Hadithi ya umslopagaas

Hadithi ya umslopagaas

Hahaah kwa nini mkuu?
Mkuu ni kwamba nimeona tangu hayo mapendekezo yatokewe hakujakua na muendelezo nadhani kwa siku 2 sasa tangu uweke chapter iliyopita.

Haraka haraka nikadhani kuna baadhi ya changamoto unazipata kuweka yote at once

Basi mimi kwa arosto niliyo nayo nikaona bora twende na mwendo ule ule wa akina Ignosi
 
Yule Mjivuni akautikisa mkuki wake mrefu, akacheka sana kwa muda mrefu, akajibu, ‘’Laiti tungeweza kushindana mimi na wewe peke yetu, ningekuonyesha kazi.’’ Aligeuka aende zake huku anacheka.
Umslopogaas akajibu, na ‘sauti yake ingali ikinguruma,’
‘’Usiwe na shaka, tutashindana peke yetu mimi na wewe.’’
‘’Utashindana uso kwa uso na Umslopogaas, wa damu ya Chaka, wa kabila la Wazulu, mkuu wa jeshi la Nkomabakosi, kama wengi wengine walivyofanya; nawe utajisalimisha mbele ya Inkosikazi kama walivyofanya wengi wengine. Ndiyo, cheka, cheka ila mwisho wako nakuhakikishia fisi watakuwa wanacheka na huku wanavunja mifupa na kuzitafuna mbavu zako.’’

Tuendelee....
SURA YA SITA

Alipokwisha kwenda Yule Mjivuni, mmoja wetu alilifungua lile kapu. Ua zuri sana lilionekana ndani yake, tena barua ndogo iliyoandikwa katika karatasi iliyofungiwa chakula alichokichukuwa, maneno ya barua hiyo ni haya:

‘’Wapenzi Baba na Mama, Wajivuni wametukamata tulipokuwa tukirudi pamoja na ua hili. Nilijaribu kukimbia nisiweze, Hawakunizuru wala yaya, lakini wamesema watanibadilisha kwa mmoja wapo wa rafiki za Bwana Quatermain, Mimi sikubali shauri hili.
Usimwache mtu yeyote atoe maisha yake kuniokoa mimi. Jaribu kuwashambulia usiku; wanafanya karamu ya ng’ombe watatu walioiba na kuchinja. Ninaogopa sana, lakini namtumaini Mungu. Siwezi kuandika zaidi, maana wanaanza kunitazama.
Kwa herini
Flossie.’’

Kwa nje ya karatasi iliandikwa, ‘’Nisalimie Bwana Quatermain. Wanachukua kapu, basi atalipata lile ua.’’

Nilipoyasoma maneno yaliyoandikwa na Yule mtoto mwanamke shujaa wakati wa hatari ambayo ilitosha kumtia wazimu mtu mzima mwenye nguvu, nakiri ya kuwa nililia machozi, tena, katika moyo wangu nilinuia hafi kabisa ya kuwa hafi ikiwa maisha yangu yanaweza kumuokoa.

Basi, hapa tulianza kuzungumza kwa bidii juu ya shauri la kufanya.

Nikasema tena ya kuwa nitakwenda, na tena Bwana Mackenzie alikataa, na Sir Henry na Bwana Good kama watu wema na waaminifu walivyo, walisema nikienda, basi na wao watakwenda pamoja nami na kufa pamoja nami.

Mwisho, nilisema, ‘’Ni lazima kabisa tufanye jambo kabla ya kufika mapambazuko.’’
Tulikaa pamoja na bwana Mackenzie na kupanga shauri, mwisho tulikubaliana kuwa tuwavamie kijeshi ifikapo muda wa mapambazuko kwa kujua muda huo ulikuwa ni mzuri kwani watakuwa wapo kwenye usingizi mzito.

Pamoja na kuwa hatukuwa na jeshi la kutosha kwani walinzi wengi wa pale mission walikuwa wamesafiri mbali lakini hatukukata tamaa.

Hao hao wachache waliokuwepo tuliona kuwa wanatosha kabisa kuwaunganisha pamoja na kwenda kupambana na wale Wajivuni.

Cha kwanza tuliunda kundi dogo la wapelelezi waende kule kwenye boma la ng’ombe walipoweka kambi yao kwa ajili ya kuwapeleleza na kutupatia ripoti ya nini kinaendelea kila waonapo inafaa kufanya hivyo.

Basi, tulipokwisha weka mambo yote tayari, ilikuwa karibu saa saba ya usiku, tukasubiri. Wapeleleze wetu walituambia kuwa Wajivuni wamekwisha kunywa damu ya ng’ombe na kula nyama nyingi sana, na sasa wamelala kuizunguka mioto yao, lakini watu wakulinda zamu wamewekwa kila mlango.

Flossie, Yule mtoto mdogo alikuwa amewekwa karibu ya ukuta katikati ya upande wa magharibi ya boma, na yaya wake yu karibu naye, na punda weupe amefungiwa kigingi.

