyesha ana kitu kichwani mwake. Nilipofika nilimsalimia kwa kuwa ni mtu wangu wa karibu hasa pale hospitali alikuwa amenisaidia mengi.
"Dokta mbona upo mbali?"
"Unajua bwana kuna watu wanapenda kila kukicha kutuingiza kwenye dhambi."
"Kwa nini daktari?"
"Kuna mwanamke mmoja kila kukicha anafikilia kuua tu."
"Kuua ! kivipi?"
"Unajua japo tunafanya makosa kutoa roho ya viumbe wasio na hatia, kuna kipindi hufanya vile kuokoa ndoa za watu pale mwanamke anapopata ujauzito nje ya ndoa. Lakini akirudia huwa hatupo radhi kufanya tendo lile haramu kwa kujua mfanyaji ni mdhamiliaji.
Hapo lazima humkatalia hata aseme atatoa milioni, basi kuna mwanamke mmoja ambaye sasa ni mara ya tatu anatoa mimba hapa, mara ya kwanza alikuja na mtu mmoja tunaheshimiana sana na kukubali kumtoa.
Mara ya pili alikuja na bwana mmoja mwarabu ambaye kwa kweli ni mtu wangu wa karibu. Nikashindwa kumkatalia nilimtoa ujauzito na kumuonya iwe mara ya mwisho na kushauri atumie kondomu zaidi ya hapo ajiandae kuzaa.
Huwezi kuamini ndani ya miezi mitano alitoa mimba mbili, kwa kweli alipumzika kidogo mara aliletwa na jamaa mmoja ambaye ni mwenye wadhifa serikalini. Kwanza nilikatalia lakini alinibembeleza kwa kuwa yule mwanamke ni mke wa mtu kwa hiyo itamchafulia sifa kwa familia yake na kwa jamii iliyomzunguruka.
Nilikuwa sina jinsi nilikubali kumtoa kwa shingo upande na kumuomba safari ijayo nitamtoa kifuko cha uzazi ili akome kabisa. Baada ya kumtoa alikaa kama mwezi mmoja na kurudi hapa kwa kweli sijui alifanya nini na kujikuta ananitaka na mimi kimapenzi.
Lakini lazima mwanaume usalimu amri mwanamke mwenyewe si umemuona?"
"Hata simkumbuki kwa kuwa nimekutana na wengi."
"Aah! Mr Lyasi mtu umekutana naye mlango wakati unaingia," kauli ile ilinishtua niliye kutana naye mlangoni ni mke wangu Waridi Mmmh..haiwezekani nilijisemea ina maana daktari hamjui mke wangu. Ni kweli hamjui mke wangu zaidi kujuana naye pale hospitali lakini mengine yanayonihusu hayajui, nilijibu kwa kubabaika huku mapigo ya moyo yakiwa juu.
"Ni.ni.memuona lakini sikumtilia maanani."
"Ngoja nikuonyeshe picha yake," Daktari alisema yale hku akivuta droo ya meza na kuniweke bahasha yenye picha juu ya meza. Nilichukua na kuanza kuiangalia, nilitamani kupiga kelele kama mwendawazimu lakini nilijikaza kiume.
Zilikuwa picha za wifi yako Waridi akiwa amepiga kwenye pozi nyingi chafu, zingine amevaa nguo ya ndani na nyingine mtupu kama alivyozaliwa, jasho lilinitoka kama nilikuwa nimefungiwa kwenye chumba chenye joto kali.
"Lyasi unaona toto hilo, mwanaume yoyote halazi damu hata wewe sidhani akija kwako utamwacha hivihivi.Lakini wanawake kama hawa ndio wanaoua wanaume.Najua wengi wanaingia kichwa kichwa bila kinga, huwezi kujua kwa mwanamke kama huyu jamvi la wageni, kama anao ataondoka na wengi.
Lakini mimi sijagonga pekupeku kila akija lazima nitumie kinga, sasa uzuri wa mwanamke huyu akija lazima aniletee pesa. Hapa kaniachia pesa kibao," Alisema yale ya kuvuta droo na kutoa kiasi cha pesa kisicho pungua laki mbili, wakati huo nilifanya ujanja na kuchomoa picha mbili na kuzificha.
"Hii ni kazi ya leo amekuja kufunga kizazi kabisa amechoka kila siku kuchokonolewa, kwa uamuzi kama ule nilimsifu na kutupunguzia dhambi, lakini kwa upande mwingine nilimuonea huruma kwa kuwa bado binti mdogo. Kutokana na maelezo yake japo siamini mwanamke aliye olewa afanye upuuzi kama ule na kama kaolewa nina imani mume wake huenda jogoo lake haliwiki linalomfanya mkewe haangaike nje."
Maneno yale yalikuwa kama radi kwenye ubongo wangu hata kufanya nisikie kama mtu naukwangu ubongo.Hata sikumbuki niliondoka vipi hata niliendeshaje gari, nilishtukia nikiwa hospitali nimelezwa nikiwa na plasita kichwani baada ya kupata ajali.
Lazima niliendesha gari kwa mwendo wa kasi nikiwa sioni mbele,Mungu alininusuru kwa kuwa nilipasuka kidogo kichwani na kushonwa nyuzi sita. Lakini kama ulivyoona nilitoka baada ya siku tatu.
Kwa kweli sikutamani kumuona yule mwanamke, lakini nilishindwa kuanzie wapi kwa kuwa mama alinikataza kukubali ya kuambiwa.Vilevile ushahidi wa picha nilizochukua haukutosha. Nilikuwa nipo naye kwa vile mke wangu na dini yetu hairuhusu kuachana. Mabadiliko yangu hata yeye aliyaona mara nyingi alikuwa kuwa karibu yangu na kusingizia ugonjwa nilijua ni janja yake.
Mwanzo niliona aibu kulisema lile, lakini moyo ulishindwa kustahimili, niliamua kumfuata mama na kumweleza yote niliyoelezwa na daktari.
Mama baada ya kunisikiliza alitulia picha alikataa kuziangalia, baada ya kutafakari kwa kina alisema:
"Japo maelezo yako ni mazito yenye kukufanya uchukue kisu au siraha yoyote na kumtoa roho mtuhumiwa. Lakini bado hayajaniingia kichwani. Pamoja na hayo mwanangu umeonyesha moyo wa kiume la muhimu kabla ya kutoa hukumu ulitakiwa ufanye uchunguzi.
“Yaani mkeo uko naye kwenye ndoa afanye uchafu kama ile zaidi ya mara tatu wewe mwanaume hujui. Si kweli fanya uchunguzi wa kina usikubali ya kuambia, huyo mkeo ana kizazi gani na tumbo gani.
Hata awe anatoa mimba wewe hujui amekufunga kiasi gani? Basi inamaana hata haki yako ya ndoa huwa hakupi ikiwa hivyo. Sikubaliani na uamuzi unaotaka kuchukua pata ushahidi ndipo utoe hukumu," mama alinipa ushauri.
Kwa kweli siku ile kwa mama nilinawa mikono na kuona nimefeli mtihani wa kwanza. Nilitaka kwenda Dar kwa dada kumpelekea habari zile. Lakini niliona bora nimwambie ma mdogo japo maamuzi yangu ya kumuoa Waridi aliyapiga, niliona kuna umuhimu wa kumweleza ma mdogo.
Nilipofika kwake hata kabla ya kusema akigundua kuna kitu kimenikwaza ndipo alipokata kujua kulikoni. Ukweli nilikuwepo pale kimwili lakini kimawazo nilikuwa mbali ma mdogo alinishtua katikati ya dimbwi la mawazo mazito.
"Vipi mwanangu mbona unaonekana upo mbali kimawazo una tatizo gani baba?"

Itaendelea.
 
SEHEMU: 12

ILIPOISHIA:
“Yaani mkeo uko naye kwenye ndoa afanye uchafu kama ile zaidi ya mara tatu wewe mwanaume hujui. Si kweli fanya uchunguzi wa kina usikubali ya kuambia, huyo mkeo ana kizazi gani na tumbo gani.
Hata awe anatoa mimba wewe hujui amekufunga kiasi gani? Basi inamaana hata haki yako ya ndoa huwa hakupi ikiwa hivyo. Sikubaliani na uamuzi unaotaka kuchukua pata ushahidi ndipo utoe hukumu," mama alinipa ushauri.
Kwa kweli siku ile kwa mama nilinawa mikono na kuona nimefeli mtihani wa kwanza. Nilitaka kwenda Dar kwa dada kumpelekea habari zile. Lakini niliona bora nimwambie ma mdogo japo maamuzi yangu ya kumuoa Waridi aliyapiga, niliona kuna umuhimu wa kumweleza ma mdogo.
Nilipofika kwake hata kabla ya kusema akigundua kuna kitu kimenikwaza ndipo alipokata kujua kulikoni. Ukweli nilikuwepo pale kimwili lakini kimawazo nilikuwa mbali ma mdogo alinishtua katikati ya dimbwi la mawazo mazito.