Miguu ya mtoto imefungwa kwa kamba, na Wajivuni wamelala huko na huko kumzunguka.

Basi kwa kuwa hakuna jambo tena la kufanya, tulikula kidogo, tukalala kwa muda wa saa mbili.

Niliona ajabu jinsi mzee Umslopogaas alivyoweza kujitupa chini na kupata usingizi mara ile, ingawa mambo makubwa yanamngojea.

Sijui habari za wale wenzangu, lakini mimi sikuweza kulala usingizi. Kwa hakika niliogopa, na sasa kwa kuwa nilikaa kimya, nilianza kufikiri juu ya mambo tunayojaribu kuyafanya, nami sikuyapenda hata kidogo.

Tulikuwa watu thelathini jumla na hawakosi wengine hawakuzoea kupigana, nasi tunakwenda kuwashambulia watu wakali mia mbili na hamsini, watu hodari na stadi wa vita kuliko wenyeji wote wa Afrika, na zaidi ya hayo, walikuwa wamelindwa kwa boma la mawe.

Kweli ni jambo la hatari, na hasa kwa sababu hatuna budi kupafikia mahali petu bila kufanya kelele zozote, tena bila kuonekana na wale Wajivuni waliowekwa kulinda zamu.

Hakika, tukiwaamsha kwa jambo lolote kama vile bunduki ikifyatuka kwa habahati mbaya basi, tumekwisha potea wote, maana Wajivuni wote wataamka mara ile, na tumaini letu la kushinda ni kuwatokea ghafla.

Baada ya kupita muda, nilimsikia Bwana Mackenzie akinong’ona nje ya chumba changu, maana kila jambo lazima lifanywe kimya sana, akaniambia kuwa ni saa tisa, nasi hatuna budi kuanza kazi yetu saa tisa na nusu.

Basi, nilimwambia aingie chumbani, na wakati huo kila mtu alikuwa akivaa na kujitengeneza tayari.

Huku nyuma Umslopogaas alikuwa akiwakusanya watu kiwanjani chini ya ule mti mrefu, akawakagua kuona kama kila mtu ana silaha zake tayari.

Mwisho tulibadili shauri kidogo, tulitoa watu wawili katika wale waliokuwa na bunduki, tukawapa ngao na mikuki ya Kijivuni, tukawaambia wafuatane na Sir Henry na Umslopogaas na Yule Mkazi kuulinda mlango mkubwa wa boma lote tuliona kwa dhahiri ya kuwa watu watatu, hatakama ni hodari na wenye nguvu namna gani, hawatoshi kwa kazi ile.
 
Dah, hii story huwa naisoma kwenye kitabu chake japo kimechakaa na karatasi zake zimenyofoka ila, haiishi utamu kwa kweli...!
 
Pana kipande umekisahau hapo pale inkubu aliposema basi tujaribu kuwa shambulia ndipo yule mtu mkubwa alipo sema "umesema kama mwanamume inkubu ya nini kuogopa yule mtoto amesema watachinja ng'ombe na kufanya karamu? basi na iwe karamu yao ya mazikoni yule mbwa ninae tumaini kumuumbua kutakapo pambazuka alisema haogopi kuwa tutawashambulia sababu tu wachache walijua boma walilowewaliloweka kambi?
 
Dah! Mkuu hichi kipande sina kama unacho kiunganishie tu hapo, utakuwa umetusaidia sana.
 
MAAJABU YALIYOWAPATA ALLAN QUATERMAIN NA WENZAKE
HADITHI YA UMSLOPAGAAS

SURA YA KWANZA

SIKU saba zilikuwa, zimepita tangu mwana wangu mpenzi alipozikwa na jioni ilipofika, nilikuwa Nikitembea huko na huko chumbani mwangu nikifikiri, mara mlango unabishwa, Nikaenda nikaufungua mlango mwenyewe, Kumbe rafiki zangu wa zamani Sir Henry Curts na Bwana John Good wapo nje.

Niliwakaribisha ndani wakaingiaa chumbani. Wakakaa mbele ya moto uliokuwa ukiwaka humo.

‘’Mmefanya vyema kuja kunitazama.’’

Hawakujibu neno, ila Sir Henry alishindilia tumbako katika kiko chake akakiwasha kwa kaa alilolitoa motoni, Alipokuwa akiinama mbele kufanya hivyo moto, uliwaka zaidi ukaangaza chumbani, nikafikiri jinsi alivyo mtu mzuri mno.

Uso wake mtulivu wenye nguvu, sura yake thabiti, macho yake makubwa ya kijivu ndevu na nywele zake rangi ya manjano.

Sura yake yote ilikuwa ya mtu aliye bora, tena umbo lake halikuwa kinyume cha uso wake, Sijapata kuona mabega mapana, zaidi wala kifua kinene kama chake.

Umbo la Sir Henry ni pana, ingawa ni mrefu wa futi sita na inchi mbili lakini haonekani kuwa mrefu nilipokuwa nikimtazama hivi, sikuweza kujizuia nisifiri namna mimi nilivyo mwembamba mfupi na namna nilivyohitilafiana na uso wake mzuri, na umbo lake bora.

Embu wazeni basi juu ya mtu mfupi aliyesinyaa, mwenye uso wa rangi ya manjano na umri wa miaka sitini na mitatu mwenye mikono membamba, macho makubwa ya kahawia, kichwa kimefunikwa na nywele zinazoingia mvi na kusimama wima kama brashi iliyotumika, kiasi uzani wake pamoja na mavazi aliyovaa ratili mia moja thelathini na mbili tu.

Basi hapo ndipo mtakapofahamu namna alivyo Allan Quatermain, ambaye kwa desturi huitwa Mwindaji Quatermain, na Waafrika humwita ‘’Makumazahn,’’ maana yake akeshaye usiku, yaani mtu mwerevu asiyedanganyika.

Tena, yupo Bwana Good ambaye hafanani na Sir Henry wala na mimi maana ni mfupi, mweusi kidogo, mnene mnene sana ana macho meusi yang’aayo na katika jicho moja siku zote huvaa rodi, yaani miwani ya jicho moja.

Nilisema yeye ni mnene, lakini neno hilo halitoshi kueleza namna alivyo mnene. Sir Henry humwambia ya kuwa amenenepa hivi kwa sababu yu mvivu, tena anakula sana, ingawa Bwana Good hapendezwi kwa maneno yake , lakini hawezi kuyakana.

Tulikaa kwa muda mfupi, kisha niilichuka kiberiti ili niiwashe taa, kwa sababu niiona giza linachosha, maana ndivyo inavyoelekea hasa ikiwa muda wa siku saba tu umepita tangu mtu alipozika tumaini la maisha yake.

Huku nyuma Sir Henry na Bwana Good walikuwa wamekaa kimya, wakiona nadhani, ya kuwa hawana la kusema linaloweza kunifariji, wakaridhika kunifariji kwa kuwapo kwao ni rambirambi zao za kimya.

Ni kweli ya kuwa twapata tumaini na faraja katika saa za majonzi kwa kuwapo wengine, wala si kwa maongezi yao ambayo huelekea kutuudhi tu. Wakakaa wakivuta tumbako, na mimi nilisimama mbele ya moto nikivuta tumbako pia na kuwaangalia.

Halafu kidogo nilisema, ‘’Je rafiki zangu wa zamani, tangu tuliporudi toka nchi ya Ukukuana hata leo, miaka mingapi imepita? ‘’Bwana Good akasema, ‘’Miaka mitatu. Kwa nini unauliza?’’.

Nikajibu, ‘’Nauliza kwa sababu nafikiri ya kuwa muda niiokaa pamoja na watu mijini umenitosha kabisa, Nitarudi mwituni tena.’’

Hapa Sir Henry alikipeleka nyuma kichwa chake, akacheka mcheko wake wa kindani, akasema, ‘’Ama ni ajabu sana, sivyo Good?’’

Bwana Good akaniangalia, na huku anacheka katika rodi yake, kama kwamba anaficha siri, akasema, ‘’Ndiyo, ajabu sana ajabu kweli kweli.’’

Mimi ni mtu asiyependa mafumbo na mambo ya sirisiri, basi niliwatazama mmoja mmoja, kishanikasema, ‘’Siwezi kufahamu vizuri,’’

Sir Henry akasema, ‘’Hufahamu? Basi, nitaeleza. Good na Mimi tulipokuwa tukija hapa tuliongea.’’

Nikayakatiza maneno yake kwa ukali kidogo, nikasema, ‘’Nadhali kama Good alikuwapo, hamkosi mliongea maana Good ni mtu apendaye sana maongezi. Je, mliongea habari gani?’’

Sir Henry, akauliza, ‘’Ee wafikiri tuliongea habari gani?’’
Nikatikisa kichwa changu.

Haiwezekani nikajua Good aliongea nini, maana mara nyingi huongea habari za mambo mengi.

Sir Henry akasema, ‘’Tuliongea juu ya shauri dogo nililoliwaza yaani kama wewe utakubali tutafunga mizigo yetu na kuiendea nchi ya Afrika kufanya safari nyingine,’’

Nilipoyasikia maneno yake, nilishtuka sana, nikasema, ‘’Ni kweli usemayo?’’ akajibu, ‘’Ni kweli, na Good naye amekubali pia, sivyo Good?’’
Na yeye akaitikia, ‘’Ndiyo.’’

Basi, Sir Henry akaendelea, na sauti yake ilionyesha namna anavyoona hamu, akasema, ‘’Nami pia nimechoka kukaa bure kiubwana katika nchi iliyokinai mabwana.

Kwa muda wa mwaka mzima na zaidi nimekuwa nikitukutika kama tembo mzee anusaye batari.