"Vipi mwanangu mbona unaonekana upo mbali kimawazo una tatizo gani baba?"
SASA ENDELEA…

"Nilimsimulia kwa unyonge iliyochanganyikana na aibu, baada ya kunisikiliza kwa kina akinisogelea na kunisika mgongoni na kunipiga taratibu huku akisema:
"Pole sana japo ni ubishi wako lakini siwezi kukulaumu kukosea ni sehemu ya maisha ya mwanadamu la muhimu ni kujifunza kutokana na kosa alilokosa."
"Ma’ mdogo nitanisaidiaje?"
"Jambo lisilo na ushahidi ni vigumu kulitolea hukumu hata mahakamani huwezi kumtia hatiani mtu bila ushahidi."
"Ma’ mdogo picha hizi ni ushahidi tosha."
"Hakuna ushahidi wowote wa kufanya mtu akubali kwa kuwa picha ni ya kawaida ambayo amepiga japo kapiga uchi lakini bado haujawa ushahidi wa kumtia hatiani.Labda angekuwa amepiga na mwanaume lakini vile vile sio ushahidi haijulikana amepiga lini."
"Sasa unaniambiaje?"
"La muhimu ni kumfuatilia kwa karibu tu mkeo japo najua ni kazi ambayo inaweza kukufanya uchanganyikiwe."
"Yaani mama kama kuna uwezekano nikikifika nimtimue sitaki hata kumuona."
"Lakini Lyasi tusimhukumu huenda ni njama za watu kutaka kuivunja ndoa yenu, fanya uchunguzi wa kina ili kumkamata lazima ufanye uchunguzi wa kina bila kuonyesha wasiwasi wowote."
"Mmh! Mama nitajaribu yaani nilitaka mnipe rukusa ya kumfukuza tu na si kitu kingine."
"Siwezi kuingilia ndoa ya mtu leo niivunje ndoa yenu kesho mkirudiana nionekane mbaya."
Niliondoka kwa ma mdogo nikiwa nimechoka sijui nifanye nini, nilipofika nyumbani nilimkuta mke wangu akiwa anisubiri akiwa analia. Niliweka hasira zangu pembeni na kumuuliza:
"Nini kimekusibu mke wangu?"
"Rafiki yangu amefariki."
"Yupi huyo?"
"We humjui."
"Kwa hiyo unaniambiaje?"
"Nilikuwa naomba ruhusa niende nikazike."
"Wapi?"
"Iringa."
Sikutaka kumuhoji sana nilishukuru kupata ule msiba ili aniondokee na kunifanya kidogo niondoe kinyaa mbele ya uso wangu. Japokuwa taarifa za mke wangu niliziamini lakini akili nyingine haikubali yaani na uzuri wa Waridi awe malaya kiasi kile. Nilijua uenda kweli ni uongo wa daktari.
Lakini niliamua kujifanya sijui chochote kwa kuogopa kujua na kama kweli anafanya vile na kuficha makucha yake. Nilimpatia kiasi cha pesa na siku ileile niliondoka, kwa kweli moyo wangu ulipata faraja ya muda huku nikipanga arudipo nitatafuta mtu wa kumfuatilia kwa karibu nyendo zake zote.
Siku ya pili nilikwenda mpaka hospitali kwa yule daktari ili kumdodosa kujua ana jipya gani. Kama kawaida nilipofika nilimkuta na kuanza kudodosa mambo ya Waridi.
"Vipi shemeji wa siku ile leo hajaja?"
"Amenipigia simu kuwa amesafiri amekwenda Zanzibar kwenye harusi, lakini siamini lazima atakuwa amekwenda kwa bwana yake mmoja wa Kipemba."
"We umejuaje?"
"Yule mwanamke siri zake zote zipo mkononi mwangu kwa hesabu ya karibu ana mabwana zaidi ya watano ukichanganya bwana yake wa ndoa na mimi mchovu tunakuwa saba. Lakini namuonea huruma mumewe."
"Sawa bwana nilikuwa napita hasa nikizingatia wewe mtu wangu wa karibu nikipita karibu na hospitali hata kama siumwi lazima nipite kukusalimia."
"Asante nashukuru."
Nilimuaga na kwenda zangu nilizidi kuchanganyikiwa habari zile niliamua kumpelekea ma mdogo. Ma mdogo alicheka sana na kuniona sasa nimechanganyikiwa.
"Lyasi utachanganyikiwa kwa kusikiliza maneno yasiyo kuwa na ukweli wowote."
"Mbona anajua amesafiri amejuaje?"
"Lakini na wewe umekuwa bwege kiasi gani cha kumruhusu mkeo bila kujua anakwenda wapi?"
"Nilimuamini."
"Acha upumbavu umuamini vipi wakati unajua tayari amekuwa si muaminifu."
"Ma mdogo nilitaka aondoke ili nipumzike sikutaka kuwa naye karibu."
Ma’ mdogo baada ya kumweleza vile alichukua simu yake na kumpigia mke wangu kwa sauti ya nje.
"Haloo mkwe."
"Aaah! Ma mdogo shikamoo unasemaje?"
"Uwapi mwanangu?"
"Nipo msibani Iringa."
"Umesifiwa na nani?"
"Na rafiki yangu kwani Lyasi hajakuambia."
"Kaniambia Iringa sehemu gani?"
"Hapahapa mjini."
"Mmeishazika?"
"Tunazika jioni hii na kesho asubuhi nageuka."
"Sasa mwanangu mimi nipo Iringa nimefika muda si mrefu Lyasi alinieleza upo huku sasa tutaweza kuonana?"
"Umesema upo wapi?"
"Iringa na sasa ndio namalizia kazi zangu na muda si mrefu nitaondoka kurudi."
"Mmh! Mama siwezi kuonana na wewe."
"Kwa nini?"
"Elewa hivyo siwezi kuonana na wewe kwa heri tutaonana Dar," Waridi alikata simu Mama mdogo aliniangalia kisha alicheka na kusema:
"Sasa nimeamini kuwa mwanangu umenunua mbuzi kwenye gunia mkeo sawa na maua ya jeneza juu yanapendeza ndani kuna mzoga."
"Sasa unaniambiaje?"
"Hii kazi niachie nitakwambia siku moja siwezi kukupoteza hivihivi nakuona mwanamke yule atakuua tena mwanangu kuna umuhimu wa kwenda kupima kwa sababu kwa sifa hizo sidhani kama mkeo ni mzima."
Kauli ile ilinifanya nikose raha na kujiuliza kama nitakutwa nimeathilika nitakuwa mgeni wa nani. Nilipanga mdogo wangu nikikutwa nimeathirika ningejiua na kukimbia aibu iliyokuwa mbele yangu.
Siku ya pili niliongozana na ma mdogo hadi kituo cha ushauri nasaa, pamoja na kunipa ushauri mwingi kwa upande wangu haukunisaidia lolote zaidi ya kupima na kujua nipo kwenye hali gani?

Nilichukuliwa vipimo na kusubiri kwa dakika kumi na tano kisha niitwa na muuguzi wa kituo kile ili kujulishwa majibu ya kipimo changu, baada ya kuingia niliketi kwenye kiti.
“Bwana Lyasi,” aliliita jina langu.
“Naam,”
"Upo tayari kupokea majibu yako?"
"Nipo tayari."
"Kama umeathirika unafanyaje?"
"Nitafanyaje na hali imeisha kuwa."
"Na kama upo salama utafanyaje?"
"Ni kumshukuru Mungu na kuwa makini na kuzidi kumuomba Mungu kila siku."
"Basi bwana Lyasi majibu yako ni haya..."
Hapo nilisikia kama ngoma za sikio zikitaka kupasuka na kuuona mwili wangu mwepesi.Kwa kweli nilikuwa namwangalia daktari lakini nilikuwa nimehama hata pumzi zangu nilihisi kusimama. Hata majibu aliyotoa sikusikia. Daktari alinishtua tena akiendeleza alipoachia...
"Basi ndio hivyo Mungu bado anakupenda japo najua bado huamini," nilijikuta nikimuuliza tena alikuwa akisemaje.
"Yaani furaha uliyonayo unafanya husikii ungekuwa umeathirika
ungeuliza hivyo?"
"Ina maana sijambulizwa?"
"Ni kweli lakini…" kauli ile ilinishtua na kuuliza tena.
"Lakini nini tena?"
"Unatakiwa kurudi tena baada ya miezi mitatu ukiwa hujakutana na mwanamke au kutumia kinga kila mfanyapo tendo la ndoa."
Nilipiga magoti na kumshukuru Mungu huku machozi yakini toka daktari alininyanyua na kunikumbatia huku akinipiga piga mngongoni.
"Hongera ni ujasiri kuamua kupima jilinde na kuwa muangarifu."
Niliagana na mshauri na kutoka nje nikiwa bado sijafuta machozi ma mdogo aliponiona aliniwahi kunikumbatia huku akisema:
"Pole mwanangu lakini usikate tamaa," alijua damu yangu si safi.
"Hapana ma’ mdogo nipo sawa."