Kila mara ninaota ndoto za nchi ya Ukukuana, na bibi kichawi Gagula, na Mashimo ya Mfalme Sulemani. Nakuambia ya kuwa nimenaswa na hamu nisiyoweza kuieleza.
Dah, shukran sana mkuu kwa kutusaidia kwa kutuletea hizi story mubashara
 
SURA YA SABA

Basi, sasa tulingoja, tukasimama kimya katika baridi na kimya na giza tukiungojea wakati wa kuondoka.

Labda wakati huo wa kungoja ulikuwa wakati mbaya kuliko nyakati zote, muda wa robo saa tu, lakini ulikuwa kama haupiti, jinsi ulivyokawia.

Umslopogaas tu ndiye aliyeonekana kama kwamba hawazi kitu, amesimama ameliegemea shoka lake Inkosikazi, na mara kwa mara ananusa tumbako.

Mwezi ulishuka kabisa ukaiacha dunia nzima giza tupu isipokuwa ukungu wa kijivu katika mashariki, dalili ya mapambazuko yanayokaribia.

Bwana Mackenzie akasimama ameshika saa yake mkononi, na mke wake amemshika mkono akijaribu kujizuia asilie.

Akasema, ‘’Saa kumi kasoro dakika ishirini: nadhani mwangaza utatosha kushambulia saa kumi na dakika ishirini! Bwana Good, nadhani afadhali wewe uanze kwenda, maana lazima utangulie wewe.’’

Bwana Good akaisugua rodi yake, akaivua kofia yake akamuaga Bibi Mackenzie, akaondoka kwenda mwisho wa boma la ng’ombe kwa njia za kuzunguka zilizotokana na watu wake.

Hapa kijana mmoja akaja akatoa habari ya kuwa Wajivuni wote katika kambi wamelala usingizi isipokuwa wale wanaolinda zamu,. Mmoja anatembea mbele ya mlango mkubwa, na mmoja mbele ya mlango mdogo wa nyumba.

Basi, hapo sote tuliondoka. Kwanza kiongozi alitangulia, kisha Sir Henry na Umslopogaas na Yule Mkazi na wale watu wawili wa Bwana Mackenzie waliochukua mikuki mirefu na ngao.

Mimi nilifuata pamoja na wenyeji watano wenye bunduki, na Bwana Mackenzie akafuatana pamoja na watu wake sita kulielekea lile boma la ng’ombe walimofanya kambi Wajivuni.

Lilikuwa chini ya mwinuko ule, ambao juu yake nyumba ya misioni imesimama kadiri ya yadi mia nane.

Tulikwenda yadi mia tano za kwanza kwa mwendo wa haraka kidogo kimya kimya; kisha tukaanza kwenda mbele kwa kimya zaidi kama chui anayewinda, tukinyemelea toka mti mpaka mti na mwamba mpaka mwamba.

Basi, tulinyemelea hivi, tukafika karibu na boma la ng’ombe kadiri ya yadi hamsini. Sasa ikawa lazima tupite mahali pa wazi mpaka kulifikia boma, lakini, hapa tulipo tumefichwa katika kichaka. Kulianza kupapazuka na nyota nyingi tukaweza kuona ukungu unazificha.

Mashariki tuliweza kuliona boma kwa shida kidogo, tukauona mwangaza wa mioto ya kambi ya Wajivuni.

Basi, tulisimama tukaangalia, maana tulijua ya kuwa Yule anayelinda zamu amewekwa katika mlango wa boma.

Baadaye kidogo alionekana mtu mshupavu, akipita taratibu huko na huko mbele. Ya mlango uliozibwa kwa miiba. Tulikuwa tumetumaini kumwona ameshikwa na usingizi, lakini sivyo. Alikuwa macho kabisa.

Kama hatuwezi kumuua Yule mtu, tena kumuua bila kufanya kelele, basi tmekwisha potea. Tukajikunja na huku tunamwangalia.

Halafu Umslopogaas aliyekuwa karibu nami, alinigeukia, akafanya ishara, kisha, akalala kitumbotumbo kama nyoka, akamwangalia Yule mlinda zamu, na mara alipopata nafasi alianza kujinyonganyonga mbele katika majani bila kufanya hata sauti.

Yule mlinda zamu asishuku hatari, akaanza kuimba kwa sauti ndogo na Umslopogaas akazidi kujinyonganyonga mbele, na mlinda zamu akaendelea kutembeatembea. Halafu aligeuka akatazama juu ya ukuta katika boma.

Mara ile Yule nyoka mwanadamu aliyekuwa akimnyemelea alijinyonganyonga mbele zaidi kadiri ya yadi kumi, akajificha nyuma ya chungu ya majani.

Yule mlinda zamu alipogeuka tena, aliiangalia chungu ile ya majani kama kwamba ameona kitu, akaikaribia kidogo, kisha aliinama akaokota jiwe akalitupa katika yale majani.

Jiwe likampiga Umslopogaas kichwani bila kufanya kishindo.

Basi, Yule mlinda zamu alionekana kama ameridhika, akauegemea mkuki wake, akayatazama yale majani kivivu vivu. Alisimama hivi kwa muda wa dakika tatu, kama kwamba anafikiri, na sisi tulijikunja tukiogopa kuwa jambo baya litatokea.

Mwisho alitazama mashariki kama kwamba anaona zamu yake I karibu kwisha, akaisugua mikono yake, akaanza kwenda upesi upesi ili kujipasha moto.

Mara alipogeuka tena, Yule nyoka mweusi mrefu alijinyonga mbele tena, akajificha nyuma ya chungu nyingine ya majani ambayo ilikuwa hatua mbili tu kutoka mahali Yule mlinda zamu anapofika katika mwendo wake.
 
Mkuu blackstarline naona hili shauri la kuiweka yote lime slow process, tafadhali usipate tabu, twende tu kwa mfumo ule ule tulioenda nao tukamaliza Mashimo ya mfalme Suleiman bila tatizo, sura moja kwa siku

Kunradhi kama nimemkwaza yeyote
Mkuu unaweza kunipa link ya Mashimo ya Mfalme Suleiman
 
Yule Mjivuni akageuka akaenda kupita ile chungu ya majani asishuku kuwa adui amejikunja nyuma yake.

Aliipita, ndipo adui yake aliposimama wima akainyosha mikono yake akamfuatia nyuma.

Dakika moja ikapita, na Yule Mjivuni alipotaka kugeuka tena, Yule Mzulu mkubwa alimrukia, na katika mwangaza uliokuwa ukizidi tuliweza kuiona mikono yake mirefu membamba ikimzunguka Mjivuni shingoni na kumkapa koo.

Sasa miili yao wote wawili ilinyongwa pamoja, mara nikaona kichwa cha Mjivuni kinavutwa kwa nyuma, nikasikia kilio kikali kama kwamba kijiti kimevunjwa, akaanguka chini na viungo vyake vinapapatika.

Umslopogaas alikuwa amezitumia nguvu zake za ajabu na kuivunja shingo ya Yule Mjivuni.

Kwa dakika moja zaidi alimkalia mtu wake angali akimkapa koo tu, mpaka akajua hakika hakuna la kuogopa tena kwake, ndipo alipoondoka akatuashiria tuendelee mbele, tukatambaa mbele kwa miguu na mikono kama kundi la nyani.

Tulipolifikia boma tuliona ya kuwa Yule Mjivuni alikuwa amezidi kuuziba mlango ambao upana wake ulikuwa kadiri ya futi kumi kwa kuuvutia matawi mengine.

Basi, hapo tuligawanyika ; Bwana Mackenzie na watu wake walitambaa katika kivuli cha ukuta upande wa kushoto, na Sir Henry na Umslopogaas walishika mahali pao mbele ya mlango, mmoja upande huu na mmoja upande huu wa wale watu wawili wenye mikuki na Yule Mkazi wakalala chini mbele ya mlango.

Mimi na watu wangu tulitambaa upande wa kuume wa boma, ambao urefu wake ulikuwa kadiri ya hatua hamsini.

Nilipofika katikati nilisimama, nikawapanga watu wangu, nikaacha nafasi ya hatua nne katikati yao, kisha, nilichungulia juu ya ukuta wa boma.

Sasa kulianza kuwa kweupe kidogo, nikamwona Yule punda mweupe, na karibu naye niliweza kuuona uso mweupe wa mtoto Flossie, aliyekuwa ameketi kama Yule kijana alivyoeleza, kadiri ya hatua kumi toka ukutani.

Wajivuni wengi walikuwa wamelala kumzunguka, wameshikwa na usingizi. Huko na huko niliona mioto, na kuzunguka kila moto Wajivuni wapatao ishirini na watano walikuwa wamelala, wameshiba sana.

Pengine mtu mmojawapo aliinuka kidogo na kupiga miayo na kutazama mashariki; lakini hapana aliyeondoka.

Nikafikiri kungojea dakika tano zaidi kwanza, ili mwangaza uzidi kidogo nione shabaha vizuri zaidi, tena, kumpa Bwana Good na watu wake nafasi wajipange tayari.

Mara nilipokuwa nikijifanya tayari kutoa ishara ya kuanzisha shambulio, meno ya mtu mmoja aliyekuwa karibu nami yalianza kugongagonga kwa baridi au kwa hofu, na mara ile Mjivuni aliyekuwa karibu sana aliamka akatazama huko na huko akitafuta kitu kinachofanya kelele.

Mimi nilimkasirikia sana mtu Yule kwa sababu ya kufanya kelele, hata nikaingiwa na shaka, nikampiga tumboni kwa kitako cha bunduki yangu ili kuikomesha kelele yake.

Kweli ilikoma, lakini alipojikunja kwa kupingwa, bunduki yake ilifyatuka na risasi yake ilipiga karibu na kichwa changu.
 
Basi, sasa hapakuwa na haja ya kufanya ishara. Kutoka pande zote mbili za boma la ng’ombe, mifulilizo ya risasi ilipigwa, nikaipiga bunduki yangu pia, nikawahi kumwangusha Yule Mjivuni aliyekuwa karibu na Flossie.