"Una maana gani?"
"Damu yangu safi."
"Acha utani na machozi hayo ya nini?"
"Ya furaha nilikuwa siamini," kauli ile ilimfanya ma mdogo anibebe juu kwa juu huku akisema:
"Sasa tunalitoa bomu kabla halijalipuka."
"Kweli ma mdogo," nilimuunga mkono.
"Lakini kazi hiyo niachie na akirudi usionyeshe mabadiliko yoyote, lakini usikutane naye kimwili, sawa baba."
"Sawa mama nitazingatia ushauri wako."
Nilirudi nyumbani na kusahau yote zaidi ya kufurahia kuwa safi, lakini nilijiuliza Waridi huenda ana pepo wa ngono yaani hesabu ya wanaume aliokuwa nao ilinitisha. Na kunifanya nilione kaburi linamwita. Hakurudi hadi siku ya tatu na kunikuta nimeisha toka kwenye shughuli za kutwa nzima.
"Vipi mpenzio za kazi?"
"Nzuri."
"Unajua mpenzi ma mdogo anaweza kunilaumu."
"Kwa nini?" nilijifanya sijui
"Au basi, ehe za hapa?"
"Kama ulivyo ziacha."
"Sasa mume wangu kwa vile nimerudi sijisikii vizuri naomba nifike hospitali."
"Ipi hiyo?" alinitajia ileile tuliyokutana kwa rafiki yangu.
"Sawa usichelewe."
"Lakini mume wangu kwa vile uchunguzi utachukua muda naweza kupata kitanda pale mpaka asubuhi."
"Hakuna tatizo," alinisogelea na kunipiga busu, siku zote dada yangu mwanamke akiisha kugeuza kipofu anaamini hutaona milele. Kama mwanzo alikuwa anafanya kwa siri anaamua kufanya kwa dhahili na usipoona anaingiza mwanaume ndani."
Kauli ile ilimfanya Sundi akumbuke mkasa uliompata shoga yake pale alipomtawala mumewe ikifikia hatua ya kuingiza mwanaume ndani juu ya kitanda cha mumewe. Picha ilizidi kumuonyesha jinsi matatizo ndani ya ndoa yanavyo shabihiana.
"Basi mdogo wangu baada ya kunipiga busu aliondoka baada ya kuweka begi lake. Baada ya kuondoka nilimpigia simu ma’ mdogo na kumweleza yote.
"Sasa nafikiri leo ndio siku ya arobaini yake."
"Kwa hiyo unaniushauri nini?"
"Umeniambia yule daktari hajui kama Waridi mke wako?"
"Ndiyo."
"Una uhakika?"
"Kwa asilimia mia."
"Basi mpigie simu tujue ana habari gani juu ya Waridi kama hakwenda huko tutajua."
"Sawa nitakujulisha," nilikata simu na kumpigia daktari.
"Haloo best."
"Ooh! mheshimiwa upo wapi?"
"Tena ungekuwa karibu leo ungemuona kwa karibu."
"Kwani yupo wapi?"
"Amekwenda kula ila leo nitakuwa naye mpaka asubuhi."
"Ina maana leo mzee umeibua mzigo?"
"Kaka cha wote akiachwi, mpemba kamaliza zamu yake na mimi zamu yangu harua haina makombo."
"Ni kweli," japo nilijibu mdogo wangu nilihisi kama mtu kaupasua moyo wangu bila ganzi. Niliamua kukata simu baada ya hali kuwa mbaya, nilipumua kwa shida mbele niliona kizunguzungu na kujikuta najilaza kitandani.
Nilishtushwa na simu nilipoangalia nilikuta ni simu ya ma’ mdogo na kuipokea, muda ulikuwa saa mbili usiku.
"Vipi ma mdogo?"
"Mbona kimya," nilimweleza kila kitu.
"Sasa unapafahamu kwa daktari?"
"Mmh, hapo ndipo nimekosea."
"Lyasi unafanya ujinga gani au unafurahia upumbavu unaofanyiwa?"
"Hapana mama."
"Sasa tunafanya nini bila kujua kwa daktari tutakuwa tumefanya kazi bure."
"Ma mdogo yaani nimechanganyikiwa naomba msaada wako."
"Sasa ni hivi tusipoteze muda nakupitia hapo sasa hivi," nilikata simu na kujiandaa bila kujua ma mdogo anataka kunipeleka wapi. Baada ya robo saa mama mdogo alifika na kuniambia niingie kwenye gari lake na safari iliendelea.