Alipokuwa katika kuondoka. Basi, hapo nilisikia sauti kutoka mwisho wa boma iliyopanda juu ya kelele zote, nikatambua ni sauti ya Bwana Good, nikafurahi, na katika dakika iliyofuata, mambo yalitokea ambayo sijaona mfano wake wala sitauona tena.

Wale Wajivuni wote walio ndani ya boma waliruka wakainuka kwa sauti moja ya hofu na hasira, na wengi walianguka palepale wamepigwa risasi za bunduki kabla hawajawahi kujijongeza hata yadi moja.

Wale wengine wasiopigwa walisimama kwa muda wameshangaa, kisha walisikia kelele zinatokea upande wa juu wa boma, wakaduwaa kwa risasi zinazowamiminikia, kisha, wote kwa nia moja walijipeleka kuuendea mlango uliozibwa kwa miiba.

Walipokuwa wakienda, sisi tuliwapiga risasi upesi kadiri tulivyoweza kuzishindilia bunduki zetu.

Nilikuwa ndiyo kwanza nimemaliza kupiga risasi kumi zote zilizokuwa katika bunduki yangu, nikataka kutia nyingine, nikamkumbuka Yule mtoto Flossie.

Nikamwona anapanda juu ya ukuta akisaidiwa na yaya wake aliyekuwa amelala juu ya ukuta, akawahi kupanda juu salama na kuteremka upande wa pili; nikajua ya kuwa yu salama kwa kadiri ilivyowezekana.

Mambo hayo yanachukua muda kuyasimulia, lakini nadhani labda yalichukua nukta kumi na tano tu kufanyika.

Basi hapa nilitia risasi nyingine katika bunduki yangu, nikaanza tena kupiga, si katika wale waliojilundika mlangoni mwa boma, ila katika wengine waliojaribu kupanda ukutani na kukimbia.

Basi, sina haja kusimulia habari zaidi juu ya vita vikali ambavyo vilikuwa mauaji makubwa ya kutisha.

Neno moja tu lastahili kusimuliwa. Nilikuwa nikitumaini ya kuwa vita vimekwisha, na mara ile nikaona mtu akiruka kwa nyuma ya maiti alipokuwa amejificha, akaruka juu ya chungu za maiti, akakimbia mbio karibu na mahali nilipokuwa.

Lakini, kumbe, hakuwa peke yake, Mara ile nilimwona Umslopogaas anamfuatia, na waliponikaribia zaidi, nilimtambua Yule Mjivuni, ndiye Yule tarishi aliyetujia usiku.

Basi, Yule Mjivuni alipoona ya kuwa ingawa anakimbia kadiri awezavyo, lakini Yule anayemfuata anazidi kumkaribia tu, akasimama na adui yake ili apatane naye.

Umslopogaas naye akasimama vile vile, akasema kwa dhihaka.

‘’Ah,ah, ni wewe niliyesema nawe usiku, Mkubwa wa Wajivuni! Tarishi! Mkamata watoto wa kike aliyekuwa tayari kumuua mtoto wa kike! Ndiwe uliyetumaini kusimama uso kwa uso kuwahiana na Umslopogaas, mkubwa wa ukoo wa Makwilisini, wa kabila la Wazulu? Tazama, mambo yako yametimizwa! Nami, niliapa kuwa nitavikongoa viungo vyako, mbwa mfidhuli wewe, Tazama, nitaitimiza nadhiri yangu sasa!’’

Yule Mjivuni aliyasaga meno yake kwa hasira, akamrukia Umslopogaas na mkuki wake mkubwa.

Alijidanganya, Umslopogaas aliepa vizuri, akalipunga shoka lake juu kichwani kwa mikono yote miwili, akalishusha tena kwa nguvu, likampiga Yule Mjivuni nyuma ya mabega shingo inapoungana na kiwiliwili.

Na makali yake yalikata mfupa na nyama na mishipa, yakawa karibu kutenga kichwa na mkono mmoja na kiwiliwili. Pale pale Yule Mjivuni alidondoka chini akiwa maiti.

Umslopogaas aliitazama maiti ya adui yake, akasema, ‘’Basi, Nimetimiza nadhiri yangu ama lilikuwa pigo zuri.’’
 
daaahh chief unatisha " lete mambo aisee "..
 
In most cases hadithi za kubuni is from reality au maisha ya maeneo flani. James Hadley chase novel zake zote zilitokana na miji na maisha ya eneo flani. Mfano ni kweli kwamba Kenya kuna Mto Tana kama ilivyozungumziwa hapa. Pia wamasai niliowaona Kenya tamaduni zao ni sawa kabisa na walioko Tanzanian, kuna kipindi wamasai wa Tanzania wakiiba mifugo walikuwa wanaipeleka Kenya.
nashukuru mkuu kwa ufafanuzi,nategemea upo sahihi,lakini nakuwekea hapa screenshot ya english version pamoja na plot summary kutoka wikipedia,kote wametumia masai sehemu ya wajivuni kwenye swahili version.
 