Nilishangaa kumuona tunaelekea upande wa hosiptali, tulipofika hospitali ma mdogo aliniambia nisubiri kwenye gari na kuingia hospitali peke yake. Baada ya muda alirudi ameongozana na mtu na kuja naye kwenye gari.
Baada ya kuingia ndani ya gari ma mdogo aliondoa gari, yule jamaa alinisalimia.

Itaendelea
 
SEHEMU: 13

ILIPOISHIA:
Niliamua kukata simu baada ya hali kuwa mbaya, nilipumua kwa shida mbele niliona kizunguzungu na kujikuta najilaza kitandani.
Nilishtushwa na simu nilipoangalia nilikuta ni simu ya ma’ mdogo na kuipokea, muda ulikuwa saa mbili usiku.
"Vipi ma mdogo?"
"Mbona kimya," nilimweleza kila kitu.
"Sasa unapafahamu kwa daktari?"
"Mmh, hapo ndipo nimekosea."
"Lyasi unafanya ujinga gani au unafurahia upumbavu unaofanyiwa?"
"Hapana mama."
"Sasa tunafanya nini bila kujua kwa daktari tutakuwa tumefanya kazi bure."
"Ma mdogo yaani nimechanganyikiwa naomba msaada wako."
"Sasa ni hivi tusipoteze muda nakupitia hapo sasa hivi," nilikata simu na kujiandaa bila kujua ma mdogo anataka kunipeleka wapi. Baada ya robo saa mama mdogo alifika na kuniambia niingie kwenye gari lake na safari iliendelea.
Nilishangaa kumuona tunaelekea upande wa hosiptali, tulipofika hospitali ma mdogo aliniambia nisubiri kwenye gari na kuingia hospitali peke yake. Baada ya muda alirudi ameongozana na mtu na kuja naye kwenye gari.
Baada ya kuingia ndani ya gari ma mdogo aliondoa gari, yule jamaa alinisalimia.
SASA ENDELEA…

"Za saizi mheshimiwa?"
"Nzuri tu sijui za kwako."
"Zangu nzuri."
Baada ya salamu kulitawala kimya kifupi ndipo ma mdogo aliposema:
"Lyasi japo kanielekeza anapokaa daktari ambapo si pakupotea lakini imekuwa vizuri na bwana huyu anaelekea huko."
"Ooh! itakuwa vizuri."
"Nashukuru sana yaani sasa hivi nilikuwa nafikiria usafiri wa kunirudisha nyumbani."
Ma mdogo hakuwa na wasiwasi aliendesha gari kwa mwendo wa kawaida. Hadi sehemu moja ambayo ilikuwa nje kidogo ya mji. Ilikuwa ni sehemu iliyokuwa kimya wanayokaa watu wengi wa serikali. Yule jamaa tuliyembeba kwenye gari aliomba ateremke kwa kuwa amefika.
Tulimteremsha kwa kuwa nyumba yenyewe alituonyesha kwa macho kwa pale alipoteremka, tulimshukuru kwa msaada wake.
"Tuna shukuru kwa msaada wako."
"Hata ninyi vilevile umenipa msaada kubwa hata nyumbani kwangu watashangaa kuniona nimewahi kurudi si kawaida yangu."
Tuliangana naye na sisi kubakia kwenye gari tukipanga jinsi ya kuingia mule ndani na kuweza kufumania. Kwanza nilimuuliza aliwezaje kupata msaada wa haraka namna ile.
"Niliwaulizia wakasema ametoka kumbe anaitwa daktari Mwakaringa."
"Ehe?"
"Basi niliwaeleza nina shida naye ya kifamilia kwa kuwa mimi ni dada yake nimetoka Iringa leo na nipo kwenye semina na sijawahi kufika kwake. Kwa vile yule bwana alikuwa na safari ya kurudi nyumbani ilikuwa rahisi japo sehemu aliyonielekeza nisingeweza kupotea kutokana na mpangilio wa nyumba na namba zale."
"Ma mdogo ka mpelelezi."
"Mwanangu tumesoma hadithi za upelelezi za kina Willy Gamba nasi tunazifanyia kazi."
"Mhu! Sasa nini kinaendelea?"
"Twende tukabishe hodi akifungua tu tunaingia ndani kwani daktari mwenyewe anakuzidi nguvu?" Ma’ mdogo alikuwa na ubavu alijiamini kukabiliana na mwanaume.
"Hapana ubavu namzidi."
"Basi kazi ndogo."
Lakini wakati huo nguvu zilikuwa zinanipungua taratibu na kujiuliza kama kweli Waridi atakuwa kwa daktari itakuwaje?"
Tulikwenda hadi kwenye mlango na kugonga mlango, ndani kulikuwa na mlio wa muziki lakini hakukuwa na sauti za watu. Baada ya kugonga kwa nguvu kidogo nilisikia sauti ya daktari ikiuliza:
"Nani tena muda huu?"
"Ni mimi best."
Alikuja hadi mlangoni na kufungua mlango aliponiona alishtuka.
"Vipi mheshimiwa mbona usiku?"
"Nilikuwa nimekuja kwa mdogo wangu anakaa kwenye kota za serikari hapo juu kwa vile ulinijulisha unapokaa nikaona bora nikujulie hali rafiki yangu unajua napenda sana kukuona swahiba wangu hasa ninapokuwa karibu na maeneo ulipo nikaona nipite kama sitapotea basi ipo siku nikija kwa ma mdogo na wewe upo nitapita kwako."
"Hakuna tatizo..ma’ mdogo shikamoo."
"Marahaba baba."
"Karibuni ndani mpate soda japo mmenitembelea usiku."
Tuliingia ndani na kukaa sebuleni, dakta Mwakaringa alituletea soda wakati huo tuliulizana kwa macho "yupo?"
Macho yangu yalishtuka baada ya kuuona mkoba wa mke wangu juu ya kochi, nilimuonyesha ma mdogo kwa ishara naye alikubali kwa kichwa kwamba kaona.
"Jamani karibu japo usiku au kuna mnywaji wa pombe kali?"
"Hakuna."
Baada ya kutufungulia soda nilisikia sauti ya mke wangu Waridi ikimuita daktari.
"Sweet mbona imekuwa mwaka wageni wa usiku wanao haribu starehe za watu," ilionyesha ni sauti ya kulevi.
"Vipi kifaa kilikuja?"nilijifanya sijui kitu.
"Nawe mheshimiwa umesahau si nilikwambia leo mamaa ndani ya nyumba."
"Mwambie aje atusalimie."
Alimwita kwa sauti ya juu:
"Sweetie njoo uonane na rafiki yangu."
"Mi sio matangazo siwezi kuamka kwa ajili ya mtu kuniona akitaka aje yeye. kwanza mwambie aje kesho maana naona umenikatili raha zangu hebu njoo mara moja kwanza nikutume."
"Jamani nakuja mara moja,"daktari alielekea chumbani kwake.
Tulibonyezana na mama na kukubalia kuvamia chumbani kwa daktari, tulinyanyuka kwa pamoja na kwenda moja moja chumbani kwa daktari na kuingia ndani bila hodi na kumkuta daktari akiwa amemuinamia Waridi.
Sikuamini picha niliyoiona Waridi alikuwa ni yeye akiwa kwenye shuka akiwa hana nguo ya ndani ikionyesha si muda mrefu walikuwa kwenye uchafu wao wa kuisaliti ndoa yangu. Nilijikuta napiga kelele na kuishiwa nguvu.
"Haaaa! mke wangu Waridi!"
"Ha! Maskini mume wangu nimekwisha."
Nilijikuta nakaa chini bila kujielewa,ma mdogo kwa hasira alinipiga kibao kizito mgongoni kilichonifanya ninyanyuke.
"Pumbavu mwanaume gani kama mweanamke badala ya kufumania unakuwa kama umebemendwa."
Nilijikaza kiume na kumuangalia Waridi aliyekuwa amesimama akiwa mtupu akitetemeka huku akiomba msamaha. Nilitamani nimchanechane kwa hasira nilipotaka kumshika ma’ mdogo alinishika na kuniambia:
"Ushahidi umepata unataka kesi nyingine twende nimeisha piga picha zote za ushahidi." ma mdogo alinishika mkono na kunitoa nje nikiwa nalia kitu kilicho muudhi na kuanza kunitukana kama mtoto mdogo.
"Pumbavu unalia nini si ulitaka mwenyewe leo nina imani umeona kwa macho yako."
Tuliingia kwenye gari na kurudi mjini nikiwa nimejiinamia,ma mdogo alinipeleka hadi kwake tulipofika ndani aliniacha sebuleni na kwenda chumbani na kurudi na glasi iliyokuwa na maji na kunipa.
"Hebu kunywa kwanza hiki kinywaji," nilikipokea na kukinywa kwa kweli baada ya kukinywa kilichoendelea sikukijua hadi siku ya pili nilipoamka nilijikuta nipo kwa ma mdogo nimelala.