Attachments

  • Screenshot_2018-10-01-21-33-38.png
    Screenshot_2018-10-01-21-33-38.png
    213.7 KB · Views: 101
  • Screenshot_2018-10-01-21-36-29.png
    Screenshot_2018-10-01-21-36-29.png
    86.8 KB · Views: 80
nashukuru mkuu kwa ufafanuzi,nategemea upo sahihi,lakini nakuwekea hapa screenshot ya english version pamoja na plot summary kutoka wikipedia,kote wametumia masai sehemu ya wajivuni kwenye swahili version.
Dah mkuu thanks for sharing this English version, na labda yawezekana am wrong. Nimejifunza kitu kimoja hapo hao Masai outcast ambao babu yangu pia aliwahi nisimulia wanaitwa WAKWAVI ni kweli kabisa.
 
Yule Mjivuni akautikisa mkuki wake mrefu, akacheka sana kwa muda mrefu, akajibu, ‘’Laiti tungeweza kushindana mimi na wewe peke yetu, ningekuonyesha kazi.’’ Aligeuka aende zake huku anacheka.
Umslopogaas akajibu, na ‘sauti yake ingali ikinguruma,’
‘’Usiwe na shaka, tutashindana peke yetu mimi na wewe.’’
‘’Utashindana uso kwa uso na Umslopogaas, wa damu ya Chaka, wa kabila la Wazulu, mkuu wa jeshi la Nkomabakosi, kama wengi wengine walivyofanya; nawe utajisalimisha mbele ya Inkosikazi kama walivyofanya wengi wengine. Ndiyo, cheka, cheka ila mwisho wako nakuhakikishia fisi watakuwa wanacheka na huku wanavunja mifupa na kuzitafuna mbavu zako.’’

Tuendelee....
SURA YA SITA

Alipokwisha kwenda Yule Mjivuni, mmoja wetu alilifungua lile kapu. Ua zuri sana lilionekana ndani yake, tena barua ndogo iliyoandikwa katika karatasi iliyofungiwa chakula alichokichukuwa, maneno ya barua hiyo ni haya:

‘’Wapenzi Baba na Mama, Wajivuni wametukamata tulipokuwa tukirudi pamoja na ua hili. Nilijaribu kukimbia nisiweze, Hawakunizuru wala yaya, lakini wamesema watanibadilisha kwa mmoja wapo wa rafiki za Bwana Quatermain, Mimi sikubali shauri hili.
Usimwache mtu yeyote atoe maisha yake kuniokoa mimi. Jaribu kuwashambulia usiku; wanafanya karamu ya ng’ombe watatu walioiba na kuchinja. Ninaogopa sana, lakini namtumaini Mungu. Siwezi kuandika zaidi, maana wanaanza kunitazama.
Kwa herini
Flossie.’’

Kwa nje ya karatasi iliandikwa, ‘’Nisalimie Bwana Quatermain. Wanachukua kapu, basi atalipata lile ua.’’

Nilipoyasoma maneno yaliyoandikwa na Yule mtoto mwanamke shujaa wakati wa hatari ambayo ilitosha kumtia wazimu mtu mzima mwenye nguvu, nakiri ya kuwa nililia machozi, tena, katika moyo wangu nilinuia hafi kabisa ya kuwa hafi ikiwa maisha yangu yanaweza kumuokoa.

Basi, hapa tulianza kuzungumza kwa bidii juu ya shauri la kufanya.

Nikasema tena ya kuwa nitakwenda, na tena Bwana Mackenzie alikataa, na Sir Henry na Bwana Good kama watu wema na waaminifu walivyo, walisema nikienda, basi na wao watakwenda pamoja nami na kufa pamoja nami.

Mwisho, nilisema, ‘’Ni lazima kabisa tufanye jambo kabla ya kufika mapambazuko.’’
Tulikaa pamoja na bwana Mackenzie na kupanga shauri, mwisho tulikubaliana kuwa tuwavamie kijeshi ifikapo muda wa mapambazuko kwa kujua muda huo ulikuwa ni mzuri kwani watakuwa wapo kwenye usingizi mzito.

Pamoja na kuwa hatukuwa na jeshi la kutosha kwani walinzi wengi wa pale mission walikuwa wamesafiri mbali lakini hatukukata tamaa.

Hao hao wachache waliokuwepo tuliona kuwa wanatosha kabisa kuwaunganisha pamoja na kwenda kupambana na wale Wajivuni.

Cha kwanza tuliunda kundi dogo la wapelelezi waende kule kwenye boma la ng’ombe walipoweka kambi yao kwa ajili ya kuwapeleleza na kutupatia ripoti ya nini kinaendelea kila waonapo inafaa kufanya hivyo.

Basi, tulipokwisha weka mambo yote tayari, ilikuwa karibu saa saba ya usiku, tukasubiri. Wapeleleze wetu walituambia kuwa Wajivuni wamekwisha kunywa damu ya ng’ombe na kula nyama nyingi sana, na sasa wamelala kuizunguka mioto yao, lakini watu wakulinda zamu wamewekwa kila mlango.

Flossie, Yule mtoto mdogo alikuwa amewekwa karibu ya ukuta katikati ya upande wa magharibi ya boma, na yaya wake yu karibu naye, na punda weupe amefungiwa kigingi.

Miguu ya mtoto imefungwa kwa kamba, na Wajivuni wamelala huko na huko kumzunguka.

Basi kwa kuwa hakuna jambo tena la kufanya, tulikula kidogo, tukalala kwa muda wa saa mbili.

Niliona ajabu jinsi mzee Umslopogaas alivyoweza kujitupa chini na kupata usingizi mara ile, ingawa mambo makubwa yanamngojea.

Sijui habari za wale wenzangu, lakini mimi sikuweza kulala usingizi. Kwa hakika niliogopa, na sasa kwa kuwa nilikaa kimya, nilianza kufikiri juu ya mambo tunayojaribu kuyafanya, nami sikuyapenda hata kidogo.

Tulikuwa watu thelathini jumla na hawakosi wengine hawakuzoea kupigana, nasi tunakwenda kuwashambulia watu wakali mia mbili na hamsini, watu hodari na stadi wa vita kuliko wenyeji wote wa Afrika, na zaidi ya hayo, walikuwa wamelindwa kwa boma la mawe.

Kweli ni jambo la hatari, na hasa kwa sababu hatuna budi kupafikia mahali petu bila kufanya kelele zozote, tena bila kuonekana na wale Wajivuni waliowekwa kulinda zamu.

Hakika, tukiwaamsha kwa jambo lolote kama vile bunduki ikifyatuka kwa habahati mbaya basi, tumekwisha potea wote, maana Wajivuni wote wataamka mara ile, na tumaini letu la kushinda ni kuwatokea ghafla.

Baada ya kupita muda, nilimsikia Bwana Mackenzie akinong’ona nje ya chumba changu, maana kila jambo lazima lifanywe kimya sana, akaniambia kuwa ni saa tisa, nasi hatuna budi kuanza kazi yetu saa tisa na nusu.

Basi, nilimwambia aingie chumbani, na wakati huo kila mtu alikuwa akivaa na kujitengeneza tayari.

Huku nyuma Umslopogaas alikuwa akiwakusanya watu kiwanjani chini ya ule mti mrefu, akawakagua kuona kama kila mtu ana silaha zake tayari.

Mwisho tulibadili shauri kidogo, tulitoa watu wawili katika wale waliokuwa na bunduki, tukawapa ngao na mikuki ya Kijivuni, tukawaambia wafuatane na Sir Henry na Umslopogaas na Yule Mkazi kuulinda mlango mkubwa wa boma lote tuliona kwa dhahiri ya kuwa watu watatu, hatakama ni hodari na wenye nguvu namna gani, hawatoshi kwa kazi ile.
Salute mkuu
 
Dah! Mkuu hichi kipande sina kama unacho kiunganishie tu hapo, utakuwa umetusaidia sana.
Kitabu kipo mbali nami ila hukumbuka sana hapo kwani yule mzee mzulu alipanga mashambulizi si mchezo. Siwezi kwenda neno kwa neno ila kifupi ilikuwa hivi. Basi tubahatishe kuwashambulia usiku alisema inkubu. "Ndio umesema kama mwanamume inkubu ya nini kuogopa bwana mkubwa (mackenzie anao watu 20 na kuna watu weupe hawa tunatosha yule mtoto alisema watakula na kufanya karamu kwa ng'ombe waliowaiba basi na iwe karamu yao ya mazikoni yule mbwa ninae tumaini kumuumbua kutakapo pambazuka alisema haogopi kuwa tutawashambulia sababu tu wachache walijua boma waliloweka
Kambi mimi nililiona asubuhi tizama vita vitakuwa hivi wakati mwangaza unaanza kuziangazia pembe za ng"ombe na si kabla mimi na wewe inkubu na yule mlinzi mwenye kifua kipana ni mtu jasiri twende kimya kimya tumuue yule mlinzi anae shika zamu penye ule mlango mkubwa wa boma bila kufanya kelele zozote kisha watu waliobaki wagawanywe wewe makumazahn wanane na wanane waende na bwana Mackenzie bougwan aende na watu wake katika ule mmwemba wangoje huko.
Kisha makumazahn utakapo toa ishara ya mlio wa ng 'ombe waanze kushambulia lakini wasimpige yule mtoto wa kike. Bas. Mmoja upande huu mmoja upande ule m basi hilo ndilo shauri langu makumazahn kama nawe una shauri zuri lilete.
Kwa kweli wote tulifurahishwa na shauri la yule mzee ikabidi niwatafsirie baadhi ya maneno na sote tulikubaliana naye nikawa namtania mzee simba unajua mahali pa kushika na wakati wa kushika! akasema ndio makumazahn vita vitakuwa vyema.
 
Back
Top Bottom