Nilipoamka nilikuta tayari nimendaliwa kifungua kinywa baada ya kustafutahina niliongozana na ma mdogo hadi nyumbani.Tulipofika tulimkuta Waridi yupo nyumbani akiwa analia na alipotuona alituangukia akiomba msamaha
Ma mdogo alimuuliza maswali kuhusiana na yote niyajuayo kwake na kukubali bila kupinga hata moja mwisho alimuuliza:
"Sasa mwanangu sisi tunataka kukusamehe na wewe umefunga kizazi kuna faida gani?"
"Jamani ni shetani naomba mnisamehe nipo radhi aoe mwanamke mwingine ili apate mtoto na mimi nitakuwa mlezi wao."
"Hapana Waridi taarifa zako tunazo muda mrefu kwa kutufanya wajinga vipofu, lakini tulikutafutia taimingi umeingia mwenyewe huna wa kumlamu na ukienda mahakamani kuna picha zako zote za ushahidi zikiwemo za kujidharirisha kama hizi."
Mama mdogo alitoa picha zilizokuwa amempa daktari, hapo ndipo nguvu zilimwisha.
"Kwa upole na kwa ustaarabu ingia ndani uchuke chake na utokomee na nisikuone hapa na lazima nifike kwenu kuwasilisha upuuzi huu na ikiwezekana tunakufunguli mashtaka kwa kumuambukiza UKIMWI mwanangu tumepima na kukuta umemuumiza.
Kwa kweli yataka moyo jinsi alivyokuwa Waridi kama paka aliyetumbukia kwenye tundu la choo. Aliondoka ningekuwa mimi ningemsaidia huruma iliniingia. lakini kuongeza kauli yoyote ni kumuudhi ma mdogo baada ya yeye mwenyewe kuumeza mfupa nitakuwa mimi mtoto wa kiume.
Basi mdogo wangu siku ile ndio ikawa mwanzo na mwisho wa ndoa yangu aliyosimamia ma mdogo. Basi toka siku ile nimekuwa nawachukia wanawake na kufuta wazo la kuoa sasa hivi japo ipo siku nitafuta uamuzi ule mzito lakini si leo."
Baada ya mkasa uliomfanya Sundi abakie mdomo wazi kwa vituko vya wifi yake. Alishindwa amlaumu nani kwa kuwa aliisha elezwa kuwa ndoa au mapenzi ni bahati nasibu ule au uliwe. Alishusha pumzi na kumpa pole kaka yake.
"Pole sana kaka yangu."
"Asante yamepita."
"Ni kweli yamepita lakini yanauma, pia mshukuru Mungu kukulinda na gonjwa hili kwa tabia chafu za mkeo lazima atakufa kwa ukimwi tu."
"Basi watu kama hao unaweza kukuta mpaka anazeeka hapatwi na ugonjwa huo tena hata kodomu hawaijui."
"Mmh, haya yako nimeyasikia kesho kutwa nina safari ya kwenda kwa dada Cathy."
"Mmh, na yeye joto la jiwe alilipata lakini mwenzetu sasa hivi amesahau anakula maisha nina imani na yeye atakusaidia."
"Sawa kaka wacha nikuwache, lakini huwezi kuamini mama hajui najua yeye atakuwa wa mwisho baada ya kukusilizeni nyote."
"Sio mbaya subiri basi tupike siku hizi nimekuwa kaka yako msela."
"Acha nitakula nyumbani."
Sundi aliagana na kaka yake na kurudi nyumbani, alipofika alimkuta mama yake akisoma biblia alipomuona alimsalimia:
"Mama za saizi?"
"Sundi mbona leo umechelewa ulipitia wapi?"
"Mama nilikuwa kwa ma mdogo na pia nilipitia kwa kaka Lyasi."
"oooh kumbe ulikuwa na safari ndefu hawajambo wote?"
"Wazima wa afya njema."
"Mhu wanasemaje?"
"Wanakusalimia ila mama ma mdogo amenituma kesho niende kwa dada Cathy."
"Wapi? Dar?"
"Ndiyo mama."
"kuna nini tena?"
"Sijui amesema atanijulisha hiyo kesho kutwa."
"Mimi sina tatizo mjulishe na baba yako tu nisije nikaulizwa."
Jioni baba yake aliporudi alisubiri mpaka usiku baada ya chakula cha usiku ndipo alipomweleza. Lakini baba yake alisema ameisha pata taarifa la muhimu awahi kurudi.
"Mume wangu mwache mtoto akapumzike hata wiki ili aone na jiji."
"Na kazi za hapa?"
"Na akiolewa atafanya nani?"
"Mpaka akiolewa."
"Lazima tujifunze kukaa peke yetu ili akiolewa tusiwe wakiwa."

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom